Ndege za Tanzania zapigwa marufuku kutua viwanja vya Kenya kutokana na janga la Corona

Mbona Tz haijatajwa? Msitafute uchonganishi. Hapa ni issue ya kisayansi, Tz Haina udhibiti madhubuti wa Corona, watu hawavai barakoa wala kupima, Sasa ulitegemea Nani akaribishe contaminated people kwake? Hata Burundi watawatimua
 
Kunyaland hawatubabaishi kwenye malori mbona walinyoosha mkono!!? Waendelee na Covid-19 yao sisi mbona tumeshasahau kama kuna Covid-19
 
Mlishasema sana tu lakini tunadunda tu!
 
Tunasubiri tamko la mkuu wa mkoa wa kilimanjaro kuhusu kadhia hii. i
 
We jamaa tangu April ukionaga story za Corona unashupaza shingo sana. Ulikomaa na lockdown weeeee mpaka ukajiona mjinga. Shule zimefunguliwa tangu July mpaka leo shwari tu. Mmebaki mnaokoteza maneno tu. Last week watu wamejaa uwanja wa Mkapa kumuaga Ila hakuna cha mlipuko wa COVID19 wala nini., Mmejazana airport kumpokea Lissu na hakuna cha COVID19 wala nini. Bado unakomaa na Corona tu????, Huonagi aibu mkuu?.. Tanzania hakuna Corona, kama mnaipenda sana CORONA si muhamie huko KENYA??
 

Tanzania locked out as Kenya resumes international flights
 
Hao watalii umewaona wapi mkuu? Hayo matangazo unayosikia ungeona uhalisia wake pengine ungefunguka akili.
Wewe nyang'ao tuliza mshono! Mtanyooka tu kama mlivyonyooka kwenye malori. By the way mashirika mangapi ya TZ yanayoenda Kenya kama siyo Precision Air tu ambayo KQ wana share?
 
Kamanda Twambie huo ugonjwa Tanzania uko wapi? Hahahahahhaha au kuna ndugu yako anaumwa?
Jamaa mshenzi sana!

Sijui kwanini anafurahia sana habari za corona!

Alishaweka utabiri wake wa vifo vya maelfu ukabuma. Ana hasira balaa!
 
Nimekwambia utumie common sense, nimekuuliza Mkapa angekuwa na Corona wangeruhusu mtu Kama Kikwete aonane nae waongee ana kwa ana zaidi ya saa 1 siku 1 kabla hajafa??!??, Jibu hili swali, kama huwezi jibu hili swali ndo sababu ya kukuita MPUMBAVU, sihitaji kukujua ndo nitambue upeo wako wa kufikiri. Michango yako tu humu inaonyesha unachokiwaza.
 

Mkuu Wewe Ni Mtanzania kwanza au mpinzani kwanza.
 
Kwa kupindisha maneno hamjambo sijaona zilipotajwa ndege za Tanzania bali ni nchi zilizoruhusiwa raia wa nchi 11,ungeandika basi hata kuwa Dar Exoress, Tahmid bus na mengine hayaruhusiwi kuingia Kenya
 
Katika kutumia common sense sasa ndio useme hali ya ugonjwa iko vipi hapa nchini. Yani watu wana ambiwa wakaugulie nyumbani? Hizo oksijeni wanafungiwa huko nyumbani?

Kuwa serious mkuu, unaielewa covid mziki wake vizuri kweli?
Tatizo la corona ni kwamba ukipima watu ndio utawakuta wanayo hiyo corona japo hawaugui kwa maana ni wazima kabisa,ndio hata Tz wakati ule tunapima watu basi case za waliyokuwa na corona ilikuwa inazidi tu japo watu hawaugui. Mfano humu kwenye nyumba za ibada mwanzoni walikuwa kidogo walikuwa wanazingatia masuala ya kuacha distance na kunawa mikono ila sasa kama humu misikitini hivyo vitu havipo tena hakuna kuachiana nafasi wala uzingatiaji wa kunawa mikono na sabuni.
Ni wazi tungeanza kuona athari za corona huko kwa maana wangekuwepo wengi wenye kuugua kwa wingi na hata ongezeko la vifo hasa ukizingatia huko kuna idadi kubwa ya wazee na wengine wagonjwa na nyumba za ibada watu wanajuana wangeona tu athari kwa uwepo wa waumini wengi kuugua na vifo.
 
Hivi unaelewa wewe?! Kuna mahali nimesema corona imekoma hadi uhoji ina maana nasema nyungu imekomesha corona?

Kama hawaugulii nyumbani, weka hapa coronavirus data! Hata ZERO Case na yenyewe ni Data! Mbona hutoi?! How come unasema hakuna corona wakati serikali imeacha kutoa data na kwa upande mwingine bado madereva wanarudishwa mipakani baada ya kuonekana +Ve?!


Narudia, June 26, Wizara ya Afya ya Uganda walisema:=


Hizo ndo official data kutoka nchi ambazo HAZIDANGANYI watu wake!!! Na kama nilivyopata kusema miezi ya nyuma, kuficha takwimu ni bad move kwa sababu kila mmoja anafahamu COVID-19 ipo duniani kwahiyo no country would be judged kwa kuwa na cases nyingi, but countries will be judged by their level of transparency over the issue!!

Bora ya Shetani Unayemjua kuliko Malaika Usiyemjua! Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuamini eti TZ hakuna COVID-19 kwavile walifanya maombi!!! So, dunia bado itaendelea kuiona Tanzania kama nchi inayoficha tatizo!!

Stay blessed... endelea kuimba mapambio, am out!!
 

Direct flight from Heathrow To Jomo airport sawa itakuwepo ila from Jomo to Tz ndio hapo flight route za KQ zinatolewa. Halafu watalii sio wajinga kwamba utawadanganya tu kiuwepesi. Kumbuka hao watalii wana mawakala wao huku ambao ni raia wa huko kwao. Ndio ma leader kwenye msafara huo wa watalii. Hivyo hali ya TZ wanaijua vizuri wakiwa huko huko kwao.

Na hao ma Agents wa ke ndio itakuwa target sasa kwa bongo maana wao ndio wanaowadanganya watalii washukie ke, unadhani serikali ikiwaongezea kodi ma agent na watalii kutokea kenya bado watalii wata prefer kushukia kenya?
 
Kenya hauwezi kunyooshwa na Tanzania kwa lolote lile hata pamoja na kutokuwapo gonjwa la Covid-19 na kuwa na ugonjwa wa moyo tu. Kiwanja world class anachosema huyu mjinga hakishindani kwa lolote na Kenyatta International Airport cha Nairobi jiji lenye hotel za kitalii za kimataifa nyingi kuliko zilizopo Tanzania nzima ikiwa ni pamoja na zile za Zanzibar we, Arusha mji muhimu Kanda ya utalii, ina hotel moja tu ya kimataifa iliyofinguliwa mwaka Jana zinazobaki ni Mangi Guest Houses. Mombasa mahoteli karibu yote ya kitalii ufukweni ni ya kimataifa na madege yanayoleta watalii kwenye mji huo karibu yote ni Charter tu. Ule Uwanja wa kimataifa wa Eldoret ni kwa ndege za mizigo tu sisi hata mbuzi zinasafirishwa kupitia 'world class' airports. JNIA cha Dar chenye uwezo wa kusafirisha abiria milioni 5 tu kwa mwaka kwenye nchi yenye watu milioni 60 ni kakiwanja kadogo sana kangefaa kuwa Chato au Mwanza.
 
Tangia wafunge mipaka Yao kipindi chote Cha Corona, Tanzania imeathirikaje kiuchumi

Kwakuwa kulikuwa na biashara baina ya nchi hizi mbili, kwa vyovyote imeathirika na hali hiyo. Huenda hujui unachokiongea ndio maana unasema hivyo. Kuathirika kupo, labda uzungumzie imeathirika kwa kiwango gani, na sio imeathirikaje.
 
Inaonekana hata kutumia ndege hasa international flights hujawahi au mara chache sana umesafiri nje ya TZ. Unaposema direct flights from where to where? Hapa TZ kuna direct flights from Dar to Dubai, Amsterdam etc. ambako ndiko kwenye hub ya kwenda US na sehemu nyingine duniani. Sasa unaposema eti lazima uende Nairobi wakati kuna mashirika mengi tu yanayokuja Dar ya direct flights to those hubs mentioned above yakiwemo KLM, etc.
 

Kwako hiyo tweet ndio reliable source kwamba TZ ipo corona? Nimekuuliza mziki wa corona unaujua kweli au unausikia tu? UNajua mfano kenya hapo hospitali zimejaa wagonjwa na bado vifo vipo juu? unajua ni wahudumu wangapi wa afya wameathirika hadi sasa huko kenya?

Sasa ndio hapa kwetu unasema watu wanaugulia nyumbani, wanauguzwa na kina nani ambao hawana hata ABC za maswala ya afya na namna ya kujikinga? Si kungekuwa na mlipuko mkubwa sana ndani ya jamii? Hapa naona wewe ndio unaimbishwa pambio bila kujitambua.
 

Unaifahamu vyema biashara ya utalii, na ni kwa jinsi gani Kenya ni gateway ya watalii hapa nchini? Napenda nifahamu kama unajua hilo ili tuwe na uelewa wa pamoja. Isije ikawa unaongozwa na uzalendo academia na sio facts.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…