Ndege ya precious Air yashindwa kutua Dodoma

Ndege ya precious Air yashindwa kutua Dodoma

#HABARI: Ndege ya Precision Air PW 600, iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Jijini Dodoma imeshindwa kutua kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma na kulazimika kurudi mkoani Dar es Salaam baada ya moja ya injini zake kuzima wakati ikikaribia kutua.
Sasa kwanini haikutua Dodoma Kwa injini moja, ikarud Dar,,hatuoni ilihatarisha Maisha ya abiria
 
Kwanini ilishindwa kutua Dodoma ambako ilikuwa imefika tayari mpaka ikalazimika kwenda Dar ambako ni mbali zaidi..?

Utasikia majibu mepesi tu " Ooooh Dodoma hakukuwa na zimamoto na tayari ndege ilikuwa na matatizo ya engine

" Utasikia Ooooh ilikuwa ni drill aka majaribio na ndege haikuwa na abiria"
 
Sibishi bali nahoji iweje ndege yenye hitlafu ya injini moja kuzima ishindwe kutua hapo Dodoma na badala yake igeuze na iweze kusafiri mamia ya kilometa ikitumia engine moja hadi kutua tena Dar ilhali ilishindwa kutua hapo Dom baada ya engine kuzima?

Sijaelewa sijaelewa kabisa maana kama engine ya pili nayo ingezima wakati wa kurudi Dar lazima ndege ingepiga sarakasi.
sijui unachobisha ni nini hapo?
 
soma kitabu kinaitwa "Aircraft Manufacturing in the New Era"utaelewa jinsi ndege inavyoweza kutua Manually kunapotokea tatizo la kiufundi,kikubwa Uwanja husika uwe na technology hiyo,kwa Tanzania ipo Dar tu sina uhakika kuhusu KIA kama ipo
Nimesoma maelezo yako toka mwanzo.

Sasa Waeleze hivi"ndege ina uwezo wa kuzurura angani ikiwa na injini moja,nzima ingine mbovu."

Hiki ndicho kinachotufikirisha.
 
Back
Top Bottom