Ndani ya Katiba: Tai nyekundu kuwa vazi la Mwenye Mamlaka imeandikwa kwenye ibara gani?

Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere hakuwahi kuvaa tai nyekundu.
Huyu jamaa alikuwa anatuvalisha kaunda suti za kaki,ikifuliwa suruali inaruka.Mambo ya suti na tai tuliyaanza baada ya Mzee Ruksa kuingia madarakani!
 
Halafu hiyo chupi nyekundu nani atakuwa anaiona kwa mfano??
Mambo mengine ukilazimisha kupinga unaonyesha uwezo wako wa kufikiri ulipofikia.
Hiyo ndiyo kuingilia privacy ya mtu; serikali haimnunulii mbunge tai, kwa hiyo isimchagulie avae tai gani. Kama serikali huwa inatoa tai za bure kwa wabunge basi iseme.
 
Ni suala la kiitifaki.
Hii inatokana na utamaduni wa kidiplomansia.
Spika wa Bunge yupo sahihi kiitifaki
Na pale ametoa utaratibu wa kiitifaki.
Hizo maana za rangi ya tie (tai) ni kutokana na utamaduni Wa magharibi! Tunaiga!! Sina uhakika tutaishia wapi kuiga! maana safari moja huanzisha Nyingine!
 
Huyu jamaa alikuwa anatuvalisha kaunda suti za kaki,ikifuliwa suruali inaruka.Mambo ya suti na tai tuliyaanza baada ya Mzee Ruksa kuingia madarakani!
Nyerere hakukwahi kukununulia Kaunda suti za Kaki; kama ulikuwa unanunua nguo z a kufananan na zake ukawa unanunua kaki, basi hayo yalikuwa ni matatizo yako tu. Hakuwahi kumlazimisha mtu yeyeote avae vipi. Mwone hapa amepiga tai yake

Kwenye kabinet yake George Kahama alikuwa anavaa suti na tai muda wote, ambayo ndiyo ilikuwa sababu ya kuitwa Sir george kahama
 
Hapa alikuwa bado anashikamana na ubeberuni miaka ya 60.Baada ya hapo ilikuwa kaunda suti za kaki kwa kwenda mbele tena vitambaa toka viwanda vya ndani visivyo na ubora.Na hiyo kaki ikichanika unaweka kiraka!
 
Labda Itafiki ya Lumumba
Kwengine kote duniani watu wanavaa tai zao nyekundu kama kawaida wakati marais wao wanahutubia mabunge yao.
Sio kila kitu kipo kwenye katiba
Licha ya ukubwa wake, bunge linaongozwa kwa kanuni ambazo hazipo kwenye katiba.
Ndio mana nimesema hapo juu kuwa kwenye nyanja ya diplomansia, kuna mambo tumekubaliana nayo kama sehemu ya itifaki.
Ila hazipo kwenye katiba.
 
Hiyo ndiyo kuingilia privacy ya mtu; serikali haimnunulii mbunge tai, kwa hiyo isimchagulie avae tai gani. Kama serikali huwa inatoa tai za bure kwa wabunge basi iseme.
With due respect.Kwani Serikali inawanunulia wabunge mavazi ya kuvaa wanapokuwa bungeni?Mbona wanalazimika kufuata dress code?Vaa basi msuli au jeans uingie nao bungeni kwa kisingizio hununuliwi na ni privacy yako!!
 
Tumeonywa mara nyingi sana na wanasheria kwamba kutokujua sheria , iwe kwa sababu ya elimu yako duni , uzembe wako au labda ujinga wako wa kutokufuatialia sheria na makatazo mbalimbali ya nchi yako hakukufanyi usichukuliwe hatua za kisheria pale unapokosea , ukikutwa na hatia utahukumiwa bila huruma yeyote ile.

Naomba nikiri hadharani kwamba mimi ni mvaa Tai wa siku nyingi na ninazo zaidi ya Tai 50 zenye rangi nyekundu , ambazo nazivaa ninapotaka na tena nazivaa hata kwenye hafla za kitaifa , kiukweli sikuelewa kama natenda kosa , hakika usilolijua ni sawa na usiku wa giza nene !

Naomba sana Wanasheria mliomo humu mkiongozwa na Petro E. Mselewa mnionyeshe andiko lililomo ndani ya Katiba yetu linalokataza kapuku kuvaa Tai nyekundu ili iwe fundisho kwangu na kwa mbumbumbu wenzangu wengine wasiojua chochote ili tuepuke jela ya kizembe.

Natanguliza Shukrani.
Protocol and etiquette
 
With due respect.Kwani Serikali inawanunulia wabunge mavazi ya kuvaa wanapokuwa bungeni?Mbona wanalazimika kufuata dress code?Vaa basi msuli au jeans uingie nao bungeni kwa kisingizio hununuliwi na ni privacy yako!!
Dress code huwa haihusishi rangi ya vazi.
 
Kwahio tukisema chama chenu unahitaji kulewa ama kua na tundu kichwan kuwaelewa tutakua tumekosea? Sasa tai na katiba wap wap ndugu?
 
With due respect.Kwani Serikali inawanunulia wabunge mavazi ya kuvaa wanapokuwa bungeni?Mbona wanalazimika kufuata dress code?Vaa basi msuli au jeans uingie nao bungeni kwa kisingizio hununuliwi na ni privacy yako!!
Ndio Serikali inawanunulia wabunge mavazi ya kuvaa, au umesahahu kuwa wabunge wanapatiwa hela za kununulia suti?
 
Kwanini hii issue usiipotezee very minor...
haina afya yyte katika ukuaji wa kiuchumi taifani

sasa chadema watasema nn kusipokua na mtukio kama haya, chama kimefika stage kinaraise mjadala kisa tai nyekundu kukatazwa, hicho ni chama ama?
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Sio kila kitu lazima kiandikwe.

Wewe ukisimamishwa barabarani upishe rais anapita hua unauliza hii imeandikwa wapi?

Bavicha akili mapeleka wapi?

Ziko sheria/miongozo kuhusu emergency traffic, priority traffic na presidential/VIP motorcade traffic.
 
Tumeonywa mara nyingi sana na wanasheria kwamba kutokujua sheria , iwe kwa sababu ya elimu yako duni , uzembe wako au labda ujinga wako wa kutokufuatialia sheria na makatazo mbalimbali ya nchi yako hakukufanyi usichukuliwe hatua za kisheria pale unapokosea , ukikutwa na hatia utahukumiwa bila huruma yeyote ile.

Naomba nikiri hadharani kwamba mimi ni mvaa Tai wa siku nyingi na ninazo zaidi ya Tai 50 zenye rangi nyekundu , ambazo nazivaa ninapotaka na tena nazivaa hata kwenye hafla za kitaifa , kiukweli sikuelewa kama natenda kosa , hakika usilolijua ni sawa na usiku wa giza nene !

Naomba sana Wanasheria mliomo humu mkiongozwa na Petro E. Mselewa mnionyeshe andiko lililomo ndani ya Katiba yetu linalokataza kapuku kuvaa Tai nyekundu ili iwe fundisho kwangu na kwa mbumbumbu wenzangu wengine wasiojua chochote ili tuepuke jela ya kizembe.

Natanguliza Shukrani.
Kikatiba na kisheria, hapa Tanzania, hakuna hilo takwa. Rangi za tai ni mambo ya kimapokeo na ya kiutamaduni tu kwenye uga wa kidiplomasia na kiutawala. Hakuna sheria iliyoandikwa kuhusu hilo
 
Back
Top Bottom