Kwa hiyo ulitaka afuate masharti yenu yale ya kijinga na kihayawani ambayo mliyaweka mkijuwa hayatekelezeki? Kila mtu anafahamu ya kuwa mlifanya vile kwa uoga wenu wa kuogopa mdahalo hasa baada ya kugundua kuwa mtaumbuliwa ulafi,uroho na ufisi wenu wa kutaka kuwa na wabunge wawili katika kila jimbo ilihali mnafahamu ya kuwa jambo hilo litamuongezea na kumbebesha mzigo mtanzania mnyonge anayelipa kodi.
Lakini mmeona aibu baada ya kutambua kuwa hoja zenu ni dhaifu na tayari mheshimiwa Makonda alikuwa ameshaeleza hadharani madai yenu dhaifu na kuyatolea majibu ambayo yalieleweka vyema kwa watanzania ambao kwa sasa wanawadharau tu kwa uroho na ulafi wenu wa madaraka muliouonyesha katika kutaka mlango mkubwa wa kupatia madaraka ya ubunge kwa ajili ya kushibisha na kujaza matumbo yenu..