Pre GE2025 Ndio maana Bunge linapitisha tozo, kumbe wao haziwahusu!
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Inauma sana hii yaani Wanyonge ndio tunakatwa tozo lakini wale waliopitisha hizo sheria hawakatwi tozo. Hata Mpesa hawachukui ada yao ya transaction ya miamala na serikali pia haikati Government Levy.
Eeeh Mwenyezi Mungu Baba tuepushe na hiki kikombe tunapitia mazingira na hali ngumu sana. Pia hata haki zetu za msingi tunazikosa 🙏
View attachment 3030586
tushakubaliana hii ni nchi ya amani, tuache tulale, watawala wale kwa urefu wa kamba
usitutingishe
 
INASEMEKANA: Hapo kale wafanyakazi wa TANESCO walikuwa hawalipi umeme; Wafanyakazi wa ATC (sasa ATCL) walikuwa wanapanda ndege zao bure; hali kadhalika mashirika kama TRC na NHC. Pengine ni kamtindo kalizoeleka, kila mtu kula urefu wa kamba yake...ndiyo maana mashirika mengi yalikuwa dhaifu..!
 
Yaani 20k duuuh kweli acha nieendeleee kulima kumbe maskini sio mm tupo wengi.........
Ye sio mjinga angetuma milioni 5 hapo mngeanza kuhoji na kutoa povu kwamba wanalamba asali.
 
Yawezekana kweli ikawa hakuna tozo sawa.... Mbona hakuna makato yoyote? Mimi nikituma hata 500 nakatwa 🙌🙌
 
Ndio niliona kumbe wao hawakatwi ndio maana Mwigulu kashupaza shingo
 
Salaam Wakuu,

Tulia amekuwa akiwatunuku followers wake mara kadhaa kwa kuwatumia mialama mara kadhaa, na mara zote amekuwa akiweka copy ya miamala hiyo kuonesha kuwa wahusika wamepokea.

Siku zote hizo amekuwa akiedit text hizo na kuondoa kisehemu kinachoonesha makato ya ada na tozo ya serikali, sasa jana akajichanganya kwa kushea screenshot yote ya muamala ambapo inaonesha hakuna makato yoyote anayokatwa!


Ila pia katika maongezi ya hapa na pale nikafamu pia kuna taasisi hapa nchini mfano CRDB wafanyakazi wao hawakatwi makato hayo pia!

Kumbe ndio maana wanashadadia tukwatwe kwasababu wao hawapati maumivu haya?

Kama tozo hizi ni kwaajili ya maendeleo ya taifa kwanini wengine hawakatwi? Yaani mbali na kuwa tunalipa mishahara, yao na posho zao nono bado bado pia wawe exempted kwenye kulipa tozo? Mbali na kutufanyia ufisadi wote huo unaoibuliwa na ripoti za CAG bado na huku muondolewe, kweli?

Watanzania bado tutaendelea kukaa kimya? Makato haya yanatakiwa kuondolewa tuwe tunatuma pesa bure.
Ni misukule ya jiwe!
 
Back
Top Bottom