Ndege zilizotengenezwa Tanzania, zinauzwa milioni 500, Kwa bei hii wewe tu 'Upae au daladala'

Ndege zilizotengenezwa Tanzania, zinauzwa milioni 500, Kwa bei hii wewe tu 'Upae au daladala'

Thamani ya ndege moja aina ya Skyleader 600 ambayo imetengenezwa nchini Tanzania, imetajwa kuwa ni zaidi ya Dola za kimarekani 220,000 sawa na shilingi milioni 500 za Kitanzania.

Gharama Thamani ya ndege moja aina ya Skyleader 600 ambayo imetengenezwa nchini Tanzania, imetajwa kuwa ni zaidi ya Dola za kimarekani 220,000 sawa na shilingi milioni 500 za Kitanzania,

Bei inayolinganishwa na gari zenye gharama kubwa zaidi kama vile V8 land cruiser, defender na Range rover.

Afisa Mawasiliano kwa umma katika kampuni ya utengenezaji wa ndege hizo ya Airplanes Africa Limited, Bw. Freddie Monento ametoa ufafanuzi huo katika kipindi cha "Wekeza Tanzania" ambapo ameweka wazi kuwa kwa sasa ndege hizo zinavibali na zimethibitishwa kuruka.
View attachment 3218902
Kuna kipindi zamani wakati naanza kazi nilipewa kazi ya kununua printers za ofisini na bosi wangu.

Basi nikawa natafuta printers zenye bei nafuu na ubora mkubwa.

Bosi wangu kama alijua nitafanya hivyo, akaniambia unavyonunua printers, usiangalie bei na ubora wa printer tu, angalia na running costs za hiyo printer, angalia bei ya wino na huo wino unadumu kwa muda gani.

Nilivyokuja kuangalia na hilo jambo, nikakuta printers zilizofaa kununuliwa zilikuja tofauti na zile nilizotaka kununua mara ya kwanza.

Milioni 500 watu wanaweza kuwa nazo, hiyo inaweza kuwa bei ya magari mawili tu.

Sasa, swali la running cost linabaki pale pale. Bei ya mafuta? Mshahara wa rubani? Gharama za viwanja vya ndege? Bima je?
 
Nasubilia kwa shemeji zangu wachaga na wakinga ................ila mkipanda hizo viruka kasi maana sio ndege msisahau basi kuandika urithi kuepusha magomvi ya kifamilia
 
Kwa komenti hizi bora viwanda vyote iwe ndege, magari hadi kiberiti vibaki huko huko ulaya na china.

African we're nothing!.
Pole.
 
Hizo ni glider zenye engine, ikiwekewa engine inaitwa motor glider, hakuna ndege hapo, kuna glider hazina engine zinaruka na mabawa pekee, na inaweza beba hadi watu wawili au mmoja na inaruka.

hq720.jpg

Wenyewe wanazichukua na kuongeza engine.

gliding-main.jpg.optimal.jpg

Tanzania hawana uwezo tengeneza ndege, hio ni glider iliyochangamka, na hizi glider zipo hadi zinatengenezwa na karatasi.
WENGINE WAMEFANYA UMEDHARAU,

LAKINI HAPOHAPO UNASEMA HATA TOOTHPICKS STICKS HATUWEZI KUTENGENEZA.

WEWE HIYO TIARA AU GLIDER UMESHAWAHI KUTENGENEZA?
 
Badala tukisapoti hiko kiwanda cha ndege ili kizidi kukua ndo kwanza watu wanakikosoa kwakuwa kimetengrnezwa na mtanzania mwenzetu. Tupende vya kwetu.
NI MAMBO YA KIJINGA SANA.
HAPO HIYO IKITENGENEZWA NJE WALA HAWAONI SHIDA.

MTANZANIA HAJUI ANALOTAKA.
 
Kwa komenti hizi bora viwanda vyote iwe ndege, magari hadi kiberiti vibaki huko huko ulaya na china.

African we're nothing!.
Pole.
Sad truth.
Wabongo tunajiunderrate hadi tunakera ndo maana tunakosa uthubutu wakuzalisha vya kwetu nilitegemea kuona comments zenye kujenga hicho kiwanda lakini watu wanakitukana.
 
Hizi ndege zipelekwe kupaki kwenye miji ambayo ina viwanja vya ndege ndogondogo zikapendezeshe viwanja hivyo visivyo na ndege za kutua mwaka mzima
 
Sad truth.
Wabongo tunajiunderrate hadi tunakera ndo maana tunakosa uthubutu wakuzalisha vya kwetu nilitegemea kuona comments zenye kujenga hicho kiwanda lakini watu wanakitukana.
Hawa hawa wanaokomenti ukiwafahamu age na body structure zao unaweza kuomba maji ya kunywa ndotoni.

Yaani hiki wanachoandika ni tofauti na hivyo nilivyoandika hapo!.
 
Nafikiria nilitaka kwenda kijijini nitashukia wapi?

Serikali watatoa kibali cha kutengeza runway yangu shambani kwangu
Utajenga airstrip yako binafsi kijijini shambani kwako, hiyo siyo airport.
Unapewa mashariti ukitimiza vigezo unapata kibali.
 
Thamani ya ndege moja aina ya Skyleader 600 ambayo imetengenezwa nchini Tanzania, imetajwa kuwa ni zaidi ya Dola za kimarekani 220,000 sawa na shilingi milioni 500 za Kitanzania.

Gharama Thamani ya ndege moja aina ya Skyleader 600 ambayo imetengenezwa nchini Tanzania, imetajwa kuwa ni zaidi ya Dola za kimarekani 220,000 sawa na shilingi milioni 500 za Kitanzania,

Bei inayolinganishwa na gari zenye gharama kubwa zaidi kama vile V8 land cruiser, defender na Range rover.

Afisa Mawasiliano kwa umma katika kampuni ya utengenezaji wa ndege hizo ya Airplanes Africa Limited, Bw. Freddie Monento ametoa ufafanuzi huo katika kipindi cha "Wekeza Tanzania" ambapo ameweka wazi kuwa kwa sasa ndege hizo zinavibali na zimethibitishwa kuruka.
View attachment 3218902
Hizi ni ndege ndogo zinazoundwa Morogoro Uwanja wa ndege. Ndege hizi ndogo zinazochukua abiria wawili kwa muda mrefu, zimekuwa zikiruka kila siku kutwa nzima kwenye anga ya jiji la Dar es Salaam.
Kwa wasioijua Morogoro, Morogoro ndege haziendi japokuwa upo uwanja wa ndege kwenye eneo linaloitwa Uwanja wa Ndege.
 
Hii inaonesha elimu ya watanzania ni zero maana wameshindwa kutofautisha kati ya kutengenezea na kuunganisha vipande vilivyotengenezwa tayari
Tofauti ya gari na ndege ni vifaa vya ndege kutoka nchi tofauti tofauti, mfano Boing'i ya Marekani injini imetoka Uingereza na zinatengenezwa na kampuni zinazotengeneza injini ya kufua umeme, usishangae. Ni aghari kiwanda kutengeneza vifaa vyote inavyovihitaji kutengenezea ndege zake, kutokana na uwepo wa Shirika la Viwango Duniani kumewezesha vifaa vya nchi moja kuingiliana na vya nchi nyingine kasoro vichwa vya wanaccm tu.
 
Back
Top Bottom