Ndege ya Air Tanzania yashindwa kutua Bukoba, yageuza kwenda kutua Mwanza

Ndege ya Air Tanzania yashindwa kutua Bukoba, yageuza kwenda kutua Mwanza

Huo ndio uamuzi wa busara tunaotumia sisi marubani sio kulazimisha kutua hata kama kuna ugumu kufanya hivyo
Sasa Kama una wese Kidebe,hiyo jeuri ya kugeuza ulikotoka utaipata wapi!?? Rubani wa Precision nilimuelewa sana,na alifanya maamuzi yake very professional! RIP Rubani! Wese Kidebe bado ni tatizo kubwa kwa wawekezaji uchwara, wanapenda kucheza na Maisha ya watu!!
 
Mkuu wewe basi rubani muoga. Mimi ndio zangu hizo hasa naporusha hivi vi cassena single engines. Nimeshawahi kitua kwenye hurricane bahamas.

Pia nimeshawahi kutua kwenye tornado texas. Nimeshawahi kutua kwenye dhoruba ya monsoon. Nimeshawahi kutua kwenye typhoon manilla ufilipino.

Nimeshawahi kutua kwenye tropical cyclone msumbiji tena hizi hizi single engines cassena.
Muongo
 
Inaonekana BK Airport ipo Analogy!! Ingekuwa na Automatic systems ndege inatua yenyewe ata kama kuna Ukungu , umeme umekatika etc! Inaonekana Airport ni ya 1945! No any automation! Kama ata Ndege za ATC ambazo ni mpya na zina auto pilot aziwezi shuka BK Airport basi kuna tatizo
 
Ndio maana 1010 baada ya kuambiwa mafuta yameisha wakatoa jibu peleka ziwani na wenyewe wakaendelea kuangalia movie kwenye PC zao
 
Serikali ingesimamisha matumizi ya uwanja wa ndege wa Bukoba ndege zote zitue Mwanza.
 
hapa kuna kitu nyuma ya pazia, wanajaribu kuimarisha PR na kuaminisha umma kuwa ni weather related issue and somebody R.I.P Comrade was wrong despite the fact that it's a technical issue na responsible organ hawataki kuwajibika.
 
Msimu wa mvua kipindi hiki ni shida aisee.Ila sio technical issues,ni mambo ya Hali ya hewa.
Hata kwenye viwanja vikubwa duniani kuna kipindi ndege zinashindwa kuruka au kutua kutokana na hali ya hewa kutoruhusu.

Ujenzi wa uwanja mpya unaweza kuwa na umuhimu wake kama alivyoshauri huyo mbunge wa vitu maalum, lakini si suluhisho kuondoa matatizo ya hali ya hewa.
 
Daaa!!hivi ndege kuishiwa mafuta unadhania ni kitu rahisi kama kwenye bodaboda!!kuna mambo mengine kabla hata ya kuyaandika tumia kwanza halimashauri ya ubongo wako kwanza kufikiria. Inshu ya ndege kuishiwa mafuta ,lazima kuwe na sababu ya kiufundi,iliyopelekea mafuta hayo kutumika tofauti na makadirio,sasa ndege itoke dar,izunguke anga la bukoba mala moja,mafuta yaishe?!!Toka miaka na miaka kwa uwanja wa bukoba ndege kushindwa kutua ni jambo la kawaida sana,Labda kuusaidia uwanja huo kupunguza matatizo hayo ni kuweka taa kwewnye runway,
Huwa yanaisha mkuu.

Niliwahi toka Pemba na hizi ndege ndogo nilibahatika kukaa pale mbele na pilot nilikua naona kinachoendelea.

Ndege ilikua inapiga alarm low fuel lakini tuliruka toka pemba mpaka unguja kufika pale unguja hakujaza mafuta akaruka mpaka Dar, jamaa alirisk mno. Ni Mungu tu ndio alitulinda ila yule pilot hakuna makini.
 
Ndege ya Air Tanzania imeshindwa kutua Bukoba Airport imerudi Mwanza.

Stay tuned



======

UPDATES

Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imeshindwa kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera kutokana na hali mbaya ya hewa. Badala yake ndege hiyo imelazimika kutua salama katika uwanja wa Mwanza.

Alipoulizwa kwa simu leo Alhamisi Novemba 17 kuhusu tukio hilo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari amethibitisha tukio hilo.

“Ni kweli nimepata taarifa ndege ya Air Tanzania imeshindwa kutua kutokana na hali mbaya ya hewa, kulikuwa na ukungu, mvua, radi na giza uwanja ukawa hauonekani, kwa hiyo rubani akafuta safari na kurudi Mwanza na ametua salama,” amesema.

Awali taarifa iliyotumwa na Mbunge wa Viti Maalum, Neema Lugangira kwenye mitandao ya kijamii ilieleza tukio hilo.

“Still shaken lakini Mungu ni Mwema. Nimepanda ndege asubuhi ya leo kwenda Bukoba. Safari ilikuwa na changamoto, tumefika lakini ndege ikashindwa kutua.

“Nampongeza rubani kwa uamuzi sahihi wa kurudi Mwanza na sasa narudi Dar. Serikali ibebe kwa uzito suala la airport mpya Bukoba,” ameandika.

Hali hiyo imejitokeza zikiwa zimepita siku 11 tangu ndege ya shirika la Precision ilipoanguka katika ziwa Victoria na kusababisha vifo vya watu 19 na wengine 29 wakaokolewa.

Chanzo: Mwananchi
kwa wanaojua mambo ya ndege (aviation) hakuna jipya hapo kwani ni taratibu za kawaida tu , kwenda uwanja mwingine wa karibu hali ya hewa ikiwa mbaya au kukiwa na kizuizi kingine chochote
Huyo mbunge anatakiwa aelimishwe kuwa, hali ya hewa ikiwa mbaya hata ukijenga uwanja mzuri kama wa DOHA kule Dubai ndege haitaweza kutua!
 
Maigizo ya kuizuia kampuni fulani isifanye kazi na ndio rout zake hizo
 
Huwa yanaisha mkuu.

Niliwahi toka Pemba na hizi ndege ndogo nilibahatika kukaa pale mbele na pilot nilikua naona kinachoendelea.

Ndege ilikua inapiga alarm low fuel lakini tuliruka toka pemba mpaka unguja kufika pale unguja hakujaza mafuta akaruka mpaka Dar, jamaa alirisk mno. Ni Mungu tu ndio alitulinda ila yule pilot hakuna makini.
mmmmm!!!hilo ndio nalisikia leo kuwa ndege ina piga alarm ya low fuel,pasipo kuwa na dharura yoyote ile iliyojitokeza ikiwa angani!!!!??labda imezunguka sana kutokana na kushindwa kutua, uwanja iliyokusudia ,kutokana na labda matatizo ya kiufundi au hali ya hewa kuwa sio rafiki.
 
Yule rubani wa ndege iliyoanguka angefanya kama huyu angeepusha ile ajali, haya matukio ni ya kawaida hasa hali ya hewa inapokuwa hairuhusu kutua uwanja uliokusudiwa.
Huenda huyu kajifunza kupitia yule alieanguka! Ajali haina kinga
 
Kama suala lilikuwa kushusha abiria kwanini asishushe Chato kama sio chuki na ubinafsi wa kutaka uwanja ambao sio kigezo cha kuwezesha kutua kama hali ya hewa hairuhusu huwezi kutua hata kama ni Dar, KIA au Mwanza.

Sasa huyo mbunge alikuwa anaenda kufanya nini Bukoba kama baada ya ndege kuahirisha kutua hapo ikaenda Mwanza kwanini asingeshuka hapo na kwenda kwa meli au basi? Majivuno tupu

Bukoba ni lango la kuzimu kila tukio baya linaasisiwa huko kabla halijasambaa kwenda kwingine
 
Kama suala lilikuwa kushusha abiria kwanini asishushe Chato kama sio chuki na ubinafsi wa kutaka uwanja ambao sio kigezo cha kuwezesha kutua kama hali ya hewa hairuhusu huwezi kutua hata kama ni Dar, KIA au Mwanza.

Sasa huyo mbunge alikuwa anaenda kufanya nini Bukoba kama baada ya ndege kuahirisha kutua hapo ikaenda Mwanza kwanini asingeshuka hapo na kwenda kwa meli au basi? Majivuno tupu

Bukoba ni lango la kuzimu kila tukio baya linaasisiwa huko kabla halijasambaa kwenda kwingine
ccm huwa nibwatu wa hila sana.
Kuna mambo yanafanywa twaweza kuona kuwa ni jambo la kawaida kumbe kuna ajenda nzito nyuma yake.
Tusubirie siku zitaongea
 
Ni kawaida sana hiyo kwenye ndege..kuna siku ndege ya usiku tulikua tumetoka Dar to mwanza na fastjet ile ndege ya mwisho saa nne usiku ilishindwa kutua mwanza airport sababu mvua na hali ya hewa,tukarudi Dar tena.

Baada ya kama 3 hours tukaamsha tena kwenda mwanza..tulifika almost kunakucha . Nilijuta sana kupanda ndege ya mwisho
Hata Songwe, fastjet iliwahi kushindwa kutua ikabidi irejee Dar!!
 
Back
Top Bottom