Habari WA JF
Siku nyingi sijafika humu, Leo Nani ninene.
Ni kweri nimesikiliza Awamu zote Mbili mazungumuzo ya Ndugu Pole Pole na Wana Habari . Nimezitafakri Sana na haya ndiyo niliyoyaona.
1. Kwamba Hadi sasa Pole Pole Kwa namna yeyote Kwa hayo aliyoyasema hayana mazara yeyote Kwa CCM na mwenyekiti wao.
2. Pole pole asipotubu kutoka Moyoni Kwa wananchi Yale yote waliyo yaasisi yenye na mwenda zake hataeleweka vizuri Kwa jamii. Yaani atubu ukweri Kwa mbaya CCM na mwenda zake kisha na aseme Kwa uwazi nini na Nani alifanya nini hasa mauaji ya kuteka kwa wapinzani wa mwenda zake, kisha aseme kabisa Kwa zati katika uongozi wa Maza kuwa katika maongozi yake mbaya yake haya , mfano mauaji Nani anafanya Kwa black and white. Bila Hilo watanzania wa kawaida hawatamuelewa.
3. Kivuli kuwa alikuwa balozi hivyo hataki kusema yote aliyoyajua akiwa balozi au katika uongozi wake. Atambue kuwa amekwisha mwaga mbonga hivyo kitendo cha kujihuzuru Tu ubalozi amepoteza credibility Kwa Maza hivyo hakuna kingine cha kupoteza asipopambana Kwa triki ya kuyasema maovu yote aliyoyajua akiwa ndani. Atambue pia akikaa nayo kimya hata pata chochote kile katika serikali hii na ijayo pia. Atakufa na Siri zake na mateso juu yake ya kusaliti chama bila kuongea Kwa Wananch. Atambue kuwa CCM naishitaki Kwa Wananch.
4. Mapambano aliyoyaazisha atambue kuwa yanahitaji nguvu ya umma na kuleta hofu Kwa watawala, hivyo asipoyasema aliyoyapata akiwa huko na wadhalimu jamii haitamuunga mkono na hivyo atakuwa anajirisha upepo Tu. Na kujihuzuru kwake itakuwa Sawa na bure kabisa na itaonesha ni uroho wa kutaka madaraka yeye na genge lake tu si huruma Kwa wananchi wa kawaida kutokana na udhalimu wanaotendewa na viongozi wao waliotokana na CCM.
5. Pole pole usipolizungumuzia swala la Lisu Kwa kivuli cha kwamba lipo mahamani wakati wananchi wote wanatambua ni sehemu ya ukiukwaji wa haki za upinzani. Wananchi wanakuona kama kwamba. Wewe ni mpinzani WA maza lakini siyo mpigania haki za watanzania. Unaonekana ni msaka tonge tu ambaye umekosa ulaji Kwa mama unatafuta genge lako liingie madarakani ili ule vizuri.
6. Mwisho pole pole wananchi ndiyo wanaweza kumuazibu Maza Kwa nguvu ya umma. Waeleze ufisadi wa bandali ilivyouzwa, mbuga za wanyama huko ngorongoro, eleza Kwa evidence, eleza ufisadi wote Kwa nyaraka vizuri. Sisi wananchi tutamwajibisha Maza, bila hivyo ushafeli CCM hii haiwezi kukuogopa Kwa porojo tu. Umma ndiyo utachukua Hatua kuinusuru Inch na siyo Maza atajitoa Kwa porojo za press zako.
Ujumbe huu umfikie mhusika na ajitafakari vita aliyoianzisha na alipofikia hata kama ataficha kitu hakitamusaidia katika vita hii. The losser is Pole Pole asipokuwa serious na vita alivyoviazisha yeye ndo anapoteza
Jumamosi njema.