Ndege mbili za Airbus kupokelewa siku ya Ijumaa, Uwanja wa Abeid Aman Karume Zanzibar

Ndege mbili za Airbus kupokelewa siku ya Ijumaa, Uwanja wa Abeid Aman Karume Zanzibar

Mimi huwa najiuliza hivi ni kero gani za muungano ambazo kila siku tunaambiwa zimetatuliwa kisirisiri maana juzi eais wa zanzibar na waziri Jafo walikuwa wakiongea na kupongezana kuhusu kutatuliwa kwa kero nyingi toka mama samia amekuwa rais, tukumbuke wazanzibar waliondoa kinyemela swala la mafuta na gesi kuwa la muungano lakini mama samia alipoingia madarakani alienda kusaini haraka haraka mkataba wa bomba la gesi na kenya kwa gesi inayotoka Tanganyika.
Meli wanataka tugawane nusu kwa nusu ndege pia wanataka tuwape za kazi gani watanganyika tuamke tusiuze uhuru wetu kwani ndege zimenunuliwa kwa kodi za watanyika mbona meli zao kama za Mapinduzi hatuhusiki nazo ila za kwetu wanataka ziwe za kwao
Kifupi huu muungano uvunjwe haraka
 
Serikali yetu ilikuwa nia njema sana kufufua atcl lkn kimtazamo ni km hatukujipanga sababu biashara ya ndege ina mnyonyororo mrefu sana ktk uendeshaji wake mosi shirika ni lazima liwe na mawakala wa kutosha ndani na nje ya nchi wa mauzo ya ticket pili kwa kuanzia shirika angalau lingekuwa na safari ktk miji mitano mikubwa kibiashara na utalii mfano Mumbai India.. Guaxhuu China...Johannesburg South Africa London UK na magharibi ya Africa kuna shida sana ya usafri ni Ethiopia airline peke yao ndio wanakwenda huko ktk mashirika ya kiafrika na nauli zpo juu kuliko hata ulaya..Kwa kutumia hz Dreamline na airbus shirika linaweza kuoperate hz route tena kwa faida na baadhi ndege zikawa zinatumika uber kukusanya abiria ktk nchi majilani zetu km Congo,Zambia, Burundi, Malawi, Uganda,nk kwani nchi zote hz kwa sasa hazina shirika madhubuti km atcl..Tatu shirika lilitakiwa kuingia mikataba na mahotel kwa ajili ya abiria wanakuwa transit pamoja na usafiri wa uwakika kutoka Airport kwenda mahotelini hiki kitu Ethiopia airline wamefanikiwa sana ..Nne Kupunguza ghalama za uendeshaji mashirika mengi yanakufa ama kujiendesha kwa hasara sababu kubwa ni ghalama za uendeshaji unakuta soda ya kopo supermarket inauzwa 1000 lkn mzabuni analiuzia shirika la ndege 20,000 uwo mfano mmoja kati ya mingi ndio mwisho wa siku shirika linaonekana linaendeshwa kiasara lkn ukweli kbs hasara nyingi ni zakutengeneza ..Tano na mwisho hapa ndio kwenye tatizo kubwa Africa inaonekana usafri wa ndege ni anasa na ni kwa ajili ya watu flami tu ili ni tatizo kubwa nauli one way kwenda kigoma 500,000 tsh wakati nauli ya Dubai kwa fly Dubai 370 usd go and return..jibu rahisi nauli ya Dubai rahisi kuliko kigoma kwa ndege..Hv kipi bora kuweka nauli ya 500,000 kwenda kigoma alafu unapata abiria saba au nauli ya 200,000 upate abiria arobaini ..mwisho biashara ya ndege angani sio ardhini kuna mikoa km mwanza kigoma kilimanjaro,mbeya, dodoma inatakiwa iwe hata na route kumi kwa siku km nauli itakuwa rafiki hayo ndio maoni yangu km mtanzania mpenda nchi yangu
 
Imeandikwa Zanzibar kwani imenunuliwa na wazanzibar?
Hivyo ni vivutio tu vya utalii. Kumbuka sio rahisi Mzungu aliyeisikia Zanzibar, akashawishika akaenda kuitembelea halafu huku Bara tukakosa kuambulia hiyo dola.
 
mimi nafikiri wangeanza kwa kuangalia gharama za uendeshaji ziwe realistic/competitive, then waweke bei rafiki kabisa mfano Arusha/dar 70,000shs flat rate; ili ndege ijae kila siku. Mbona ulaya wana hizo bei ($20/$30) na ndege kubwa zinaruka kila siku kati ya mji na mji na husikii wakilalamika kuwa wamepata hasara?
Huku kwetu ndege inafanywa anasa na hivyo kuwekwa bei isiyo rafiki hivyo route nyingi hazijai na kufanya ziende kwa hasara.
Unatoa ndege mpanda to Dar shs 300,000pp unapata abiria 35; Je ungechaji 100,000 ukapata abiria 170? kila siku
badala yake tunafuta route kuwa hailipi bila kuangalia kipato cha soko husika
Ni mtazamo tu
Hii kitu wataalamu wa masoko tunaiita price strategy. Kitu ambacho watu wengi hawakiwezi.
 
Hoja yako ni muhimu sana, tunajiuliza haya mambo ya Muungano yanapelekwa kwa Rais wa Zanzibar ambaye hatukumchagua sisi.
Posho mkuu posho hapo kuna watu watakuwa padiemu kwenda kwenye upokezi wa ndege Zanibar.

Yaani hii nchi tuna viongozi wa ovyo kabisa
 
Ndege zenyewe zinaenda Arusha,Kigoma na Mwanza zikitoka nje ya nchi ni India na China au mpaka zikodishwe na Yanga iende Nigeria.

Hizo hela zipelekeni kutengeneza barabara za vijijini wananchi wasafirishaji mizigo kwa unafuu,pelekeni zikajenge madaraja au kama zipo nyingi sana wakopesheni SUMA JKT,Magereza na Shirika la maendeleo la taifa(NDC) ili waanzishe mashamba ya michikichi na waanzishe viwanda vya kukamua mafuta ya mawese .Nchi ina mamilioni ya hekari lakini mafuta ya kupikia yanatoka Malaysia aibu sana hii.
😂😂😂
 
Kwani hapa inafuatwa sera ya nani?
Si ni mikataba ilikuwa tayati imeshasainiwa labda?
 
Naam, kumekucha tena siku ya ijumaa mchana tarehe 08 Oktoba, 2021 katika uwanja wa ndege wa Abeid Aman Karume kutapokelewa ndege mbili za Airbus aina ya 220 - 300. Ndege hizo zitapokelewa na Dr. Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Itoshe kusema ATCL inaendelea kupata ndege zaidi za Airbus ambazo kimsingi zinatakiwa kuwa za masafa ya kati, mfano Dar to Nairobi, Entebe, Lusaka, OR Tambo Nk. Swali linabaki, Je wamejipanga kufika huko kiushindani?
Kwanini zipokelewe Zanzibar ilhali ziliahizwa na JPM. Je kwenye ununuzi wa ndege Zanzibar ilichangia chochote kile. Jasho la watanganyika huliwa na wazanzibar
 
Ila CCM ni wajinga, wanatwambia shirika halitengenezi faida na ndege ni hasara tupu. Miezi mitano baadae wananunua ndege. Bora hata wangekuwa wajinga ila ni mahayawani (wapumbavu).
 
Back
Top Bottom