G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,795
- 36,704
- Thread starter
- #121
Nchi zote mbili zinategemeana na nitakupa mfano. Kenya wanaitegemea Tanzania kwa abiria wake kusafiri na KQ kutokea JKNIA hadi Nairobi na hatimaye kuunganisha kwenda wanakotaka pia Tanzania inaitegemea Kenya kwa kukuza mapato pale ambapo ndege zake zinapotua katika viwanja vyake.Asante kwa maelezo mazuri. Pia tambua inawezekana hivyo kwa sababu ya KQ, ila umeshajiuliza kwa uamuzi huo itakuwaje TZ ikaizuia KQ kuja bongo nani ata athirika zaidi? Kwamb kuwe na link ya Bole to Dar airport. ATCL na Ethiopia wafanye hiyo service. Nani anamuhitaji mwenzie zaidi katika usafiri wa anga kati ya TZ na ke?
Ila kwa ishu ya Corona ilivyochukuliwa Tanzania sitashangaa kuona tunapigwa ban zaidi na kuathirika pakubwa. Nadhani ulisoma pia tangazo la nchi ya Dubai kuhusu watanzania wanaotaka kuingia huko kuanzia kesho. Kenya ingetaka kufanya usanii kama sisi wala wasingeshindwa ila walijiangalia hasa kwenye mambo ya usafiri wao wa anga na utalii ikabidi wawe wazi ili hata itakapoanza kupungua Corona then takwimu ziwe za wazi pia.
Sisi ni kama tulichekesha tena kichekesho cha kitoto pale ambapo usiku mmoja tulikuwa na cases zaidi ya 500 na vifo 16 halafu ghafla hakuna tena kitu au tangazo lenye data zilizothibitishwa kutoka wizarani! Hicho ni kichekesho tena cha aina yake mkuu.