Ndege ya kwanza kutengezwa Tanzania yaanza safari zake

Viwanda vingi kwa taarifa ni assembly mfano wewe binafsi unashindwa nini kuanzisha kiwanda cha ku assemble baiskeli?

Minyororo ya bsiskeli ,taa,tairi viti vya kukukalia vya baiskeli vinauzwa madukani.Mabomba tunayo ,mafundi bomba na welding tunao wa kuweza kutengeneza yale mabomba ya baiskeli ili u a semble hivyo umenunua unashidwa nini?
Pili engineer wa nje kazi yake kuachia knowledge wazawa shida yako nini?.

Hako.ka kingereza kako tu ka goodmorning mzungu ndie alikuja kwanza akafunza watu weusi wakajua ndio na wewe ukambulia
Kuanzisha kiwanda kidogo cha kuunganisha sio tatizo
Tatizo ni usimamizi, hivi hujiulizi kwanini viwanda vikubwa nje wanawekeza China, Bangladesh, Taiwan, Turkey na hata kenya
 
Unawashwa ww siyo bure

Nilichouliza umekifahamu
Nilitaka kujua kuhusu ivo vi mini airbus
Nan anatengeneza
Kampuni la ndani au wawekezaji
Ni vya kazi gan hivo vya abiria au vya kusafirishia chanjo
details kama izo
Siyo upige campan hapa
Mapovu ya kipumbavu haya ndio yanabatilisha maelezo yangu hapo Juu?

Ni kampuni ya Kigeni yenye ubia na Wazawa ndio wanatengeneza,Toka mwaka juzi walikuwa wameanza hiyo project.

Soma hapa Ndege ya Kwanza kutengenezwa Tanzania yazinduliwa
 
Mimi naitambua hii kama ndege halisi ya kitanzania. Hiyo mnayosema ni ya mabeberu.
 
Attachments

  • NDEGE.jpg
    NDEGE.jpg
    686.9 KB · Views: 3
Kampuni ya Airplanes Africa Limited (AAL) yenye makao yake Morogoro, imetangaza kuanza safari za ndege tatu za kwanza zilizotengenezwa Tanzania, aina ya Skyleader 600. Mkurugenzi wa AAL, Bw. David Grolig, alisema ndege moja imetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kama sehemu ya uzinduzi.
Grolig alithibitisha kuwa kampuni yao imepata kibali cha mamlaka husika baada ya kuthibitisha ubora wa ndege hizo, ambazo ni za kisasa na zina viwango vya kimataifa. Ndege hizi, zikiwa na uwezo wa kubeba abiria wawili pamoja na rubani, ni suluhisho bora la usafiri kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
AAL, kampuni ya kwanza Tanzania kutengeneza ndege za aina hii, imetengeneza ndege hizi kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji nchini. Gharama za kununua ndege hizo ni nafuu kama kumiliki gari. Ndege hizo pia zilioneshwa katika Maonyesho ya Watengenezaji wa Bidhaa ya Tanzania (TIMEXPO 2024) yanayoendelea katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa kampuni ya Airplanes Africa Limited (AAL) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Ndege hiyo aina ya Skyleader 600,kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 1) kwa mara ya kwanza katika historia.
Nilitaka kuwa rubani kumbe Tanzania hakuna chuo chà urubani
 
Mimi hata kwa bure kabisa sipandi we are good in nothing.

Haikawii kutokea itilafu za kiufundi.
 
Back
Top Bottom