Ndoa hapana! Sitaki

Ndoa hapana! Sitaki

Ipo philosophy moja kuna rafiki yangu humu jf aliwahi kuniambia kwamba ukienda kutoa posa halafu utajiwe kutoa mahari kubwa hiyo huwa ni mbinu ya kukufukuza kama endapo familia haijakupenda
Itakufukuza ikiwa hujamharibu binti yao ila wakigundua ana kidude wanarudisha majeshi kwa 5G!

Nilipotea miezi baada ya kuchapishiwa mkeka wa mahari 4.5M😀 ila walipoona binti yao kavimba uso wakaona ni muda muafaka wa kulegeza masharti.
 
Ndo kifuatacho itv
Ukiuliza hawana hoja ya msingi....hoja kuu ukiwasikiliza ni Ubinafsi tu na kukwepa majukumu.
Mbona wapo wengi tu walioolewa, hao ni ridhaa yao na wala haishangazi kwa sasa, ndio Mashoga yenyewe hayo...!!!

Ila haimaanishi Mwanaume asipooa lazima aolewe yeye BIG NO! Wanaume Hawaoi ila wana wanawake zao hata wawili mpaka watatu na hata wa kuishi nao ila ndoa HAPANA

Btw, naamini ulisoma habari za kijana Massawe aliyefariki juzi kwa stress za mke na mke alitaka jamaa azikwe KLM badala ya Bagamoyo ili akaendelee kutanua na hawara wake

Sasa ile type ya yule Mwanamke ndio wamejaa sasahivi mtaani japo sio wote ila wengi
 
Nilikwenda kuchumbia mahali fulani...majibu yakatoka nikaambiwa nipeleke milioni mbili..,nimejitafakari aisee ni hapana sijajua wazazi wa Binti watanifikiria vipi ...ila watanisamehe tu.

Kwanza naenda kumnunua mtu...pesa inatoka hapo,pili natakiwa niwe namhudumia kwa kila kitu nikiwa naye nayo ni pesa hio,tatu Mwanamke atakuja kunibana aisee nishazoea kulala pekeangu,nne nahofia tukiachana nitapoteza hata hivi vichache nilivonavyo...mwisho kabisa Mwanamke nimemuona mtu wa lawamalawama sana...kwanza ni ngenye ndio zilisababisha harakaharaka nichumbie

Binafsi nikifikisha miaka 40 labda ndio nifikirie kuoa kwa saivi najitafuta kwanza nahitaji niimarike kiuchumi

Mikakati ninayokuja nayo

1.naacha pombe,sigara
2.nakuwa mtu wa ibada na kusoma vitabu.
3.nakuwa mchumi na mbahili lakini nataka nifanye kazi kwa bidii sana
4.naweka akiba
5.nakuwa mtu wa kujipenda na kupendeza kuvaa vizuri
6.mbinafsi.

Note:ndoa ni muhimu lakini sio lazima
wait when you hit 65yrs ndipo utajutia uamuzi wako wa kijinga
 
Back
Top Bottom