DOKEZO Ndege za Dubai zinaendelea kutua Serengeti! Tunaibiwa

DOKEZO Ndege za Dubai zinaendelea kutua Serengeti! Tunaibiwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mungu uilinde nchi hii.
Pole yetu sote.

Lakini utasubiri sana kudhani Mungu atailinda nchi.

Hata hao wanaotunyang'anya wao pia wanamtegemea Mungu huyo huyo awalindie nchi yao na washirika wao..

Acha tu tuwe kitoweo, labda siku moja tutafika mahali tukatae upumbavu huu.
 
Iko Twitter
Acha kujitoa ufahamu
Nchi inaibiwa kuliko unavyojua
Madini wanyama imegeuka mali ya wachache
Msikomaze shingo
Katiba Mpya muhimu tufunge wezi
Nchi haikuanza kuibiwa leo kwa hiyo usipate tabu Watanzania wanajiibia wenyewe acheni wale kwa urefu wa kamba yao
 
Pori tengefu ni kama misitu ya jeshi inayotuzunguka nchi nzima, public access is off limits. Huwezi kupata close-up HD video ya ndege inashuka na kupandisha wanyama. Cameraman alifanya alichoweza katika mazingira yaliyomkabili.

"Iacheni serikali yetu itutumikie" ni mentality za Mtanzania wa pre-1990. Muda umekuacha nyuma.

Enzi hizi wananchi wanachagizwa kujihusisha na majadiliano huru ya mambo yanayowahusu kama sehemu ya mchakato wa demokrasia.

Binafsi siamini watawala kutoka visiwani wana uchungu na Tanganyika.
Camera man huyo huyo aligundua kwamba ndege haina alama?
Kweli mnataka tuamini ndege zisizosajiliwa ndio zinatua kuchukua wanyama.
Huu ujinga na kutofikiri na ubaguzi mtaacha lini?
 
Ila kiukweli kuna kaupendeleo ka waarabu awamu hii.
Hata uingizwaji wa mafuta ya kupikia kutoka nje ya nchi awamu hii ni hao hao waarabu, sera ya kulinda viwanda vidogo vidogo vya alizet vya wazawa imewekwa kapuni.
Hakuna tena protectinism, wakulima wazawa wapate taabu kwa bei ya alizet yao kuporomoka kwa faida ya waarabu!.
Leta ushahidi wa kutosha kuunga mkono hoja yako.JF sio kikao cha mbege kwamba tutaamini tu madai yako.
Kama una ushahidi leta.
 
Leta ushahidi wa kutosha kuunga mkono hoja yako.JF sio kikao cha mbege kwamba tutaamini tu madai yako.
Kama una ushahidi leta.
Miaka yote waingiza mafuta au wafanya biashara nchi hii ni watu weupe kama ni upendeleo sio mafuta tu hata mabisi maroli viwanda nk hata vituo viama futa ya magali robo 3 viakwao
 
Hii tabia ya kuleta habari za uzushi hapa jukwaani siku hizi inanikera sana, watanzania wenyewe ndio sisi wezi vibaya mno! hii hali ya ufisadi na ubadhirifu kwenye miradi yote tunayoisikia wasababishi ni sisi wenyewe serikali imetekeleza wajibu wake wa kupeleka fedha sisi wenye dhamana ndio majambazi wakubwa, jambo la kusikitisha sana.
 
Sasa mtu kama wewe hata kuandika lugha yako tu kwa ufasaha huwezi,utaweza kujadili vitu vinavyohitaji akili na maarifa ya utambuzi?
Huu muda unaoutumia kutapika hapa ni vizuri ukautumia kujifundisha kuandika lugha yako kwa ufasaha.
Ngoja nimtafute muisihamu wa kiarabu aje kunifunza lugha.....niachane na kiswaili na mimi niwe najua kiswahili
 
Hii Nchi , sijui ihamishiwe sayari ya kipekee. Wanyama wanauzwa Bei zinafahamika hata wewe unaweza Kununua. Mia 2 iliopita Rwanda wamefikisha Faru 10 kwenye Akagera national park. Je hao walio wagawia majirani zetu hawawqpendi?

Lakini pia mtakiwa mjue Hawa wanyama wanazaliana wanaugua na wanakufa , Bado tuna na ujangiri.
Yawezekana huko wanako enda siku moja wakaja kuturudishia kama wataweza kuishi.
 
Wewe Kwa uelewa wako ndege zinazotua mbugani zote ni za waarabu na zote zinakuja kubeba wanyama?...huko mbugani hakuna ndege zinazotua Kwa utalii wala kubeba wazungu?
Mleta mada ndiye aliye iona hiyo ndege na ndiye Aliyesema inabeba wanyama. Sasa nyie mnaobisha matumia ushahidi gani. Ningeelewa tu kama mngethibitisha haikuja kubeba wanyama bali imekuja kwa masuala mengine. Alternatively, mngeomba ushahidi zaidi ingawa Inawezekana kabisa asiweze kuupata kwa sababu ya ulinzi mkali kwenye haya mambo.
 
Unaibiwa nini?

Nani anayekuibia?

We badala ufanye kazi unalia unaibiwa na kitu kisichokufaidisha
 
Ingawa picha haionekani clear, ila chini ya uongozi wa Mama lolote linawezekana!.
Huyo mama amemilikishwa hii Nchi? Kwamba Ndege zinakuja zinatua zinapakia zinaondoka bila utaratibu wowote? Bas kama Nchi imefika hapo kosa sio lake Bali Mifumo mibovu. Nawewe tafuta hata mikumi ujimegee Anza kuua hata Swala uza kwa mafungu.
 
Back
Top Bottom