( 21- 35 ) MWISHO
21
Cm ya Mahamood ikaingia, nikajiuliza nipokee au niachane nayo? Nikasema ngoja nipokee maana ni Mume wangu, halow Mamujee unaendeleaje? Nikamwambia cjambo, eti mke wangu naomba univumilie, najua unaumia sawa, ila nivumilie mama, huyu mwanamke ni mkorofi sana, amechukua namba yako kwenye cm yangu, ctaki kumwambia kuhusu swala la mimba, nahofia anaweza kufanya hata kitu kibaya, ndio sababu nipo kimya kwa sasa, nasubiri ujifungue kwanza,, nilimuoa huyu mwanamke sababu ya bi mkubwa kukosa uzazi , ckujua kama hata yeye atachelewa kuzaa, wakati namuoa yeye nilimuhakikishia kuwa sitaoa tena yeye ndio wa mwisho, Sasa ningefanya nn na yeye uzazi umekuwa wa shida kwake? Ina maana nikae bila mtoto kweli?! Hapana naomba univumilie,, kama unashida yeyote ya pesa bc nikutumie, naomba utulie, acha presha, ujifungue kwanza,
Aliongea mengi sana kunibembeleza nikamwambia sawa inatosha, maana tyr nilikuwa naona kabisa presha yangu iko juu
Nikamuuliza tu vp ujenzi wangu kule Salasala, maana alimuachia mtu ausimamie, akaniambia unaendelea vzr na wameanza kupaua,, bc nikamwambia sawa bye
Niliendelea kukaa pale kwa Kaka ila akawa amepunguza kidogo Mambo ya wanawake, anawaleta ila wawili, wenyewe hata hawajuani kila mtu anajijua yupo mwenyewe na mm nilikuwa hata siwaopoi maana mie kwangu tupo watatu maisha yaliendelea na cku zikazidi kuisha,, tulikubaliana na Mahamood kabla kuwa nisubiri uchungu niombe Opareshen coz tulihofia watoto wawili harafu marinda sina mhhhh, bc tukawa tyr tunajua mm ni Opareshen tu, hata wakati nipo dar doctor wangu aliniandikia ivo so kwenye fairi langu ilikuwa ipo wazi kuwa nataka opp, nazani mnajua hospital za kulipia hazina shida zinakusikiliza mteja unataka nn,, na nilivyofika Arusha tyr nilishatafuta hospital ya kujifungulia, trh yangu ya opp ilifika nikaenda hospital vzr nilipelekwa na Kaka pamoja na wifi mmoja, nilifika hospital nikalazwa ili kuandaliwa kwa opp,, Kaka alimtafuta Mahamood ila hakupatikana, nikafanyiwa opp vzr nikajifungia salama watoto wa kiume,, nilifurahi sana pamoja na Kaka yangu maana tyr tumeongezeka, tulikuwa wawili ila sasa tupo wanne bc nilikaa hospital kama cku tano iv nikaruhusiwa kurudi nyumbani, niliendelea kula uzazi pale kwa Kaka wala sikuwa na hofu tena kuhusu Mahamood nilisema akinitafuta sawa ila asiponitafuta pia sawa , nilikaa hadi namaliza 40 Mahamood kimya ukimtafuta pia hapatikani, nikasema mhhhh hii sio kawaida kulikoni? Namba ya bi mkubwa sina huwa naongea nae kupitia cm ya Mahamood, nikaona hii hali sio ya kawaida,, namtafuta vp sina njia nyingine? Ila namba ya bi mdogo ninayo aliyonitumia matusi, ila cwez mtafuta!! Nikaongea na Kaka kuhusu ile hali na wasiwasi wangu,, Kaka aliniuliza tu ile ghorofa hati yake jina la nani?? Yaan Kaka unaacha kufikilia wanangu kuhusu Baba yao unawaza ghorofa?? Akaniambia Amamu hao watoto ni wangu, Baba yao awepo au asiwepo wala usijali, niambie tu hati ya nyumba yako inajina la nani?? Nikamwambia inajina langu,, akaniuliza tena una uwakika?? Nikamwambia ndio, akasema bc achana nae yaaan Kaka mipombe imemuaribu jmn,, cjui na mirungi pia, maana anaongea kihuni tu, aliniuliza kuhusu gari yangu nimeacha wap nikamwambia pale pale kwangu ila usalama upo tu, huwa nampigiaga jirani yangu ananiangalizia, bc Kaka akasema kama huumpati huyo mumeo achana nae nikamwambia bc mm nikifikisha miezi mitatu narudi kwangu, akaniambia sawa, kula uzazi kwanza kwa Kaka yako,, bc niliendelea kukaa kwa Kaka ila ckuacha kumtafuta Mahamood ila mafanikio hakuna
Cku moja nipo zangu tu sina hili wala lile, nishaanza kupendeza uzazi umenipenda mwenyewe kuhusu mengine nimemuachia Mungu,, nashangaa mlinzi wa Kaka ambaye ndio house boy, anakuja kuniita eti kuna mgeni wangu,, nimetoka namuona Mahamood, alivyoniona alifurahi, akaniambia nilijua tu tyr umejifungua, nikamwambia kwahyo ulifanya makusudi?? Nikamwambia karibu ndani,, akasema hapana siingii ndani, naomba toa maelekezo kwa watu wako humo ndani tutoke mara moja,, bc nikawaaga madada nikatoka na Mahamood, tukaenda kwenye hotel moja iv, tukaagiza chakula na vinywaji hatukuchukua room,, wakati tunakula na kunywa ndipo akaanza kuniomba samahani, kumbe bi mdogo alivunja cm na alikata kata laini zote za cm, kwahyo alikosa mawasiliano kabisa, mhhhh nikaamua kumuelewa tu, ndipo akaniuliza umejifungua watoto gn?? Nikamwambia wa kiume, maana mda wote huo alikuwa hajauliza chochote kuhusu watoto, akaniambia naomba picha nikamuonyesha ,, Watoto wangu wote machotara nywele Sasa kama Baba yao Mahamood alifurahi akasema nilitegemea hili,, bc alikuwa na cm nyingine kweli tofauti na ile ya mwanzo, akampigia cm bi mkubwa,, yaan bi mkubwa alifurahi jmn yule mwanamke cjui ana roho gn jmn, nikaongea na bi mkubwa akanipa hongera,, Mahamood akamtumia bi mkubwa picha,, bc Mahamood akaweka status yake watoto wake akaandika inshallah, hatimae nimekuwa Baba,, nikamwambia huogopi?? Akasema nilikuwa nasubiri wazaliwe salama tu mm sio mjinga wa kupelekeshwa na wanawake he mara ananionyesha status ya bi mkubwa nae kawaweka watoto kaandika My babies , nikasema bi mdogo lazima aue mtu
Itaendelea
22
Adimin sory sana pamoja na wajumbe, nilitamani kurudi ila bize sanaa walah! Hii sikukuu kwa sisi wafanya biashara ndio wakati wetu wa kupata chochote, sasa nimejikuta hata muda wa kushika cm sina kabisa!!! Natamani kuimaliza hii story......
Bc tulikaa pale Hotelini tukimaliza chakula chetu,,, tulirudi nyumbani ili Mahamood akawaone watoto wake, bc alifurahi sana kuwaona wanae akasema hii kweli damu yngu,, alikaa pale akimsubiri Kaka ili amshukuru,, akaniambia Mamujee naomba turudi dar, nikamwambia sawa ila tulipatana na Kaka watoto wafikishe miezi mitatu, akaniambia hapana, nataka tuwahi nikasimamie ile nyumba iishe kwa haraka, kabla sijarudi Dubai muwe mmehamia na watoto, nikamwambia sawa, MUDA uliisha Kaka hakurudi mapema cku hio, Mahamood aliondoka kulala Hotelini,, bc Kaka aliporudi nilimpa zile habari akakubali mm kurudi dar na Mahamood,, bc asbh tuliamka mapema sana tukajiandaa kuondoka, Kaka akanipa msichana wa kazi mmoja nije nae, Mahamood alitufata tukaanza safari ya kurudi
Tumefika dar vzr tukaanza maisha mapya ya ulezi wa mapacha ( Mtanisamehe majina ya watoto wangu sita yataja kurinda heshima ya familia yangu maana humu tupo wengi na tayari nishajitaja jina langu Mamujee so watu watanijua) bc Mahamood alinitafutia msichana mwengine kwa watu wa makampuni nikawa na wasichana wawili,, tuliishi vzr sana Mahamood alipenda sana watoto wake, nyumba yangu iliisha kabisa, namshukuru Mungu mnoo, nikahamia kwenye nyumba yangu na familia yangu,, kipindi hicho chote choko choko za bi mdogo zinaendelea, mara anitumie matusi, yaan shida tupu, Mahamood alinisisitiza sana nisimjibu kitu hadi pale atakapo yaweka sawa
Nipo zangu kwangu Salasala nishaanza kuzoea maisha yangu na Mahamood yupo anaenda kwenye biashara zake anarudi jioni,, nakumbuka cku moja shangazi yangu alinipigia cm nimuelekeze kwangu anataka aje anishukuru,, mumewe amepona,, nikamwambia shangazi usijali haina haja akasema hapana nielekeze kwako nije,, nikaongea na Mahamood kwanza akaniambia sawa mwache aje,, nikamwambia shangazi kwa sasa mm naishi Salasala, akasema sawa nitakuja jumapili nikitoka kanisani, bc jumapili ilifika kweli shangazi akaja na familia yake , amefika pale kwangu hakuamini akakosa furaha akawa mnyonge sana,, watoto wake wakawa wananiuliza Dada hapa ni kwako? Nikawaambia ndio,, shangazi alishangaa mm kujifungua bila kumjulisha, nikamwambia nilikwenda Arusha kwa Kaka, bc Mahamood alionana na shangazi yangu wakafahamiana ,. Ila shangazi alishikwa na butwaa sana hakuamini Amamu mm kuishi nyumba kama ile na Mume wangu Muarabu bc tuliongea mengi akanishukuru kwa ile pesa niliyompa kumuuguzia mumewe, nikamwambia shangazi usijali sisi ni ndugu uwe na amani,, muda wao wa kuondoka uliisha wakaondoka zao
Kumbe yale maisha yangu aliyoyaona shangazi yangu hapa kwangu yalimpa maswali sana na akaingia na chuki moyoni mwake, shangazi yangu ana mtoto wake wa kike mkubwa tu, tunalingana na mm kiumri ila mm ni mkubwa kama mwaka,(anaitwa Roby) pia na yeye alikuja nyumbani kwangu na mama yake, nashangaa Roby ananipigia cm Dada naomba nije kwako nina shida na ww,, hapo sijui chochote wala sifikirii kama anaweza kunifanyia jambo baya,, nikamwambia sawa njoo,, hapo Mahamood anajiandaa kusafiri kwenda Dubai,, alikuja kwangu vzr nilitegemea labda anakuja na kuondoka kumbe amekuja kuishi nashangaa amefika na begi kubwa, nikajiuliza kulikoni? Dada wa kazi akampokea vzr akaingiza room kwao,, hee kumbe mgeni kaenda kuoga kabadilisha na nguo kabisa Sasa nguo aliyoenda kuivaa jmn bora aliyovua,, kavaa kipensi kifupii na kisingrendi tumbo lote nje,, kaja kakaa sebleni hapo sebleni nimekaa na Mume wangu,, yaan mara ashushe mguu mara apandishe juu hadi Mahamood akashindwa kukaa akaenda chumbani,, kweli sikujua lengo lake ila kwa vitendo vile tu nilijua hapa ametumwa na Mama yaje anichukulie Mume
Itaendelea
23
Wapenzi nataka kuimaliza hii story,, nitapunguza baadhi ya sehemu, nipo bize mnoo na nyinyi nazidi kuwachosha
Nikashangaa sana roby kujiachia kiasi kile tena mbele ya Mume wangu?? Mahamood hakusema chochote aliingia chumbani akalala,, nikamwambia Roby ulisema unashida na mm bc njoo tuongee, akanijibu mbona unaharaka Dada? Tutaongea tu ucjal, bc nikakaa zangu kimya sikutaka kuendelea kuongea,, usiku ulifika tukaingia kulala, Mahamood akaniambia Mamujee, unajua huyo mdogo wako alichofata hapa?? Nikawaambia bado hajaniambia ila amesema ana shida na mm,, akaniambia hana shida yeyote Zaid ya kunitaka mm na ametumwa na Mama yake,, na hajaja mikono mitupu yupo na dawa za kienyeji kwenye begi lake uwiiiii wee Mahamood umejuaje haya yote na Roby ndio kwanza amefika,,??? Au hutaki ndugu zangu waje hapa??? akaniambia Mamujee subiri kesho pakuche uende ukakague begi lake,, mhhhh haya, tukalala, ila akili yangu yote ilikuwa juu ya roby, na yale maneno aliyoniambia Mahamood,, nikajiuliza hivi Mahamood ni nani?? Ni mtu wa aina gn?? Mhhhh, nikasema ngoja pakuche nikaangalie hilo begi nijihakikishie ni kweli au,, bc palikucha vzr, Mahamood alitaka kutoka maana alikuwa kwenye maandalizi ya safari ya kwenda kwake
Nakumbuka hio cku ilikuwa cku ya kuwapeleka watoto kliniki, nikaongea na Mahamood akaniambia Dada awaandae watoto dereva atakuja kuwafata awapeleke, bc nikamwambia Dada tukawaandaa watoto fasta, Mahamood akaniambia nimwambie na Roby aende akasaidiane na Dada, then Dada mwingine abaki kwa kazi za nyumbani, bc roby hakuonyesha kukataa alijiandaa na yeye na nguo zake za uchi,, tumekaa tunamsubiri dereva afike, roby akanifata, Dada Amamu, mwambie shemeji twende wote na yeye kliniki huyo dereva asije, nikamwambia shemeji yako ana mambo mengi nyie nendeni tu, akaniambia bc sawa ila hatuchelewi, nikamwambia sawa, dereva akafika wakaondoka zao,, nikamwita Dada nikamwambia niletee begi la roby, hapo tupo na Mahamood,, tukaanza kulifungua, mhhhh sikuamini jmn, madawa kama yote tena yanamaelekezo yake,, dawa za mvuto,, matumizi,, nawia usoni asbh na jioni,, nyingine tafuna,, nyingine ya mfarakano, weka kwenye chakula na chumbani kwao yaan jmn dawa kibao, cjui shangazi ananichukia kwa nn?? Utasema sijazaliwa na Kaka yake jmn,, mbona mm siringi? Hata sikumbuki walio nifanyia? Wakipata shida nawasaidia tu?? Mahamood akaniambia c nilikwambia?? Umeamini sasa?? Nikawaambia sasa tutafanyaje na dawa ndo izo?? Akaniambia subiri,, akaingia chumbani akatoka na viunga unga navyo ni dawa,, akamwagia kwa kila dawa, kisha akamwambia Dada rudisha hilo begi na msimwambie chochote akirudi,, Mahamood akatoka zake, nikabaki na Dada, akaanza kuniambia walivyokuwa chumbani usiku Roby alikuwa anaongea sana na cm yaan kama anapokea maagizo iv,, mara ile nyingine nitafune mara ngp au kila wakati?? Yaan mambo kibao,, nikabaki mdomo wazi, shangazi, shangazi shangazi, kwann unanichukia kiasi hiko??
Waliporudi kliniki kitu cha kwanza,, shemeji yupo wapi?? Nikawaambia katoka na leo usiku anasafiri,,, hee anaenda wapi tena?? Nikawaambia Dubai,, nikamuona kapooza aliduwaa utadhani kamwagiwa maji akanyanyuka akaenda nje kuongea na cm,, alivyomaliza akaja kuniuliza tena, eti atarudi lini shemeji akiondoka leo?? Nikawaambia Roby kwan vp? Umenifuata mm hapa au shemeji yako?? Kwan akisafiri ww unapata tabu gn wakati mm nipo?? Akanijibu amna nampenda shemeji Sasa akiondoka hapa kutapooza nikamwambia ndio kutapooza sana tu kwa sababu harudi leo wala kesho,, akanyanyuka akaenda chumbani kwao akalala
Chakula kilipoiva akaamshwa aje ale alitoka kavaa dera vzr, wamekaa mezani wanakula,, Mara Mahamood anaingia tunasalimiana na Mahamood, yeye kanyanyuka kaenda chumbani kwao, ametoka kavaa kimini kifupii na kiblauz kitovu chote nje,, huku mdomoni anatafuna mzizi wake wa dawa,, akawa anamsogelea Mahamood kumpa mkono, eti shikamoo shemeji,, Mahamood akakataa mkono akamwambia nina uzu naingia kuswali akabaki hee jmn
Itaendelea
24
Cjui shangazi yangu nilimkosea kitu gani kikubwa ambacho ameshindwa kunisamehe, kadri ninavyoandika hii story ya maisha yangu ndipo nazidi kukumbuka vitu vingi sana nilivyopitia, niliishi na shangazi yangu wa damu ila kama nilikuwa naishi na mtu baki, mara nyingi usiku alikuwa ananilaza njaa eti chakula kimepikwa kidogo niwaachie watoto wale, mm ni mtu mzima naweza kuvumilia njaa bc nilikuwa nalizika tu naingia chumbani nalala wao nawaacha mezani wanakula,, asbh chai sipewi eti vitafunio vichache niwaachie watoto ,,, leo nimepata kwangu bado anaendeleza chuki juu yngu?? Niliumia sana,,, mumewe kanibaka ila hakujali wala nn ,, maisha ni safari,,,,
Tuliingia chumbani na Mume wangu, maana ucku alikuwa anasafiri sasa nikaenda kumpa haki yake habari za kwa mparange hazikuwepo kipindi hiko tena nilimuandalia vitu vyake vzr akakaa na wanae huku anawasemesha maneno utadhani labda walikuwa wanamuelewa,, bc tukiwa tunaendelea kuagana, mara bi mdogo akapiga cm kwa mumewe, kama kawaida yao wakaanza kuongea kiarabu wenyewe, mara namsikia Mahamood, naenda Dubai leo natoka Tz, mwanamke alikuwa anamuambia mumewe asiende Dubai aende tena kwake maana amekaa sn Tz, wakaanza kuzozana, Mahamood akaanza kuongea Kiswahili, akamwambia, ww ni mke wangu sawa, na Shakira nae ni mke wangu ( bi mkubwa) ana haki zote kama ulivyokuwa ww,, tena ngoja nikwambie tu, huku Tz nimeoa, na nina watoto, Sasa kuanzia Sasa naomba uelewe nitapanga ratiba iwe sawa sawa, heee bi mdogo kapaniki mbona umeoa bila kunishirikisha?? Njoo unipe taraka yangu Mahamood akamwambia kama unataka taraka bc sio lazima mm nije huko naweza hata kukutumia kwenye cm ila uwe na uhakika kweli unataka taraka,, mhhhh, bi mdogo akakata cm nikasema hii ligi itahamia kwangu jmn ,, nikamwambia Mahamood asifanye ivo, akaniambia amechoka sana ataki tena kusumbuliwa na wanawake,, akaniambia alikuwa anataka watoto, amehangaika sana na wake zake kutafuta uzazi, amepoteza pesa nyingi sana, hadi wakafikia wapandikize , ila Mahamood alikuwa hataki kupandikiza, alitaka achukue yatima hata wawili awafanye kuwa wake,, ila tatizo alikuwa bi mdogo hataki yatima anataka apandikize ndipo wakawa wanapishana na Mahamood,, yeye bi mkubwa alikuwa tyr kupokea yatima,, bc Mahamood akaniaga kuwa anaenda Dubai then atarudi tena Tanzania nikamwambia vip kwa bi mdogo c uende kwanza? Akaniambia yeye apangiwi cha kufanya, amesha panga,, mhhhh nikasema ngoja ninyamaze bc muda ulifika dereva akamfata akasepa zake
Asbh kumekucha natoka sebleni nakutana na roby kavaa kanga moja ndani ana chupi tu tena bikini,, tukasalimiana , eti ananiuliza shemeji yuko wap?? Nikawaambia kasafiri, hee mbona kimya kimya,, nikamwambia kwako ndio kimya kimya ila me mkewe kaniaga jmn, nikashangaa ananisonya, nikamwambia roby vp mbona unanisonya?? Nimekukosea nn?? Au Mume wangu kusafiri kunatatizo gn?? Akaondoka akaingia ndani,, nimekaa zangu nakunywa chai nikashangaa anashuka na mabegi yake,, eti kwa heri mm naondoka,, nikamwambia mbona gafra?? Akasema nitakuja cku nyingine,, nikamwambia sawa msalimie shangazi,, katoka hadi getini, akarudi eti naomba hela ya nauli nikapandisha juu kumchukulia hela nikampa elfu 50,, hata asante hana akasepa zake
Nikasema huyu simsemeshi ngoja aondoke na asirudi tena hapa,,
Bc tumekaa na familia yangu, hapo bado sijaanza biashara zangu,, imepita kama wiki nawasaliana na Mahamood vzr hadi bi mkubwa,, nashangaa nashika cm yangu nakutana na vitisho vya bi mdogo eti nisipo achika labda sio yeye,, nikamjibu vzr, nikamwambia pambana na Mume wako achana na mm,, nikamblok,,
Niliamua kujiongeza nilikuwa na hela kwenye akaunti yangu na zile alizonipa Kaka nikaamua nitafute kiwanja ili nijenge nyumba ya kawaida nipangishe,, nikaongea na mtu maana tyr nilikuwa nishafahamiana na watu, nikapata kiwanja, mbele kidogo na kwangu, nikaanza ujenzi wangu kimya kimya
Shangazi akanipigia cm eti Mamujee nashukuru sana, kisa pesa zako ndio umeamua kumfukuza ndugu yako ,, eti usijisahau haya maisha tu,, umesahau nilivyokutoa kijijini kukuleta mjini? Eti nisingekuwa mm huyo mwanaume ungempata vp
Itaendelea
25
Ile sim ya shangazi wala haikunistua, nilishazoea lawama mie, nilimuacha aongee hadi alivyochoka yeye akakata cm, nikatafakari yale maneno ya Mahamood, kuwa huyu ndugu yangu kaja kwangu kwa nia mbaya,, na nilivyoona zile dawa kwenye begi la roby niliamini kabisa kuwa shangazi hana nia nzuri na Maisha yangu,, nilimpigia cm Kaka yangu nikamueleza kila kitu kinachoendelea, alinishangaa sana, akaniambia Mamujee hayo yote umeyataka mwenyewe, iv hao watu kwa wema upi waliokufanyia hadi una waweka karibu yetu?? Nilikwambia tangu mwanzo achana nao,, akaniambia subiri kwanza,, akakata cm,, kumbe akampigia cm shangazi akamwambia achana na Mamujee please, ni ndugu yangu, kama umeona hakuna umuhimu wa kutupenda bc tuachee,, Kaka akanipigia cm, akaniambia shangazi akinipigia cm nisipokee, nikamwambia sawa,, niliendelea na Maisha yangu , Mahamood tulizidi kuwasiliana na alizidi kuwapenda wanae sanaa,, ilipita kama miezi miwili iv Mahamood bdo yupo Dubai kwa mke wake, alinipigia cm akaniambia ananifanyia mpango wa visa na passport ili niende huko nipeleke watoto akawatambulishe ndugu zake maana asilimia kubwa ya ndugu wa Mahamood wapo huko,, nikamwambia sawa,, ila nilikuwa muoga mnoo but sikuwa na jins lazima wanangu wapajue kwao , akaniambia nichague Dada mmoja kwa ajili ya kunisaidia watoto, namshukuru Mungu sana Dada zangu wa kazi wote nimeishi nao vzr kama ndugu zangu, yaan ukifika kwangu huwezi kumtambua Dada wa kazi ni yupi na ndugu ni yupi,, nikamchukua yule nilietoka nae Arusha kwa Kaka, tukaandaa picha kila kitu Mahamood alimuagiza mtu akawa anashuhurikia hilo jambo,, nilitafuta mlinzi wa getini kutoka kwenye kampuni ili nikiondoka niache usalama nyumbani kwangu,, nilimtaarifu Kaka yangu kuhusu safari, alinitakia kila la heri,, bc tukaendelea kusubiri vitu vikamilike ili tuondoke,,, nakumbuka siku hio nipo tu nyumbani kwangu nilikuwa nafua,, huwa nafanya kazi za nyumbani kwangu japo kuwa nina wasichana wawili, napenda sana kufanya kazi,, cm yangu ikaita kuangalia namba ngeni,, nikapokea nikasikia sauti ya mwanaume,, Halow Amamu hujambo?? Nikamsalimia vzr, nikamuuliza nani mwenzangu?? Akaniambia mm ni Baba yako mdogo nikamsikiliza,, akaniambia yupo dar amemleta mtoto wake hospital ya oshen rod anasumbuliwa na kansa, walikuwa Bugando hospital Mwanza ndipo wamepewa rufaa kuja huku,, na amepimwa amekutwa na kansa ya utumbo nikampa pole,, akaniambia anaomba akutane na mm tuongee vzr,, nikamwambia sawa ila nitakujulisha,, nilishangaa sana, nikajiuliza namba yangu kapata wapi,, nikapata jibu ni shangazi tu,, nilikumbuka kile kipigo cha mbwa mwizi alichonipiga hadi nikapoteza fahamu,, wakaniburuza hadi chumbani,, mhhhh!! Dunia hii jamani, haina mwenyewe kwa kweli,, leo hii Amamu mm najulishwa kwenye matatizo,, mhhhh,, nikasema hapa nikimwambia kaka hili Jambo, atampandia gari amfate maana ana uchungu nae sana huyu Baba mdogo, nikanyamaza zangu,, na wao pia wanamuogopa matatizo yao yote wanaleta kwangu mie mnyonge wao,, bc niliendelea kusubiri vitu vikamilike vya safari yetu,, ikaisha kama wiki mbili, sijamjulisha Baba mdogo kitu chochote wala sim sijampigia,,, Mahamood alituambia kila kitu tyr tujiandae kwa safari wiki inayofata tunaondoka, bc tukazidi kufanya maandalizi mimi na Dada, huku tunacheka wenyewe na Dada, tunaambiana huko kwa waarabu tutaenda kuongea vp na watu bc tunacheka wenyewe,, mara tunaulizana iv tukichunwa ngozi jee tunachekaa huku tunajipa moyo, bhana wee liwalo na liwe
Safari iliwadia ilibaki kama cku tatu iv,, nipo zangu kwangu napiga story na madada zangu pamoja na mlinzi,, tupo nje,, nakumbuka siku hio tulikuwa tunabishana Kati ya Diamond na Kiba nani mkali wawili wanamtetea kiba, wawili wapo kwa Mond,, yaan tuligawana, bc ikawa kelele tunabishana haswa,, gafra geti likagongwa,, mlinzi akafungua kuangalia, wakaanza kujitambulisha, maana mlinzi alikuwa mgeni,, akaniuliza niwaaingize? Wanasema ni shangazi yako,, nikamwambia waache wapite,, jamani jamani,, alikuwa shangazi,, Baba mdogo, Roby,, eti wamemleta Baba mdogo nyumbani kwangu aje akae kwa kipindi chote anachouguza mtoto wake, na niwe nampa nauli kila cku ya kutoka Salasala kwenda oshen rod na ya chakula chake na mgonjwa,, kiufupi niwahudumie,, niliwasikiliza vzr hata sikujibu kitu,, nikamwambia Dada awape chakula,, nikaingia chumbani kumlaza mtoto alilala,, nikampigia cm Kaka nikamueleza kila kitu,, akaniambia waache hapo hapo usiwaambie chochote,, Naanza safari mda huu kuja huko,, nataka nionane nao mwenyewe,, usiwaambie chochote kama mm nakuja maana watakimbia,,
Itaendelea
26
Jmn wanawake wenzangu nimepitia Coment zote leo, najua wengi wananilaumu kuwa mm nashindwa kujitetea mwenyewe,, kiufupi mm sio muongeaji sn,, tangu nikiwa mdogo najulikana na ndugu wote kuwa Amamu sio muongeaji, nimerithi kutoka kwa Mama yangu, alikuwa mpole mnoo,, ndugu wa Baba walimfanyia kila aina ya vituko lkn Mama yangu hakuwai kunyanyua mdomo,, bc nimerithi kila kitu cha Mama yangu na iv watu wanasema cha kurithi kinazidi bc naona mie nimezidi
Bc nikarudi sebleni baada ya kuongea na Kaka,, nikawakuta wageni bado wanakula,, yaan Roby ndio kamuona Mama yake ndio anazidi kufanya makusudi, mara ashike hiki mara aulize hiki yaan ilimradi tu,, Mara da Amamu nifundishe kuendesha gari kwa gari yako,, au nimpigie rafiki yangu aje kesho anifundishe,, nikamjibu usijali nitakupa,, tumekaa tunaongea namuona Baba mdogo jicho halitulii Mara kangalia huku mara kageukia huku yaan anaonekana ni mtu mwenye maswali mengi kichwani kwake,, nilikaa zangu kimya nawaangalia tu,, ucku umefika nashangaa shangazi na mwanae hata hawaagi kuondoka maana walisema wamemleta Baba mdogo?? Nikashangaa hadi saa nne bdo wapo nikamuita Dada nikamwambia akaandae chumba cha mgeni wa kiume,, hao wengine watalala nao chumbani kwao,, niliwaaga nikawaambia naingia kulala,,, shangazi akaniambia na wao watakao hapa ili asbh tuwahi hospital kwa pamoja nikamwambia sawa,, nikaingia zangu chumbani kwangu,, niliwasiliana na Mahamood kama kawaida huku alinishangaa nisibebe minguo mingi nichukue chache au nisibebe kabisa eti kwenye ndege mizigo inapimwa uzito sasa nisije acha mizigo mingine airport,, bc tuliongea mengi ila sikumwambia kuhusu ule ugeni,, nilivyomaliza kuongea nae nikampigia Kaka nijue kafika wap maana ilikuwa kama saa sita ucku IV, akaniambia ndio anaitafuta charinze,, bc nikamwambia Mungu amlinde nikalala zangu
Asbh kumekucha hata sebleni sijashuka Roby kanifata chumbani,, eti Dada fungua,, nikamuuliza vp kwani?? Eti Mama kasema muanze kujiandaa,, hata sijamjibu na mlango sikufungua nikaendelea kulala,, mara mlinzi ananipigia cm, kuna mgeni getini amejitambulisha ni Kaka yako, nikamwambia aingie, bc kaka akawa amefika kwangu tyr, nikashuka hadi chini, nilifurahi sana kumuona Kaka, akaniuliza vp huyo Baba yako mdogo yupo wp?? Nikawaambia chumbani, akasema nenda kamwambie namwita nikamwambia atatoka mda c mrefu , hadi shangazi yupo hapa,, akasema na shangazi kalala hapa?? Nikawaambia ndio,, akasema kwa sauti,, HUU UKOO MASIKINI HUU nikamwambia Kaka usiseme ivo watasikia,, akaniambia unamuogopa mtu??? Mara shangazi anashuka kwa mbwembwe mwenyewe huku anaimba ( nimeuona mkono wa Bwana nimeuona) ghafra anakutana uso kwa uso na Kaka eti Mwita umelala hapa?? Upo dar hii hii?? Yaan Mwita hajajibu hata swali moja tyr kashamuuliza kumi Mwita akamjibu nimekuja leo,, Mara Baba mdogo nae huyoo,, alivyomuona Mwita akawa mpole,, eti shangazi ananiambia mie, Amamu bado haujajiandaa, nikawaambia bado,, Kaka akauliza kwani mna safari asbh yote hii?? Akasema ndio, Obara anaumwa amelazwa oshen rod wiki ya tatu sasa amegundulika ana kansa ya utumbo,, Kaka akasema sasa Amamu ndio anahusika nn huko hospital?? Shangazi kabla hajajibu, Kaka akamwambia, shangazi iv kwa nn mnapenda sanaa kunyanyasa watu?? Huyu Amamu ana watoto wadogo bado mbaya aende huko kwenye magonjwa ya hatari hatari aje alete shida kwa watoto?? Shangazi akasema amna sio lazima aingie ndani,, Kaka akamwambia shangazi sikia,, huyu Mamujee haendi kokote,, iv we Baba mdogo unakumbuka ulivyompiga huyu Amamu kiasi cha kutaka kumtoa uhai wake?? Sasa ungemuua leo hii ungelala nyumba ya nani? Nani angekupeleka huko hospital?? Baba mdogo kimya,, akamgeukia shangazi, akamwambia shangazi naomba muachane na Amamu please, mumempitisha kwenye shida mnoo na mateso, leo Mungu amempa nafuu bado mnamfata tena? Shangazi akasema Mwita mwanangu, tusikumbushe yaliyopita tugange yajayo,, Mwita akasema yajayo ndo kumfata fata nyumbani kwake? Iv hamuoni hata aibu kuja kujazana hapa? Mnadhani mumewe Amamu atawachukuliaje? Bc walijitetea ila aibu ikawashika,, Kaka akamuuliza Baba mdogo kwani ulivyotoka nyumbani kuja hapa dar ulimtaarifu amamu kama unakuja dar?? Akasema hapana,, Sasa kwa nn unamwambia kwa kumshtukizia kuwa unakaa kwake?? Ba mdogo, kimyaa,, Kaka akawaambia hapa kwa Amamu hakai yeyote kila mtu atakaa kwake au alipofikia, kama msaada unahitajika bc niambieni mm sio Amamu,, acheni kujitia aibu,, mnajidharirisha tu,, mhhhh Kaka aliongea jmn wote kimya,, Kaka akanigeukia mm,, ww Amamu sio unapokea pokea watu tu hapa kwako, umeolewa juzi tu leo mumeo anakuta ukoo wako wote umejaa hapa c atakuzarau?? Acha huruma ya kijinga, hapa mjini kila mtu apambane na familia yake heee Kaka anaongea kihuni tu bc walikubaliana shangazi amchukue ndugu yake akae nae kama misaada tutamsaidia huko huko
Bc tulipanda gari ya Kaka hadi hospital tukamuona mgonjwa kweli hali mbaya
Kaka akasepa zake nikarudi zangu kwangu
Safari ikawadia haoo tukaondoka zetu Dubai
Itaendelea
27
Hayaaaaa mjeeeeeee tumalize
Tulifika Dubai salama salmini, tukapokelewa vzr, bonge la jumba jmn waarabu kibao humo ndani ila wafanyakazi wako wa ndani wapo wanne, wawili wa Tz, mmoja mkenya,, mwengine wa Msumbiji,, nikapewa chumba changu cha kukaa na watoto ila Dada akapelekwa kwa wenzie, mhhhh nilikuwa naogopa jmn, nikimtazama bi mkubwa alivyo na mm nilivyo vitu viwili tofauti bi mkubwa masharah! Mzuri kaumbika haswa na rangi yake tamu,, yupo soft yaan ananukia balaa , nikajitazama mm na weusi wangu huu nikasema huyu Mahamood kipo alichofata kwangu sio bure,, nyumba imejaa watu, ukitambulishwa hadi unachoka,, mtoto wa shangazi, mara huyu mjukuu wa Dada yaan ndugu kibao wote weupe,, ila nashukuru walinipokea vzr kwa kuniheshimu sana mm na wanangu, tumekaa km cku tatu iv za kuondoa uchovu, cku ya nne nikaamka zangu asbh nikaenda kusaidiana na wadada kazi,, maana nishaoga kazi jmn, kukaa bure cwez tena kwa watu ndio kabisa, nikafika uani nikaanza kazi,, wale wadada wakawa hawataki niwasaidie, eti Dada acha hizo ni kazi zetu,, yule binti yngu akawa anawaambia huyu kazoea hata kwake tunafanya nae kazi , cjui ikawaje akaniona ndugu mmoja wa mule, mbio hadi kwa bi mkubwa,, wee bi mkubwa akashuka chini, a aniita Mke mdogo,, mbona?? Kwann unafanya kazi na watu wa kazi wapo?? Hayo sio majukumu yako,, unataka Mumeo akukute hapo atulaumu sisi huku sisi hatufanyagi kazi,, kumbe hawafanyi kazi yeyote jmn hata chupi wanafuliwa mhhhh mie cwez hivo vitu aka,, bc niliacha nikaingia ndani,, niliendelea kukaa pale huku najiona kama nipo kifungoni tu, cku hio nimekaa zangu chumbani kwangu nipo peke yngu maana asbh watoto wanatolewa wanakaa huko kama kulishwa, kuogeshwa kila kitu huko mm narudishiwa watoto usiku wakiwa wamelala,, bc nipo zangu chumbani, mara hodi bi mkubwa akaingia,, akaniuliza vp mbona huna raha? Nikawaambia amna Dada nipo sawa mbona? Akasema hamna bhana sifurahii ww kuwa ivo?? Niambie bi mdogo au umemmiss Mumeo?? Nikamjibu mbona kila cku namuona tu , akaniambia unakataa tu ila mm ni mtu mzima najua umemiss Mumeo mhhhh nikamwambia Dada hapana mm nipo vzr tu ondoa hofu,, bc tukawa tunapiga story ananiambia walivyokutana na Mahamood, kumbe alichumbiwa tu bila kuonana na Mahamood, wala walikuwa hawajuani ila wazazi wa Mahamood ndio walimpenda bi mkubwa, wakamuomba aolewe na mtoto wao,, akaniambia alikuwa bikra kabisa alivyoingia kwa ndoa, tuliongea mengi sana hadi alivyomruhusu Mumewe kuoa mke wa pili alipo jiona yeye uzazi umekuwa wa shida kwake,, akasema hata Yule bi mdogo wa Uingereza kumbe bi mkubwa ndio alimtafutia Mumewe ili amuoe Akaniambia nilivyojiona uzazi umekuwa wa shida kwangu nikawaambia Mume wangu AOE ila Mume wangu alikuwa hataki hata kusikia, nilimlazimisha sana hadi kushirikisha ndugu zake ndipo akakubali kuoa ila kwa sharti mm nimtafutie huyo mke, bc nilimuahidi kumtafutia, akasema cku moja alivoenda kwenye shughuri ya Mama ake mdogo alikuwa anaozesha mwanae ndipo akakutana na bi mdogo na yeye alikuja harusini upande wa Bwana harusi,, bc bi mkubwa akampenda yule Dada, akamuomba mawasiliano wakabadilishana vzr, bc wakaanza kuwasiliana taratibu ndipo kumuuliza kama kaolewa, akamwambia hajaolewa,, ndipo bi mkubwa kumuomba aolewe na mumewe Kama bi mdogo,, ndipo yule bibi kukubali akakutaniswa na Mahamood , wakaridhiana ndipo ndoa ikafungwa,, ndipo yeye kupelekwa kuishi huko Uingereza maana Mahamood anabiashara zake huko pia na nyumba zake mbili , nilimshangaa huyu mwanamke nikasema huyu mwanamke ana moyo wa dhahabu jmn,, mhhhh, bc tuliongea mengi mnoo,, akanitania leo nitakuachia Mumeo ulale nae ingawa ni zamu yngu ila acha nikupe mdogo wangu uondoe uchovu uchangamke nikaona aibu, nikamwambia Dada hapana bhana,, bc tukatoka kwenda kula,, ucku umefika nikaingia chumbani kwangu nikaletewa wanangu, nikawalaza kwenye kitanda chao, nikaingia bafuni ili nioge nilale,, natoka bafuni mlango wangu unagongwa, kufungua Mahamood, nikamwambia vp mbona ucku, akasema amekuja kulala,, nikawaambia kivp c upo kwako?? Akasema bi mkubwa amemuomba alale kwangu wiki nzima mhhhh,, nikamwambia c zamu yake?? Akasema ndio ni zamu yake ila amekuruhusu,, Mahamood akaniambia akiwa Dubai bc ni zamu ya bi mkubwa,, akiwa Tz ni zamu yngu,, na kwa bi mdogo ivo ivo,, bc tukaenjoy kwa penzi la ugenini,, Mahamood ananiambia nilivyokumiss nilikuwa najikaza tu nitafanyaje sasa ,, bc asbh Mahamood kaenda kazini kwake,, bi mkubwa akaanza kunitania,, Leo bi mdogo umechagamka,, kumbe kweli ulimmiss Mumeo , eti c ungeniambia Dada namuomba Mahamood anifanyie massage nitoe uchovu, mm wala nisinge kunyima nikacheka sana huyu Dada ana moyo wa tofauti
Itaendelea
28
Daah hadi naona haya natamani ingekuwa wtsap nikatuma voice note nimalize,,
Nilikaa pale Dubai kwa raha sana outing kama zote kiufupi nilienjoy sana sana, wakati wa kurudi Tz uliwadia, nikaanza kujiandaa kurudi, bi mkubwa akanishauri nisikae bure nitafute kitu cha kufanya, akaniambia nikifika Tz nitafute frem nzuri ya kuuza nguo then yeye atakuwa ananifungia mizigo Dubai ananitumia Tz, kweli nilikubari wazo lake,, jion ilivyofika Mahamood alirudi bi mkubwa akamwambia kuhusu wazo la biashara, Mahamood hakubisha akamwambia tu bi mkubwa aanze kunitafutia huo mzigo coz mm nikifika Tz tu naanza kutafuta flem,, kweli nilijiona mwenye bahati mnoo wala sikuwahi kuwaza kwenye maisha yangu kama ipo siku na mm nitakuwa mtu kwenye watu , niliendelea kukaa pale nikisubiri Mahamood anashuhurikia tiket,, ila nikiwa pale nikawa sielewi,, kuna chumba maalumu ambacho hakifunguliwi ovyo,, na ikitokea kimefunguliwa bc Mahamood yupo hapo au bi mkubwa anaingia ila mara moja moja mno labda kufanya usafi,,. Mhhhh mara ya kwanza nilikuwa sijali, ila kadri nilivyozidi kukaa pale nikawa natafakari sana,, mara nyingine watu wanakuja watu wenye hela ukiwaona mwenyewe unakubali kuwa hawa watu pesa wanayo,, yaan hao watu wanakuja wakati Mahamood yupo na wakija tu wanaingia kwenye hiko chumba,,, nikajiuliza hawa watu niwakina nani?? Na humu ndani wanaenda kufanya nn?? Kweli mwanzo niliumiza kichwa sana na sina wa kumuuliza,, japokuwa mm ni mke wa Mahamood ila nilikuwa sijamzoea sana kumuuliza uliza vitu ovyo nilikuwa cwez, nikasema moyoni hapa hadi nijue humo ndani kunafanyika nn,, hiko chumba kiko chini, nyumba ni ghorofa moja ila ina vyumba vingi,, iko chumba Sasa kipo chini na mm nalala juu, kwenye hio nyumba kuna sebure mbili, juu na chini,, hio sebure ya chini kiufupi haitumiki,, inafanyiwa usafi kila cku ila hawakai wote wanakaa juu,, hiko chumba chenyewe kilichonipa hofu kipo chini pembeni mwa sebure,, nikaanza uchunguzi wangu wa kimya kimya sikumuuliza bi mkubwa wala Mahamood,, chumba changu cha juu dirisha lake linatizama geti kubwa la magari,, nikiona gari linaingia getini watu wakishuka tu, nasogea hadi karibia na ngazi nachungilia kwa chini bc nawaona hao wageni wanavyoingia kwa hiko chumba,,, nilifanya upelelezi wangu ila sikugundua kitu,, nikawa na hofu nikakosa amani najiuliza hawa ni wakina nani hasa?? Mbona wana siri zao wanazificha kwangu??
Bc safari ya kurudi Tz ilizidi kuwadia zilifika kama cku tatu safari ianze, na hapo sijajua chochote kuhusu hiko chumba,,, Waarabu wanapenda sana mambo ya kutoka out sana,, kwenda kwenye pikinik,, mara kula Ice cream, yaan wanapenda sana,,, mm tangu nifike Dubai walishanipeleka sana izo sehemu,,, nakumbuka ilikuwa cku ya jumapili,, wamejiandaa vzr wote wanataka kutoka, kasoro madada wa kazi tu,,, nilikuwa chumbani kwangu,, akatumwa mtoto aje aniambie nijiandae,,, wala sikumbishia nilijiandaa vzr nikajipodoa hasa kisha nikalala,, wakaja kuniita nikawaambia kichwa kunauma sana,,, bi mkubwa akaja hadi chumbani kwangu akaniuliza Mamujee vp? Nikawaambia Dada kichwa kinaniuma sana cwez kutoka leo,, bc akaniletea dawa akaniambia nipumzike kama kuna shida yeyote niwapigie cm,, bc nikamwambia sawa,, Mahamood akuwepo cku hio
Walivyoondoka tu nikamwita Dada yangu wa kazi,, maana kabla alikuja kuniambia kuwa kuna madada wale wa kazi, Sasa wale wawili wa Tz,, wameomba cku tukiondoka bc watupe mizigo kidogo na pesa tuwapelekee ndugu zao,, nikamwambia aniitie mmoja wao,, bc alimwita nikashuka chini maana wao wanalala nje kuna vyumba sio mule ndani,, alivyokuja nikaanza kumuuliza kuhusu kwao akanielekeza vzr nikamwambia sawa nitakwenda,, nikamuuliza kuhusu pale na watu wanavyokuja,, akaniuliza kwan hujui?? Ww c mkewe?? Kwann ajakwambia Mumeo?? Nikawaambia wala hajaniambia na mm sijaolewa mda mrefu sana,, akaniambia bc nikikwambia usimwambie hadi akwambie mwenyewe,, nikawaambia wala usijali mm shida yangu kujua tu bc
Akaniambia Mumeo ni MGANGA Tena Mganga mkubwa sana Dubai,, anatubu watu wakubwa,, Viongozi na Matajiri anafahamika sana sana heeeee Mamujee mm nimeingia wapi?? Tobaaaa,,, nikaishiwa pozi mwili wote ukaingia baridi,,, nikajiuliza kumbe mara ya kwanza nilivyokutana na Mahamood akaniambia nina nyota kali sana tena ya utajiri sikujua ana maana gn kumbe yeye ni mganga??? Hata Roby alivyokuja kwangu na dawa aliziona nilijiuliza amejuaje kama roby ana madawa kumbe ni mganga??? Hata nilivyojifungua wanangu kipindi nipo Arusha alivyokuja hakuwa na haraka ya kujua watoto jinsia gn kumbe alishawaona kwa uganga wake???
Nilikosa raha kwann amenificha hakuniambia mapema?? Nikamchukia kuanzia hapo
Vipenzi nipo bize sana nikipata mda nitaandika tena,, ila ndo ivo
29
Nilijikuta namchukia Mahamood, kwann amenificha hakuniambia mapema kama yeye ni mganga?? Nirirudi ndani nikaingia chumbani kwangu nikalala, mara wakarudi waliokwenda matembezi, bi mkubwa akaja chumbani kwangu kunijulia hali, nikawaambia naendelea vzr, bc aliniletea Ice cream na zawad nyingine,, tukatoka hadi sebleni tukawa tunapiga story,, akawa ananipa mbinu za biashara na jins ya kuliteka soko,, bc nilimsikiliza,, akazidi kuniambia jins ya kufanya biashara, kwanza nikae mwenyewe dukani hata km nitakuwa na wasaidizi,, nilimshukuru sana,, akawa anasema atawakumbuka sana mapacha wangu,, anatamani wakue awachukue akae nao, nikawaambia usijali wakikua tu atakaa nao,,
Cku iliwadia safari ya kurudi Tz ikafika,, wakati tunajiandaa kuelekea airport, Mahamood alinitazama usoni akaniambia Mamujee NAKUPENDA SANA MHHH nikajiuliza au amejua nimejua? Bc nikajiandaa fasta watoto wameandaliwa, na Dada nae, hao tukaelekea airport,,
Tumefika Tz salama kabisa, ila nikawa sina amani na Mahamood,, kwann hakuniambia?? Tulikuwa tunawasiliana vzr ila sikumwambia kuhusu uganga wake,, bc nilipumzika kama wiki mbili tu, Mahamood alikuwa ananisisitizia kuhusu flem,, nikawaambia sawa naanza kutafuta,, akaniambia niende mliman cty nikatafute flem pale ndani,, kweli niliuliza nikapewa utaratibu wa kupata pale,, nilifanikiwa kupata flem pale mliman cty,, Mahamood alinitumia pesa nikalipia,, ndio duka langu la kwanza nililofungua na lipo mpaka leo,,,
Bi mkubwa alinitumia mzigo, ulikuwa mzigo mzuri wa kutosha, nguo za watoto tu kiume na wakike,,, namshukuru Mungu sana sana ndio biashara yangu ya kwanza,,, bc nikawa na biashara yangu,, niliwasiliana na Kaka yangu nikamueleza kuhusu nyumba yangu ambayo najenga mm mwenyewe,, Kaka aliniongezea tena hela ili nimalize ujenzi,, kweli nilimaliza kila kitu na kuipangisha,, kiukweli namshukuru Mungu sana,, hata kama Mahamood anaitumia Nyota yangu bc na mm nafaidika,, nyumba ya Salasala ni jina langu kwenye hati,,, gari jina langu kwenye kadi,, duka ni jina langu,, nikasema hata ivo nashukuru
Niliendelea na biashara zangu ilipita kama miezi miwili na nusu iv Mahamood akaja Bongo,,, nilipunguza mapenzi kwake nikawa namuogopa sana,, cku hio nimekaa zangu dukani kwangu nipo na mdada mfanyakazi wangu,, Mahamood alikuja dukani,, akazunguka mle dukani kama Kuna vitu anavifanya,, nilimuoa ila nikakausha,, bc kuanzia muda huo wateja wakaanza kuingia mfululizo,, tena nikauza sana tofauti na cku zote,, nikasema hili silinyamazii lazima nimuulize,,, tulirudi nyumbani tukala, wakati tupo chumbani nikamuomba nimuulize jambo, akasema niulize mke wangu,, nikamuuliza naomba uniambie pale dukani ulikuwa unafanya nn na ulipomaliza tu wateja wakajaa dukani?? Kwanza alicheka, then akataka kukataa, nikawaambia niambie ukweli na ukinificha tu mm na ww bc hatuwezi kuwa mke na Mume then tunafichana vitu,,,, ndipo akaanza kufunguka,,, yeye ni mganga amerithi kutoka kwa marehemu Baba yake,, alikuwa hapendi kufanya hio kazi ila alilazimishwa sana,,, kumbe bi mkubwa wazazi wa mwanaume walimuona anafaa ndio wakamuolea mtoto wao,, ananiambia uganga wa Baba yake umewasaidia wengi sana. Na alivyofariki mikoba akapewa yeye,, nikawaambia sasa kwa nn umenificha?? Akaniambia angeniambia tu,, akazidi kuniambia anatibu watu wengi mnoo nikamuuliza kwahyo utajiri wako unahusiana na uganga?? Akaniambia sio asilimia kubwa,, akaniambia wao ni Matajiri sana kuanzia Babu yake akaja Baba yake Sasa amerithi yeye ,, nilimsikiliza akaniambia vitu vingi sana
Akaniambia cku ya kwanza niliyokuona niliona Nyota yako, nilitaka nikutumie tu kama wanawake wengine ila nilivyomaliza kufanya nilichofanya nikaambiwa nisikuache,, nikajiuliza nitakupataje tena?? Ndio sababu nikakupa cm na zile pesa,, ila ulivyokuwa hujanitafuta nikauliza wakubwa wangu wakaniambia kila kitu kuhusu ww,, nikawa nakufanyia dawa hadi ukawasha cm Akaniambia nimekupenda hadi wakuu wangu wamekupenda ndio sababu sijakufanya tena kinyume na maumbile ni ww tu ambaye sikufanyi hivo tena coz nakupenda sana na wakuu wangu wamekupenda,, ila bi mkubwa namfanya kinyume na maumbile pamoja na bi mdogo daaahh niliishiwa nguvu
30
ml wapenzi nimepitia comments zenu,, bi mkubwa na bi mdogo walikuwa wanaingiliwa kinyume na maumbile na Mume wao, ila sio mara zote au sio nyuma tu hata mbele kwenye njia ya uzazi walikuwa wanaitumia pia ndio sababu walitafuta watoto,, binafsi Mahamood aliniingilia kinyume mara mbili tu yaan cku mbili tofauti ila kwa kiasi gani sijui coz alikuwa ananiwekea madawa maana nilikuwa sijitambui kabisa ila nikiamka ndio najikuta nimechafuka na maumivu makali
Bc alivyoniambia vile nikashikwa na butwaa, akaniambia Mamujee NAKUPENDA SANA , ww ni mwanamke ambaye nimekupenda mm mwenyewe, nilikuona nikakufata, sio kama sijawahi kuwa na wanawake wengine kabla yako? Nilikuwa nao wengi tu ila ww nimekupenda kutoka ndani ya moyo wangu, nikawaambia sasa kwann unaendelea kuwaingilia hao wake zako kinyume?? Akaniambia wao wenyewe wamezoea wanaona kawaida tu mhhhh nikaziacha hizo habari maana nilikuwa naona kama naumiza moyo wangu nikikumbuka alivyoniingilia na mm
Akaniuliza Mamujee mbona unafanya vitu vyako kimya kimya na hunishirikishi mm?? Mhhh nikashangaa nikamuuliza vitu gn? Akaniambia ww mwenyewe unajua ni vitu gn unavifanya,, nikamwambia niambie ni vitu gn bhana,, akaniambia mbona umejenga nyumba bila kunishirikisha?? Mhhh, nikamwambia kweli Kaka yangu alinipa hela kwa mara ya kwanza nilivyokutana nae ndio nikanunua kiwanja na kujibana ndio nikajenga, akasema wala sikulaumu kujenga,, ni vzr na una akili nzuri, tatizo kwa nn umenificha?? Nikamwambia nilitaka nije nikwambie, bc akanyamaza, kiufupi Mahamood ni mtu muelewa sana,, kuhusu uganga wake ulizidi kunipa mashaka sana, niliogopa sana, kiufupi siwapendi waganga wa kienyeji nawaona kama wachawi tu,
Maisha yaliendelea huku nipo bize na biashara yangu, Mahamood nae yupo bize na biashara zake,, akiwa huku Tz hafanyi uganga wake,, Mahamood alikaa sana Tz kama miezi minne iv, mzigo dukani kwangu ukapungua, nikamuagiza tena bi mkubwa akanitumia, mawasiliano yangu na bi mkubwa yalizidi kuongezeka, tukatoka kwenye uke wenza tukawa marafiki wakubwa tu, bi mdogo akazidi kumsumbua mumewe anataka taraka,, Mahamood akaniambia Mamujee ngoja niende kwa bi mdogo nikampe taraka yake nikamwambia sababu nn ya kumpa taraka?? Akasema sitaki kupangiwa maisha, mhhh nikayaacha km yalivyo,, wakati Mahamood anajiandaa kusafiri,, nilipatwa homa kali sana, nikapimwa nikagundulika mjamzito,, hapo mapacha wangu wana miaka miwili kama na nusu iv,,. Mahamood alifurahi mapenzi yakazidi kwangu,, akajisahau kabisa kama ana wanawake wengine,, safari ya kwa bi mdogo iliwadia akaondoka zake,, mimba ilinisumbua sana tofauti na mimba ya mapacha, nikawa mtu wa kulala ndani tu,, dukani ikanibidi niongeze mtu mwingine,, nashukuru Mungu nilipata watu waaminifu sana,,, bc Mahamood alifika kwa bi mdogo akamwambia umetaka taraka nimekuja kukupa, bi mdogo akaanza kulia akimlaumu Mahamood kuwa yeye ndio chanzo cha yeye kuomba taraka,, hata ivo hataki taraka bado anampenda mumewe , bc waliyazungumza wao wakasameheana ,, Mahamood alikuwa ananipa taarifa zote za huko,, bi mdogo akakubali Mamujee kuwa mke mwenzie na kuniachia cheo cha bi mdogo
Bi mdogo alinipigia cm tukaongea akanikaribisha nyumbani kwake kwanza then yeye ndio aje kwangu,, tuliongea vzr, ila kuhusu mimba yangu hakuwa anajua chochote
Kiufupi mm sikuwa na shida na yeyote yule wote nilikuwa nawaona sawa, Mahamood hakukaa sana kwa bi mdogo alikaa kama wiki tatu tu akarudi Tz,, akakaa kwangu hadi mimba yngu ikafika miezi sita,, ile hali ikamkasirisha bi mkubwa,, nikashangaa tu nikimpigia cm hapokei, nikimtumia msg hajibu kwa wakati,, sikumwambia Mahamood kama bi mkubwa hapokei cm zangu, nikaanza kupata nafuu kidogo kidogo,, nikaongea na Mahamood nikamwambia nipo sawa Sasa aende kwake,, Mahamood akawa hataki kabisa kuniacha,, nakumbuka siku hio karudi zake nyumbani vzr,, nikakaa nae chini nikaongea nae kwa hekima,, nikamwambia Mume wangu,, ukumbuke ww una wanawake watatu,, sio Mamujee peke yake,, Sasa hao wanawake wengine nao wanakuhitaji nenda kawape haki zao,, nilimbembeleza sana mwisho akakubali kwenda Dubai,, akaniambia ila hatokaa sana,, nikamwambia hapana nenda kakae na mkeo
31
Mahamood aliondoka zake kwenda kwake, nikabaki mwenyewe najiuguza huku nikisaidiwa na madada zangu wa kazi, hali yangu iliendelea vzr, ilipita kama wiki tangu Mahamood aondoke ila tulikuwa tunawasiliana mara kwa mara, nikashangaa napigiwa cm na bi mkubwa, nikajiuliza kulikoni tena? Maana yeye CM zangu alikuwa hapokei, nikapokea vzr nikamsalimia wala sikuwa na shida, akaniitia Mama wawili, eti ww mjamzito?? Nikawaambia ndio Dada, akaniambia sasa kwa nn umenificha?? Nikawaambia Dada nilimuachia Mahamood akwambie mwenyewe kwan hakukwambia?? Akaniambia wala hakuniambia,, Sasa kwa nn umenificha mdogo wangu?? Mm nakulaumu kwa kosa la kuruhusu Mume wetu akae kwako mda mrefu, kumbe upo na shida? Bc nisamehe sana mdogo wangu, sikujua kama mjamzito na inakusumbua kiasi hicho, nikawaambia Dada usijali, nisamehe na mm kwa kukosa kukwambia mapema, akaniambia Mamujee huyu mwanaume ni Mume wetu wote, ukiona anafanya kitu cha kumuonea mwingine inabidi uikemee hio hali, usiiache ikakomaa, tumekubali wote kuwa wake wenza, bc tupendane tuishi kwa kupendana, ungeniambia mapema kama ni mjamzito wala nisinge kulaumu,, bc tuliongea mengi na Dada tukasameheana,
Nilipigiwa cm na shangazi kunipa taarifa za msiba, yule mgonjwa mtoto wa Baba mdogo amefariki, nikampigia Kaka kumpa taarifa kumbe na yeye tyr amazipata, msiba utasafirishwa kupelekwa nyumbani Musoma, bc nikamwambia kaka hali yangu ya afya tukakubaliana Kaka ndio ataenda mm nipumzike, bc nikawa nipo tu nyumbani kwangu,. Shangazi akawa anapiga cm kama ugomvi, we Amamu kwann huji msibani? Maana msiba waliweka nyumbani kwake kwanza taratibu za kusafirishwa zikiendelea, nikamwambia shangazi mm naumwa, bc kama nilimchokoza, unaumwa? Kuumwa ndio kukufanye usije msibani?? Nyie watoto mnaringa sana, mnajiona mmefanikiwa ndio mmekuwa na dharau, Sasa itajulikana tu, kwanza nyie sio damu yetu ingekuwa damu yetu bc mngekuwa mnatusikiliza na kutuheshimu,, shangazi aliongea hadi alichoka,, cm ilivyokata nikampigia Kaka nikamueleza, Kaka akaniambia Mamujee tulia niachie mm, mm nakuja huko leo, nikawaambia mbona mda umeenda sana utaanza safari usiku? Akasema atakuja kwa ndege,. Bc nikamsubiri Kaka aje ili tujadiriane tunafanyaje, nikampigia cm Mume wangu kumpa taarifa za msiba, alinipa pole akaniambia atanitumia pesa ya mchango ila mm nisiende popote,,
Kaka alifika alikuja moja kwa moja nyumbani kwangu, tukakubaliana yeye ataenda hadi Musoma, bc nikamwambia awahi kwenda msibani maana shangazi asizidishe lawama zake, Kaka alienda, shangazi alipomuona Kaka akapumua maana alichanganyikiwa kuhusu msiba ila alitaka huzuni zake azilete kwangu, nikajulishwa kuhusu mchango, wakati huo Mahamood alikuwa tyr amenitumia na mm nikatuma mchango wangu, walisafirisha msiba hadi nyumbani, wakazika vzr, Kaka alinipigia na kunipa wazo la kuwajengea wazazi wetu makaburi nikamwambia kaka sawa, ngoja nikutumie hela, Kaka akaniambia ni vzr na ww utoe hela ili wazazi wetu huko walipo waone tunawathamini, bc nilimtumia Kaka hela na yeye akatoka yake tukawajengea wazazi wetu , makaburi ya wazazi wetu yapo karibu,, tulimshukuru Mungu kutupa uwezo na akili ya kuwakumbuka wazazi japokuwa wametangulia mbele za haki,,
Biashara yangu iliendelea vzr mauzo yakawa makubwa cjui Mahamood alifanya kitu gn jmn ila nikazidi kumshukuru Mungu, na watu niliowaweka dukani walikuwa waaminifu kwa kiasi furani
Mimba yangu ilipofika miezi 8 hapo bado Mahamood yupo Dubai, Mahamood alinipigia cm akaniambia bi mkubwa anakuja kwangu kunihudumia hadi nijifungue, nikashukuru nikamwambia sawa, bc bi mkubwa nae akaniambia kuhusu safari yake, ila ananifungia mizigo kabisa anaanza kuusafirisha, bc tukakubaliana ivo,, kweli nilipokea mzigo wangu, wiki iliyofata bi mkubwa akaingia Tz, nilienda kumpokea airport na mimba yangu, aisee bi mkubwa alifurahi kuniona mie mjamzito, tulikumbatiana pale safari ya nyumbani ikaanza tuliongea mengi maana bi mkubwa hakutaka kabisa kulala chumba cha wageni tulilala pamoja, mtoto tumboni akicheza bc anashika tumbo langu anafurahi mwenyewe ananiambia cku akipata mimba bc Dubai nzima itajua ilikuwa raha sana bi mkubwa alivyo kuja kwangu, akanipa wazo la biashara lingine, akaniambia Mama wawili, iv unaonaje hapa kwako ukajenga fremu? Then ukawa unauza vitu vya umeme kutoka Dubai?? TV, friji, brenda NK? Nikawaambia Dada wazo zuri, akaniambia bc lifanyie kazi, hata sikuchelewa nikawaita mafundi wakaanza kunijengea fremu
Itaendelea
33
Shangazi yangu mkorofi sana namjua vzr ananitafutia sababu na hii mimba niliyonayo sijui yukoje anafahamu fika mm na Roby hatuwezi kukaa pamoja hata nusu saa ila ameamua kumuacha nyumbani kwangu wala hafikilii kuhusu hali yangu, niliwatizama mtu na mama yake wanaenda kusengenya tena nyumbani kwangu
Roby akarudi baada ya kuachana na mama yake, akaanza kunikejeri vp da Amamu unaenda kuzalia wp Ulaya au Buza? Nikaishia kumtazama tu, nikamwita Dada wa kazi aniletee matunda nile maana kula yangu ilikuwa ya tabu sana akarukia yeye mletee ale si unajua tena mke wa muarabu anatakiwa ale ashibe huko leba si mchezo kuwekwa mitambara?? Nikamwambia Roby naomba tuheshimiane kama umekuja nyumbani kwangu kwa heri bc ukae kwa heri ila kama umekuja na yako yatakurudia mwenyewe
Bhana eee kwani uongo? Si mnafirwa nyie? Nani asiyejua kama waarabu wafiraji?? Nikamwambia ndio kwani nikifirwa mkundu si wangu? Ww kinakuwasha nn?? Kama kufirwa kunalipa na ww c ukafirwe kwan mkundu huna? Nilimjibu wala sikumkawiza sikujali hata kama Dada yangu wa kazi anatuangalia
Eti bana ee mm ndio nishakuja kwako hata ukichukia sitoki ww ulivyokuwa unakaa kwetu? Malipo ndo haya shoo kama hupendi kunya huyo mtoto atoke
Dada yangu wa kazi akaniambia Dada acha usijiumize
Basi roho iliniuma yaan natukanwa nyumbani kwangu? Nikanyanyuka nikamuacha Roby nikaenda chumbani nikamkuta bi mkubwa amelala na watoto nikatoka tena nikashuka chini nikaenda nje kwa mafundi waliokuwa wananijengea frem nikakaa kimya
Nimekaa nje na mafundi wao wanajenga mie nawaangalia vp Dada mbona kama una mawazo sana? Hapana nimetoka kupunga upepo tu bc tukawa tunapiga story na mafundi
Bi mkubwa alitoka alikuwa akinitafuta akanikuta nipo na mafundi, Mama Wawili mbona huko huku? Nikamwambia nipo tu nimeona wote mmelala nikaona nisiwasumbue,
Tulirudi ndani tukaenda kukaa sebleni mara Dada wa kazi akaniletea yale matunda niliomuagiza, tupo sebleni na Roby nae akaja sijui alitoka kuoga maana alikuwa kabadilisha nguo kavaa kikaptura kifupi vile vinaitwa vikumanina nadhani mnavipata kavaa na kitop tumo lote wazi, kaona nipo na mtu na hamjui ila hata salamu hajampa kafika katukuta tunaangalia mieleka kaja nilipokaa kachukua limoti kabadilisha kaweka miziki
Nilibaki namuangalia, Bi mkubwa akaniuliza huyu ndugu yako? Nikamwambia ndio ni mtoto wa shangazi yangu bi mkubwa aliguna tu mhhh
Jioni nikiwa nimejilaza kwenye kochi nipo na huyo Roby alikuwa bize na cm yake bi mkubwa yupo juu anawapa chakula cha usiku watoto mara cm yangu ikaita kuangalia ni bi mdogo wa kati nikasema mama mama mama nafwa na hivi kapewa taraka moja mbona hasira zake zote juu yangu mie Mamujee? Niliogopa kupokea ila nikasema ngoja nipokee tu sina jinsi halow habari za mida? Nikaduwaa maana kanisalimia kwa heshima na utulivu, nikamjibu salama Dada,, mdogo wangu nisamehe sana kwa nilivyokwambia mara ya kwanza nikamwambia haina shida Dada wala usiombe msamaha mm sina tatizo na ww, Sawa Mamujee ila nataka nikuambie jambo ila uniambie kama utakuwa na kifua? mhhh nikamwambia Dada kama unahofu na mie bc usiniambie ila mie sina shida, haya ngoja nikwambie huyo mke mwenzio hapo hakuja kwa bahati mbaya usione amekuja huko ukadhani kweli unapendwa kaja kukuuguza huyo mwenzio kafata huyo mtoto akishirikiana na mumeo lengo lao ni KAFARA na damu ya Mahamod ndio inatakiwa itoe alitakiwa atoe hio kafara mda tu kwa hao mapacha ila Mumeo alikataa kwa sababh hana watoto wengine ila ulivyopata ujauzito ndio wameamua wamtoe huyo wa tumboni na huyo mke mkubwa yupo kusubiri mtoto,,,, nimeamua nikaambiwa ukweli si wamejifanya kunipanda kichwani wameshauriana nipewe taraka sasa nimekwambia ukweli akili kichwani mwako ukimtaka mtoto huyo bc nenda kajifungulie kwenu huyo mke mwenzio sio mtu mzuri pamoja na huyo mumeo
Daaahhh nilichoka hapo Roby ananitazama usoni nilivyokuwa naongea na cm
Itaendelea
34
Yale maneno ya mke mwenzangu yalinifanya nitafakari anayosema ni kweli au ameamua kugombanisha sababu kapewa taraka? Nikazidi kuchanganyikiwa mbona kama asemacho ni kweli mbona adui zangu wanazidi kuongezeka Mamujee mm? Nilibaki na bumbuwazi sijui nifanye nn? Nimuamini mke mdogo wa Mahamod? Au nimuamini Mahamod kwa kumleta mkewe nyumbani kwangu anisaidie kazi? Nilipooza nikawa mnyonge sana huku shangazi na mwanae sijui wanapanga nn juu yangu? Huku nako naambiwa haya?
Sikuongea chochote maana Roby alikuwa ananiangalia kama anataka kujua nimeongea na nani na nimeongea nn
Nikaanza kupata wasiwasi cjui ulitokea wapi ila nilipata hofu sana
Roby alikaa kwangu kama siku tatu iv akaniaga anaondoka nikamwambia sawa wasalimie sikumpa hata mia
Aliondoka zake nikabaki napambana na maisha yangu,, bi mkubwa sikumwambia chochote kuhusu ile cm ya mke mwenzetu nilikaa kimya
Maisha yakaendelea hatimae mimba ilifika miez tisa na ujifunguaji wangu ni Opp nikaandikiwa cku ya kufanyiwa opp bc nilikaa kujiandaa ila nipo nimechanganyikiwa nafikilia maneno ya bi mdogo bado yapo kichwani hata nijisaulishe vp ila hayatoki,,,, mume wangu ananipigia cm kunitia moyo maana presha ndio lilikuwa tatizo kwangu inapanda mara kwa mara nilitamani nipate mtu wa kumuhadisia yale maneno ila sikumpata nimwambie nani? Kaka yangu? Hapana sina uhakika nayo kama sio ya kweli huoni nitakuwa nimeweka doa kwa kaka yangu juu ya Mahamod?? Cjui nimwambie nani matatizo yangu sina Wazazi hata shangazi yangu simuamini yeye ndio yupo tayari kufurahia kifo changu
Nikapata wazo ngoja nimuhadisie Dada yangu wa kazi yeye nipo nae kwa mda mrefu ananifahamu vzr na anawafahamu vzr wakina Mahamod nilishaenda nae Dubai
Zilibaki kama wiki mbili ndio tarehe yangu ya Opp nilimuaga bi mkubwa kama nanyoosha miguu kidogo nafanya mazoezi, huwezi kufanya mazoezi kipindi hiki huoni unajitafutia matatizo Mamujee?? Bi mkubwa alikuwa ana wasiwasi na hali yangu, nikamwambia siendi mbali nanyoosha miguu tu pia sitakuwa peke yangu naenda na Dada, bc aliruhusu ila kishingo upande nikamwita Dada nikamwambia twende tukafanye mazoezi
Tukiwa njiani na Dada nikaanza kumsimulia yale maneno niliyoambiwa na bi mdogo, Dada akaniambia Dada Mamujee usikatae wala simuamini Mwanadamu yule unaemuamini ndio huyo ana kuhumiza? Aisee Dada wa kazi alinipa kauli ambayo ilinifanya niamini kuwa inawezekana bi mkubwa na mumewe hawana nia nzuri na mm na hivi Mahamod ni mganga na chumba chake cha Uganga haruhusiwi kuingia mtu yeyote zaidi ya Mahamod mwenyewe na bi mkubwa tu
Nikamuuliza Dada sasa mm nifanyaje? Akaniambia nenda kwenu kama ulivyoambiwa,, mhh kwetu wapi? Inamaana niende Musoma? Kwa nani yule Baba mdogo aliyeshirikiana na mkewe kunipiga hadi kunusurika kifo?? Nilijiuliza mwenyewe baada ya Dada yangu wa kazi kunambia niende kwetu,, nikawaza au niende tena kwa Kaka Arusha nikajifungue huko kama hawa mapacha?? Lkn kaka namwambia nn? Hata ivo kaka mwenyewe hata mke hana kila cku kunibadirishia wanawake tu mara waje wanipe makesi yao niwasuruhishe yaan ni shida tu
Bc nikasema liwalo na liwe nitakaa hapa hapa nione
Nilirudi nyumbani na Dada nikamkuta bi mkubwa ana wasiwasi kweli vp mbona mmechelewa nilijua umepata shida bado kidogo nikupigie cm kumbe cm hukubeba? Nikamwambia Dada ondoka shaka nipo sawa
Cku zilikimbia hatimae cku ya kujifungua ilifika nikapelekwa hospital nikalazwa ili kesho yake nifanyiwe opp nikiwa pale hospital nikaanza kuota mandoto ya ajabu ajabu mara nimejifungua mtoto kafa mara mtoto wangu kaibiwa
Usiku presha ikapanda sana nikapewa vidonge Dactar akaniambia Mamujee acha kupaniki relax, nikamwambia docta mbona najiona nipo sawa? Akaniambia presha ipo juu sana so jitahidi kutoa mawazo, bc asbh palikucha kabla sijaingia kwenye chumba cha Opp nimeingia kwenye vipimo mapigo ya mtoto hayaonekani nikawaisha kwenye operation presha bado ipo juu ikabidi nipewe vidonge kwanza operation isubiri presha ishuke, badala ya saa 4 asbh nimekuja kufanyiwa opp saa kumi jioni,,, nimekuja kupata fahamu nipo wodini kitu cha kwanza nikaomba mtoto nikaambiwa subiri upate nguvu nimekaa mtoto sipewi jmn mwisho nikaamua kuuliza mtoto wangu yuko wapi? Nimekuja kupewa jibu usiku kwamba mtoto wangu amefariki
Itaendelea
35
Mtoto wangu alizaliwa amekufa alikuwa ni mtoto wa kike iliniuma sn nikakumbuka yale maneno ya bi mdogo ndio yalizidi kuniumiza nilikaa hospital kwa muda wa siku tatu then nikarudi nyumbani tatizo la presha halikuniacha likazidi kunisumbua but sio kama wakati wa ujauzito, nilikosa amani nukimfikiria mtoto wangu kwann amekufa??
Bi mkubwa hakukaa sana tangu nimejifungua alihakikisha nipo vzr bc akaanza maandalizi ya safari kurudi nyumbani kwake
Muda mwingi Mahamod alikuwa akinipigia cm kunitia moyo sikutaka kumwambia chochote kama mke wake mdogo ameniambia kuhusu wao na mtoto wangu,,, bi mkubwa alisafiri kurudi nyumbani kwake nikabaki na familia yangu zilipita kama cku tatu tangu bi mkubwa aondoke bi mdogo wa kati alinipigia cm kunipa pole na kuniambia si nilikwambia Mamujee? Mbona hukunisikiza? Nilikwambia nenda kajifungulie nyumbani kwenu? Ona sasa umepoteza mtoto wako? Nikamwambia sawa ila kama binadamu ndio amenifanyia haya bc Mungu atamlipa ila kama ni kazi ya Mungu bc acha nishukuru akaniambia nakutumia hela ya pole ndugu yangu ila ipo cku nitakuja Tz ngoja tumalize mgogoro na Mume wangu nikamwambia nashukuru sn
Maisha yangu yaliendelea nikapata nguvu nikapona kabisa nikarudi kwenye mishe zangu watoto wangu wawili walifika miaka miwili na nusu nikaamua kuwapeleka shule
Nikajikita san kwenye kufanya biashara zangu bi mkubwa bado alikuwa ananigizia mzigo kutoka huko kwao nikaona nifungue duka lingine la nguo
Nikaongea na Mahamod aniongezee pesa nataka kufungua duka la nguo jumla na rejareja bc hakusita sana akaniambia subiri
Bc pale nyumbani kwangu zile fremu ziliisha nikaamua niweke duka la vyakula (Duka laMangi) kwakuwa nilikuwa na wasichana wa kazi wawili bc mmoja nikamuweka dukani hapo nje mmoja akabaki ndani na watoto wanashinda shule,,,, wasichana wangu nilikuwa naishi nao kama ndugu niliwafanya kuwa ndugu zangu na walikuwa waaminifu sana hata ukisahau pesa bc utaikuta
Niliamua nizidi kupambana nijisimamie mwenyewe kuhusu kuzaa niache kwanza
Mume wangu alinitumia pesa ya kuongeza mtaji wangu hapo ndio nikafungua duka kariakoo na mzigo wangu wa kwanza wa hapa dukani kwangu nilichukulia China, nakumbuka hii safari nilisafiri kimya kimya bila ya kumuaga Mume wangu nilifika china nikakaa kama wiki mbili nikarudi Tz niliwaaga wasichana wangu wa kazi wa nyumbani kwangu tu
Lkn nikiwa China Mahamod alinitumia msg Whtsp ukirudi huko ulipo utaniambia nije Tanzania nione watoto nilishangaa nikasema amejuaje kama mm sipo Tz?
Nilirudi Tz nikapumzika kama wiki nikaanza biashara kariakoo sikumtafuta Mahamod nikawa niko bize nashukuru Mungu nilianza biashara kariakoo kipindi sikukuu zinakalibia na nilikuwa na mzigo wa kutosha nauza jumla na rejareja biashara ikapamba moto
Mahamod alinipigia cm anataka kuja Tanzania nikamwambia sawa bc niliendelea na maisha yangu
Mahamod alifika Tz, alifurahi na watoto wake nilijiwahi nikenda kuweka vijiti vya uzazi wa mpango sikutaka kuzaa na Mahamod tena kila nikikumbuka nilivyoteseka na mimba then mwanangu kufariki nilikuwa nachukia kuzaa na Mahamod
Mahamod aliniuliza kwann umeenda China bila ruhusa yake? Nikamwambia nilifata mzigo wa biashara bc alikasirika akafoka kwamba kuniacha nifanye biashara kusinipe kiburi anauwezo wa kuniachisha hio biashara nikakaa nyumbani,, nikamwambia nisamehe Mume wangu bc alikubali yakaisha tulienda nae hadi kariakoo akaona biashara
Itaendelea
Mamujee
Furaha naomba nijibu baadhi ya comment, maana story yangu nakaribia kumaliza,, kuna watu wanacoment eti sina marinda, ni kweli kabisa ndio sababu nimeleta kisa mjifunze wengine, maana kuna baadhi ya wasichana wanavunja utu wao kwa makusudi kuingiliwa kinyume na maumbile bila ya kupata chochote, then wapo wengine wanadhani hii story ni ya kutungwa, wapenzi hii ni true story tena ni yangu mm mwenyewe, maisha yangu niliyopitia hadi sasa nilipo, leo ukiniona natembelea gari nzuri naishi nyumba nzuri unaweza ukatamani maisha yangu ila nilipotoka huwezi kupita,, then kuna mtu amecoment kuwa kwann naandika kwamba akanipeleka hadi kwenye hard yake ya magari?? Naandika ivo ili watu wote wanielewe maana uwelewa tumetofautiana, ningeweza kuandika TU akanipeleka kwenye hard yake,,, haya maisha nimepitia mm Amamu,, ni kama past tu, ila kwa Sasa nina maisha tofauti kabisa, wengi hawajui nilipotoka ila wakiniona naendesha prado wananiona mchawi tutaendelea tulipo ishia kesho
MWISHO S01/ S02 SOON