DOKEZO Ndege za Dubai zinaendelea kutua Serengeti! Tunaibiwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mnaibiwa kitu gani?

Mbona hata Ndege yenyewe haionekani vizuri ili kujua ni Ndege ya wapi?

Ina maana pia hiyo Ndege imetua ndani ya nchi bila mamlaka husika kujua hilo?
Mijitu mingine kutumia akili kidogo tu shida, kuna ndege itaingia nchini bila kupata ruhusa na mamlaka. Halafu unaibiwa nini Simba? Fisi au Sungura mbona tunatafuta soko la bidhaa kwenda nje tupate pesa sasa shida iko wapi kama wanauza wanyama kama wako wengi shida iko wapi.
 
Kabisa hawajui wale Dubai parking fees za magari kama za huku za kwetu makusanyo yao kama budget yetu ya miaka miwili sasa atuibie nini sisi? sema wamenunua sio kuiba
 
Ila kiukweli kuna kaupendeleo ka waarabu awamu hii.
Hata uingizwaji wa mafuta ya kupikia kutoka nje ya nchi awamu hii ni hao hao waarabu, sera ya kulinda viwanda vidogo vidogo vya alizet vya wazawa imewekwa kapuni.
Hakuna tena protectinism, wakulima wazawa wapate taabu kwa bei ya alizet yao kuporomoka kwa faida ya waarabu!.
 
Ulienda kuomba kibali wizara ya viwanda wakakwambia "Hadi uwe mwarabu "ndo tunakupa kibali?
 
Halafu yupo yule mmarekani mwenye lodge yake hataki hata watz wakanyage pale na aliwahi kuwatimua hata ile kamati ya bunge, amegombana na kulalamika na wamiliki wa kila upande wa eneo lake na aliwahi hata kutaka kuweka airstrip huko mbugani. Lakini watu humu kimyaa, leo wanaona ndege imeshuka tu hata hawaijui inatokea wapi basi tayari imekuwa ya kuiba wanyama.
 
Maasai walituma ushahidi wa ndege kubwa isiyo na alama ikitua na kuruka kutoka Pololeti

View attachment 2473424
Mnaoleta mada za aina hii kitu ambacho mnakosea kwa makusudi au hamkijui ni ukweli kuwa Tanzania ya sasa yote inamulikwa na rada nne zilizowekwa kimkakati katika kona nne.

Hakuna ndege inayoweza kuingia na kutoka tu kama shamba la bibi, haya mambo yalifanyika miaka hiyo ya nyuma kwa sasa haiwezekani ndege ikatua mgodini na kuondoka tu bila ya kutazamwa na rada.

Na hizi rada ni chanzo cha mapato, kila ndege inavyokatiza angani taarifa zinakwenda mamlaka ya anga ambao wanatuma invoice ya moja kwa moja katika nchi inayotoka hiyo ndege, mambo yamebadilika mno na mengi sio kama ya miaka ile.

Hivyo mnavyoanzisha uzi kwa nia ya kuitangazia chuki Tanzania kumbukeni kuandika uzi wenye elimu angalau, msiishie kutunga vitu visivyowezekana kwa sababu ya kukariri tu hulka za siku za nyuma.
 
Mimi nimeiamini serikali kuwa wamasai wanafanya uharibifu wa mazingira...Hadi hapo kutakapo jitokeza habari zingine za uhakika ndo ntawahukumu tofauti..sitaki kuihukumu serikali Kwa kuhisi au kusikia habari ambazo hazina ukweli
The Axis Of Evils
 
Kama unajua ni uongo. Tuambie basi hiyo ndege inafanya nini huko.
 
Umbea katika kiwango chake, hata kuwadadisi hao waliopiga picha mkakosa huo muda. Ukijihisi unaonewa kila wakati hata kujiamini inakuwa ngumu sana. TUWAWAZIE NA MEMA VIONGOZI WETU.
Iko Twitter
Acha kujitoa ufahamu
Nchi inaibiwa kuliko unavyojua
Madini wanyama imegeuka mali ya wachache
Msikomaze shingo
Katiba Mpya muhimu tufunge wezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…