Ndege zashindwa kutua KIA kisa taa za runway kutofanya kazi, KLM yaenda kutua Entebbe

Ndege zashindwa kutua KIA kisa taa za runway kutofanya kazi, KLM yaenda kutua Entebbe

Hivi serikali kwanini inaendele kutoa ajira kwa watu hovyo kama hawa. Yaani hata airport ya Kia parking lot wameshindwa kutengenezaza. Hawa wakuu wa mashirika ni ulaji tu kwenda mbele.
 
View attachment 2578766

Ndege ya KLM kutoka Amsterdam imeshindwa kutua uwanja wa ndege wa KIA masaa machache yaliyopita na kusababisha watalii na watu wengine karibu 150 kushindwa kuingia nchini.

Ndege hiyo ililazimika kwenda kutua Entebbe ambako taa zilikuwa zinaangaza kwa manjonjo yote. Pamoja na watu wazima wengi ndege hiyo imebeba wamama wajawazito, watoto na wazee ambao sasa wanahangaika kutafuta usafiri wa haraka.

Haieleweki tatizo ni taa au umeme au upepo. Kuna watu wengine wamesikika wakilitaja Jina la yule Marehemu Mpendwa, wakionesha kusikitishwa na Tanzania kuzidiwa na umeme wa Jinja.
taa zimeangaza kwa manjonjo yote ? hahahaaaa
 
Kwa Precision Air tulitaarifiwa kuwa ndege ingechelewa kuondoka KIA kuelekea Mwanza..

... baadae nikapigiwa simu kwa mabadiliko mengine na tulipofika Uwanjani tukapewa taarifa kwa mabadiliko mengine tena na kuambiwa tatizo la taa lililotokea usiku...na hivyo tungeondoka saa nane...

.. lakini tulipokuwa sehemu ya kusubiria, tukapewa taaraifa na kuombwa radhi kwa sababu ya mabadiliko mengine zaidi.....na abiria wote wakapatiwa lunch bure, ilipofika saa tisa tukaondoka kuelekea Mwanza.

Ingawa tulichelewa angalao Precision walijitahidi kutupa updates na kutujali kwa lunch.
 
Wataalam mtusaidie why iende Jinja huko Entebe, sio wanatazama nearby airport?!
Nilidhania Nairobi au Unguja au Nyerere Dar!!!
 
NA JANA TENA LIMESHINDWA KUTUA HII NI AIBU NA BADO KUNA MAJITU, YANA ROL V8 HUKU YANAPANGUSA I PHONE 14 KWENYE KITAMBI AMBACHO KIMEFUNIKWA NA SUTI MARIDADI KUTOKA ITALY. Mungu tunusuru na hizi aibu.
 
NA JANA TENA LIMESHINDWA KUTUA HII NI AIBU NA BADO KUNA MAJITU, YANA ROL V8 HUKU YANAPANGUSA I PHONE 14 KWENYE KITAMBI AMBACHO KIMEFUNIKWA NA SUTI MARIDADI KUTOKA ITALY. Mungu tunusuru na hizi aibu.
Dodoma Sasa Zinatua Usiku
 
RAIS ANAJITAHIDI MNO, WASAIDIZI WAKE NAO WANAMSAIDIA KWA NAMNA YA KIPEKEE, HAO WASAIDIZI WAKE WADUMU WADUMU WADUMU ZAIDI NA ZAIDI MAOFISINI.
 
Wanabodi, hii imetokea jioni hii, mpaka sasa ndege zimeshindwa kutua KIA, chanzo kikiwa kutokufanya kazi kwa taa za runway.

Precison iliyotoka Dar jioni hii imekua re routed to Nairobi as we speak, wameambiwa matengenezo might take up to 5 hours.

Wahusika changamkeni kurekebisha tatizo.


=======

UPDATES;

=======

Alipotafutwa kutoa ufafanuzi juu ya taarifa hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uendeshaji na Uendelezaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro wa Kia (KADCO), Christine Mwakatobe amesema amesikiliza swali kisha akasema yupo kikaoni na kukata simu.

Hata alipotafutwa baadaye kwa kupigiwa simu na kutumiwa ujumbe wa maandishi (SMS) hakutoa ushirikiano.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa, amethibitisha Taa za njia ya ndege zilizima kuanzia saa moja Usiku hadi saa tano Usiku kutokana na Mvua nyingi zinazoendelea kunyesha na kuathiri miundombinu.

Ndege iliyokuwa itue muda huo, ililazimika kwenda kutua Entebbe Nchini Uganda.

Hakuna abiria hata mmoja aliyetelekezwa na na Wote watarudi Tanzania.

Ameongeza Uwanja wa KIA baada ya kufanyiwa Marekebisho, kuanzia jana Usiku saa tano na nusu hadi sasa Uwanja unafanya kazi kama kawaida.
View attachment 2578583
View attachment 2578472View attachment 2578473View attachment 2578474View attachment 2578475
Watanzania siku hizi wanachat kimalkia😁😁😁😁
 
Hii ni aibu kubwa sana Kwa taifa lililo Uchumi wa kati.
Tanesco walizingua,Je hamna generators.?
NB..Hali ya hewa imesingiziwa
 
Back
Top Bottom