Ndoa ikifika hali hii mnakaribisha zinaa kama bado haijaingia

Ndoa ikifika hali hii mnakaribisha zinaa kama bado haijaingia

Sky, kwanini mnapenda sana kukimbilia eti kutoka Out ? sijui kwenda hotel !, watu kule vijijini (ambapo hakuna hizo beach resort) wanaweza kuishi vizuri na kwa miaka mingi bila kukwaruzana, tena katika hali ya maisha duni, lakini wanawake kule ni wavumilivu, huku mjini mwanamke anakuangalia tu, akiona humpeleki hoteli kubadirisha upepo anakuona wewe lofa, maisha yenyewe haya ya magufuri ni magumu jamani, hela za kwenda kustarehe hotelini huku mmeacha nyumba yenu zinatoka wapi ?, wamama jifunzeni kupenda waume zenu hivyhivyo
Ukiona Mwanamke anakukamua sana,ujuwe kabisa huyo hakupendi kwa dhati,anakutumia tu kiuuchumi!!
 
Bwana mmoja kazini alinisimulia, huwa ananunua nyama J’mosi. Asipoacha pesa ya kila siku asubuhi akirudi anakuta a na bakuli la nyama iliyochemshwa, haina limao, kitunguu wala nyanya. Nilimjibu hata kule Syria kuna ushirikiano ingawa wako vitani.
Mwanaume gani huyo anashindwa kuendesha Nyumba yake,alafu anakuletea malalamiko yake weye!? Mwambie aache upumbavu na amuambie Mkewe kile kitu anachopenda kula ndiyo kipikwe hivyo la sivyo mashariti na Vigezo kuzingatiwa ebo!!
 
Hii ianawapata sana wale wanandoa ambao tangu mwanzoni walijijengea utaratibu huo lakini mkiwekana sawa tangu urafiki , uchumba hadi kuoana wala haisumbui

Na tatizo hili linasababishwa zaidi na sisi wanaume wakati wa kuanzisha mahusiano huwa hatupo halisia i.e mambo mengi huwa tunayaficha kwa kujifanya wavumilivu jambo ambalo hutuletea shida sana yanapoanza majukumu mwakubwa hasa ya watoto tunajikuta tunaelemewa na kwakuwa mke hukumuandaa kwa utaratibu wa kushirikiana na kusaidiana ukimuanzishia ndani ya mwenendo wa maisha ndoani anaanza kujuona gaidi

Mwanamke wa kumuoa ni lazima tangu mwanzo umuwekee utaratibu wa kufuata tangu awali hataki unajua kabisa huyu ni mbinafsi hatanifaa unaacha unatafuta wa kukufaa
Umeongea vizuri sana, ni kweli baadhi yetu hujifanya tunayaweza sana, na bahati mbaya mambo yanapoenda mlama ndipo hapo unapoanza kuuona ugumu, kama ulimzoesha mke kumtotoa out mara mmeenda sijui beach, maana yake utakuwa umemzoesha na haitakuwa rahisi kumbadirishia aina ya maisha, si unajua wanawake huwa hawakubali mambo yanapobadirika, nashauri tuwe manunda wote ili kujiweka safe
 
Haya yote kabla hamjaoana kila mtu anakuwa anayajua ila mkishaoana tu,kama hamko kwenye mstari shetani anapora vyote mnabaki kama mlivyo yanaanza mapambano....
Hahahahaaaa,mkuu kumbuka we ndio unatakiwa usimamie hayo mambo.KWENYE NDOA mwanaume onyesha njia mwanamke atakuunga mkono
 
Tunasahau wa nje hufurahisha kwa sababu mnaonana kwa wizi

Cha wizi kitamu, nae mkioana mtakinai tu hatakuwa na aliyokuwa anakufanyia mlipokua wezi
Yaan sijui kwanin watu hawajuagi hili
 
Sio lazima iwe hotel. Mwanamke hata ukitoka nae nyumbani mkatembea kwa pamoja njiani au barabarani kwa miguu huku mkiongeleshana hili na lile walau mara moja au mbili hata kwa mwezi anajipata anapendwa sana na mume wake.

Kuna wanaume hata kuingia bafuni akaoga na mkewe hawajawahi!! Yaan yeye ni serious tuuuuuuuuu hana hata muda wa kutaniana na mkewe utafikiri askari magereza na mfungwa wake huo upendo utatoka wapi?

Mke hujawahi mnunulia hata chuppi tu ukamletea mkeo nyumbani ukaingia nae bafuni mkaogeshana ukamwambia mama fulani / mke wangu fumba macho nikusspraizi akafumba ukamvalisha kyupi kizuuuri akapendeza ukamwambia fumbua macho akatabasamu mkakumbatiana mkacheka mkafurahi.

Kuna zile moments ambazo mnakumbushana namna mlivyokutana mkapendana mkatongozana hadi mkawa marafiki kisha wachumba hadi kuoana ni muhimu sana pia kwa baadhi ya nyakati

Mke na mume hawawezi hata kuambizana neno mke/mume wangu nakupenda hakuna!!

Halafu hakuna watu wanaopenda na wanajiskia furaha kama wake zetu ukiwasifia. Yaan we msifie tu mara kwa mara. Mwambie mke wangu nakupenda sana wewe ni mwanamke mzuri kuliko wanawake woooooote duniani hata kama sivyo alivyo msifie tu anajipata yuko na furaha sana moyoni mwake

Mpe zawadi hata kama ni pipi au nguo au kiatu au mafuta ya kupakaa au manukato kulingana na uwezo wako we mpe atafurahi na atathamini sana upendo wako kwake
Mkuu umeongea vizuri sana, lakini utambue kwamba sio wanawake wote wanaweza kusema hata asante, unaweza kufanya kati ya hayo na bado asikushukuru hata chembe, mfano halisi ni mimi hapa, mke wangu ni kati ya hao wasio na muda wa kusema asante, hicho unachosema suprize inaweza onekana ni bure na ukaambulia kashfa, siku moja niliingi mlimani city nikanunua gauni (ambalo kwangu mimi nililiona linapendeza machoni) nilipotoka pale nikapita duka jingine hapo jirani nikanunua viatu (ambavyo kwangu niliona ni vizuri vya kuvutia) huwezi amini nilipofika nyumbani alishindwa hata kuigiza kwamba amefurahi, na vile viatu vilikaa chini ya kitanga muda mrefu sana hakuwahi kuvivaa, hapo nilitumia kama shilingi laki 1 hivi, mtu mmoja aliwahi kusema wanawake wenyewe huwa hawajui wanataka nini.
 
View attachment 1627217
Sababu mojawapo ni kumkosoa mwenza mbele za watu. Mkisha funga ndoa nyinyi ni mwili mmoja. Mume wako akichemka hadharani unaimeza aibu mpaka mfike chumbani ndiyo mnaongea. Mfano unajua mume wako Kimalkia hakipandi, akivunja mbele za watu meza.

Kumkumbatia mume wako asubuhi akiwa anakuaga ni muhimu. Kwa mila za Afrika ni ngumu kufanya haya kama mpo na wazazi au wakwe. Mkumbatie chumbani na busu hata akirudi kutoka kazini.

Jiepushe na marafiki wasio mkubali mke/mume wako. Maneno yao yatakua sumu katika penzi lenu.

Jifunze kuomba msamaha kwa mke/mume wako. Kiburi ni sumu ya mapenzi.

Kuwa muwazi kwa mwenza wako. Mfano Haya mambo ya kuja kufahamu ulizaa kabla ya ndoa mkiwa tayari kwenye ndoa yana leta hatari sana.

Wengine neno niache au tuachane limekaa mdomoni kila mkikwaruzana kidogo tu.

Kila ukipata nafasi weka manjonjo kwenye ndoa yenu. Hata kutumia weekend hotelini kubadilisha mazingira na kuwa na nafasi yenu.
Juzi Kati wife anataka niweke wazi bank statements yangu ili ajue kinacho ingia na kinacho toka, nimegoma hadi mida hii kanuna ndoa ina miezi sita, wakuu hii imekaaje?
 
Mkuu umeongea vizuri sana, lakini utambue kwamba sio wanawake wote wanaweza kusema hata asante, unaweza kufanya kati ya hayo na bado asikushukuru hata chembe, mfano halisi ni mimi hapa, mke wangu ni kati ya hao wasio na muda wa kusema asante, hicho unachosema suprize inaweza onekana ni bure na ukaambulia kashfa, siku moja niliingi mlimani city nikanunua gauni (ambalo kwangu mimi nililiona linapendeza machoni) nilipotoka pale nikapita duka jingine hapo jirani nikanunua viatu (ambavyo kwangu niliona ni vizuri vya kuvutia) huwezi amini nilipofika nyumbani alishindwa hata kuigiza kwamba amefurahi, na vile viatu vilikaa chini ya kitanga muda mrefu sana hakuwahi kuvivaa, hapo nilitumia kama shilingi laki 1 hivi, mtu mmoja aliwahi kusema wanawake wenyewe huwa hawajui wanataka nini.
Nakubaliana na wewe upo sahihi. Lakini usisahau huyo ni mkeo na kamwe haiwezekani ukawa haumjui mkeo nje ndani. Mke ni mtu ambaye unakuwa unamjua kwa karibia kila kitu na ndio sababu uliridhia nafsini mwako ukamuaprochi na ukamuoa vinginevyo basi ulilazimishwa tu kuwa naye ambapo hilo ni jambo jingine kabisa.

Ukishamjua mbwa jina lake wala hakusumbui maana lazima utajua namna ya kuendana naye sio! Kumbuka kwamba pengine huenda huyo huyo mkeo anaweza kupewa zawadi na mtu mwingine tena ikawa hata ya pipi tu lakini akaifeel na akashukuru hadi kutokwa na machozi ya upendo na furaha ndani yake (hapo jambo la kulidadavua ni je?... Kwanini hali hii isitokee kwako lakini ikawa kwa mwingine tu)?. "HUU NI MFANO TU"~ ambao ilishawahi kunitokea mimi mwenyewe kwa mwanamke ambaye alikuwa na mumewe lakini alikuwa akinieleza kwamba yeye mume wake hata ampe zawadi gani hajisikii furaha wala upendo na hata akishukuru anakuwa anafake tu, baada ya kumtafiti kwa kina sana nikagundua kwamba mwanzoni wakati wanaanza mahusiano haikuwa hivyo lakini baadaye mambo yakaharibika.

Nimejifunza kutimiza haki na wajibu pasipo kutarajia malipo chanya tu! (Tenda wema nenda zako usingoje kurudishiwa wema) nakuhakikishia ipo siku huyo mkeo atakuja kuapolojaizi kwako kwa hayo anayoyaona kwa sasa hayana maana kwake. Jambo hili lahitaji kuwa mvumilivu sana.

Kuna wakati mke/mume hana hamu na mwenza wake lakini hii haimaanishi kwamba huyu mwenye hamu na mwenzie achukulie hali ya mwenziwe kwa chuki ama alipe kisasi ama amkomoe au la, upo wakati mambo yatakaa sawa ikiwa nyote wawili ni soul mate kwa maana ya kwamba mnaendana
 
Umeongea vizuri sana, ni kweli baadhi yetu hujifanya tunayaweza sana, na bahati mbaya mambo yanapoenda mlama ndipo hapo unapoanza kuuona ugumu, kama ulimzoesha mke kumtotoa out mara mmeenda sijui beach, maana yake utakuwa umemzoesha na haitakuwa rahisi kumbadirishia aina ya maisha, si unajua wanawake huwa hawakubali mambo yanapobadirika, nashauri tuwe manunda wote ili kujiweka safe
Yeap, tunatakiwa kuwa wawazi na wakweli tangu mwanzo mwa mahusiano ili kujenga msingi bora wa maisha ya ndoa
 
Juzi Kati wife anataka niweke wazi bank statements yangu ili ajue kinacho ingia na kinacho toka, nimegoma hadi mida hii kanuna ndoa ina miezi sita, wakuu hii imekaaje?
Hiyo ndoa bado ni sawa na chekechea, unatuletea ndoa ya miezi ??!!m are you kidding ?.
 
Somo zuri

Ila hiyo PC sijui ndoa imefikia AGAPE relationship
 
Juzi Kati wife anataka niweke wazi bank statements yangu ili ajue kinacho ingia na kinacho toka, nimegoma hadi mida hii kanuna ndoa ina miezi sita, wakuu hii imekaaje?
Mkuu kama umemwamini kumpa moyo wako,kwanini umfiche kipato chako?
 
Mkuu kama umemwamini kumpa moyo wako,kwanini umfiche kipato chako?
Ooh yes....

Moyo Umezungumzwa kwenye BIBLIA(kwa wanaoiamini)
Mwili Umezungumzwa kwenye BIBLIA(kwa wanaoiamini)

Nikumbushe....PESA,MALI,KIPATO kimezungumzwa PIA?!!!

Halafu ndoa za zamani za KIMILA na KIDINI hazikuwa zinavunjwa...ama kuvunjika hata IWEJE....

Mwanamke alishakuwa subservient wa MWANAUME na harudi nyuma(kwao) hata IWEJE....

Je dunia ya leo?!!!

Hii dunia iliyo kiganjani....

Mwanaume anawaza na kuipenda PESA kuliko famili yake....
Mwanamke anawaza na kuipenda pesa kuliko MUMEWE.....
👆👆
WALA HAWALAUMIKI SANAAA....kwani changamoto ya mahitaji(yanayoyatuliwa na pesa) imekuwa ni KUBWA mno....

Mfano VIJIJINI Kabisa...umuhimu wa watu ni kulima,kuvuna,kuhifadhi ya CHAKULA na KUUZA(kupata pesa ya ada,nguo n.k)

Hapa MIJINI Hakuna MASHAMBA....tumbo lako linajazwa na UKUBWA WA MFUKO WAKO...

Asubuhi nitoe hela ya CHAKULA...
Mchana nitoe hela ya CHAKULA...
Usiku nitoe hela ya CHAKULA....
Bado ADA...bado UMEME...bado BILLS za maji...bado WEAVINGS na Madera ya mama NAYRAT....

Pressure ya PESA hasa humu mijini ni ROBUST......
 
Mkuu mi siyo mtaalamu wa maandishi matakatifu,ila unachozungumza ni kweli kabisa kwamba kuna mabadiliko makubwa ya kimfumo wa maisha wa mahusiano(ndoa),Ila bado UWAZI katika mahusiano ni muhimu sana.Mkiwa wawazi kuna migogoro isiyo na lazima hupungua
 
Sure...

Uwazi ni MUHIMU...

UWAZI
UWAZI
UWAZI

👍
 
Back
Top Bottom