Ndege ya Air Tanzania yashindwa kutua Bukoba, yageuza kwenda kutua Mwanza

Huo ndio uamuzi wa busara tunaotumia sisi marubani sio kulazimisha kutua hata kama kuna ugumu kufanya hivyo
Sasa Kama una wese Kidebe,hiyo jeuri ya kugeuza ulikotoka utaipata wapi!?? Rubani wa Precision nilimuelewa sana,na alifanya maamuzi yake very professional! RIP Rubani! Wese Kidebe bado ni tatizo kubwa kwa wawekezaji uchwara, wanapenda kucheza na Maisha ya watu!!
 
Muongo
 
Inaonekana BK Airport ipo Analogy!! Ingekuwa na Automatic systems ndege inatua yenyewe ata kama kuna Ukungu , umeme umekatika etc! Inaonekana Airport ni ya 1945! No any automation! Kama ata Ndege za ATC ambazo ni mpya na zina auto pilot aziwezi shuka BK Airport basi kuna tatizo
 
Ndio maana 1010 baada ya kuambiwa mafuta yameisha wakatoa jibu peleka ziwani na wenyewe wakaendelea kuangalia movie kwenye PC zao
 
Serikali ingesimamisha matumizi ya uwanja wa ndege wa Bukoba ndege zote zitue Mwanza.
 
hapa kuna kitu nyuma ya pazia, wanajaribu kuimarisha PR na kuaminisha umma kuwa ni weather related issue and somebody R.I.P Comrade was wrong despite the fact that it's a technical issue na responsible organ hawataki kuwajibika.
 
Msimu wa mvua kipindi hiki ni shida aisee.Ila sio technical issues,ni mambo ya Hali ya hewa.
Hata kwenye viwanja vikubwa duniani kuna kipindi ndege zinashindwa kuruka au kutua kutokana na hali ya hewa kutoruhusu.

Ujenzi wa uwanja mpya unaweza kuwa na umuhimu wake kama alivyoshauri huyo mbunge wa vitu maalum, lakini si suluhisho kuondoa matatizo ya hali ya hewa.
 
Huwa yanaisha mkuu.

Niliwahi toka Pemba na hizi ndege ndogo nilibahatika kukaa pale mbele na pilot nilikua naona kinachoendelea.

Ndege ilikua inapiga alarm low fuel lakini tuliruka toka pemba mpaka unguja kufika pale unguja hakujaza mafuta akaruka mpaka Dar, jamaa alirisk mno. Ni Mungu tu ndio alitulinda ila yule pilot hakuna makini.
 
kwa wanaojua mambo ya ndege (aviation) hakuna jipya hapo kwani ni taratibu za kawaida tu , kwenda uwanja mwingine wa karibu hali ya hewa ikiwa mbaya au kukiwa na kizuizi kingine chochote
Huyo mbunge anatakiwa aelimishwe kuwa, hali ya hewa ikiwa mbaya hata ukijenga uwanja mzuri kama wa DOHA kule Dubai ndege haitaweza kutua!
 
Maigizo ya kuizuia kampuni fulani isifanye kazi na ndio rout zake hizo
 
mmmmm!!!hilo ndio nalisikia leo kuwa ndege ina piga alarm ya low fuel,pasipo kuwa na dharura yoyote ile iliyojitokeza ikiwa angani!!!!??labda imezunguka sana kutokana na kushindwa kutua, uwanja iliyokusudia ,kutokana na labda matatizo ya kiufundi au hali ya hewa kuwa sio rafiki.
 
Yule rubani wa ndege iliyoanguka angefanya kama huyu angeepusha ile ajali, haya matukio ni ya kawaida hasa hali ya hewa inapokuwa hairuhusu kutua uwanja uliokusudiwa.
Huenda huyu kajifunza kupitia yule alieanguka! Ajali haina kinga
 
Kama suala lilikuwa kushusha abiria kwanini asishushe Chato kama sio chuki na ubinafsi wa kutaka uwanja ambao sio kigezo cha kuwezesha kutua kama hali ya hewa hairuhusu huwezi kutua hata kama ni Dar, KIA au Mwanza.

Sasa huyo mbunge alikuwa anaenda kufanya nini Bukoba kama baada ya ndege kuahirisha kutua hapo ikaenda Mwanza kwanini asingeshuka hapo na kwenda kwa meli au basi? Majivuno tupu

Bukoba ni lango la kuzimu kila tukio baya linaasisiwa huko kabla halijasambaa kwenda kwingine
 
ccm huwa nibwatu wa hila sana.
Kuna mambo yanafanywa twaweza kuona kuwa ni jambo la kawaida kumbe kuna ajenda nzito nyuma yake.
Tusubirie siku zitaongea
 
Hata Songwe, fastjet iliwahi kushindwa kutua ikabidi irejee Dar!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…