Nchini Tanzania, bullying ni kitu cha kawaida?

Nchini Tanzania, bullying ni kitu cha kawaida?

Salama wakuu?

Kuna hii kitu inaitwa bullying ama Kwa lugha ya kiswahili tuite labda uonevu.hii kitu ni common sana na inachukuliwa kawaida na jamii yetu kiasi inaleta madhara lakini hatuyaoni na hata tukiyaona tunayafumbia macho na kuona ni kawaida.

Kuna bullying za aina tofauti kama

• Kimwili: Kupigwa, kusukumwa ovyo, au kuumizwa.
• Kinywa / Maneno: Kuitwa majina yasiyofaa, kutukanwa, au kutishwa.
• Kihisia na Kisaikolojia: Kutengwa, kudhalilishwa nk

Ningesema ni tatizo la hivi karibuNi lakini nikikumbuka katika ukuaji wangu na matukio naona ni kitu haakijaanza Leo na akili zetu zimeadapt kwamba ni kawaida Haina shida.
Kuanzia wanawake,wanaume,vijana,watoto na wazee.
Sio shuleni,sio vyuoni,sio ma hospital hasa za serikalini,viongozi wa serikali,viongozi wa vyama vya siasa,mbaya zaidi mtaani.

Ni kawaida kukuta watu wanatungana majina Kwa muonekano, maumbile ama changamoto,ama tukio
Unakuta mtu mweusi anaitwa cheusi Mangala,mfupi wanamuita kijeba,kidingi..
Mpaka wanaume weupe wanakuwa bullied na wanaume wenzao wakiwaona kama wanawake,mtu mrefu anaitwa ngongoti
Mtu aliezaliwa na changamoto ya miguu kupishana urefu wanamuita chiba,mtu mwenye akili ziko slow kuadapt wanamuita zezeta.mwenye kushindwa kuelewa jambo na kulifanya Kwa ufanisi anaitwa kilaza nk
Na mengine mengi sana.
imekuwa common sana.hali inayopelekea wengine kushindwa kustahimili,Kuna wanaojidhuru,Kuna wanaathirika kisaikolojia na kuwa na msongo wa mawazo,na wengine wanajichukia na kukosa kujiamini haswa Kwa watoto na ma teenager ambao bado hawajakomaa kisaikolojia na kiakili kukabiliana na mengi.

Wakati nchi za ughaibuni wamepitisha kama ni kosa kumbully mwenzio.Mfano nchini Korea ikiwa mwanafunzi atambully mwenzie basi atakuwa suspended.

Sawa najua Africa sio kwaajili ya mtu dhaifu,tuna namna yetu ya kurespond Kwa bullies aina zote,lakini ingependeza kama tulngelichukulia Kwa uzito kama lenye madhara Kwa ustawi wa watu na jamii Kwa ujumla.tunaweza kuona ni kawaida ila ni ajabu na aibu.

Juzi juzi tu hapa Kuna cashier wa supermarket kapigana na mteja baada ya mteja kudai kamuita "shangingi"

Mashindano yanaoyoendelea ya Miss grand international waTanzania wameingia kwenye shutuma za bullying Kwa kuachia comments zinazosanifu washiriki wengine,Yale wanayoandika nchi nyingine Wana translate wanasoma.imefikia wanashangaa.

Yangu ni hayo tu.
Tanzania mtu ana ku bully, ukimwambia hii ni bullying anakwambia nakutania tu, mbona uko sensitive sana?

Yani hapo hapo kaku bully halafu kaku gaslight.

Sasa unamtaniaje mtu ambaye hamna matani naye?
 
Kwenye kusoma kwangu, nimewahi kufundishwa na Wazungu kuanzia level za chini

Wenzetu kwenye jambo walikuwa hawapendi ni kum-bully mwanafunzi

Walikuwa wanasema inamwondolea mwanafunzi ari ya kujiamini tena
Ndio hivyo
Lakini sisi tukaona kuzomea na kuzodoa ndio njia ya kumpa mtu morali ya kufanya vyema.matokeo atafanya vyema akiwa ameambatana na nidhamu ya uoga wa kushindwa na sio kujiamini
 
Ndio hivyo
Lakini sisi tukaona kuzomea na kuzodoa ndio njia ya kumpa mtu morali ya kufanya vyema.matokeo atafanya vyema akiwa ameambatana na nidhamu ya uoga wa kushindwa na sio kujiamini
Hakika

Ndiyo maana Watanzania wengi wana tatizo la kushindwa kujiamini

Kumbe chanzo kilianzia zile bullying za shule ya msingi 🙌
 
Bullying kwa kiswahili ni uonevu , na ukiona unaonewa jua wewe ni mnyonge, kuepuka kuwa bullied acha unyonge, acha kutia huruma, pambana
Unampa mbinu gani mwanao kudeal na bullies?
Na ikiwa anaembully ni mtu mzima?
Mfano mwalimu anaembully mwanafunzi,ikiwa mwanafunzi atareact kosa atapewa nani kama bullying sio kosa kisheria?
Ndio maana wenzenu Wana Sheria zao na ni marufuku.kuna namna ya kudeal na mambo kama haya zaidi kupigana huko mtaani.

Hakuna mtu mzima atakaekaa tu hivi kinyonge anaonewa bila kuchukua hatua.

Naongelea Kwa niaba ya watoto
 
Siyo kweli
Siyo kweli nini ?

Mmeamua kujitoa ufahamu ili kujipendekeza kwa watawala, mara ngapi huwa mnausema vibaya ulemavu wa Lissu?
Ukizingatia ulemavu wake aliupata kwenye utawala huu huu

Mmekuwa wajinga na wapumbavu kwa sababu ya kuendekeza UCHAWA ila kumbuka upepo wa Wanasiasa sio wa kuuamini ( Yusuf Manji utawala wa Jakaya alimuita Magufuli Mbwa ) lakini Mbwa akaja kuwa Simba. Mmekuwa wapuuzi kupindukia yaani mpaka mnamfanyia bullying rais 😂😂😂
 
Tanzania mtu ana ku bully, ukimwambia hii ni bullying anakwambia nakutania tu, mbona uko sensitive sana?

Yani hapo hapo kaku bully halafu kaku gaslight.

Sasa unamtaniaje mtu ambaye hamna matani naye?
Na wanaona ni kitu Cha kawaida tu.
Mi naona ianze kuwa somo mashuleni na athari zake.itasaidia mbeleni kizazi kitabadilika.kuna mambo tunayachukulia kiwepesi lakini yana effect kubwa kisaikolojia.
 
suala la bullying, hasa ya maneno ni ngumu sana kuidhibiti, changamoto kuu ikiwa ni malezi,.....
lakin kuikomesha hiyo ni ngumu sana,...
Ni too late
Hasa Kwa sie jamii zilizovurugwa kichwani.lakini mmoja akiamua anaweza
Kwahiyo imekuwa JINO KWA JINO ?
Namuonesha jinsi kulivyojaa bullies humu
 
Salama wakuu?

Kuna hii kitu inaitwa bullying ama Kwa lugha ya kiswahili tuite labda uonevu.hii kitu ni common sana na inachukuliwa kawaida na jamii yetu kiasi inaleta madhara lakini hatuyaoni na hata tukiyaona tunayafumbia macho na kuona ni kawaida.

Kuna bullying za aina tofauti kama

• Kimwili: Kupigwa, kusukumwa ovyo, au kuumizwa.
• Kinywa / Maneno: Kuitwa majina yasiyofaa, kutukanwa, au kutishwa.
• Kihisia na Kisaikolojia: Kutengwa, kudhalilishwa nk

Ningesema ni tatizo la hivi karibuNi lakini nikikumbuka katika ukuaji wangu na matukio naona ni kitu haakijaanza Leo na akili zetu zimeadapt kwamba ni kawaida Haina shida.
Kuanzia wanawake,wanaume,vijana,watoto na wazee.
Sio shuleni,sio vyuoni,sio ma hospital hasa za serikalini,viongozi wa serikali,viongozi wa vyama vya siasa,mbaya zaidi mtaani.

Ni kawaida kukuta watu wanatungana majina Kwa muonekano, maumbile ama changamoto,ama tukio
Unakuta mtu mweusi anaitwa cheusi Mangala,mfupi wanamuita kijeba,kidingi..
Mpaka wanaume weupe wanakuwa bullied na wanaume wenzao wakiwaona kama wanawake,mtu mrefu anaitwa ngongoti
Mtu aliezaliwa na changamoto ya miguu kupishana urefu wanamuita chiba,mtu mwenye akili ziko slow kuadapt wanamuita zezeta.mwenye kushindwa kuelewa jambo na kulifanya Kwa ufanisi anaitwa kilaza nk
Na mengine mengi sana.
imekuwa common sana.hali inayopelekea wengine kushindwa kustahimili,Kuna wanaojidhuru,Kuna wanaathirika kisaikolojia na kuwa na msongo wa mawazo,na wengine wanajichukia na kukosa kujiamini haswa Kwa watoto na ma teenager ambao bado hawajakomaa kisaikolojia na kiakili kukabiliana na mengi.

Wakati nchi za ughaibuni wamepitisha kama ni kosa kumbully mwenzio.Mfano nchini Korea ikiwa mwanafunzi atambully mwenzie basi atakuwa suspended.

Sawa najua Africa sio kwaajili ya mtu dhaifu,tuna namna yetu ya kurespond Kwa bullies aina zote,lakini ingependeza kama tulngelichukulia Kwa uzito kama lenye madhara Kwa ustawi wa watu na jamii Kwa ujumla.tunaweza kuona ni kawaida ila ni ajabu na aibu.

Juzi juzi tu hapa Kuna cashier wa supermarket kapigana na mteja baada ya mteja kudai kamuita "shangingi"

Mashindano yanaoyoendelea ya Miss grand international waTanzania wameingia kwenye shutuma za bullying Kwa kuachia comments zinazosanifu washiriki wengine,Yale wanayoandika nchi nyingine Wana translate wanasoma.imefikia wanashangaa.

Yangu ni hayo tu.
Mkuu Abigail umegusa donda ndugu ambalo jamii yetu inalifumbia macho kwa kisingizio cha "Utani." Ukweli unaouma ni kwamba huku kwetu mstari kati ya utani wa kishkaji na uonevu (bullying) umefutika kabisa. Majina ya kashfa kama Cheusi Mangala, Kijeba, Kilaza au Zezeta yanachukuliwa kama burudani ya kawaida ya kijiweni au ya kifamilia. Hali hii inachagizwa na fikra potofu kwamba ili ufanikiwe Afrika lazima uwe na "ngozi ngumu." Mtu anayeonyesha kukwazwa huonekana mlaini, jambo linalopelekea waathirika wengi kuficha maumivu yao. Mbaya zaidi, mitandao ya kijamii imekuwa uwanja mkuu wa kejeli, kama ulivyotolea mfano wa shindano la Miss Grand International, ambapo watu wanajificha nyuma ya keyboards bila kujua ulimwengu unatusoma na kututafsiri vibaya.
Hali hii inaleta madhara makubwa ya kisaikolojia na kijamii ambayo tunayafumbia macho. Unyogovu (depression), msongo wa mawazo, na kukosa kujiamini huanzia hapa; watoto na vijana wengi wanafeli shule sio kwa sababu hawana akili, bali kwa sababu mazingira yanawavunja moyo. Zaidi ya athari za kiakili, uonevu huu unaweza kuzaa ghasia na vurugu za kimwili pale mtu anapofikia kikomo cha uvumilivu wake, kama ulivyobainisha kwenye lile tukio la cashier wa supermarket aliyepigana na mteja baada ya kuitwa jina la kashfa. Hii inathibitisha wazi kuwa uonevu wa maneno sio jambo la kawaida bali ni bomu la kimya kimya linaloangamiza ustawi wa jamii yetu.
Ili kukabiliana na changamoto hii, hatua zinapaswa kuanzia ngazi ya mtu mmoja-mmoja kwa kuweka mipaka (boundaries). Mtu anapokupa jina usilolipenda, mweleze wazi na kwa msisitizo bila kucheka kuficha aibu, na kama jamii tuache kushabikia "utani wa sumu" unaolenga maumbile ya mtu. Ngazi ya malezi nayo inahusika moja kwa moja ambapo wazazi wana wajibu wa kuwafundisha watoto wao kuheshimu tofauti za wengine tangu wakiwa wadogo. Mwisho kabisa, tunahitaji mapinduzi makubwa ya kisera kwenye taasisi zetu. Shule na maofisi yanapaswa kuwa na sera kali na adhabu zisizo na muhali (Anti-bullying policies) kama nchi za wenzetu mfano Korea. Uzi wako ni tahadhari muhimu kwamba kulinda utu na staha ya kila mtanzania ndio msingi wa maendeleo ya kweli. Uonevu sio sifa, ni ugonjwa unaohitaji tiba ya haraka.
 
Back
Top Bottom