Ndege kubwa ya abiria ya C919 yaanza rasmi kutumika nchini China

True , wachina bado sana kwenye science hiyo
Unaelewa kuhusu bidhaa ambayo ina International Standard?

Hizo ndege zimekubaliwa na viwango vya kimataifa vya usafiri wa anga wa abiria, International Airworthiness Standards

Na ina intellectual property rights kwa taarifa yako

Usifikiri ndege zinaanza tu kubeba abiria bila kukidhi viwango vinavyotakiwa kimataifa. Siku nyingine ficha ujinga wako ukiwa jf
 
Si wanabebana wao Kwa wao, nani anawakataza wakiwa ndani kwao na kiburi walichonacho kumpinga USA
 
Wachina wamekuwa wakitengeneza ndege tangu zamani miaka ya zamani huko 1960's na 1970's

Ila waliwekeza sana kwenye kutengeneza ndege za kivita na sio kwenye ndege za abiria (commercial aircraft)

Sasa wameona fursa hasa soko lao la ndani tu ni 10% ya mauzo ya ndege za abiria duniani na bado kuna soko la nje

Hivyo wameamua sasa kuwekeza kwenye ndege za abiria hivyo shirika la COMAC (Commercial Aircraft Corporation of China) likaanzishwa 2008 kwa lengo moja tu kutengeneza ndege za abiria (commercial aircrafts)

Na wamefanikiwa kutengeneza hiyo ndege C919 na imekidhi viwango vya kimataifa International Airworthness Standard

Sasa ni muda wa COMAC kuingia sokoni kushindana na makampuni makubwa kama BOEING, AIRBUS, BOMBARDIER n.k
 
View attachment 2643096Ndege kubwa ya C919 hivi karibuni iliruka kutoka Shanghai hadi Beijing ikiwa na abiria, ikiashiria kuwa ndege hiyo kubwa ya abiria iliyotengenezwa China kwa kujitegemea imeingia katika katika soko la safari za anga.

Utengenezaji wa ndege kubwa unajulikana kama kilele cha kiwango cha viwanda. Kwa muda mrefu, soko la ndege kubwa za abiria duniani lilihodhiwa na Kampuni ya Boeing ya Marekani na Kampuni ya Airbus ya Ulaya. Kampuni ya Bombardier ya Canada na Kampuni ya Mitsubishi Heavy Industries ya Japan ziliwahi kujaribu kutengeneza ndege kubwa za abiria, lakini zote zilishindwa baada ya juhudi za miaka mingi.

C919 imekaribishwa na soko la safari za anga tangu ilipokamilika na kuanza kujaribiwa. Kutokana na idara husika ya China, uwezo wa uzalishaji wa C919 kwa mwaka utafikia 150 katika miaka mitano ijayo, na hadi sasa, ndege hiyo imepata zaidi ya oda 1,200 za ndani na nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na 20 zilizoagizwa na Kampuni ya General Motors ya Marekani. Katika siku zijazo, C919 inatarajiwa kuwa ndege ya tatu kwa ukubwa wa abiria duniani baada ya Boeing na Airbus.

Mafanikio ya ndege ya C919 yameonesha hatua kubwa iliyopigwa na China katika sekta ya utengenezaji. Tukichunguza mchakato wa utafiti na utengenezaji wa C919, tunaweza kugundua kwamba ndege hiyo imehusisha karibu teknolojia zote za juu.

Ndege moja ya C919 ina vipuri zaidi ya milioni 2.5, na kila sehemu ni muhimu kwa usalama na ufanisi wa safari ya ndege, hali ambayo inaonyesha kikamilifu kwamba, sekta ya utengenezaji wa China imefikia kiwango cha juu sana.

Baada ya mafanikio ya safari ya kwanza ya kibiashara ya C919, baadhi ya watu wamesema sehemu nyingi za ndege hiyo, ikiwa ni pamoja na injini, zimeagizwa kutoka nchi nyingine, wakijaribu kukataa ukweli kuwa ndege hiyo imebuniwa na kutengenezwa na China. Lakini wanasahau kwamba, hivi leo, uvumbuzi wa kujitegemea unaendana na ushirikiano wa kimataifa. Ikilinganishwa na Boeing na Airbus, C919 imechelewa sana, hivyo ni afadhali itumie baadhi ya teknolojia ambazo tayari zipo. Zaidi ya hayo, ikilinganishwa na ndege kubwa nyingine, utengenezaji wa C919 umetegemea zaidi kampuni za ndani. Kwa mujibu wa orodha ya watoaji vipuri, asilimia 90 ya vipuri vya C919 vimetoka kwa kampuni za China, na hiki ni kiwango cha juu zaidi ikilinganishwa na kampuni za nchi nyingine za kutengeneza ndege kubwa. Aidha, kuhusu suala la injini, injini ya China aina ya “Yangtze River 1000A” inayofaa kwa ndege kubwa, imefanyiwa majaribio kwa mafanikio, na inatarajiwa kuchukua nafasi ya injini zinazotoka nje ya nchi mapema iwezekanavyo.

Katika miaka ya hivi karibuni, kutoka reli ya mwendo kasi hadi ndege kubwa ya abiria, kutoka kwa kituo cha anga ya juu hadi manowari ya kubeba ndege za kivita, China imepiga hatua kubwa katika sekta yake ya utengenezaji. Ikiwa nchi ya kwanza kwa utengenezaji duniani, China bila shaka itatoa mchango mkubwa zaidi katika kutuliza na kuboresha mnyororo wa ugavi duniani.
Sijaona idadi ya abiria kwa ndege hii ila porojo la C919 ndio imetaradad sana
 
We Jamaa kwenye maandiko yako unaandika maneno mengiii!!! yasiyo na faida.. ..lkn ikisumarize habari yako kama hii ilitakiwa uandike mistari isiyozidi 5 tu...
 
Si wanabebana wao Kwa wao, nani anawakataza wakiwa ndani kwao na kiburi walichonacho kumpinga USA
Ficha ujinga ulionawoo jitaidi usome zaidi acha ushabikki wa vijiweni kama watoto wa lapili
 
We Jamaa kwenye maandiko yako unaandika maneno mengiii!!! yasiyo na faida.. ..lkn ikisumarize habari yako kama hii ilitakiwa uandike mistari isiyozidi 5 tu...
Kusumarize Ilo ni jukumu lako msomaji siyo LA muandishi mda mwingine tumia akili Kukosoa jambo
 
Maelezo hayajitoshelezi kabisa. Mara kampuni zingine zilijaribu kutengeneza ndege kubwa bila mafanikio, mara ndege hiyo itakuwa ya tatu kwa ukubwa. Lakini wengi tumejitahidi kusoma hadi mwisho tujue IDADI ya ABIRIA watakaobebwa nalo hilo halipo.
Mi nadhani tumsaidie kujazia nyama mtoa mada. Source: Wikimedia.

C919 Aircraft Characteristics for Airport Planning[111]
Cockpit crew2
Seats158 (2-class) to 174 (1-class HD)
Length38.9 m (127 ft 7 in)
Wingspan35.8 m (117 ft 5 in)
Wing area129.15 m2 (1,390.2 sq ft)
Height11.95 m (39 ft 2 in)
Fuselage height4.166 m (13 ft 8.0 in)
Fuselage width3.96 m (13 ft 0 in)
Maximum payload18,900 kg (41,700 lb)
OEW45,700 kg (100,800 lb)
MTOW78,900 kg (173,900 lb)
Fuel capacity24,917 L (6,582 US gal)
Engines (×2)CFM LEAP-1C
TO/GA Thrust (×2)137.14 kN (30,830 lbf)[112]
Cruise Mach0.785[113][better source needed]
Range5,576 km (3,011 nmi)https://en.m.wikipedia.org/wiki/Comac_C919#cite_note-115

[TR]
[TH]Ceiling[/TH]
[TD]12,100 m (39,700 ft)[113][/TD]
[/TR]
[TR]
[TH]Takeoff (MTOW, ISA)[/TH]
[TD]2,125 m (6,972 ft)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TH]Landing (MLW, ISA, Dry)[/TH]
[TD]1,778 m (5,833 ft)

[/TD]
[/TR]
 
Kuna watu hadi leo wamekariri China anatengeneza vitu feki...

Mtu huyo huyo aanatumia mtandao wa simu ambao kwa Tanzania kwa kiwango kikubwa market share imetawaliwa na telecom NE's za Wachina...
Kuna waafrika hadi leo wamekariri kuwa Africans hawawezi kuishi duniani bila kutegemea misaada ya mabeberu, na kuna wengine hawaamini kwamba kuna uwezekano wa kuwa huru KIFRA bila kuwa chawa wa China au Russia au USA.
 
View attachment 2643096Ndege kubwa ya C919 hivi karibuni iliruka kutoka Shanghai hadi Beijing ikiwa na abiria, ikiashiria kuwa ndege hiyo kubwa ya abiria iliyotengenezwa China kwa kujitegemea imeingia katika katika soko la safari za anga.

Utengenezaji wa ndege kubwa unajulikana kama kilele cha kiwango cha viwanda. Kwa muda mrefu, soko la ndege kubwa za abiria duniani lilihodhiwa na Kampuni ya Boeing ya Marekani na Kampuni ya Airbus ya Ulaya. Kampuni ya Bombardier ya Canada na Kampuni ya Mitsubishi Heavy Industries ya Japan ziliwahi kujaribu kutengeneza ndege kubwa za abiria, lakini zote zilishindwa baada ya juhudi za miaka mingi.

C919 imekaribishwa na soko la safari za anga tangu ilipokamilika na kuanza kujaribiwa. Kutokana na idara husika ya China, uwezo wa uzalishaji wa C919 kwa mwaka utafikia 150 katika miaka mitano ijayo, na hadi sasa, ndege hiyo imepata zaidi ya oda 1,200 za ndani na nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na 20 zilizoagizwa na Kampuni ya General Motors ya Marekani. Katika siku zijazo, C919 inatarajiwa kuwa ndege ya tatu kwa ukubwa wa abiria duniani baada ya Boeing na Airbus.

Mafanikio ya ndege ya C919 yameonesha hatua kubwa iliyopigwa na China katika sekta ya utengenezaji. Tukichunguza mchakato wa utafiti na utengenezaji wa C919, tunaweza kugundua kwamba ndege hiyo imehusisha karibu teknolojia zote za juu.

Ndege moja ya C919 ina vipuri zaidi ya milioni 2.5, na kila sehemu ni muhimu kwa usalama na ufanisi wa safari ya ndege, hali ambayo inaonyesha kikamilifu kwamba, sekta ya utengenezaji wa China imefikia kiwango cha juu sana.

Baada ya mafanikio ya safari ya kwanza ya kibiashara ya C919, baadhi ya watu wamesema sehemu nyingi za ndege hiyo, ikiwa ni pamoja na injini, zimeagizwa kutoka nchi nyingine, wakijaribu kukataa ukweli kuwa ndege hiyo imebuniwa na kutengenezwa na China. Lakini wanasahau kwamba, hivi leo, uvumbuzi wa kujitegemea unaendana na ushirikiano wa kimataifa. Ikilinganishwa na Boeing na Airbus, C919 imechelewa sana, hivyo ni afadhali itumie baadhi ya teknolojia ambazo tayari zipo. Zaidi ya hayo, ikilinganishwa na ndege kubwa nyingine, utengenezaji wa C919 umetegemea zaidi kampuni za ndani. Kwa mujibu wa orodha ya watoaji vipuri, asilimia 90 ya vipuri vya C919 vimetoka kwa kampuni za China, na hiki ni kiwango cha juu zaidi ikilinganishwa na kampuni za nchi nyingine za kutengeneza ndege kubwa. Aidha, kuhusu suala la injini, injini ya China aina ya “Yangtze River 1000A” inayofaa kwa ndege kubwa, imefanyiwa majaribio kwa mafanikio, na inatarajiwa kuchukua nafasi ya injini zinazotoka nje ya nchi mapema iwezekanavyo.

Katika miaka ya hivi karibuni, kutoka reli ya mwendo kasi hadi ndege kubwa ya abiria, kutoka kwa kituo cha anga ya juu hadi manowari ya kubeba ndege za kivita, China imepiga hatua kubwa katika sekta yake ya utengenezaji. Ikiwa nchi ya kwanza kwa utengenezaji duniani, China bila shaka itatoa mchango mkubwa zaidi katika kutuliza na kuboresha mnyororo wa ugavi duniani.
Hizi ndege utawala angani kama Yutong bus.
Watapanda huko wachina wenyewe 🖐
 
Back
Top Bottom