Ndege mbili za Airbus kupokelewa siku ya Ijumaa, Uwanja wa Abeid Aman Karume Zanzibar

KQ nalo ni shirika kubwa la ndege la kutolea kama mfano?
 



 
Hivi na ATCL ni shirika la Muungano? Tuendeko kuna miiba. Tusije kuambiwa zile ndege zilizopokelewa Zanzibar ni mali ya Zanzibar kwa kuwa zilinunuliwa na SMZ kuasisi AZCL maana hawachelewi kuunganisha mambo hawa, kisha/halafu waseme ilikuwa kero kubwa ya muungano iliyotatuliwa!
 
Mkuu kwakuwa wapo pekee yao wanaweza kuamua wawahudumie watakavyo maana hakuna ushindani.

Kisa cha kuwaondoa Fast jet bado ni kitendawili
Tusipokuwa makini ipo siku tutapewa mihogo ya kukaanga, embe mbichi na pilipili😆😂
 
Halafu "Hub" ya ATCL ni Dar es salaam!. Hata kama moja iliwahi kulala Mwanza "En route" haihalalishi hizi kupokelewa Zanzibar... Labda baada ya kumaliza route... Sherehe ya mapokezi ikafanyike Zanzibar, nitajaribu kuelewa lakini sioni mantiki.

Kutesa kwa zamu, zamu yao hii yakhe!
 
Ktk ununuzi wa ndege kunaupigajinmwingi sana ndio maana wanakomaa sana kununua mandege yanayowapa hasara kwenye soko..

Mafuta na Gesi zipo ardhini lakin wamezipuuza, madini, na resources nyingi sana.. tunajitutumua kununua ndege
Huu ndiyo wakati muafaka wa kununua ndege maana zimeshuka bei kwa nusu ,tusiwe wajinga inatakiwa tununue ndege nyingi kwa mikataba kwa bei ya sasa ambayo ni nafuu
 
Your IQ is too low to understand my post.
Hahahaaaaa...lol!!!
Wakala wa shetani wewe. Kama mimi IQ yangu ni ndogo, ni ahueni mara 1000 kuliko kuwa na IQ kubwa halafu nikawa namtumikia shetani.
 
NDEGE mbili aina ya Airbus za Shirika la Ndege la Tanzania ATCL zitawasili nchini Oktoba 8 na kupokelewa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi.

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema ndege hizo zimepewa majina ya Tanzanite na Zanzibar. Ndege hizo zitapokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar zikitokea Canada.
 
Nchi nzima itazizima kwa makopo... we are stupid and rubbish!
Hivi na Sweden wanafanyaga hivyo wakinunua ndege?
 
Tunajitafutia hasara za kujitakia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…