Ndege mbili za Airbus kupokelewa siku ya Ijumaa, Uwanja wa Abeid Aman Karume Zanzibar

Ndege mbili za Airbus kupokelewa siku ya Ijumaa, Uwanja wa Abeid Aman Karume Zanzibar

Hv si ndo hili shirika juzi juzi tu limeleta hasara ya mabilioni ya hela?

Hv hizi wakaamua kujenga hata viwanda kila kanda Tanzania haitapiga hatua kweli?

Kweli kufa kwa kenge hadi sikio litoe damu🤣🤣🤣🤣
 
Naam, kumekucha tena siku ya ijumaa mchana tarehe 08 Oktoba, 2021 katika uwanja wa ndege wa Abeid Aman Karume kutapokelewa ndege mbili za Airbus aina ya 220 - 300. Ndege hizo zitapokelewa na Dr. Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Itoshe kusema ATCL inaendelea kupata ndege zaidi za Airbus ambazo kimsingi zinatakiwa kuwa za masafa ya kati, mfano Dar to Nairobi, Entebe, Lusaka, OR Tambo Nk. Swali linabaki je wamejipanga kufika huko kiushindani?
Ofcourse ni jambo jema , but zije kufanya kazi za maana na siyo viginevyo
 
Ndege zenyewe zinaenda Arusha,Kigoma na Mwanza zikitoka nje ya nchi ni India na China au mpaka zikodishwe na Yanga iende Nigeria.

Hizo hela zipelekeni kutengeneza barabara za vijijini wananchi wasafirishaji mizigo kwa unafuu,pelekeni zikajenge madaraja au kama zipo nyingi sana wakopesheni SUMA JKT,Magereza na Shirika la maendeleo la taifa(NDC) ili waanzishe mashamba ya michikichi na waanzishe viwanda vya kukamua mafuta ya mawese .Nchi ina mamilioni ya hekari lakini mafuta ya kupikia yanatoka Malaysia aibu sana hii.

Hao ndio sisiyemu adui kwa kwanza katika taifa ili. Usafiri wa anga wangewaachia makampuni binafsi wao wakaboresha viwanja na njia za kukimbilia ndege tanzania nzima. Wakasubiri kupata kodi zao.
 
Naam, kumekucha tena siku ya ijumaa mchana tarehe 08 Oktoba, 2021 katika uwanja wa ndege wa Abeid Aman Karume kutapokelewa ndege mbili za Airbus aina ya 220 - 300. Ndege hizo zitapokelewa na Dr. Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Itoshe kusema ATCL inaendelea kupata ndege zaidi za Airbus ambazo kimsingi zinatakiwa kuwa za masafa ya kati, mfano Dar to Nairobi, Entebe, Lusaka, OR Tambo Nk. Swali linabaki je wamejipanga kufika huko kiushindani?

Ama kweli kama wazanzibari hawataki Muungano muda wao ni sasa.

Ndege za ATCL tangu lini zikapokelewa Zanzibar?
 
Kwa hiyo hii ni ile order aliyoweka jiwe, nyingine ndo zinagawiwa zenj kudumisha muungano kwa mtindo wa sandakalawe aminaa.....
 
Mashirika makubwa ya ndege kama SAA, KQ hata Emirates na KLM yamekuwa na changamoto kubwa za kibiashara na hata kufilisika. Angalia SAA ya Afrika Kusini inajitahidi kufufuka kwa taabu kubwa, hili ni shirika lenye ndege zaidi ya 120 na hufanya safari zake popote duniani!

Isitoshe linamilikiwa kwa ubia na wazungu na serikali tajiri ya Africa Kusini. Sijui itakuwaje na ATCL yetu kama tu tunshindwa hapa nyumbani kuendesha TTCL na TANESCO kibiashara.

Who told you SAA ina ndege zaidi ya 120? Hivi kwanini mnaandikaga wrong data kiasi hiki, unajidanganya mwenyewe na unaonekana mpuuzi. Be smart ukiandika kitu.

How do you compare, ATCL na TTCL or other Govt Co. ni kosa kubwa, sbb business models zake ni tofauti, hakuna jinsi ya kufanya comparison. Acha siasa uchwara.
Ndege zinapokelewa tu Zanzibar alafu zinakuja TGFA, then zitakabidhiwa ATCL, sio kwamba wamepewa Zanzibar.
 
Mashirika makubwa ya ndege kama SAA, KQ hata Emirates na KLM yamekuwa na changamoto kubwa za kibiashara na hata kufilisika. Angalia SAA ya Afrika Kusini inajitahidi kufufuka kwa taabu kubwa, hili ni shirika lenye ndege zaidi ya 120 na hufanya safari zake popote duniani!

Isitoshe linamilikiwa kwa ubia na wazungu na serikali tajiri ya Africa Kusini. Sijui itakuwaje na ATCL yetu kama tu tunshindwa hapa nyumbani kuendesha TTCL na TANESCO kibiashara.
kwa hiyo hayo Mashirika yako ya Ndege,kisa yanashindwa,unatushauri na sisi Tanzania tusijaribu hiyo biashara,achaa na sisi tujaribu kuliko kutofanya kabisa! Hii ni biashara usiogope sana,ni swala la kujipanga na kusimamia biashara yako kwa karibu sana!!
 
Umeisahau ttcl ipo icu ingawa hawataki kusema makusudi
mashirika haya yalitakiwa yaendeshwe na wataalam bila kuingiliwa na siasa , hivi mnakumbuka bomba la kutoka kibamba hadi kisarawe ,halikua na sababu kabisaaaa kisa tu kimada wa mtu yuko kule , hapo kwembe tu na msumi watu wanakunywa maji pamoja na mifugo. walishaambiwa wasikubali akili ndogo kutawala akili kubwa hawaelewi.
 
Back
Top Bottom