Nchini Tanzania, bullying ni kitu cha kawaida?

Hii nchi yetu ni shida sana mkuu
 
Kazi sana...
Hivi unasikia wanavyoimba kwenye taarabu tangu miaka na miaka haswa wanawake?
 
Sasa mtu Kama chivayo unaweza kumwitaje zaidi ya bonge Nyanya SI ndio alivyo

Wakati mwingine upekee wa mtu ndio unakua utambulisho wake mfano toll, short , bonge , ras, kibonge , cheusi , zeruzeru , chiba, kilaza ipo hivyo
majina ya kuitana mkuu hayo ya kutunga mengine yamekaa kidhalilishaji..
 
Itachukuwa muda sana.
Kila mmoja labda akiamua ndio inawezekana.
Mie ni muhanga wa bullies Tena Kwa mtu nliempenda.lakini Nina Ile akili ya kupuuzia mambo nasahau.
Athari zake ninazo mpaka Leo.
Sasa nikikumbuka na mie nilivyokuwa nabully bila kuwa na uelewa najikuta nasikitika.

Hii kitu ni hasara tunahitaji kubadilika.especially mbele ya watoto wasio na hatia.mbully hata jambazi ama muuaji ila mtoto hapana muache.ni mateso ya kiakili unampandikizia.
 
Nimekuelewa mkuu
 
Kazi sana...
Hivi unasikia wanavyoimba kwenye taarabu tangu miaka na miaka haswa wanawake?
Hapo kwenye taarab umepatia mkuu,nikiwa mdogo taarab zilinifanya nijiulize watu wa pwani wanaishije maana sio kwa maneno yale. Eti mtu anajisifu kuchukua mume wa mtu😂😂😂
 
Hapo kwenye taarab umepatia mkuu,nikiwa mdogo taarab zilinifanya nijiulize watu wa pwani wanaishije maana sio kwa maneno yale. Eti mtu anajisifu kuchukua mume wa mtu😂😂😂
Kawaida kwao..bado ulieibiwa mume hujaitwa majina kibao ikiwemo sanamu la Michelin😄
 
Nipo hapa kupata ilmu,Hivi mgongo wazi ni kama alivyo petro magoti au ni kitu kingine tofauti?
 
Nipo hapa kupata ilmu,Hivi mgongo wazi ni kama alivyo petro magoti au ni kitu kingine tofauti?
Mgongo wazi yaani mgongo unakuwa na kama kishimo kabisa, hicho kishimo huwezi kukiona labda avue nguo. Wanaozaliwa na huo ugonjwa sidhani kama huwa wanatoboa kufika ukubwani. Mgongo wazi na kichwa kikubwa ni ndugu maana vyote chanzo ni mama kukosa folic acid akiwa mjamzito.
 
Tukiwa watoto tulipitia hayo.tunaweza epushia watoto wetu pia.
Wengine hawana nguvu ya kustahimili.
Nje wakimbully,wewe ndani mpe moyo na hamasa.
Ikiwa tu jamii itashindwa kubadilika
Somo hili liwafikie walimu,
Walimu wanapunguza kujiamini kwa watoto wetu kwasababu ya bullying
 
Tatizo likishaota miziz linachukua muda na juhudi sana kuling'oa.Nina Imani i
po siku tutaachana na haya.
Tatizo hili linaweza kuisha kisheria.
Serikali ikitunga sheria na adhabu yake, elimu itolewe na walimu wabadirishe mitazamo yao inaweza kutoweka ingawa inaweza kuchukua muda kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…