Habari wa JF,
Siku nyingi sijafika humu. Leo nami ninene.
Ni kweli, nimesikiliza awamu zote mbili za mazungumzo ya Ndugu Polepole na wanahabari. Nimezitafakari sana, na haya ndiyo niliyoyaona:
- Kwamba hadi sasa, Polepole kwa namna yeyote, kwa hayo aliyoyasema, hayana madhara yeyote kwa CCM na mwenyekiti wao.
- Polepole asipotubu kutoka moyoni kwa wananchi yale yote waliyoyaasisi yeye na marehemu, hataeleweka vizuri kwa jamii. Yaani, atubu ukweli kwa mabaya ya CCM na marehemu, kisha aseme kwa uwazi nini na nani alifanya nini — hasa mauaji na utekaji wa wapinzani wa marehemu. Kisha aseme kabisa kwa dhati, katika uongozi wa Maza, kuwa katika maongozi yake mabaya haya yalitokea — mfano, mauaji — nani anayehusika, kwa black and white. Bila hilo, Watanzania wa kawaida hawatamuelewa.
- Kivuli cha kuwa alikuwa balozi, hivyo hataki kusema yote aliyoyajua akiwa balozi au katika uongozi wake, hakitoshi. Atambue kuwa amekwisha mwaga mboga. Hivyo, kitendo cha kujivua ubalozi tu, amepoteza credibility kwa Maza, na hakuna kingine cha kupoteza asipopambana kwa dhati kuyasema maovu yote aliyoyajua akiwa ndani. Atambue pia, akikaa nayo kimya, hata pata chochote katika serikali hii na ijayo pia. Atakufa na siri zake, na mateso juu yake ya kusaliti chama bila kuongea kwa wananchi. Atambue kuwa CCM anaishitaki kwa wananchi.
- Mapambano aliyoyaanzisha atambue kuwa yanahitaji nguvu ya umma na kuleta hofu kwa watawala. Hivyo, asipoyasema aliyoyapata kuyaona na kuyasikia akiwa huko na wadhalimu, jamii haitamuunga mkono, na hivyo atakuwa anapiga kelele hewani tu. Kujivua kwake itakuwa sawa na bure kabisa, na itaonesha ni uroho wa kutaka madaraka yeye na genge lake tu — si huruma kwa wananchi wa kawaida kutokana na udhalimu wanaotendewa na viongozi wao waliotokana na CCM.
- Polepole, usipolizungumzia suala la Lissu kwa kivuli cha kwamba lipo mahakamani, wakati wananchi wote wanatambua ni sehemu ya ukiukwaji wa haki za upinzani, wananchi wanakuona kama kwamba wewe ni mpinzani wa Maza, lakini siyo mpigania haki za Watanzania. Unaonekana ni msaka tonge tu, ambaye umekosa ulaji kwa Mama, unatafuta genge lako liingie madarakani ili ule vizuri.
- Mwisho, Polepole, wananchi ndiyo wanaweza kumuadhibu Maza kwa nguvu ya umma. Waeleze ufisadi wa bandari ilivyouzwa, mbuga za wanyama huko Ngorongoro — eleza kwa ushahidi, eleza ufisadi wote kwa nyaraka vizuri. Sisi wananchi tutamwajibisha Maza. Bila hivyo, ushafeli. CCM hii haiwezi kukuogopa kwa porojo tu. Umma ndiyo utachukua hatua kuinusuru nchi, na siyo Maza kujitoa kwa porojo za press zako.
Ujumbe huu umfikie mhusika, na ajitafakari vita aliyoianzisha na alipofikia. Hata kama ataficha kitu, hakitamusaidia katika vita hii. The loser is Polepole, asipokuwa serious na vita alivyovianzisha. Yeye ndo anapoteza.
Jumamosi njema.