SEHEMU YA 9: HUKUMU YANGU
PART 1
NILIONA CK NI MWANAUME MWENYE UPENDO KWANGU, NISINGEMUELEZA UKWELI INGENIHARIBIA MAHUSIANO YANGU, HIVYO SASA NILIAMUA KUMUELEZA UKWELI,
Fransis Haki ya Mungu sijawahi kwenda kwa mganga ila ni mama Kely alinishauri na kuniambia nikasafishe nyota, na nikiwa na wewe nivae hiyo pete na nikiwa siko na wewe nisivae.
Fransis alinitazama na kuniambie ndio hiyo pete umeivaa kwa vile uko na mimi?
Ndio nilijibu. Kisha akaniambia Flora mimi siamini uchawi na uchawi hauna kazi kwangu na leo nitakuhakikishia na kukkudhihirishia kwamba waganga ni waongo, na kama ni wa kweli kwa wanaoogopa ila sio kwa wasio ogopa.. mimi namuamini sana Mungu flora.
ALisema hayo huku akiwa kama anahasira lakini anazizuia…
Kisha akaniambie enhe, ni nini uliwahikunifanyia ulichoabiwa na mganga?
Hakuna nilijibu.
Enhe na kuhusu mimba mbona huelezei mama?
Nilianza,, kweli Fransis nilitoa mimba kwa kuogopa tu, lakini sio kwa sababu ya uchawi.
Fransis alinitazama na kutingisha kichwa chake. Na huku akigonga gonga kalamu mezani kwako
Aliniambia Flora huna Mungu wewe, kweli unatoa mimba, sasa uliibeba ya nini? Ningekuea natka mtoto si ningekuwambia? Na hata kama ungeniambia una mimba ningetumia akili yangu ya kiume mptka huyo mtoto umzae na ingewezekana,, ila wewe ni muuaji..
Alisimama kwa hasira na kusema Devil! Wewe ni shetani,,, Aliniuliza funguo zangu za gari ziko wapi? Nilikuwa nimeziweka mezani pamoja na wallet yangu pembeni ya glass ile ya juice, alichukua ile glass na kupigiza ukutani kisha akasema Shit all women are Devil.. Aliniambia sasa ili ujue kwamba siogopi uchawi na uchawi hauna nguvu,, nakuacha na pete yako mkononi,, san asana utanipa hiyo yangu, niliyokupa,, haya vua,, alichukua mkono wangu na kuvua ile pete yake.. kisha akaniambia give me my CAR KEY,,, OPEN THE DOOR GO.. YOU DEVO. .. NILIJARIBU KUUA SUA NA AKANIAMBIA NIMEKUWAMBIA TOKA SHETANI WEWE,, NILIANZAKUMUOMBA MSAMAHA, ALINIZABA KIBAO CHA USONI NA KILINIINGIA HASWA NAKUAMUA KUJIONDOKEA MAANA NISINGEWEZA KUNDELEA KUKAAA,
ALINIAMBIA MAMA KELY NI MWANAMKE MZURI NA ANA ROHO NZURI ALINISHAURI VYEMA,, KUMBE MUMEO ANALEWA KWA AJII YA UCHAWI WAKO ILI UWE NA MIMI.. NA NITAMPA ZAWADI YAKE HII NZURI NA AUTAMUONA KAIVAA SOON.. KWENDA SHETANI WEWE..
NILITOKA NIKILIA SANAKWA UCHUNGU.. SIKUJUA NIENDE WAPI,,, OFCN AMA NYUMBANI AMA WAPI,, NILIJIULIZA NANI ATANISAIDIA? RAFIKI GANI NINAYE?
MARAFIKI WA KANISANI NILISHAWAACHA,, NIKAONA MARAFIKI WENGINE NDIO WA MAANA,, KILINIUMA,, NILIAMUA KWENDA OFCN KUMUONA BIBI KWANI NDIYE ALIKUWA FARAJA YANGU PEKEE.
NILIFIKA NA NILIPOMUONA NILIANGUKA NA KUANZA KULIA MOJA NA KUHISI KUISHIWA NGUVU,, TAYARI NILIKUWA NA LOW PRESSURE,, NILIANZA KUKOSA NGUVU NA KULEGEA.
888888888
BIBI ALNIWASHIA FENI OFCN KWAKE NA ALINIHURUMIA SANA,, ALNIPETI PETI NA KUNIAMBIA COOL DOWN MAMBO YATAKUWA SAWA..
SIKUWA NAONA MAMBO YAKIWA SAWA HATA KIDOGO, CK ALINIDHALILISHA SANA,, NILIUMIA SANA,
ILIKUWA NIMAJIRA YA SAA KUMI NA NUSU, WAFANYAKAZI WENGINE WALIKUWA WAMESHAANZA KUTOKA NA MIMI NA BIBI TULIUWA OFCN,, SARA ALIKUJA NA KUGONGA MLANGO,, KISHA AKASEMA DA FLORA SHIKAMOO NAOMBA USINICHUKIE MIMI NAKUPENDA NA NDIO MAANA NILIUAMBIA ILA UMENIANGUSHA KUNISEMELEA,,,
BIBI ALIMWAMBIA HEMBU TUPISHE KWANZA HUONI MWENZAKO ANAVYOLIA HAPA UNA NINI WEWE BINTI,,, SARA ALITOKA NA KUONDOKA,, KISHA ALIKUJA NA SPEED YA AJABU NA KUTUAMBIA MAMA KELY ANAKUJA.
BIBI ALITUAMBIA TUONDOKE… TULISIMAMA NA KUJIANDAA KUONDOKA.
MARA MAMAKELY ALIWASILI NA KUTUSUBIRI NJE YA GETI LA KAZINI, HAPO HUWA KUNA MGAHAWA NA WATU HUPENDELEA KUKAA HAPO ILI WANYWE CHAI NA KAHAWA MIDA YA JIONI.
ALIPOTUONA ALIANGUA KICHEKO,,,
Hahahahaha! Halaaaa.. hivi wewe Flora nini unawashwa na mimi mwanaizaya wee,, wmanamke usokkuwa na haya wala adabu.. mimi ni wa kutoka na bwana wako,, nakuuliza mimi ni wa kutoka na bwana wako? Hivi unanionaje mimi wee kahaba mzee? Alinisogelea na kunichoma mavidole ya usoni,, kisha pembeni nikasikia watu wakisema mpashe huyo mgeni wa mapenzi.. mshamba huyo…. … anasahaulishwa mume na hawara
HAPO NDIPO NILIJUA KUMBE WATU WALIKUWA WANAJUA.. SIKUJUA BIBI ALIPITIA WAPI,, ILA NILISIKIA BIBI AKIAMBIWA MAMA UNAJIAIBISHA KUWA NA HUYU KAHABA…
NILIPATA AIBU YA MWAKA,,
Kisha akaanza unanizodoa amimi natoka na ck,, ck ni mumeo? Nakuuliza wewe shuwain,,, Fransisi ni bwana wangu mii ama ni bwana wako kikuume nikitoka naye/ kawafuate kina mwenge ambao wanakuchukulia bwana ila sio mimi,, mwanamke huna shukrani nimekufadhili kwa lift siku zile huna lolote leo umepata gari la kuhongwa ndo unajioona umefikaaa… hahaha halaaa,,haya hilo gari liko wapi? Nakuuliza gari liko wapi?
NA UTATEMBELEA VISIGINNO MPAKA VIOTE SUGU,, SHETANI WEE USOKUWA NA HAYA..
Eti unaomba haya omba sasa basi omba…
Alikuja mama mmoja sijui alitoka wapi alimsukuma mama kely na kumwambia hata wewe ni Malaya tu, umejuaje haya yake yote, nani asokujua mama kely wewe Malaya mzoefu,, muache mtoto wa watu,, na huyo mama akaniambia haya na wewe panda taxi hiyo ondoka..
NILIONA YULE MAMA NI KAMA MALAIKA,,, NILIPATA AIBU AMBAYO SIWEZI KUIELEZEA,, NILIMWAMBIA DEREVA TAXI ANIPELEKE KWA BIBI KWANI NILIOGOPA HATA KWENDA NYUMBANI,, NLIJUA MUME ATAZIPATA HABARI HIZO,, DEREVA ALINIPELEKA KWA BIBI NIKIWA SIFAI KWA KILIO NA KWIKI,, NILITAMANI KUFA,, NILITAMANI ARIDHI IPASUKE NIINGIE NDANI,, NILIUMIA KULIKO SIKU ZOTE ZA MAISHA YANGU.
888888
MAMA NISAIDIE NIFANYE NINI NISAIDIA MAMAYANGU,
BIBI ALINITAZAMA NA KUNIAMBIA NIKUSAIDIE NINI MWANANGU? NIKIPI CHA KUKUSAIDIA SASA HIVI/
UMESHACHELEWA MWANANGU MGUU UMEOTA TENDE HUO,, TUFANYEJE SASA?
SANA SANA NITAKUSHAURI UWE TU MPOLE MAANA SASA HIVI MUMEO AKIPATA HIZI HABARI HUNA NDOA,,, NA MIMI HATA NIKIJIDANI KUKUSAIDIA NITAKUWA NAKUDANGANYA MAANA MARAFIKI ZAO WANAOKUJUA FIKA WANAHABARI ZAKO ZOTE, MWISHO WA SIKU NITAONEKANA MWANAMKE MPUMBAVU KAMA WEWE MWANANGU,, NIKUSHAURI WEWE UTULIE NA KUKUBALIANA NA MATOKEEO,, HIVI LAKINI FLORA NI SHETANI GANI ALIKUINGIA MWANANGU? AGH? BIBI ALIKARIKIRAK GHAFLA NA KUSEMA SASA AUMEMTUKANISHA MAMA YAKO MASKINI, ATOONEKANA TABIA ZAKO UMEZITOA KWAKE KUMBE MASKINI WALA HAJUI ULIPO NA UNACHOFANYA.
BIBIALIONGEA KWA UCHUNGU KISHA AKANIAMBIA SASA HIVI AFYA YAKO SIYO NZURI HATA KIDOGO,,, SIONI SABABU YA WEWE KUSUMBUKA TENA, HEMBU TULIA USIJE KUFA NA KIHORO MAMA. TULIA KABISA JIFANYE HAMNAZO MAMBO HAYA YATAPITA,, MBONA MENGI YAMEPITA,, NA HILI MAMA LITAPITA, ILA NDO UTULIE SASA.
BIBI ALINIFARIJI KIDOGO,,KISHA AKANISINDIKIZA MPAKA NYUMBANI NA KUNIACHA,, NILIINGIA NDANI NA KUAMUULIZA DADA KAMA BABA ALIKUJA, DADA ALINIAMBAI BABA HAJARUDI BADO,, NILIINGIA BAFFUNI NA KUOGA,, KISHA NIKAJITUPIA KITANDANI,, NILIKUWA NAUMWA SANA KICHWA NA KUJISIKIA DHAIFU..
NILIKUWA NIMEAMUA LIWALO NA LIWE KAMA NI MUME KUNIKUTA NA KUNIPIGA ACHA ANIPIGE NIFIE NDANI KWAKE ILA NILSEMA SITAONDOKA KABLA YA KUJUA LOLOTE TOKA KWA MUME.
NILIKUMBUKA WNAWAKE WA KANISANI, NILIKUMBUKA NILIVYOPENDWA N A KUPEWA HESHIMA,, NILIUMA SANA, NILIJIONA SIFAI KABISA NA KUTAMANI HATA SIJUI KUJIUA.. NILIANZA KUPATA PICHA NIEMEKUFA NA WANAANGU WANAVYOLIA, KISHA NIKASEMA SITAJIUA ACHA DUNIA INICHEKE LAKINI SIJUUI NG’O.
NILIAMKA NA KUANZA KUANGALIA JIKONI KAMA DADA KAPIKA VYEMA… KISHA NILIONA CHAKULA KIZURI, NILIKAA SEBULENI NIKITAFAKARI PICHA NZIMA YA SIKU HIYO,, KUANZIA KWENYE GIVE ME MY CAR KEY NA GO YOU DEVIL… NILIUMA NILIONA YOTE YAMENISTAHILI,, NILIMKUMBUKA MAMA KELY NA KUAPIZA KULIPIZA KISASI NILIJIULIZA KISASIKIPI KINAFAA?
NILISEMA AIZA NIKAPIGANE NAYE,, AMA LA NITOKE NA BWANA WAKE NA YEYE AUJUE KAMA KUFA ACHA NIFE LAKINI NITALIPIZA KISASI.
MUME ALIREJEA NANILIJIKAUSHA KAMA SIO MIMI, NILITAKA KUMSIKIA KASIKIA NINI?
SIJUI ILIKUWAJE AMA HAKUSIKIA AMA ALISIKIA NA KUJIKAUSHA LAKINI HAKUNISEMESHA LOLOTE LILE, ALILALA TU, NA ASBH PALIKUCHA ILI NIENDE KAZINI.
NILIJIANDAA NA KUDANDIA DALA DALA, MAMA KELY ALINIPITA NA GARI NA KUACHIA CHEKO,, KIINIKERA NA HASIRA ILINIPANDA NA KUSEMA MOYONI NITAMUUA.
NILIFIKA OFCN NA NILISHANGAA SANA KUKUTA BOSS AKINISUBIRI.
NILIITWA OFCN KWA BOSS AKIWEPO BOSS, CHIEF ACCOUNTANT NA MENEJA UAJIRI NA BIBI. WOTE WALIKUWA WNANISUBIRI.. ROHO YANGU ILINIPASUKA PWAAAA…
NISIJUE NI NINI NIMEITIWA,
Je ni nini Flora kaitiwa? Tutaona katika muendelezo huu wa kisa hiki cha ukweli kabisa lakini cha kutufndisha sana sisi wengine.
Usikose kufuatilia hapa hapa…
88888
MOYO ULINISHTUKA. HARAKA NILIJUA KOSA LANGU NI KUSHUTUMIWA KUTUKANANA HADHARANI. KWANI MARA ZOTE UKIITWA NA WATU HAO BASI NI KUPEWA ONYO KALI. NILIINGIA NDANI NA KUKAA KWENYE ROUND TABLE. ALIANZA KUZUNGUMZA BOSS NA KUNIAMBIA.
Flora **** shutuma nzito sana zinakuhusu wewe. Sijui kimetokea nini hadi mama kuwa katika hali hii lakini shutuma hizo zinakuhusu moja kwa moja.
Alidakia mhasibu mkuu na kusema..
Boss naona tusipoteze muda kwani ni dhahiri analigahamu hili.
Nikiwa katika kutafakari … muajiri alisema..
Flora kukosa nidhamu kazini ni kosa kubwa sana. Na ni kuaibisha shirika letu. Hivyo haitakuwa na sababu ya kujadili jambo lililoko mbele ila ni kupokea adhabu yako ambayo ni aiza… kusimamishwa kazi kwa muda ama kugukuzwa kabisa kwani kosa ni kubwa sana na la aibu.
Bibi aliitizama na kuniambia…Flora kufukuzwa kazi wewe mimi sinhependelea. Na hakuna umachohitaji wewe kujieleza isipokuwa tu kuomba msamaha. Ama una lolote uwezalo kusema?Nilushauri mwanangu..Tekla atakapokuja hapa uwe mkweli. Muombe msamaha yaishe. Kwani anavyo vizibiti vyote. Na atakapoamua kufikisha jambo hili kwa mumeo ni hatari.Tecla akiingia jishushe na uwe mpole sana.
Moyo ulinilipuka niliposikia Tecla. Nilijiuliza tecla ni nani?Na maralango uligongwa na aliingia msichana mrembo ambaye sijawahi kumuona popote. Nilianza kusikia kiu na Bibi aloniambia usiogope. Huyu ndo teclA
8888
Boss alisema karibu Tecla. Karibu sana. Tecla alisogeza kiti na kuketi. Ni msichana mdogo sana kwangu. Naweza kumzidi miaka 6 mpaka 8 hivi. ALIWASALIMIA WOTE KWA MIKONO kasoro mimi. Kisha aliambiwa je huyu ndiye uliyekuja kumshtakia? Binti huyo aliitika ndio haswaa ndo huyu mwanamke mshenzi..
Hapana binti usitumie lugha chafu. Jaribu kuzuia jazba.
Kisha boss alinitazama na kuniuliza unamfahamu binti huyu?
Hapana nilijibu.
Boss aliniangalia na kusema huyu anaitwa Tecla. Alikuja kushtakia kwamba una mahusiano na mchumba wake ili hali wewe una ndoa na akashangaa kwa nini ufanye hivyo?
Sijui nini kilitokea nikaanza kujieleza…
Mimi Fransis hakuniambia ama mchumba..
Binti yule aligonga meza na kusema shit! https://jamii.app/JFUserGuide you ana shame on you. Huoni haya kusema hakukuambia ana mchumba!una laana mama ama?wewe si mke wa mtu wewe ?
Tecla alisimama kama mwenye hasira sana. Akili yangu ilimivurugika. Mambo yamekuwa mengi. Kazi lazima sina. Sasa nasikiliza nini na kukitetea nini?nilisema endapo huyo binti atanigusa nitamalizia hasira zangu hapo na liwalo na liwe kama kuaibika nimeshaaibika vilivyo.
Nilimwambia binti usinikaripie ongea pole pole.
Aliendelea kung’aka..
Kisha akatulizwa.
Na boss kunigeukia na kunieleza…
88888
Flora hembu tulia kwanza. Tunataka kufanya suluhu. Vingimevyo tusingewaita hapa.
Tecla hebu eleza tumalize mambo haya.
Tecla alianza.
Fransis ni mchumba wangu na ananisesha urusi. Ananilipia ada yeye na kila kitu. Huu ni mwaka wa tatu wa masomo yangu. Na huwa ninawadiliana naye kama mke na mume kwani hata wazazi wanalifahamu hilo.
Hapo nyuma nilipata taarifa za mahusiano ya flora na fransis. Kilimiuma sana. Na ndipo nikapanga kuja bila kumjulisha Fransis ili niweze kufumania na kama uchumba kufa ufe kwani nilielezwa kila kitu kuhusu mwanamke huyu na mambo amfanyayo na mcbumba wangu. Nashangaa anawezaje kufanya hivi ili hali ana mume.
Hivi wewe mwanamke huna hata aibu jamani?
Muajiri alimuuliza tecla umemaliza?tecla alisema siwezi kumaliza kirahisi. Nimeingia gharama ambazo ni kubwa sana. Ticket ya ndege na hotel niliyolala. Lakini pia nimepoteza muda wangu kuja kulihakiki hili. Ninachotaka ni gharama zangu yaishe. Sinaninachotaka kwake zaidi ya ticket ya ndege nirudi chuoni.
Kila mmoja alionekana kushangazwa na madai ya tecla.
Boss alimuambia lakini unaminije watu waliokuambia?swala la sisi kukubali une hapa ni kuweka mambo sawa na sio kulipishana.
Tecla alicheka kwa kejeli na kusema.
Mh.. ha ha ha… hamnijui bila shaka. Sijashindwa kwenda hata polisi. Ninao ushahidi. Ama sijashindwa kwenda kwa mumewe. Ninatumia tu busara mpaka sasa kwani najua ninyi no waajiri wake mnaweza ku mdispline.
Haya niambieni mnataka nini?
Kwanza mapoteza muda tu hapa.
Niliwaza sana nifanye nini sasa?.. nikiwa katika kuwaza… Tecla alitoa mfuko wa malboro chini ya meza na kunipiga nao na kusema mshenzi wewe… nini hiii….. nini hii unajidai kununulia wachumba za watu nguo…
888888
Mfuko ule ulikuwa na ile kadi niliyoanfika… keki iliyorojeka chupa ya champagne na shati na suruali. Alikasirika sana akasema….. huku akimuangalia boss wangu..
Haya abishe sasa… nasema huyu mwanamke hajitambui…
Kisha tecla aliendelea kuzungumza…
Baada ya kupewa taarifa za flora na fransis na walionipenda niliamua kuja kwa siri. Lakini sikutala mpenzi wangu ajue kwamba ninakuja kumfumania kwani nilishaelezwa kila kiti juu yao mpaka flora kuishi mule ndani. Kitu nilivhojiuliza kwa nini huyu mwanamke aishi kwa mchumba ili hali ama mume? Hapo nilipoambiwa anaishi ndipo nilisema lazima nije. Yamkini sio mke wa mtu na huenda fransis anataka kuoa. Na ndio maana nikaja.
Nilifika kwa siri sana bila yeyote kutambua. Nilijua kama ni wapenzi laxima watajivinjari siku ya kuzaliwa kwa fransis na ndio maana nikaja siku hiyo ili kumsuprise fransis. Na isimgekuwa na maswali.
Nilifika mapema sana. Na kwa bahati nilichelewa kidogo tu. Ningewahi lazima ningekutana na huyu mmbwa.. Tecla alininyoshea mkono kwa dharau alinetua midomo yale aliposema huyi mmbwa…
Kisha alaendelea kwa jazba kuongea…
Nilipofika tu uwanjani nilichukua taxii na kukimbia hadi nyumbani na kukuta gari haipo. Nikajua hawako. Nikaenda ofcn kwani niliam iwa huwa hukaa huko. Nilikuta gari huko na sasa niliamua kufanya fanizi kwani ilikuwa ni usiku.
Nilipofika niliona kuna purukushani na hili limwanamke liliondoka kwa kasi na gari yake akakimbia akiwa kajifunga funga maushungi.
Ofcn walikuwa wakifanya mapenzi.
Mh…Aliposema maushungi nikajua tu huyo ni mama kely
.. sikutaka kujitetea kwani hakuna ambaye angeamini…
Aliendelea..
Baada ya hapo mimi na mpenzi tulielekea nyumbani. Nilikuwa na hasira sana. Na nilipofika ndipo nikaona hizi zawadi zake.
Sasa bado unabisha?
Nikiachana ma fransis nitaonekana mimi mbaya kwani ananisomesha… lakini flora umetia doa na domda mahusiano yangu. Heri ungekuwa msichana.. mke wa mtu.. loooo?
Kisha alianza kulia.
Bibi alinitazama.. kisha akasema…
Tumesikia yote tecla.
Maji yameshamwagika… hapa unahitaji kutoa msamaha tu basi.
Tecla alisema nitakacho ni nauli yangu basi. Mimi sina shida naye.
Nimeumia bya kutosha. Ni mfanyakazi wenu naomba nauli tu basi.
Aliulizwa ni bei gani akasema ni laki nane. Kwa wakati huo.
Mimi mshahara wangu ulikuwa ni laki mbili kwa mwezi.
Mh..
Mhasibu mkuu alisema haya flora sema tumpe?
Dah… nilikuwa naumia…
Bibi alisema flora kubali yaishe. Muombe msamaha yaishe.
Dah… nilijitosa kimaso maso.
Sikuwa na la kufanya.
Nilisogeza kiti. Nilienda mpaka alipo binti yule.
Nilipiga magoti chini na kumuomba msamaha.
Aliniambia simama yameisha.
Kisha alianfikiwa cheki yake na akaondoka.
Na kikao kikaisha.
Nilikuwa na mawazo tu.
Baada ya muda wa kazi kwisha nilipewa barua.
Nilienda kuifungulia chooni.
Barua ya lunisimamisha kazi mpaka watakapoamua kuniita.
Dah…. nililia chooni sana.
Nilitoka na kurlekea nyumbani.
Moyo wangu ukiwa na majeraha mengj ya kujitakia.
Moyo mzito sana. Unauma sana.
Nilijitupa kitandani na kulia sana.
Nikijiuliza je Deus analifahamu hili?akilifahamu itakuwaje?
Kisasi kikazidi kukomaa.
Nikawa napanga kisasi cha malipizi ya haja. Na kuyatekeleza mapema sana.
Hivi ndivyo niliamua na nikawa nasubiri pakuche NitEkeleze nilichopanga.
88888
Mume alikuja. Maisha yetu yalikuwa ya kupuuzana. Tuliishi mradi salama.
Nilisema hivi haya mume hayajui ama?ni kweli ama?kama mama yake anajua ina maana mume hajui?nilijiuliza sana. Ilikuwa ni saa nne usiku. Nilisema ngoja nimueleze kuhusu kusimamishwa kazi.
Nilimpatia barua akasoma. Kisha akasema pole. Na akalala. Hakuongea sana.
Mh.. nilijiuliza kulikoni?
Asbh aliondoka. Nilimuomba pesa kidogo ya nauli.
Aligeuka na kuniambia.nauli ya nini.?gari iko wapi?
Na fransis je hawezi kukupa pesa?
Usione nimenyamaza Flora… naogopa lawama kwa wazazi wako…. naogopa laana ya mama yako nikikutaliki. Ishi utakavyo naishi nitakavyo. Kama kuondoka ondoka wewe.aibu uliyonipa inatosha
Usitake nifanya maajabu nikafungwa maisha.
Najua kila lako wewe shetani. Tena niache.
Deusi machozi yalimdondoka na akaondoka.
Mh…. nilijiuliza kumbe anajua kanyamaza?
Looo.. nifanyeje sasa? Nikahisi akirudi usiku nauwawa. Nikaanza kifungasha kila kilicho changu na kutoa kidogo dogo. Na kupeleka kwa bibi mpaka nikamaliza mizigo yooote.