Abdallahking
JF-Expert Member
- Mar 19, 2018
- 3,985
- 10,840
Mkasa : NDOA ILIVYOTETERESHA IMANI YANGU
Mwandishi: IRENE MBOWE (Irene Mbowe Kungwi Lao)
Imeletwa kwenu na: BURE SERIES
Hiki ni kisa cha ukweli kabisa, anachokielezea Flora, Mwanamke ambaye anakiri Imani yake kutereteka kwa sababu ya Ndoa yake. Alikuwa na alilelewa kwenye familia yenye maadili mema. Na aliogopa dhambi kama ukoma, Na baada ya kumaliza elimu yake , na kufanikiwa kupata kazi, bado alikuwa ni muaminifu kwenye imani yake vibaya mno. Lakini baada tu ya kuolewa mambo yalibadilika. Hembu ongozana na mimi msimuliaji wako Irene Mbowe katika kisa hiki cha ukweli, chenye,, KUFUNDISHA, KUBURUDISHA NA KUADIBISHA.
SEHEMU YA KWANZA: MAISHA NA FAMILIA YA FRORA.
PART 1
Nilizaliwa kwenye familia ya wazazi wasomi, wenye kujua nini maana ya familia, mama yangu na baba yangu siku zote walikuwa wakinuia mamoja, walipenda na kutulea kwa upendo wa hali ya juu.
Tulijikuta sisi watoto tukiwa watoto wenye adabu sana na kusifiwa sana mtaani kwetu, wengi walifikiri baba yetu ni mchungaji lakini ukeli hakuwa mchjungaji ila alikuwa kama mchungaji kutokana na matendo yake na utu wake na namna anavyoishi kwa upendo na mkewe na wanawe.. Hiii ndiyo ilikuwa familia yetu familia ya mzee george maliki.
Tulipenda sana imani yetu, tulipendana sana sisi kwa sisi, na kwa vile tulikuwa tumelelewa kimaadili kila mmoja alipata elimu nzuri sana, mama yetu alikuwa ni nesi na baba yetu alikuwa ni mfanyakazi serikalini, hivyo pesa zao kwa pamoja zilitulea kwa kuhakikisha tunapata huduma na malezi bora, kipindi cha kumaliza mitihani ya kidato cha nne mama yangu na baba yangu waliniambia endapo nitafauli vyema basi wangenizawadia zawadi nono sana, wakati huo kaka yangu na dada zangu walikuwa tayari wako vyuoni, na mimi kama binti wa miwho kwa kudeka sana walifikiri singefanya vizuri.
Lakini nilijitahidi sana kuhakikisha nafauli masomo yangu vyema. Haikuwa hivyo baada ya matokeao, nilifeli na kupata devision 0. Mwaka 1991. Nilijisikia vibaya sana, kwani mama yangu alilia. Baba yangu alinitia moyo sana, vijana wenzangu kanisani walinicheka na kuniambia kwa nini skuwa makini kwenye masomo? Dada zangu hali kazalika walinicheka sana, lakini kaka yangu aliniambia nikisoma tena na kurudia kidato cha nne nitafaulu, na alimshauri baba yangu na mama yangu nirudie mitihan yangu.
Na hivyo sasa nilisubiri mwaka unaokuja ili nirudie mitihani yangu. Kaka yangu aliniambia nikiomba mungu nitafaulu na kikitia nia nitafaulu kikubwa nisome na kuatia nia. Alinitia maoyo sana, na kuanzia hapo nikaona ninaweza. Hivyo nilianza tena kidato cha nne katika shule nyingine. Maombi yangu siku zote yalikuwa mungu ifungue akili yangu nielewe vyema, ahivi ndivyo niliomba kila siku.
Na kweli nilifunguliwa akaiali na kuelewa kwa haraka sana, lakini pia niliomba kukumbushwa nisiwe msahaulifu na nikawpewa kumbu kumbu mzuri sana. Nilifanya maajabu kwenye mtihani wa kufunga shule mitihani ya pre natinaonal mama yangu na baba yangu hawakuamini kuona report yangu, nilipata devision 2. Hesabu ambayo nilikuwa napata f, sasa nilipata c. Ilikuwa ni maajabu kwa familia nzima.
Kaka yangu aliniambia ninaweza kufanya maajabu zaidi kwa kusoma, kutia nia na kuomba mungu akaniusia nisiache kuomba kwani yeye ndiye ambaye imemsaidia sana. Nilirudi shule kama mfalme,, nilifungashiwa kila kitu nilichotaka,, nilipewa kila kitu kizuri na wazazi, babayangu alinifurahia sana, mama pia alikuwaakailia machozi ya furaha sana, nilirudi shsuleni kwa ajili ya mitihani yangu, kipindi hicho nilikkuwa naona wanafunzi wenzangu wakiwa na boyfriiends, niliwashangaa sana.
Wanawezaje kuwa na wachumba ili hali ni wadogo vile, wengi wlinicheka na kuniita mteule ama mlokole ama sister,, jina lililojulikana kulkiko jina langu halisi la flora. Kipindi cha mitihani kilipofika sikuwa nafanya lolote zaidi ya kuomba tu, kwani nilishasoma sana, hivo niliamua kufunga siku 11 kwa ajili ya mitihani yangu niliyokuwa naifanya. Nilishangaa sana, mar ya kwanza niliingia kwenye mtihani wa siasa,, nilishangaa nilivyoweza kuufanya vyema mpaka nikawa ninacheka..
Kisha kwenye mtihani wa biology nao hali kazalika nilishangaa sana na kujiuliza je ni mtihani ama ni mchezo? Mitihani ya mwanzo ilinipa roho ya kutoogopa mitihani ijayo, hivyo nikaendelea akuomba mungu anikumbushe yote niliyosoma na hivi ndivyo kaka yangu alinipa maelezo kwambna nisisome ila niwe namuomba mungu kwani nilishasoma sana kipindi cha nyuma, na hii ilifanya wengi waone kama nimechanganykiwa na kuonekana mpumbavu,, lakini sikujali. Nilimaliza mitihani yangu yote na kurudi nyumbani.
Niliwaeleza wazazi wasijali nitafanya maajabu,, walikwua wakicheka sana, mkesha wa krismas tukiwa tunatoka kanisani, kijana mmoja alinifuata na kuonekana kunihitaji, niliogopa sana nikijua ni dhamabi kubwa na nilikumbuka amitihani yangu na kusema nikifanya hii dhambi nitafeli mitihani yangu, hivyo nilikataa kabisa nilionekana kusichana aliyekomaa lakaini sikutaka kujiingiza kwenye mahusiano ya mapenzi, nilirudi nyumbani nikiwa na hofu ya kutenda dhambi hiyo.