Ndani ya Mwaka mmoja, Rais Samia katoa Ajira zaidi ya 50 Elfu, Vijana tunashukuru sana

Kwa mara ya kwanza 2022 hii ndo naona ajira za afya zinakuwa nyingi kuliko elimu. Ni mapinduzi makubwa 🤗
 
Kwa mara ya kwanza 2022 hii ndo naona ajira za afya zinakuwa nyingi kuliko elimu. Ni mapinduzi makubwa 🤗
Ajira za Elimu ziko 12000 mwaka 2022, ualimu sec na msingi 9800 , zilizobaki 2200 ni wakufunzi wa vyuo vya ualimu nilisahau kuiweka hapo
 
Kwa mara ya kwanza 2022 hii ndo naona ajira za afya zinakuwa nyingi kuliko elimu. Ni mapinduzi makubwa [emoji847]
Afya hawajaajiriwa muda mrefu, lkn pia mleta mada kaunganisha ajira za Tamisemi na wizara ya afya, Kama angeungasha za Tamisemi na wizara ya Elimu za wakufunzi,bado wizara ya Elimu inaongoza
 
wanaoingia kwenye soko lajira ni zaidi ya 150k kwasababu wamerundikwa tangu 2015 we unataka afanyeje? aajiri 150 kwa wakati mmoja?
hiyo 150000 ni makadilio ya mwaka mmoja tu was ajira sasa ukirudisha nyuma toka 2015 hali ni mbaya sana ndio maana nilikwambia usianze kusifu iyo 50k by the way wanasema wanahitimu wajiajiri lakini katika mtazamo wa uongozi wa rasilimali watu hiyo ni matumizi mabaya ya nguvu kazi kwa maana mtu amefunzwa kufundisha au kutibu alafu unamkuta anauza genge kwamba iyo taaluma yake inapotea bila kutumika na mahitaji yapo ie Wizara ya afya pekee inaupungufu kwa 59% ya watumishi na watu wako mitaani hawajaajiriwa unaona ni sawa?
 
Umechemka, awamu Fulani Vijana walipata Ajira tokana na miradi mingi ya maendeleo mishahara kwa wakati ila kwa Sasa ata watoe Ajira million elf 10 hamna Cha maana mamboo yashaenda mrama"
Pathetic.
 
Kipindi cha Magu ajira nyingi zilikua kwenye maandishi, mleta mada unaendeleza kulagai umma kwa kupongeza ajira ambazo zipo kwenye maandishi.
Mfano; Hizo ajira 700 za mifugo na 204 za uvuvi wameajiriwa lini????
 
mwaka jana
 
Aliyeyapeleka mrama ni nani?

mimi namzungumzia SSH kwa kiasi chake

amekuta mambo yameshaenda mrama anajitahidi kuyaweka kwenye mstari na ndani ya mwaka mmoja tayari jitihada tumeziona
Apa mtanzania mwenzangu ivi unafikili hiyoo jeuri ya kusema amekuta mambo mrama anajaribu kuyaweka sawaa inakujaje"? Awamu hii walipo shika usukani tuu maisha yalibadilika pengine mwenzangu upo sehem moja huenda hujazunguka ndani ya inchi ndo maana point zinakuja Kama unakaushabiki, Samahani kwa Hilo" Ebu tujaribu kuzungumza Yale ambayo tunayaona kwenye Jamii na so ety kusimama mtetea Fulani yuko vizur hayo ndo mawazo yangu
 
mwaka jana
Huna research unaongea tu ilimradi umesifia.!

Hizo figure za ajira zimetangazwa mwezi uliopita cha ajabu wamezitia kapuni pamoja na ajira za sheria.
 
Ulipaswa ujue kwanza kwa mwaka ni vijana kiasi gani wanatoka vyuoni.

Halafu pia uweke ajira za sekta binafsi, kwa sababu hata kama huo uongo wako ungekuwa ndio ukweli ajira kama hizo kujirudia tena inaweza kuwa hadi mwaka 2025
siwezi nikaiweka sababu siijui,
 
Ulipaswa ujue kwanza kwa mwaka ni vijana kiasi gani wanatoka vyuoni.

Halafu pia uweke ajira za sekta binafsi, kwa sababu hata kama huo uongo wako ungekuwa ndio ukweli ajira kama hizo kujirudia tena inaweza kuwa hadi mwaka 2025
sijaweka mada kuchambua idadi ya wahitimu wa vyuo, nimeweka thread kuandika ajira zilizoishatolewa, elewa dhima ya thread ukitaka kuchambua wahitimu unaweza kuanzisha yako pia
 
Huna research unaongea tu ilimradi umesifia.!

Hizo figure za ajira zimetangazwa mwezi uliopita cha ajabu wamezitia kapuni pamoja na ajira za sheria.
wewe usipopata kazi unajua zimewekwa kapuni?
 
wewe usipopata kazi unajua zimewekwa kapuni?
Sijapata kivipi!?? Ninekwambia mwezi uliopita zilitangazwa ajira za walimu, afya, sheria, mifugo na uvuvi.

Wametoa ajira za walimu na afya ambazo mwisho kutuma ilikua jana tar 8.

Hizi nyingine hawajizitoa zipo kwenye maandishi kama kwa Jpm uliyekuwa unamlaumu kwenye uzi wako.

Yaani inaonesha umepata ajira juzi tu kwa hiyo umechachawaaa unajiona upo kwenye nchi ya asali na maziwa.!
 
Wanachojua ni chuki na kuropoka ila wanafahamu kwamba watu wao walishindwa kuyafanya haya.
 
Bora na Samia alisema badala ya maofisa kukaa ofisini wakafanye Kazi na salary zao zitabakia pale pale
 
MUOGOPE MUNGU. MKOA WA GEITA PEKE YAKE UNA UHABA WA WAALIMU 7500. BADO KWENYE IDARA YA AFYA.
HIZO AJIRA NI DANGANYA TOTO. HUWEZI KUAJIRI WAALIMU WA HESABU 450 WAFUNDISHE TANZANIA NZIMA.
NJOMBE KUNA SHULE INA WATOTO 540 ILA WAALIMU 5.
LEO HII KUNA MADOKTA WANAENDESHA BODABODA NA HOSPITALI HAZINA WAHUDUMU.

YAJAYO YANAHUZUNISHA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…