Ndege mbili za Airbus kupokelewa siku ya Ijumaa, Uwanja wa Abeid Aman Karume Zanzibar

Mwinyi huyu huyu aliyevunja shirika la meli la Zanzibar na kuagiza meli zote ziuzwe .... Awe tayari kupokea ndege za ATCL ambazo hazijawahi kurudisha gharama ... Achilia mbali kutengeneza faida?..

Atakuwa anajichanganya kama hili bandiko sio "Fake"🤔😲
 
Mkuu, watoto wa "majamvi" ya Lumumba na "One - Way" ni misukule.
Wao wanachojua ni kuwasifia wanaowasababishia kwenda chooni.
 
Hata yule wa Chatto alikuwa akielekea huko huko
Bora hata chato iko bara...hivi ikitokea mama akashinda tena 2025 akaamua kuipendelea znz kiwazi kama mzee wa chato ilunafikiri itakua je? Znz haiwezi kuinufaisha znz maana yenyewe haijitoshelezi
 
Hata yule wa Chatto alikuwa akielekea huko huko
Bora hata chato iko bara...hivi ikitokea mama akashinda tena 2025 akaamua kuipendelea znz kiwazi kama mzee wa chato ilunafikiri itakua je? Znz haiwezi kuinufaisha znz maana yenyewe haijitoshelezi.
 
Hizo ndege ni za zanzibar au Tanzania? Maana naona kama kuna mchezo unafanyika hapa.
Mwishon tutakuja kuambiwa ni za Zanzibar kumbe zimenunuliwa na hela ya Tanzania
Ikifikia hatua hiyo,wimbo wa Taifa lazima utapigwa kama 17 March 2021.
Wazalendo wapo.
 
Ama kweli kama wazanzibari hawataki Muungano muda wao ni sasa.

Ndege za ATCL tangu lini zikapokelewa Zanzibar?
Halafu "Hub" ya ATCL ni Dar es salaam!. Hata kama moja iliwahi kulala Mwanza "En route" haihalalishi hizi kupokelewa Zanzibar... Labda baada ya kumaliza route... Sherehe ya mapokezi ikafanyike Zanzibar, nitajaribu kuelewa lakini sioni mantiki.
 
Seikali yetu ilitakiwa iboreshe tu viwanja vya ndege, biashara ya ndege ingewaachia akina fastjet na precision. Haya madege yanakwenda kuwa mzigo mkubwa kwa mwananchi huko mbele.
Halafu hao Precision Air ni kundi la matapeli linalolindwa na Serikali, haiwezekani waruhisiwe kukusanya mitaji kutoka kwa umma halafu mambo yao wayaendeshe kwa siri kiasi hicho. Sijawahi kusikia wakiitisha mkutano wa mwaka kwa wanahisa.
 
Samia kaagiza ziwe za Zanzibar

Zanzibar ni mzigo mkubwa sana kwa Tanganyika

Nyerere alituuza utumwani kama ngamia
Acha uzwazwa...

Kwani Zanzibar ni Madagascar?!!

Hawastahili kupata "shea" ya muungano?!!!

Mpaka umri huo hujajua tu ya kwamba zote TANGANYIKA NA ZANZIBAR zilipoteza mengi tu kuingia katika muungano?!!!

Je zilipoingia muungano umekosa faida?!!

Huzitambui faida za muungano?!!!

Duuuh 😳😳🤣🤣
 
Hivi zanzibar kuna tozo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…