Ndege za Tanzania zapigwa marufuku kutua viwanja vya Kenya kutokana na janga la Corona

Ndege za Tanzania zapigwa marufuku kutua viwanja vya Kenya kutokana na janga la Corona

Asante kwa maelezo mazuri. Pia tambua inawezekana hivyo kwa sababu ya KQ, ila umeshajiuliza kwa uamuzi huo itakuwaje TZ ikaizuia KQ kuja bongo nani ata athirika zaidi? Kwamb kuwe na link ya Bole to Dar airport. ATCL na Ethiopia wafanye hiyo service. Nani anamuhitaji mwenzie zaidi katika usafiri wa anga kati ya TZ na ke?
Nchi zote mbili zinategemeana na nitakupa mfano. Kenya wanaitegemea Tanzania kwa abiria wake kusafiri na KQ kutokea JKNIA hadi Nairobi na hatimaye kuunganisha kwenda wanakotaka pia Tanzania inaitegemea Kenya kwa kukuza mapato pale ambapo ndege zake zinapotua katika viwanja vyake.

Ila kwa ishu ya Corona ilivyochukuliwa Tanzania sitashangaa kuona tunapigwa ban zaidi na kuathirika pakubwa. Nadhani ulisoma pia tangazo la nchi ya Dubai kuhusu watanzania wanaotaka kuingia huko kuanzia kesho. Kenya ingetaka kufanya usanii kama sisi wala wasingeshindwa ila walijiangalia hasa kwenye mambo ya usafiri wao wa anga na utalii ikabidi wawe wazi ili hata itakapoanza kupungua Corona then takwimu ziwe za wazi pia.

Sisi ni kama tulichekesha tena kichekesho cha kitoto pale ambapo usiku mmoja tulikuwa na cases zaidi ya 500 na vifo 16 halafu ghafla hakuna tena kitu au tangazo lenye data zilizothibitishwa kutoka wizarani! Hicho ni kichekesho tena cha aina yake mkuu.
 
Yaani mtu mwenye umri mkubwa kama mzee mkapa leo hii inakuwa ajabu kufariki,basi itakuwa ni corona tu.

Huu wimbo umekosa radha hata hao viongozi wenu wameamua kuachana nao,nyumbu bado mnaimba tu.

Nini kilichomuua? Kama sio COVID 19
 
Ndo maana nikakuuliza kwamba:-Hujajibu hilo swali! Na hakuna aliyekataa kwamba hakuna mashirika yanayotumia JKIA lakini usidhani international rooutes zinaanzishwa kirahisi rahisi tu kama unavyodhani!

Hizo daladala zenyewe huwezi tu kwenda pale SUMATRA ukatarajia utapewa route unayoitaka kama unavyoenda Kariakoo kuulizia shati utakalo, seuze international routes!!

And this's not all about Airline X kutaka Route Y, but it's all about business! Airline haiwezi tu kuanzisha safari mpya to TZ simply Tanzania finally wana uwanja mkubwa but watakachofanya ni kuangalia business potential in the region!!! Na huwezi tu kuanzisha direct route kwa kutegemea Watalii wa Msimu kama nchi husika hakuna enough socio-economic activities zinazovutia wageni throught the air!!

Ni kutokana na ukweli huo ndio maana mashirika mengi ya ndege yanafanya collabo ya kutoa abiria from Airport X to Airport Y kwenda kubadili ndege!!!

Na utakuwa unajidanganya kweli kweli kama unadhani eti kwavile hivi sasa tuna uwanja mkubwa zaidi ndo tayari JNIA kwa sasa inapokea wageni wengi zaidi kuliko uwanja wowote ule East Africa!!

Baada ya kwa East Africa, bado Bole International Airport iko mbali sana, huku wakifuatiwa na Jomo Kenyatta, na ndipo inakuja JNIA!

Naona maelezo mengi sana lakini content ni ndogo. Hiyo Jomo inakuwa maarufu sababu ya KQ. Ndege zinafanya hiyo collabo unayosema. Sasa TZ ikaizuia KQ kufika bongo sababu ya corona nani ataumia zaidi? Ishu hapa ni uamuzi kenya iliyochukua na athari zake katika sekta ya anga.

Nani anamtegemea mwenzake sana katika biashara ya anga kati ya ke na TZ
 
Nchi zote mbili zinategemeana na nitakupa mfano. Kenya wanaitegemea Tanzania kwa abiria wake kusafiri na KQ kutokea JKNIA hadi Nairobi na hatimaye kuunganisha kwenda wanakotaka pia Tanzania inaitegemea Kenya kwa kukuza mapato pale ambapo ndege zake zinapotua katika viwanja vyake.

Ila kwa ishu ya Corona ilivyochukuliwa Tanzania sitashangaa kuona tunapigwa ban zaidi na kuathirika pakubwa. Nadhani ulisoma pia tangazo la nchi ya Dubai kuhusu watanzania wanaotaka kuingia huko kuanzia kesho. Kenya ingetaka kufanya usanii kama sisi wala wasingeshindwa ila walijiangalia hasa kwenye mambo ya usafiri wao wa anga na utalii ikabidi wawe wazi ili hata itakapoanza kupungua Corona then takwimu ziwe za wazi pia.

Sisi ni kama tulichekesha tena kichekesho cha kitoto pale ambapo usiku mmoja tulikuwa na cases zaidi ya 500 na vifo 16 halafu ghafla hakuna tena kitu au tangazo lenye data zilizothibitishwa kutoka wizarani! Hicho ni kichekesho tena cha aina yake mkuu.

Tutapigwa ban na nani wakati watalii wanakuja bongo hapa? KQ kwa block hii ya EA inabebwa na route za Tz. Hivyo wao ndio wanatutegemea sisi zaidi.
 
Katika kutumia common sense sasa ndio useme hali ya ugonjwa iko vipi hapa nchini. Yani watu wana ambiwa wakaugulie nyumbani? Hizo oksijeni wanafungiwa huko nyumbani?

Kuwa serious mkuu, unaielewa covid mziki wake vizuri kweli?
Oksijeni zipi?! Hivi una habari hata wakati tunatangaza new cases kulikuwa na uhaba mkubwa sana wa ventilators! Hivi hufahamu mlivyoambiwa mpige nyungu ile ni alternative to ventilators kwa sababu inasaidia kuzibua njia za hewa na hivyo kumfanya mtu aweze kuhema vizuri?!

Na kama hujui kwamba wagonjwa wanaambiwa wakaugulie home basi inaonesha wazi you have no idea about what's going on!!!
 
Tutapigwa ban na nani wakati watalii wanakuja bongo hapa? KQ kwa block hii ya EA inabebwa na route za Tz. Hivyo wao ndio wanatutegemea sisi zaidi.
Hao watalii umewaona wapi mkuu? Hayo matangazo unayosikia ungeona uhalisia wake pengine ungefunguka akili.
 
Usiwe mpumbavu! Yani Mkapa afe kwa corona alafu system iruhusu viongozi wakuu wakae kihasara namna ile ikiwemo kumkumbatia mjane?

Hiyo system ndiyo iliyoruhusu kongamano lenu kule dodoma ambako milikopakalia hilo dude la kusababisha tatizo la upumuaji
 
Kupita Kenya kuelekea wapi? Kama hujui Ndege zao nyingi kuelekea Malawi, Zimbabwe, Zambia, Botswana, Rwanda na Burundi Lazima ziingie anga la Tanzania. Pia wanatua Mara nyingi kwa siku katika viwanja vya TZ (Dar, Kilimanjaro & Zanzibar) mfano, wastani wa Mara 42 kwa wiki pale JNIA tu
Kampuni yao kubwa sio kama hizi daladala zetu ambazo hazifikii idadi ya ndege alizokuwa amenunua Idd Amin Dada miaka ya 1970 huko Uganda.
 
Oksijeni zipi?! Hivi una habari hata wakati tunatangaza new cases kulikuwa na uhaba mkubwa sana wa ventilators! Hivi hufahamu mlivyoambiwa mpige nyungu ile ni alternative to ventilators kwa sababu inasaidia kuzibua njia za hewa na hivyo kumfanya mtu aweze kuhema vizuri?!

Na kama hujui kwamba wagonjwa wanaambiwa wakaugulie home basi inaonesha wazi you have no idea about what's going on!!!

Kwa hiyo kupiga nyungu ndio kumekomesha corona na kufanya watu wasilazwe kwa kushindwa kupumua sio? Hao wagonjwa wanaenda kuugulia nyumbani wakiwa katika stage gani sasa? Wewe binafsi umeshuhudia hayo? Ni wapi huko wanasema watu wakaugulie nyumbani mkuu? hii ni mpya kwangu.
 
Nini kilichomuua? Kama sio COVID 19
We jamaa ni MPUMBAVU SANA. Na system ikiwa inajua ni COVID19 wakaruhusu mtu Kama JK akae na Mkapa zaidi ya saa 1 wakiongea siku 1 kabla hajafa!?, Unatumia akili kufikiri?, mkiwa mnasikia uzushi muwe mnajiongeza sio mnafata mkumbo tu. Mkapa na amekufa na miaka 82 na zaidi ya nusu ya maisha yake amekuwa overweight akiishi maisha ya kifahari ya kula chochote anachopenda.Aliwahi kuugua gaut bado unaleta uzushi wa COVID19??,. Sometimes bora kukaa kimya kama huna information za uhakika.
 
Hao watalii umewaona wapi mkuu? Hayo matangazo unayosikia ungeona uhalisia wake pengine ungefunguka akili.

Nimewaona wakutosha mkuu, na hata hapa nilipo sasa nipo nao. Hata Vijiweni saivi hakuna tena vikao watu wako busy mlimani na porini huko. Wale wa mahotelini wamesharudi makazini.
 
Nimewaona wakutosha mkuu, na hata hapa nilipo sasa nipo nao. Hata Vijiweni saivi hakuna tena vikao watu wako busy mlimani na porini huko. Wale wa mahotelini wamesharudi makazini.
Duh labda wanakuja kwa mitumbwi. Haya bana
 
Ndugu yako akiwa na mapungufu, wa kwanza kumsitiri ni nani kati ya watu wa mbali au wewe ndugu yake!?

Wakenya hawakupaswa kuitangazia dunia jambo kama hili! Walipaswa kudeal na sisi kindugu yaan kaka yako anaumwa UKIMWI na kweli alifanya umalaya kwa makusudi lakini ni lazima umuuguze!

Wangetokea kutupigia debe kuwa Tanzania is a Corona free country mngeshangilia sana na kuona hiyo ndiyo sawa haswa?

Kwani kwa kuukimbia ukweli au kuuficha ugonjwa huu kutasaidia au kumesaidia nini kutuepusha nao?

Tunamwona Kenya tu? Yuko wapi aliyestufia au hata kutambua tu jitihada zetu hizo kwenye kupambana na huu ugonjwa?

Yuko wapi hata mmoja anayepiga nyungu kama sisi kwamba tumemvutia?

Kwamba mchawi ni Kenya? Tusitafute visingizio, mchawi anafahamika, anajijua na yuko baina yetu.

Mengine haya ni kelele za vyura tu.
 
Ama kwa hakika mambo si shwari. Naona ndege za Tanzania nazo zimeanza kupata hitilafu kama ile ya Kenya

---

Akizungumza jijini Nairobi wakati akitoa taarifa kuhusu mwendendo wa maambukizi ya janga la Covid-19 nchini Kenya, Waziri wa Usafirishaji James Macharia amesema kuwa anga la Kenya halitafunguliwa kwa kila mtu. Orodha ikionesha wazi Tanzania ikiwa si mmoja wa nchi inayokaribishwa kwenye anga ya Kenya.

Macharia amesema ni raia wa nchi 11 pekee wa kigeni ndio watakaoruhusiwa kutua Kenya katika viwanja vyake vinne vya kimataifa vilivyopo Nairobi, Mombasa, Eldoret na Kisumu.

Nchi zilizoruhusiwa ni China, Korea Kusini, Japan, Canada, Zimbabwe, Ethiopia, Switzerland, Uganda, Rwanda, Namibia na Morocco.
Waziri huyo amesema nchi hizo zimedhibiti janga la Covid- 19 kwa kiasi cha kuridhidha.

Amesema nchi hizo zimepunguza maambukizi ya ugonjwa huo na raia wake wamekuwa wakipata dalili za kawaida za ugonjwa wa mfumo wa upumuaji.

''Tutaendelea kuboresha orodha yetu kwa kutegemea na hali ilivyo na mazingira. Hii ni orodha yetu kwa leo tutaipitia tena kesho na siku zinazokuja.''

''Abiria wote watakaowasili kwa ndege za kimataifa wakiwa na hati zinazoonesha kuwa hawana dalili za Covid-19 na wale waliopima saa 96 kabla ya safari hawatakaa karantini,'' alisema.

Mara tu orodha ilipotolewa, Wakenya kwa haraka waligundua kuwa Tanzania haimo.

Siku ya Jumatatu tarehe 27 mwezi Julai, Rais Uhuru Kenyatta alitoa kauli ambayo haikuilenga Tanzania moja kwa moja kuwa Kenya haifichi idadi ya watu wenye maambukizi ya Covid-19.

''Sisi tuko wazi na tunajua fika kuwa ugonjwa huu upo tofauti na majirani zetu ambao wanauficha ukweli huu,'' alisema Rais Kenyatta.

Chanzo: BBC
Kwani lazima twende Kenya kwa ndege, njia za panya zipo
 
Naona maelezo mengi sana lakini content ni ndogo. Hiyo Jomo inakuwa maarufu sababu ya KQ. Ndege zinafanya hiyo collabo unayosema. Sasa TZ ikaizuia KQ kufika bongo sababu ya corona nani ataumia zaidi? Ishu hapa ni uamuzi kenya iliyochukua na athari zake katika sekta ya anga.

Nani anamtegemea mwenzake sana katika biashara ya anga kati ya ke na TZ
Look at you! Eti Jomo Kenyatta ni maarufu kwa sababu ya KQ!! Sasa unatarajia JNIA imeipiku Jomo Kenyatta kwa sababu zipi?! Kwa ile dreamliner moja, au?!

Again, kwahiyo kama ndege mathalani ina direct route from Heathrow Airport to Jomo Kenyatta, hivi sasa itafuta hiyo route kwa sababu KQ zimepigwa ban kutua Tanzania?!

Kuhusu nani ataumia zaidi, whether you like it or not TZ ndo wataumia coz' Watalii wengi wataishia KE coz' KE kuna Tour Agents wengi zaidi compared to TZ, na wao wataongea lugha nyepesi tu: The COVID-19 Status in Tanzania is unknown kwa sababu serikali inaficha takwimu!!

Watalii wenyewe wakijaribu ku-verify kuhusu COVID-19 watakuta no data since May!!! So, unless kama mnadhani Watalii ni wajinga wa kuamini TZ hakuna COVID-19 kwa sababu mlifanya maombi na kupiga nyungu, then YES, Wataunga unga ndege hadi TZ bila kupitia KE!
 
We jamaa ni MPUMBAVU SANA. Na system ikiwa inajua ni COVID19 wakaruhusu mtu Kama JK akae na Mkapa zaidi ya saa 1 wakiongea siku 1 kabla hajafa!?, Unatumia akili kufikiri?, mkiwa mnasikia uzushi muwe mnajiongeza sio mnafata mkumbo tu. Mkapa na amekufa na miaka 82 na zaidi ya nusu ya maisha yake amekuwa overweight akiishi maisha ya kifahari ya kula chochote anachopenda.Aliwahi kuugua gaut bado unaleta uzushi wa COVID19??,. Sometimes bora kukaa kimya kama huna information za uhakika.

Unajua tatizo la upumuaji linavyoattack wazee? Alafu nimekubali mimi kwako kuwa mpumbavu sababu hunijui. COVID 19 mliipakaa kule Dodoma kwenye kongamano lenu mnaloliita uchaguzi kama mlivyopakaa kipindi cha kuzindua TBC ARIDHIO. Kuna siku mtajua kuwa tu hamjui na mtatukuta huku.
 
Back
Top Bottom