Ndoa ikifika hali hii mnakaribisha zinaa kama bado haijaingia

Ukiona Mwanamke anakukamua sana,ujuwe kabisa huyo hakupendi kwa dhati,anakutumia tu kiuuchumi!!
 
Mwanaume gani huyo anashindwa kuendesha Nyumba yake,alafu anakuletea malalamiko yake weye!? Mwambie aache upumbavu na amuambie Mkewe kile kitu anachopenda kula ndiyo kipikwe hivyo la sivyo mashariti na Vigezo kuzingatiwa ebo!!
 
Umeongea vizuri sana, ni kweli baadhi yetu hujifanya tunayaweza sana, na bahati mbaya mambo yanapoenda mlama ndipo hapo unapoanza kuuona ugumu, kama ulimzoesha mke kumtotoa out mara mmeenda sijui beach, maana yake utakuwa umemzoesha na haitakuwa rahisi kumbadirishia aina ya maisha, si unajua wanawake huwa hawakubali mambo yanapobadirika, nashauri tuwe manunda wote ili kujiweka safe
 
Haya yote kabla hamjaoana kila mtu anakuwa anayajua ila mkishaoana tu,kama hamko kwenye mstari shetani anapora vyote mnabaki kama mlivyo yanaanza mapambano....
Hahahahaaaa,mkuu kumbuka we ndio unatakiwa usimamie hayo mambo.KWENYE NDOA mwanaume onyesha njia mwanamke atakuunga mkono
 
Haya yote kabla hamjaoana kila mtu anakuwa anayajua ila mkishaoana tu,kama hamko kwenye mstari shetani anapora vyote mnabaki kama mlivyo yanaanza mapambano....
Hahahahaaaa,mkuu kumbuka we ndio unatakiwa usimamie hayo mambo.KWENYE NDOA mwanaume onyesha njia mwanamke atakuunga mkono
 
Tunasahau wa nje hufurahisha kwa sababu mnaonana kwa wizi

Cha wizi kitamu, nae mkioana mtakinai tu hatakuwa na aliyokuwa anakufanyia mlipokua wezi
Yaan sijui kwanin watu hawajuagi hili
 
Mkuu umeongea vizuri sana, lakini utambue kwamba sio wanawake wote wanaweza kusema hata asante, unaweza kufanya kati ya hayo na bado asikushukuru hata chembe, mfano halisi ni mimi hapa, mke wangu ni kati ya hao wasio na muda wa kusema asante, hicho unachosema suprize inaweza onekana ni bure na ukaambulia kashfa, siku moja niliingi mlimani city nikanunua gauni (ambalo kwangu mimi nililiona linapendeza machoni) nilipotoka pale nikapita duka jingine hapo jirani nikanunua viatu (ambavyo kwangu niliona ni vizuri vya kuvutia) huwezi amini nilipofika nyumbani alishindwa hata kuigiza kwamba amefurahi, na vile viatu vilikaa chini ya kitanga muda mrefu sana hakuwahi kuvivaa, hapo nilitumia kama shilingi laki 1 hivi, mtu mmoja aliwahi kusema wanawake wenyewe huwa hawajui wanataka nini.
 
Juzi Kati wife anataka niweke wazi bank statements yangu ili ajue kinacho ingia na kinacho toka, nimegoma hadi mida hii kanuna ndoa ina miezi sita, wakuu hii imekaaje?
 
Nakubaliana na wewe upo sahihi. Lakini usisahau huyo ni mkeo na kamwe haiwezekani ukawa haumjui mkeo nje ndani. Mke ni mtu ambaye unakuwa unamjua kwa karibia kila kitu na ndio sababu uliridhia nafsini mwako ukamuaprochi na ukamuoa vinginevyo basi ulilazimishwa tu kuwa naye ambapo hilo ni jambo jingine kabisa.

Ukishamjua mbwa jina lake wala hakusumbui maana lazima utajua namna ya kuendana naye sio! Kumbuka kwamba pengine huenda huyo huyo mkeo anaweza kupewa zawadi na mtu mwingine tena ikawa hata ya pipi tu lakini akaifeel na akashukuru hadi kutokwa na machozi ya upendo na furaha ndani yake (hapo jambo la kulidadavua ni je?... Kwanini hali hii isitokee kwako lakini ikawa kwa mwingine tu)?. "HUU NI MFANO TU"~ ambao ilishawahi kunitokea mimi mwenyewe kwa mwanamke ambaye alikuwa na mumewe lakini alikuwa akinieleza kwamba yeye mume wake hata ampe zawadi gani hajisikii furaha wala upendo na hata akishukuru anakuwa anafake tu, baada ya kumtafiti kwa kina sana nikagundua kwamba mwanzoni wakati wanaanza mahusiano haikuwa hivyo lakini baadaye mambo yakaharibika.

Nimejifunza kutimiza haki na wajibu pasipo kutarajia malipo chanya tu! (Tenda wema nenda zako usingoje kurudishiwa wema) nakuhakikishia ipo siku huyo mkeo atakuja kuapolojaizi kwako kwa hayo anayoyaona kwa sasa hayana maana kwake. Jambo hili lahitaji kuwa mvumilivu sana.

Kuna wakati mke/mume hana hamu na mwenza wake lakini hii haimaanishi kwamba huyu mwenye hamu na mwenzie achukulie hali ya mwenziwe kwa chuki ama alipe kisasi ama amkomoe au la, upo wakati mambo yatakaa sawa ikiwa nyote wawili ni soul mate kwa maana ya kwamba mnaendana
 
Yeap, tunatakiwa kuwa wawazi na wakweli tangu mwanzo mwa mahusiano ili kujenga msingi bora wa maisha ya ndoa
 
Juzi Kati wife anataka niweke wazi bank statements yangu ili ajue kinacho ingia na kinacho toka, nimegoma hadi mida hii kanuna ndoa ina miezi sita, wakuu hii imekaaje?
Hiyo ndoa bado ni sawa na chekechea, unatuletea ndoa ya miezi ??!!m are you kidding ?.
 
Somo zuri


Ila hiyo PC sijui ndoa imefikia AGAPE relationship
 
Juzi Kati wife anataka niweke wazi bank statements yangu ili ajue kinacho ingia na kinacho toka, nimegoma hadi mida hii kanuna ndoa ina miezi sita, wakuu hii imekaaje?
Mkuu kama umemwamini kumpa moyo wako,kwanini umfiche kipato chako?
 
Mkuu kama umemwamini kumpa moyo wako,kwanini umfiche kipato chako?
Ooh yes....

Moyo Umezungumzwa kwenye BIBLIA(kwa wanaoiamini)
Mwili Umezungumzwa kwenye BIBLIA(kwa wanaoiamini)

Nikumbushe....PESA,MALI,KIPATO kimezungumzwa PIA?!!!

Halafu ndoa za zamani za KIMILA na KIDINI hazikuwa zinavunjwa...ama kuvunjika hata IWEJE....

Mwanamke alishakuwa subservient wa MWANAUME na harudi nyuma(kwao) hata IWEJE....

Je dunia ya leo?!!!

Hii dunia iliyo kiganjani....

Mwanaume anawaza na kuipenda PESA kuliko famili yake....
Mwanamke anawaza na kuipenda pesa kuliko MUMEWE.....
πŸ‘†πŸ‘†
WALA HAWALAUMIKI SANAAA....kwani changamoto ya mahitaji(yanayoyatuliwa na pesa) imekuwa ni KUBWA mno....

Mfano VIJIJINI Kabisa...umuhimu wa watu ni kulima,kuvuna,kuhifadhi ya CHAKULA na KUUZA(kupata pesa ya ada,nguo n.k)

Hapa MIJINI Hakuna MASHAMBA....tumbo lako linajazwa na UKUBWA WA MFUKO WAKO...

Asubuhi nitoe hela ya CHAKULA...
Mchana nitoe hela ya CHAKULA...
Usiku nitoe hela ya CHAKULA....
Bado ADA...bado UMEME...bado BILLS za maji...bado WEAVINGS na Madera ya mama NAYRAT....

Pressure ya PESA hasa humu mijini ni ROBUST......
 
Mkuu mi siyo mtaalamu wa maandishi matakatifu,ila unachozungumza ni kweli kabisa kwamba kuna mabadiliko makubwa ya kimfumo wa maisha wa mahusiano(ndoa),Ila bado UWAZI katika mahusiano ni muhimu sana.Mkiwa wawazi kuna migogoro isiyo na lazima hupungua
 
Mkuu mi siyo mtaalamu wa maandishi matakatifu,ila unachozungumza ni kweli kabisa kwamba kuna mabadiliko makubwa ya kimfumo wa maisha wa mahusiano(ndoa),Ila bado UWAZI katika mahusiano ni muhimu sana.Mkiwa wawazi kuna migogoro isiyo na lazima hupungua
Sure...

Uwazi ni MUHIMU...

UWAZI
UWAZI
UWAZI

πŸ‘
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…