DOKEZO Ndege za Dubai zinaendelea kutua Serengeti! Tunaibiwa

DOKEZO Ndege za Dubai zinaendelea kutua Serengeti! Tunaibiwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Iko Twitter
Acha kujitoa ufahamu
Nchi inaibiwa kuliko unavyojua
Madini wanyama imegeuka mali ya wachache
Msikomaze shingo
Katiba Mpya muhimu tufunge wezi
Hapa Jf labda kama unajizima data tunataka habari yenye ukamilifu si kivideo uchwara uje uteke akili za watu, tupia mzigo mzima tuone wizi wenyewe. Kumbe unataka katiba mpya ili uwafunge watu na si kwa hatma ya nchi yako kwa baadae , tambua pia nahitaji katiba mpya ili nchi iweze kusonga mbele kwa vizazi na vizazi.
 
Mijitu mingine kutumia akili kidogo tu shida, kuna ndege itaingia nchini bila kupata ruhusa na mamlaka. Halafu unaibiwa nini Simba? Fisi au Sungura mbona tunatafuta soko la bidhaa kwenda nje tupate pesa sasa shida iko wapi kama wanauza wanyama kama wako wengi shida iko wapi.
Mkuu,kuna watu wamekaririshwa mambo miaka nenda rudi na wameshindwa kujitoa kwenye hiyo fixed mind mentality,miaka yote mawazo yao ni hayo hayo tu,sijui tunaibiwa Simba,mara tunakuja kutawaliwa tena,Dunia inaenda mbele ila wao mawazo yao yapo pale pale!
 
Pori tengefu ni kama misitu ya jeshi inayotuzunguka nchi nzima, public access is off limits. Huwezi kupata close-up HD video ya ndege inashuka na kupandisha wanyama. Cameraman alifanya alichoweza katika mazingira yaliyomkabili.

"Iacheni serikali yetu itutumikie" ni mentality za Mtanzania wa pre-1990. Muda umekuacha nyuma.

Enzi hizi wananchi wanachagizwa kujihusisha na majadiliano huru ya mambo yanayowahusu kama sehemu ya mchakato wa demokrasia.

Binafsi siamini watawala kutoka visiwani wana uchungu na Tanganyika.
Mbona anachunga ng'ombe hapo, public access ipi unaizungumzia?.
 
Ila kiukweli kuna kaupendeleo ka waarabu awamu hii.
Hata uingizwaji wa mafuta ya kupikia kutoka nje ya nchi awamu hii ni hao hao waarabu, sera ya kulinda viwanda vidogo vidogo vya alizet vya wazawa imewekwa kapuni.
Hakuna tena protectinism, wakulima wazawa wapate taabu kwa bei ya alizet yao kuporomoka kwa faida ya waarabu!.
Tangu lini hayo mafuta ilikuwa tabu kuyaingiza? wakati wa corona mafuta yaliyotuokoa kureplace ya alizeti wakati wa uhaba mkali si yalitoka uturuki? au 2020 rais alikuwa anapendelea waarabu pia?.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Ni muhimu sasa, katika "Katiba Mpya," kama itatengenezwa, pawepo na vifungu vya kuwawajibisha viongozi wahujumu wa nchi hata wakishamaliza muda wao wa uongozi.

Brazil na kwingineko haya yanawezekana, kwa nini yasiwezekane hapa.
 
Maasai walituma ushahidi wa ndege kubwa isiyo na alama ikitua na kuruka kutoka Pololeti

View attachment 2473424
Raisi wenu Mama Samia si ndio ameruhusu Wanyama Wauzwe ?Alivyokwenda Uarabuni kwenye Ziara yake si aliwaambia Waarabu wanaotaka wanyama waje kuwachukuwa. Mpaka mwaka 2030 Tanzania kutakuwa hakuna tena Wanyama Twiga Tembo ,Vifaru Simba, Chui na Chita wote watakuwa hakuna nchini Tanzania. Watalii hawata kuja Tanzania kutembelea mbuga za Wanyama. Kiongozi wetu mpendwa RIP Rais Magufuli aliwahi kutabiri haya hapo unayo yaona.



 
Maasai walituma ushahidi wa ndege kubwa isiyo na alama ikitua na kuruka kutoka Pololeti

View attachment 2473424
Wenye akili walisha yasema haya tangu sekunde ya kwanza ya tangazo

1673188273826.png
 
Acheni kupandikiza uongo na kuichonganisha serikali yetu kwa Ajenda zenu za Siri, Sasa hapo hiyo ndege IPO wapi? Wanyama wanao bebwa wapo wapi? Ni ndege aina gani? Kutoka nchi gani? Kwa utambulisho wa kutoka shirika gani la ndege? Wanyama wapo wapi hapo? Mbona hatuonyeshwi hao wanyama? Mbona hatuonyeshwi wakipandishwa kwenye ndege? Mbona hatuonyeshwi ndege ikitua na kupaa?

Huu uongo unawasaidia Nini? Mnalengo gani na serikali yetu? Mnapata faida gani kuichafua serikali yetu? Mnamlenga Nani kumchafua? Kwa masilahi ya Nani? Nani anawdfadhiri huu upotoshaji?

Iacheni serikali yetu ifanye kazi za kututumikia watanzania ,hizi propaganda za kitoto hazitawafikisha popote pale na hamtaweza kuichonganisha serikali yetu na sisi wananchi
 

Attachments

  • 1673188406482.png
    1673188406482.png
    34.9 KB · Views: 1
kuna mpango kamambe wa kuunganisha shoroba zilizopo jirani na Ngorongoro ili kuweka utalii sehemu salama kwa maslahi yetu sio ya mtu binafsi so hao walikuja na ndege kuangalia mshoroba huo Maasai hakujua maskini
 
Back
Top Bottom