Ndege ya kwanza kutengezwa Tanzania yaanza safari zake

Ndege ya kwanza kutengezwa Tanzania yaanza safari zake

Hypersonic WMD

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2024
Posts
1,337
Reaction score
1,876
Kampuni ya Airplanes Africa Limited (AAL) yenye makao yake Morogoro, imetangaza kuanza safari za ndege tatu za kwanza zilizotengenezwa Tanzania, aina ya Skyleader 600. Mkurugenzi wa AAL, Bw. David Grolig, alisema ndege moja imetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kama sehemu ya uzinduzi.

Pia, soma: Ndege ya Kwanza kutengenezwa Tanzania yazinduliwa

Grolig alithibitisha kuwa kampuni yao imepata kibali cha mamlaka husika baada ya kuthibitisha ubora wa ndege hizo, ambazo ni za kisasa na zina viwango vya kimataifa. Ndege hizi, zikiwa na uwezo wa kubeba abiria wawili pamoja na rubani, ni suluhisho bora la usafiri kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla.

AAL, kampuni ya kwanza Tanzania kutengeneza ndege za aina hii, imetengeneza ndege hizi kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji nchini. Gharama za kununua ndege hizo ni nafuu kama kumiliki gari. Ndege hizo pia zilioneshwa katika Maonyesho ya Watengenezaji wa Bidhaa ya Tanzania (TIMEXPO 2024) yanayoendelea katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

1727768209663.jpeg

1727768246971.jpeg


Wafanyakazi wa kampuni ya Airplanes Africa Limited (AAL) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Ndege hiyo aina ya Skyleader 600 kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 1) kwa mara ya kwanza katika historia.
 
Back
Top Bottom