Pre GE2025 Ndio maana Bunge linapitisha tozo, kumbe wao haziwahusu!
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
::::::;Imethibitishwa Tsh20,000.00 imetumwa kwa :::;;;Tarehe 24/6/24 saa 7:17 PM Jumla ya Ada Tsh380.00 (M-Pesa Ada Tsh380.00 + TOZO ya Serikali Tsh0.00). Salio lako ni Tsh;;;;;;;;
Kwenye kutuma tozo si inakatwa ukituma kuanzia 30,000?
 
Salaam Wakuu,

Tulia amekuwa akiwatunuku followers wake mara kadhaa kwa kuwatumia mialama mara kadhaa, na mara zote amekuwa akiweka copy ya miamala hiyo kuonesha kuwa wahusika wamepokea.

Siku zote hizo amekuwa akiedit text hizo na kuondoa kisehemu kinachoonesha makato ya ada na tozo ya serikali, sasa jana akajichanganya kwa kushea screenshot yote ya muamala ambapo inaonesha hakuna makato yoyote anayokatwa!

Ila pia katika maongezi ya hapa na pale nikafamu pia kuna taasisi hapa nchini mfano CRDB wafanyakazi wao hawakatwi makato hayo pia!

Kumbe ndio maana wanashadadia tukwatwe kwasababu wao hawapati maumivu haya?

Kama tozo hizi ni kwaajili ya maendeleo ya taifa kwanini wengine hawakatwi? Yaani mbali na kuwa tunalipa mishahara, yao na posho zao nono bado bado pia wawe exempted kwenye kulipa tozo? Mbali na kutufanyia ufisadi wote huo unaoibuliwa na ripoti za CAG bado na huku muondolewe, kweli?

Watanzania bado tutaendelea kukaa kimya? Makato haya yanatakiwa kuondolewa tuwe tunatuma pesa bure.
Ole wenu waandishi na Mafarisayo kwa maana munawabebesha watu mizigo ambayo nyinyi wenyewe hamuigusi hata kwa "VIDOLE" vyenu, siku zinakuja pale mutakapo kimbia wakati hakuna awakimbizaye....
 
Wananchi wa hali kama ya kwangu naombeni majibu kuhusu hili.

Spika wa bunge amepost hii ikimuonesha kwamba hakatwi makato tunayokatwa sisi kwenye simu zetu.

Je, hii ndio sababu ya wao kutuongezea kodi zisizo na huruma wala utu kwakuwa wao hawapati uchungu si ndio?

Mtu anamshahara mkubwa, anapewa gari, allowances za kutosha, vocha sijui viinua mgongo na bado KODI HAWALIPI!!!!!

Msitutoze hiyo mikodi kama nyinyi hamlipi hamna uchungu na wananchi hata kidogo
 
Attachments

  • IMG_8301.jpeg
    IMG_8301.jpeg
    227.9 KB · Views: 3
Wananchi wa hali kama ya kwangu naombeni majibu kuhusu hili.

Spika wa bunge amepost hii ikimuonesha kwamba hakatwi makato tunayokatwa sisi kwenye simu zetu.

Je, hii ndio sababu ya wao kutuongezea kodi zisizo na huruma wala utu kwakuwa wao hawapati uchungu si ndio?

Mtu anamshahara mkubwa, anapewa gari, allowances za kutosha, vocha sijui viinua mgongo na bado KODI HAWALIPI!!!!!

Msitutoze hiyo mikodi kama nyinyi hamlipi hamna uchungu na wananchi hata kidogo
Tusome basi kabla ya kupanic na kupost, miamala yote ya chini ya TZS 30,000 haina tozo
 
Shut up
Hata buku ina makato ya mtandao.
Makato ambayo kwa miamala ya 30000 kushuka chini ndiyo hakuna makato ya serikali ila ya mtandao husika yapo.
Sasa makato ya mtandao ambayo si tozo yanahusika vipi na serikali? Namba za biashara (LIPA NAMBA) hazifanani makato na namba za simu za kawaida.
 
Back
Top Bottom