DOKEZO Ndege za Dubai zinaendelea kutua Serengeti! Tunaibiwa

DOKEZO Ndege za Dubai zinaendelea kutua Serengeti! Tunaibiwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hii Nchi , sijui ihamishiwe sayari ya kipekee. Wanyama wanauzwa Bei zinafahamika hata wewe unaweza Kununua. Mia 2 iliopita Rwanda wamefikisha Faru 10 kwenye Akagera national park. Je hao walio wagawia majirani zetu hawawqpendi?

Lakini pia mtakiwa mjue Hawa wanyama wanazaliana wanaugua na wanakufa , Bado tuna na ujangiri.
Yawezekana huko wanako enda siku moja wakaja kuturudishia kama wataweza kuishi.
Hiyo exchange ya wanyama inafanyika kwa nchi zenye mbuga tayari kama Kenya, South Africa, Botswana.......huwezi kusema unapeleka wanyama kwenye sanctuary uarabuni wakati wao wanatengeneza mbuga za kitalii ili wapige pesa, hapo unakuwa unajipiga mwenyewe risasi mguuni.
 
Umbea katika kiwango chake, hata kuwadadisi hao waliopiga picha mkakosa huo muda. Ukijihisi unaonewa kila wakati hata kujiamini inakuwa ngumu sana. TUWAWAZIE NA MEMA VIONGOZI WETU.
Unawezaje kumuwazia mema mtu ambaye yeye hakuwazii mema!!???
 
Sasa mtu kama wewe hata kuandika lugha yako tu kwa ufasaha huwezi,utaweza kujadili vitu vinavyohitaji akili na maarifa ya utambuzi?
Huu muda unaoutumia kutapika hapa ni vizuri ukautumia kujifundisha kuandika lugha yako kwa ufasaha.
Yaani upo JF lakini hujui tofauti ya miandiko ya kukosea na miandiko ya "kificho" iliyodhamiriwa!!!???
 
Mimi sioni kosa hapo
Kuchukua mali za mpumbavu na mjinga ni kosa?.
2020 nimeshudia wajinga na wapumbavu wengi wakihamasishwa na wajumbe wa CCM wakaipigie kura kwa kupewa sh. Elfu 5 au 10.
 
Ndo maana wagalatia wanasemwa ni watu wabaya maana wanakufa mapema, siyo? sisi tutaamini vipi kama wanakufa vifo vya kawaida......maana siyo kwa kunangwa kule.
Wagalatia wamekufa kipindi Nani anaongoza!?..maana jakaya alilalama 'mzee mkapa nilikua nae Jana,hakuwa na tatizo'
 
Mimi sioni kosa hapo
Kuchukua mali za mpumbavu na mjinga ni kosa?.
2020 nimeshudia wajinga na wapumbavu wengi wakihamasishwa na wajumbe wa CCM wakaipigie kura kwa kupewa sh. Elfu 5 au 10.
Mbona hakuna mali za mpumbavu wala mjinga zilizochukuliwa??? Kama ni biashara, ni biashara kama biashara zingine. Ukisha thibitisha kwamba hiyo biashara ni kweli ipo; basi angalia: Je, vigezo na msharti vimezingatiwa? Yaani iko hivi; kama tunalalamika kuuzwa kwa wanyama basi tulalamike pia kuzaliana(kuongezeka) kwa wanyama. Unataka ujilimbikizie lundo la wanyama (kama ss huku ndani-ndani huku) halafu tunaendelea kuvaa matairi ya gari. Tukiambiwa ni matajiri tunakuwa wakali. Tuamke na kushiriki kwa roho nyeupe kuvuna mazao yetu kwa utaratibu mzuri na unaokubalika e.g. Ref. mazao ya kilimo, mifugo, mazao ya bahari, mito na maziwa(Lakes) na misitu huvunwa kwa utaratibu fulani. Mbona hamtaki iwe hivyo pia na kwa w/pori??? Kwani hayo siyo mazao??
Vipi, Mbona tunahusisha mambo ya siasa katika utendaji?
NB: Nasimama hapa - ruksa mnishambulie.
 
Wagalatia wamekufa kipindi Nani anaongoza!?..maana jakaya alilalama 'mzee mkapa nilikua nae Jana,hakuwa na tatizo'
Mgalatia alikufa kipindi anaongoza, baadaye tukasikia kwamba watu wabaya hufa mapema........wenye akili tukatafakari ule usemi kwamba ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya.
 
Maasai walituma ushahidi wa ndege kubwa isiyo na alama ikitua na kuruka kutoka Pololeti

View attachment 2473424
Umefanya vizuri Masai.

Na hiyo si maana ya pori tengefu la Pololeti. Bali hiyo ni maana ya "Kikwete amerudi." na ndo maana ya "Kazi iendelee."

Kazi inayoendelezwa sio ya Magufuli, bali ni ya Kikwete na Mwinyi.

Pwani Gang.

Kwa wale vijana wa zamani mtakumbuka suala la wanyama wa Tanzania kupelekwa Uarabuni alianzaga Mwinyi. Tena alianzia kwa wanyama waliokuwa pale Ikulu.
 
Back
Top Bottom