Ukinunua bus la abiria, arafu Nauli ikawa juu, watoto wako wakashindwa kupanda bus la baba yao, wakaenda kupanda mabus mengine ya bei nafuu, unadhan watakuelewa??
Maoni yangu, serikali itafute namna ya kupunguza Nauli za ndege hili watu wapande wengi na root ziwe nyingi.
Sasa hv unakuta ndege inaenda safar moja arafu kwa kukosa abiria inalala yooooo mpaka next day. Safar hiyo hiyo moja operation costs ziko juu balaa!
Jambo lingine, haswa safar za ndan, waruhusuni wawekezaji wa ndege za ndan wawe wengi ndo ushindan utakuwepo. Nadhan mlio ishi nchi Kama India mtakubaliana na mm ile nchi ilivyo na demostic flight nyingi Sana na hivyo naul ndogo na hivyo wasafir wanakuwa wengi!
Sasa apa kwetu..... , Ata Fast jet sijui ilikufia wap! .Juz nilikuwa Tunduma naenda kukata tiketi ya ATCL kutokea Songwe to Mwanza. Naambiwa hapa mzee unalipia Nauli ya root ya dar, then unalipia Nauli ya dar to mwz. Gharama walizo nipa root nzima inafikia milion na point .
Baada ya kuona hiyo gharama nikasema hapa kweli Shikamoo ATCL na Kaz iendelee.!!!
Serikali, ongezeeni wafanyakaz mishahara mizuri, punguzeni au kufuta kabisa vimatumizi vya kijinga arafu hela zipelekeni kweye mishahara ya watumishi..
Mfano wa vimatumizi vya kijinga ni Kama gharama za kukimbiza mwenge nchi nzima ukiwa chini ya ulinzi mkali wa police na bunduki n.k. inatusaidia nn kwa mfano?????
Wafanya biashara wapunguzien makodi..arafu muone Kama ATCL haitajaza abiria mpaka faida nono. Si nyie mnao tuambia Tanzania ni nchi Tajiri? Sasa ndugu Yetu Mwigulu mtaalam wa uchumi, mshaurin raisi wetu vizuri, mambo ya kutwambia Tozo Tozo zitajenga vituo vya afya kwan kikwete, Magufur walivijengaje? Na walipovijenga vilibomoka lini au vip jaman!!!!!
Ndege nunueni tu hata zifike 1000 lakin Kama hazipat abiria na root ku ongozeka ,hv kweli shirika letu litaepuka maden hapo jaman?