Ndani ya siku 100 za Uongozi wake, Rais Samia amefanya mambo makubwa

Hatushindani na nchi yoyote kiuchumi, Sisi tunapambana kukuza uchumi kwa faida yetu.

Unataka tusiuze gesi tuuze nini, ubuyu?
Au kwa kuwa Kenya ni waafrika wenzetu kwa hiyo tusiwauzie gesi, ila ungesikia tunaiuza ulaya ungeona poa tu.

Kama tunashindana na wakenya kiuchumi, basi tusiwauzie Kenya Chakula ili afya zao zidhoofike tuwashinde kiuchumi au vipi?
 
Una umri gani kamanda??
 
Mi namshukuru sana kuwadhibiti viongozi wa kujimwambafai maana walijiona miungu,, kuwa wana amri yoyote juu ya utu wa mtu.

Hili ni kubwa sana kwangu.

Asante mama. Mungu ambariki rais SSH
 
Ongezeko kubwa la kodi wakati huo huo mishahara haijaongezwa kwa miaka sita sasa.
 
Mama anapiga kazi nzuri
Lakini udini kwa mbali naona ni mdini. Jingine, she is so obsessed with gender balance. Anadhani bado ni mwanaharakati wa enzi ziilee akiwa kwenye ma NGO ili apate wafadhili ilibidi ujitoe fahamu kuitetea gender equality. Kosa la tatu uzanzibari vs ubara yuko oversensitive kuitetea kwao zenj. Akirekebisha hayo matatu akajiona kwanza yeye ni Mtanzania mengine ndipo yanafuata hakika atakuwa rais bora wa awamu zote tangu tupate uhuru. She is very balanced to be honest.
 
Mkuu ulitaka avue hijabu na asiteue muislamu hata mmoja ili uthibishe kuwa siyo mdini?

Mimi naona teuzi zake hazina viashiria vya udini labda kama tunakubaliana kuwa ili rais muislamu asiwe mdini basi ateue waislamu kidogo sana kadri iwezekanvyo.

Hoja za udini hazina mashiko
 
Mashehe wa Uamsho chini ya Sheikh Farid ni hatari kama Osama.

Siku watakayoachiwa tu tutaanza kusikia, Kanisa limelipuliwa, padri kauliwa au kituo cha Polisi kimevamiwa.

Watanzania tuwe wakweli, matukio ya 2014 Mbagala, Bukoba na Zanzibar yalitia doa amani ya nchi yetu. Tanzania iko salama kwa mashehe kuwa rumande. Potelea pote.

Kuna kitu Serikali inakijua sisi hatukijui, tisijelaumu wakileta madhara
 
Naunga mkono hoja. Kwa kweli Rais SSH anaupiga mwingi kama Ngolo Kante wa Chelsea. Anakaba, anatoa assist halafu ana speed ya hatari.

Naamini hata Katiba bora ya wananchi atatuachia. Mungu enedelea kumbariki Rais wetu SSH azidi kuiweka nchi inapotakiwa
 
Mama Samia wewe tuachie katiba bora tu ya Jaji Warioba (ikiwa na marekebisho machache tu) ili jina lako tuliandike makumbusho ya Taifa kwa wino wa dhahabu!

Otherwise uchapakazi wako tunauona na sisi wapenda soka tunasema "unaupiga kwa miguu yote miwili"

Chapa kazi mama tuko nyuma yako!
 

Tutumie common sense bhas wakat mwingine, hayo mambo makubwa unayoyasemwa kuna watu nyuma yake walianzisha, acheni sifa za kipumbavu
 
Mi namshukuru sana kuwadhibiti viongozi wa kujimwambafai maana walijiona miungu,, kuwa wana amri yoyote juu ya utu wa mtu.

Hili ni kubwa sana kwangu.

Asante mama. Mungu ambariki rais SSH
Hili ni jambo. muhimu sana ili wateule wakumbuke kuwa cheo ni dhamana!
 
Huhitaji orodha ndefu kiasi hicho kupigia debe.

Mstari mmoja tu wa anapoharibu unatosha kabisa kufuta hizo rasharasha unazoweka hapa.

Ni kama sifa alizopewa mtangulizi wake katika mambo kadhaa aliyoyafanya yakionekana kuwa mzazuri kwa taifa; lakini jambo moja au mawili mazito zaidi zaidi yamevuruga kila kitu alichokisimamia Mwendazake.

Vuta subira, utapewa huo mstari mmoja au miwili itakayokuonyesha kwamba mama anaiuza Tanzania kwa walanguzi na wachuuzi kwa bei cheee! Hapo ndipo utakapogundua kwamba hajafanya lolote la maana katika hizo siku 100.
 

Ni Mpaka hilo unalolisema litokee kwanza, hatuwezi kupiga ramli kwa sasa kuwa lazima itakuwa hivyo unavyofikir

Lakini so far so good Mama anakwenda vizuri
 
Ni Mpaka hilo unalolisema litokee kwanza, hatuwezi kupiga ramli kwa sasa kuwa lazima itakuwa hivyo unavyofikir

Lakini so far so good Mama anakwenda vizuri
Hizi si ni siku 100?
Hayo mazito huwezi kuyaona katika siku 100, ila misingi yake na dalili zake (mwelekeo) ndio unaoonekana.

Hayo ya rasharasha ni utamu wa peremende tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…