Ndege ya Air Tanzania yashindwa kutua Bukoba, yageuza kwenda kutua Mwanza

Ndege ya Air Tanzania yashindwa kutua Bukoba, yageuza kwenda kutua Mwanza

hapa kuna kitu nyuma ya pazia,wanajaribu kuimarisha PR na kuaminisha umma kuwa ni weather related issue and somebody R.I.P Comrade was wrong despite the fact that it's a technical issue na responsible organ hawataki kuwajibika.
Dawa ya utawala huu ni Mungu auiite haraka na kulitawanyisha gwaride wakiwa vichwa chini ni uzandiki, inda, ulaghai na chuki dhidi ya push-up na tumbuatumbua kwamba alikosea kujenga uwanja kwao na kuacha Bukoba haina uwanja mkubwa kwa madai kwamba kitendo kinasababisha kuhatarisha maisha ya abiria!!!!
Siasa ya kuchafua kisichokuwepo kujikosha kwa maji ya mtaroni!!!!

CCM inatakiwa waadhibiwe kwa kuondoshwa madarakani haraka sana maana wanajifanya miungu watu na wamiliki wa nchi

*They are looking for a scapegoat for sacrifice to evade being held accountable for gross negligence that led to the downing of the recent aircraft into the lake causing several passengers drowned. to death.
 
Yule rubani wa ndege iliyoanguka angefanya kama huyu angeepusha ile ajali, haya matukio ni ya kawaida hasa hali ya hewa inapokuwa hairuhusu kutua uwanja uliokusudiwa.
Mkuu usemalo inaweza kuwa kweli ila inawezekana pia ruban aliona uwezekano wa kutua salama ni mkubwa na bila shaka maana wale ni wazoefu sana kwenye viwanja vya nyumbani.
Huwa nawaza na naujuwa uwanja wa Bukoba vizuri sana inawezekana rubani alikutana na cross wind dakika za mwisho kwenye kutua akashindwa kuhimili ndege.
 
Mkuu wewe basi rubani muoga. Mimi ndio zangu hizo hasa naporusha hivi vi cassena single engines. Nimeshawahi kutua kwenye hurricane Bahamas.

Pia nimeshawahi kutua kwenye tornado texas. Nimeshawahi kutua kwenye dhoruba ya monsoon India. Nimeshawahi kutua kwenye typhoon manilla ufilipino.

Nimeshawahi kutua kwenye tropical cyclone Msumbiji tena hizi hizi single engines cassena.
Box ulimwachia nani?🤣🤣🤣
 
Siku 11 baada ya ajali ya ndege ya Precision Air nchini Tanzania, iliyoua watu 19, Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imeshindwa kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera, kutokana na hali mbaya ya hewa.

Kwa mujibu wa Mwananchi Digital, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari amethibitisha hilo na ndege hiyo ililazimika kurudi katika uwanja wa Mwanza na kutua salama.

Mbunge wa Viti Maalum, Neema Lugangira aliyekuwepo kwenye ndege ameandika kwenye mtandao wake wa twitter akieleza tukio hilo, na kutaka Serikali ibebe kwa uzito suala la uwanja wa ndege wa Bukoba.



Novemba 6, 2022, Ndege ya Precision Air, iliyokuwa imebeba watu 43, ilidondoka katika ziwa Victoria, mita chache kutoka uwanja wa ndege wa Bukoba, na kuua watu 19, huku 24 wakinusurika.

 
Wewe Mbunge uliyepanda Leo Ndege ya ATCL iliyoshindwa Kutua Bukoba kulikoni unayelalamika Mitandaoni uko peke yako tu wakati Abiria mliopanda ni wengi?

au labda mnadhani wenye Akili Kubwa na Kuwazidi akina GENTAMYCINE hatutojua kuwa AGENDA mnayotaka Kutuaminisha hapa ni kwamba tatizo la Ajali ya Ndege ya Precision Air Wiki iliyopita haikutokana na Uzembe wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege Bukoba ( uliyo chini ya Serikali nikimaanisha Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ) na kwamba ilitokana na tatizo la Hali mbaya ya Hewa ( Mvua na Upepo ) kwa Kipindi hiki?

Kwahiyo Wenyewe mkaona leo mje na hii Sinema mpya kwa Kutumia Ndege ya Serikali Kiumiliki ( ATCL ) kisha kwenda nayo hadi Bukoba na kujifanya imeshindwa Kutua kutokana na Hali mbaya ya Hewa na kurudi Mwanza Ili mtuaminishe kuwa ile Ndege ya Precision Air ( inayomilikiwa na Kampuni Binafsi na siyo ya Serikali kama ATCL yenu ) kuwa kuanguka Kwake vile Majini hakukutokana na labda Hujuma ya Kiushindani au Uzembe wa Watu wa Control Tower Bukoba Airport na kwamba ni tatizo tu la Hali mbaya ya Hewa kwa sasa Bukoba.

Kwa kifupi mnachokifanya na Kuhangaika nacho kwa sasa ni Kutuandaa Kisaikolojia Watanzania kwa Ripoti yenu ya Uchunguzi wa Ajali ya Ndege ya Precision Air ambayo wenye Akili Kubwa Kuwazidi tumeshajua kuwa sababu Kuu mtakayokuja nayo ni Changamoto ya Hali mbaya ya Hewa kwa sasa Jijini Bukoba ( Mkoani Kagera ) na kwamba haikutokana na Uzembe wenu ( hasa wa Mamlaka husika ) hapo ( pale ) Bukoba Airport.

Mwambieni aliyeiandaa hii Script yenu ya hii Sinema yenu ya Kipuuzi na Kitoto kuwa GENTAMYCINE namwambia kuwa hana Akili na kama wako wengi walioiandaa pia waambie nawaambia hawana Akili.
 
Daaa!!hivi ndege kuishiwa mafuta unadhania ni kitu rahisi kama kwenye bodaboda!!kuna mambo mengine kabla hata ya kuyaandika tumia kwanza halimashauri ya ubongo wako kwanza kufikiria. Inshu ya ndege kuishiwa mafuta ,lazima kuwe na sababu ya kiufundi,iliyopelekea mafuta hayo kutumika tofauti na makadirio,sasa ndege itoke dar,izunguke anga la bukoba mala moja,mafuta yaishe?!!Toka miaka na miaka kwa uwanja wa bukoba ndege kushindwa kutua ni jambo la kawaida sana,Labda kuusaidia uwanja huo kupunguza matatizo hayo ni kuweka taa kwewnye runway,
Huo ndo ukweli kwamba
1, mafuta yaliisha akaona hata kama hali mbaya hawezi kurudi mwanza wese litakata angani wote wafe
2:technical issue ambayo ilisababisga tail zisitoke.

Hali ya hewa haikuwa chanzo cha ajali, coz alikuwa na option ya kurudi mwanza au the choosen big international airport in chato town. upo?
 
kwa wanaojua mambo ya ndege (aviation) hakuna jipya hapo kwani ni taratibu za kawaida tu , kwenda uwanja mwingine wa karibu hali ya hewa ikiwa mbaya au kukiwa na kizuizi kingine chochote
Huyo mbunge anatakiwa aelimishwe kuwa, hali ya hewa ikiwa mbaya hata ukijenga uwanja mzuri kama wa DOHA kule Dubai ndege haitaweza kutua!
Big up Mkuu...
Kanda ya ziwa ni famous kwa thunderstorms, jumlisha na issue zingine za hali ya hewa kama fog na wind.
Hata huo uwanja mpya ujengwe bado kama hali ya hewa ni mbovu lazima ndege zitadivert kwenda mwanza au any nearest airport.
 
Me najiuliza maswali mengi, pale chato ni jirani zaidi kuliko mwanza. Kwanini wasiende kutua pale na badala yake waende mwanza?
 
Huo ndo ukweli kwamba
1, mafuta yaliisha akaona hata kama hali mbaya hawezi kurudi mwanza wese litakata angani wote wafe
2:technical issue ambayo ilisababisga tail zisitoke.

Hali ya hewa haikuwa chanzo cha ajali, coz alikuwa na option ya kurudi mwanza au the choosen big international airport in chato town. upo?
Hizi zote ni assumptions.
To my thinking possibility ya ulichozungumza hapa ni ndogo:
1. Airlines lazima wawe na mafuta ya kuwawezesha kwenda kwenye alternate airport just incase wameshindwa kutua kwenye destination airport.
Based on abiria walionusurika alizunguka hewani kwa muda usiopungua dkk 10 akitafuta namna ya kutua.
Kama angetaka kwenda mwanza angefika bila shida assuming other factors are constant, simply because distance from bkb to mwanza by air ni fupi sana approx. 15-20 mins.
2. Possibly rubani alijiamini kupita kiasi ukizingatia ana uzoefu wa kutosha kwenye hiyo route akaamua kutua regardless of poor weather.
And maybe wakati anatua ndio other technical faults zilitokea na kusababisha ndege kuwa uncontrolled...
 
Me najiuliza maswali mengi, pale chato ni jirani zaidi kuliko mwanza. Kwanini wasiende kutua pale na badala yake waende mwanza?
Lazima uende sehemu ambayo utapata full support ya ndege na abiria wako.
Rubani anapochagua alternate airport anaangalia vitu vingi ikiwemo upatikanaji wa mafuta nk.
 
Huo ndo ukweli kwamba
1, mafuta yaliisha akaona hata kama hali mbaya hawezi kurudi mwanza wese litakata angani wote wafe
2:technical issue ambayo ilisababisga tail zisitoke.

Hali ya hewa haikuwa chanzo cha ajali, coz alikuwa na option ya kurudi mwanza au the choosen big international airport in chato town. upo?
Hivi wewe kwa kutumia akili tu za kawaida,ndege ilikuwa inatoka dar inakwenda mwanza kupitia bukoba,kwa hiyo baada ya kushusha abiria wa bukoba,na kuchukua wale wa mza na dar, ingetokaje bukoba,kama haikuwa na mafuta ya kutosha?!!na bukoba hakuna kituo cha kujazia mafuta ndege?!!eti chato ni international airport!!ambayo haina hata radar,uwanja hauna taa,unafikiria ndege ni kama lori,unaamua tu nilipaki wapi?!!kama ndege ina matatizo ya kiufundi,pilot atakachofanya ni kutafuta uwanja ulio karibu yake,kwa wakati huo,au sehemu yoyote ya wazi ambayo ana hisi inaweza msaidia,hasa kwa hizi ndege ndogo!!lakini kama ni hali ya hewa ya kwenye eneo analotaka kutua,ana uamuzi wa kuipeleka ndege uwanja wowote ule baada ya kuwasiliana na control tower iliyopo karibu yake.Kwa case ya uwanja wa ndege wa bukoba control tower ipo mwanza,ndege ikiwa inatoka mza kwenda bk,ataacha kuiongoza pindi tu inapokuwa umbali wa km 45 kutoka uwanja wa ndege wa bk.Hapo sasa Rubani anakuwa anakaribia kutua hivyo,asilimia kubwa ni kutumia macho kuangalia.Ndio maana huwa wanasema kama pilot hana uwezo wa kuona umbali wa km 5,mbele pale anapotaka kutua,anashauriwa asijaribu kutua.
 
Sasa Kama una wese Kidebe,hiyo jeuri ya kugeuza ulikotoka utaipata wapi!?? Rubani wa Precision nilimuelewa sana,na alifanya maamuzi yake very professional! RIP Rubani! Wese Kidebe bado ni tatizo kubwa kwa wawekezaji uchwara, wanapenda kucheza na Maisha ya watu!!
Acheni hizo bnana!!hiyo ndege ilikuwa inatoka dar kwenda Mza kupitia bukoba,sasa kama angetua salama bk, mza angefikaje kama hakuwa na mafuta ya kutosha?!!wakati bukoba hakuna sehemu ya kuongezea mafuta?!!na unaufahamu wowote ule wa mafuta yanayotumika kwenye hizo ndege kama iliyopata ajari?!!kwa taarifa yako hata bei ya diesel inaweza ikawa juu kidogo.
 
Mkuu wewe basi rubani muoga. Mimi ndio zangu hizo hasa naporusha hivi vi cassena single engines. Nimeshawahi kutua kwenye hurricane Bahamas.

Pia nimeshawahi kutua kwenye tornado texas. Nimeshawahi kutua kwenye dhoruba ya monsoon India. Nimeshawahi kutua kwenye typhoon manilla ufilipino.

Nimeshawahi kutua kwenye tropical cyclone Msumbiji tena hizi hizi single engines cassena.
Ulimaanisha Cessna?
 
Ndege ya Air Tanzania imeshindwa kutua Bukoba Airport imerudi Mwanza.

Stay tuned



======

UPDATES

Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imeshindwa kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera kutokana na hali mbaya ya hewa. Badala yake ndege hiyo imelazimika kutua salama katika uwanja wa Mwanza.

Alipoulizwa kwa simu leo Alhamisi Novemba 17 kuhusu tukio hilo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari amethibitisha tukio hilo.

“Ni kweli nimepata taarifa ndege ya Air Tanzania imeshindwa kutua kutokana na hali mbaya ya hewa, kulikuwa na ukungu, mvua, radi na giza uwanja ukawa hauonekani, kwa hiyo rubani akafuta safari na kurudi Mwanza na ametua salama,” amesema.

Awali taarifa iliyotumwa na Mbunge wa Viti Maalum, Neema Lugangira kwenye mitandao ya kijamii ilieleza tukio hilo.

“Still shaken lakini Mungu ni Mwema. Nimepanda ndege asubuhi ya leo kwenda Bukoba. Safari ilikuwa na changamoto, tumefika lakini ndege ikashindwa kutua.

“Nampongeza rubani kwa uamuzi sahihi wa kurudi Mwanza na sasa narudi Dar. Serikali ibebe kwa uzito suala la airport mpya Bukoba,” ameandika.

Hali hiyo imejitokeza zikiwa zimepita siku 11 tangu ndege ya shirika la Precision ilipoanguka katika ziwa Victoria na kusababisha vifo vya watu 19 na wengine 29 wakaokolewa.

Chanzo: Mwananchi
Duh hapa naona kama kaitaba ijajitosheleza
 
Back
Top Bottom