Ndg Polepole amekwishapoteza, asipotubu nafichua yote ya gizani

Ndg Polepole amekwishapoteza, asipotubu nafichua yote ya gizani

ruby garnet

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2017
Posts
2,922
Reaction score
3,916
Habari wa JF,

Siku nyingi sijafika humu. Leo nami ninene.

Ni kweli, nimesikiliza awamu zote mbili za mazungumzo ya Ndugu Polepole na wanahabari. Nimezitafakari sana, na haya ndiyo niliyoyaona:
  1. Kwamba hadi sasa, Polepole kwa namna yeyote, kwa hayo aliyoyasema, hayana madhara yeyote kwa CCM na mwenyekiti wao.
  2. Polepole asipotubu kutoka moyoni kwa wananchi yale yote waliyoyaasisi yeye na marehemu, hataeleweka vizuri kwa jamii. Yaani, atubu ukweli kwa mabaya ya CCM na marehemu, kisha aseme kwa uwazi nini na nani alifanya nini — hasa mauaji na utekaji wa wapinzani wa marehemu. Kisha aseme kabisa kwa dhati, katika uongozi wa Maza, kuwa katika maongozi yake mabaya haya yalitokea — mfano, mauaji — nani anayehusika, kwa black and white. Bila hilo, Watanzania wa kawaida hawatamuelewa.
  3. Kivuli cha kuwa alikuwa balozi, hivyo hataki kusema yote aliyoyajua akiwa balozi au katika uongozi wake, hakitoshi. Atambue kuwa amekwisha mwaga mboga. Hivyo, kitendo cha kujivua ubalozi tu, amepoteza credibility kwa Maza, na hakuna kingine cha kupoteza asipopambana kwa dhati kuyasema maovu yote aliyoyajua akiwa ndani. Atambue pia, akikaa nayo kimya, hata pata chochote katika serikali hii na ijayo pia. Atakufa na siri zake, na mateso juu yake ya kusaliti chama bila kuongea kwa wananchi. Atambue kuwa CCM anaishitaki kwa wananchi.
  4. Mapambano aliyoyaanzisha atambue kuwa yanahitaji nguvu ya umma na kuleta hofu kwa watawala. Hivyo, asipoyasema aliyoyapata kuyaona na kuyasikia akiwa huko na wadhalimu, jamii haitamuunga mkono, na hivyo atakuwa anapiga kelele hewani tu. Kujivua kwake itakuwa sawa na bure kabisa, na itaonesha ni uroho wa kutaka madaraka yeye na genge lake tu — si huruma kwa wananchi wa kawaida kutokana na udhalimu wanaotendewa na viongozi wao waliotokana na CCM.
  5. Polepole, usipolizungumzia suala la Lissu kwa kivuli cha kwamba lipo mahakamani, wakati wananchi wote wanatambua ni sehemu ya ukiukwaji wa haki za upinzani, wananchi wanakuona kama kwamba wewe ni mpinzani wa Maza, lakini siyo mpigania haki za Watanzania. Unaonekana ni msaka tonge tu, ambaye umekosa ulaji kwa Mama, unatafuta genge lako liingie madarakani ili ule vizuri.
  6. Mwisho, Polepole, wananchi ndiyo wanaweza kumuadhibu Maza kwa nguvu ya umma. Waeleze ufisadi wa bandari ilivyouzwa, mbuga za wanyama huko Ngorongoro — eleza kwa ushahidi, eleza ufisadi wote kwa nyaraka vizuri. Sisi wananchi tutamwajibisha Maza. Bila hivyo, ushafeli. CCM hii haiwezi kukuogopa kwa porojo tu. Umma ndiyo utachukua hatua kuinusuru nchi, na siyo Maza kujitoa kwa porojo za press zako.
Ujumbe huu umfikie mhusika, na ajitafakari vita aliyoianzisha na alipofikia. Hata kama ataficha kitu, hakitamusaidia katika vita hii. The loser is Polepole, asipokuwa serious na vita alivyovianzisha. Yeye ndo anapoteza.

Jumamosi njema.
 
Ww uwe na akili polepole alikuwa askari lini au usalama lini naje anachosema hakijafanywa na hao wasasa au kukiuka katiba haipo lipi anaongea uongo ,?acheni ujinga nyie kila kitu kipo bayana kwanini asiseme? Nakwanini munazima fb,kama anacho ongea siyo kweli?
 
Ww uwe na akili polepole alikuwa askari lini au usalama lini naje anachosema hakijafanywa na hao wasasa au kukiuka katiba haipo lipi anaongea uongo ,?acheni ujinga nyie kila kitu kipo bayana kwanini asiseme? Nakwanini munazima fb,kama anacho ongea siyo kweli?
Umesoma kweri?
 
Umma upi huo!? Huu unaoshabikia simba na Yanga
Habari WA JF
Siku nyingi sijafika humu, Leo Nani ninene.
Ni kweri nimesikiliza Awamu zote Mbili mazungumuzo ya Ndugu Pole Pole na Wana Habari . Nimezitafakri Sana na haya ndiyo niliyoyaona.
1. Kwamba Hadi sasa Pole Pole Kwa namna yeyote Kwa hayo aliyoyasema hayana mazara yeyote Kwa CCM na mwenyekiti wao.
2. Pole pole asipotubu kutoka Moyoni Kwa wananchi Yale yote waliyo yaasisi yenye na mwenda zake hataeleweka vizuri Kwa jamii. Yaani atubu ukweri Kwa mbaya CCM na mwenda zake kisha na aseme Kwa uwazi nini na Nani alifanya nini hasa mauaji ya kuteka kwa wapinzani wa mwenda zake, kisha aseme kabisa Kwa zati katika uongozi wa Maza kuwa katika maongozi yake mbaya yake haya , mfano mauaji Nani anafanya Kwa black and white. Bila Hilo watanzania wa kawaida hawatamuelewa.
3. Kivuli kuwa alikuwa balozi hivyo hataki kusema yote aliyoyajua akiwa balozi au katika uongozi wake. Atambue kuwa amekwisha mwaga mbonga hivyo kitendo cha kujihuzuru Tu ubalozi amepoteza credibility Kwa Maza hivyo hakuna kingine cha kupoteza asipopambana Kwa triki ya kuyasema maovu yote aliyoyajua akiwa ndani. Atambue pia akikaa nayo kimya hata pata chochote kile katika serikali hii na ijayo pia. Atakufa na Siri zake na mateso juu yake ya kusaliti chama bila kuongea Kwa Wananch. Atambue kuwa CCM naishitaki Kwa Wananch.

4. Mapambano aliyoyaazisha atambue kuwa yanahitaji nguvu ya umma na kuleta hofu Kwa watawala, hivyo asipoyasema aliyoyapata akiwa huko na wadhalimu jamii haitamuunga mkono na hivyo atakuwa anajirisha upepo Tu. Na kujihuzuru kwake itakuwa Sawa na bure kabisa na itaonesha ni uroho wa kutaka madaraka yeye na genge lake tu si huruma Kwa wananchi wa kawaida kutokana na udhalimu wanaotendewa na viongozi wao waliotokana na CCM.
5. Pole pole usipolizungumuzia swala la Lisu Kwa kivuli cha kwamba lipo mahamani wakati wananchi wote wanatambua ni sehemu ya ukiukwaji wa haki za upinzani. Wananchi wanakuona kama kwamba. Wewe ni mpinzani WA maza lakini siyo mpigania haki za watanzania. Unaonekana ni msaka tonge tu ambaye umekosa ulaji Kwa mama unatafuta genge lako liingie madarakani ili ule vizuri.
6. Mwisho pole pole wananchi ndiyo wanaweza kumuazibu Maza Kwa nguvu ya umma. Waeleze ufisadi wa bandali ilivyouzwa, mbuga za wanyama huko ngorongoro, eleza Kwa evidence, eleza ufisadi wote Kwa nyaraka vizuri. Sisi wananchi tutamwajibisha Maza, bila hivyo ushafeli CCM hii haiwezi kukuogopa Kwa porojo tu. Umma ndiyo utachukua Hatua kuinusuru Inch na siyo Maza atajitoa Kwa porojo za press zako.


Ujumbe huu umfikie mhusika na ajitafakari vita aliyoianzisha na alipofikia hata kama ataficha kitu hakitamusaidia katika vita hii. The losser is Pole Pole asipokuwa serious na vita alivyoviazisha yeye ndo anapoteza
Jumamosi njema.
 
Ndio Kwanza kafika 50%, wananchi tupo Polepole,
Na ukiangalia wimbi lake kama tsunami!
Ndiyo, afungue turbo kabisa. Maswa mala hili ni kosa kulisemea siyo sahihi, cama dollar kinatenda kinyume ya Sheria katika maswala mengi Sana hivyo unapaswa kudiri nao hivyo hivyo. Ukiremba unapotea mwenyewe
 
Kwani kipindi cha magu, mama nae si alikua kiongozi?

Polepole hawezi kusema sana kuhusu serikali kwa sababu kuna viapo vya utumishi, usipofuata kiapo unaeza kuhukumiwa miaka 20 jela
Kwa kitendo alichofanya cha kujihuzuru Kwa barua Ile hata asiposema atakuwa Sawa Sawa na kwamba yupo gerezani Tu. Bora aseme afe kuriko kukaa kimya akafa
 
Back
Top Bottom