Ndo nimemaliza C-section ya 6, nimechoka akili na mwili. Halafu kuna Wanasiasa kwa mwezi wanakula 11 M na bado wanajiongezea mshahara 40%

Pole,tafuta kazi Botswana au Canada huko ukaenjoy mshahara mzuri.Hapa Tanzania tunaambiwa Udaktari na Ualimu ni wito.
 
Pole sana daktari ila karibu huku ulanga usipokimbia wewe mwanaumme huku ni balaa tupu yaani unayosimulia hayo ndio yananitokea huku kuna nyingine hii 5previous scar in labour
 

Ndugu [mention]Carlos The Jackal [/mention] acha kujitukuza na kujiona bora kimajukumu kuliko wengine, maisha ni kutegemeana.

Imagine, askari mpiganaji aliyekoswa risasi akihakikish usalama wa raia wengine waliolala aje hapa na tambo za kudai fedha zaidi akijilinganisha na idadi ya risasi zilizomkosa au majeraha ya risasi aliyonayo?

Rubani wa ndege aliyekurusha masaa mengi angani na kukufikisha salama destination husika, naye aje kujilalamisha kiasi cha kuapa kukosa control ya chombo akiwa angani na ku-risk maisha ya watu wengi aliowabeba kwa sababu fedha nyingi wanalipwa wanasiasa?

Kila mmoja ni muhimu kwa nafasi yake. Kwa mtazamo wako, leo hii roboti ya upasuaji (medical surgery bot) italalama kufanya kazi kwa muda mrefu na ufanisi zaidi kukuzidi. Na je, ikitaka ufutwe kazi kwa sababu hauna dili tena, isikilizwe?

Mchango wako kama daktari ni mkubwa, lakini sio kwa umuhimu unaojipa. Sipati picha ungekuwa “Neurosurgeon” hizo tambo zake, acha ulimbukeni dogo.

Mwisho, kufanya kazi masaa yote hayo sio sifa. Kuna daktari mwenzako (kama kweli nawe ni daktari) amefariki huko Nigeria (Lagos Teaching Hospital) baada ya kujipinda masaa 72 mfululizo kwenye surgery na kukosa pumziko.

Fanya kazi ulijenge taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…