Ndani ya Mwaka mmoja, Rais Samia katoa Ajira zaidi ya 50 Elfu, Vijana tunashukuru sana

Ndani ya Mwaka mmoja, Rais Samia katoa Ajira zaidi ya 50 Elfu, Vijana tunashukuru sana

ngebe

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2020
Posts
1,789
Reaction score
5,117
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, baada ya kusota kwamiaka sita tangu 2015 mpk 2021 bila ajira huku tukidanganywa kama watoto eti tuuzie biashara popote hata barabarani na kwenye round about za miji hatimaye 2021 march tulipata mkombozi wa vijana,

Ni ukweli usiopingika Samia umejaribu kuangalia maisha ya vijana kwa kuwapa ajira, Japo tunajua huwezi kuwamaliza wote kulingana na kua walirundikana sana kipindi cha awamu ya tano lakini wewe angalau unajitahidi kwa kiasi chako,

Magereza, TRA, uhamiaji, Arshi, Afya, Elimu, Polisi, Jwtz, Na serikali za mitaa,

Tangu march 2021

AFYA - 2726 may 2021 + 10285 (2022)
ELIMU - 6949 (2021) + 9800 (2022)
TRA 2129
ARDHI 1440
POLISI 3275
UVUVI 204
MIFUGO 700
TAKUKURU 350
MAGEREZA 534
UHAMIAJI 350
Jumla ya hizi ni 38772 ndani ya mwaka mmoja kitu ambacho hakijawai kutokea tangu 2015 mpaka 2021 march,

na bado kuna ajira nyingine 13000 za serikali za mitaa na mashirika ya serikali ziko kwenye mchakato zitoke kabla ya july 2022

Kwakweli umejitahidi sana na tunaomba uendelee kwa moyo huo huo vijana tuliteseka sana awamu ya tano tuliishi kama digidigi,

Tutazunguka sana na kuzungusha maneno lakini ukweli hautabadilika awamu ya tano ilitengeneza maskini wengi

IMG_20220509_102231.jpg

Tumshukuru Mungu
 
Kwa hiyo baada ya wewe tu kupata, ukaamua kujigeuza kuwa msemaji hata kwa wale vijana maelfu ambao wanataabika mtaani kwa miaka sasa.
umesoma ukaelewa kweli?
 
Mkuuu [emoji849][emoji849] ni ajira zipiii
sekta zote mf TAKUKURU, TRA, UHAMIAJI, MAGEREZA, AFYA, ELIMU, JWTZ, POLISI, ARDHI, MIFUGO, inamaana hizi nyie hamzioni au?
 
Tuzisubir hiz ambazo Sina uhakika kua SI za Mchongo
 
type na idadi ya watu kutoka vyuo vikuu, vya Kati na vyuo vya ufundi wanaoingia kwenye soko la ajira kwa mwaka ili tufanye tathimini kabla ya kumpongeza huyo mama yenu
 
Hakika raisi Samia anastahili kupongezwa, kwa kuajiri vijana wengi katika muda mchache aliokaa madarakani. Hakuna raisi au taifa lolote lililowahi kuajiri vijana wote nchi nzima. Hata huko Marekani, Ulaya, Canada, Australia, China, Japan nk kuna jobless wa kumwaga tu. Kwahiyo kwa hatua aliyofikia anastahili pongezi. Ila mleta mada umekosea kumuingiza hayati Magufuli kwenye uzi wako. We ungeandika tu kuhusu raisi Samia kuajiri maelfu ya watanzania bila kumuingiza Magufuli na hoja yako ingeeleweka vyema tu ndugu yangu.
 
type na idadi ya watu kutoka vyuo vikuu, vya Kati na vyuo vya ufundi wanaoingia kwenye soko la ajira kwa mwaka ili tufanye tathimini kabla ya kumpongeza huyo mama yenu
nimeweka hapo juu idadi
 
Ajira nzuri ni za kujiajiri; ukiwapa umeme wa uhakika bila katikakatika watu wanaingiza kipato, ukiwathamini mama ntilie na machinga na waliojiajiri kwa mitaji midogo utakuwa umeajiri wengi!

Sasa hizi figure ni kama zimerudi zile ajira za kwenye makaratasi,
Watu wanakula mishahara ya waajiriwa HEWA
 
kwa upande wako ajira nzuri ni kujiajiri, lakini sio kwa wote, wengine ajira nzuri ni kuajiliwa kila mtu ana interest zake
 
Umechemka, awamu Fulani Vijana walipata Ajira tokana na miradi mingi ya maendeleo mishahara kwa wakati ila kwa Sasa ata watoe Ajira million elf 10 hamna Cha maana mamboo yashaenda mrama"
 
Basi kabla haujasifu outputs jaribu kuangalia inputs. unasifu ajira 50k kwa mwaka wakati wanaoingia kwenye soko ni zaidi 150k
wanaoingia kwenye soko lajira ni zaidi ya 150k kwasababu wamerundikwa tangu 2015 we unataka afanyeje? aajiri 150 kwa wakati mmoja?
 
Umechemka, awamu Fulani Vijana walipata Ajira tokana na miradi mingi ya maendeleo mishahara kwa wakati ila kwa Sasa ata watoe Ajira million elf 10 hamna Cha maana mamboo yashaenda mrama"
Aliyeyapeleka mrama ni nani?

mimi namzungumzia SSH kwa kiasi chake

amekuta mambo yameshaenda mrama anajitahidi kuyaweka kwenye mstari na ndani ya mwaka mmoja tayari jitihada tumeziona
 
Back
Top Bottom