Ndoa na Mirathi: Nafasi ya Mahakama ya Kadhi kwa Wanawake

Ndoa na Mirathi: Nafasi ya Mahakama ya Kadhi kwa Wanawake

Status
Not open for further replies.
Wewe tamka kwamba adui wa waislamu sio Wayahudi...., bali ni Wakristo! Si tutakuamini wewe na kumuona Allah ni muongo! Umebaki jielimishe! Jielimishe! Mbango ya nini? Nielimishe hapo kwanza! sawa eeh!

hivi na wewe unataka nikujibu nini hapa mmmm! kama huu ndio uwezo wenu basi bana ok..
 
Hivi aliyekwambia kwamba waislamu ni more than 50% ya population ya Tanzania ni nani? Halafu kwa nini hupendi ku-face facts kila saa wewe ni wa kusema unachukiwa unachukiwa. Huo ni mtindio wa kuona kuwa kila asiyekupa unachodai basi ana chuki na wewe na huoni kwamba huna haki ya kupata.

Kama umechelewa umechelewa tu ndugu yangu, huwezi kuwahi kwa kuwarudisha nyuma waliotangulia. Kuna maswali ya msingi humu yameulizwa na Mgen naomba uyajibu sio kurudia rudia. Na hizi OK OK ni dalili za kuwa unapenda kuwalazimisha watu waamini vile unavyoamini wewe. Nyinyi wenyewe kwa wenyewe tu mnatofautiana ktk hili. Kama unachohitaji ni haki ya kuwa hakimu, nenda kasome. Hii ya kupitia kwenye dini kwa kuwa unajua huko elimu siyo ishu haina nafasi

Hoja hapa wewe mkristo wa Tanzania unakosa nini kwa sisi waislamu kuwa na Mahakama ya Kadhi??? jibu hilo swali

Mengine nilishakwambia ukiacha majivuno unaweza kuwa na akili lakini zaidi ya hapo..ni bure tu wewe huwezi kushindana na dini Adam, Musa, Yesu na Muhammad ambayo ni UISLAM..utaishiwa kukasirika weee kila siku dini inapaaa..
 
Naomba mjadala ujikite kwenye mambo yafuatayo ya msingi..niseme tu siwezi kujibu hoja nje ya yafuatayo:-

a. Mkristo anayepinga Mahakama ya Kadhi anapinga kwababu gani?

b. Waislam kuwa na mahakama ya kadhi wanavunja sheria ipi ya nchi?

c. kuna tatizo gani mahakama kutambulika kisheria kwani zinasaidia state courts?

d. Kuna tatizo gani mahakama hizo kuwa financed na state??

Ukianza kuhubiri dini gani sahihi au quran vipi na vile..naomba u-google kina mazinge watakufundisha biblia mimi sina huo muda hapa..pia unaweza kuni PM nikakuelekeza darsa letu liko wapi kila jumamosi.
 
Wakristo hawana sababu ya msingi ya kupinga mahakama ya kadhi, kwanza kabisa haiwahusu wao ndee wala sikio.
 
Hivi aliyekwambia kwamba waislamu ni more than 50% ya population ya Tanzania ni nani? Halafu kwa nini hupendi ku-face facts kila saa wewe ni wa kusema unachukiwa unachukiwa. Huo ni mtindio wa kuona kuwa kila asiyekupa unachodai basi ana chuki na wewe na huoni kwamba huna haki ya kupata.

Kama umechelewa umechelewa tu ndugu yangu, huwezi kuwahi kwa kuwarudisha nyuma waliotangulia. Kuna maswali ya msingi humu yameulizwa na Mgen naomba uyajibu sio kurudia rudia. Na hizi OK OK ni dalili za kuwa unapenda kuwalazimisha watu waamini vile unavyoamini wewe. Nyinyi wenyewe kwa wenyewe tu mnatofautiana ktk hili. Kama unachohitaji ni haki ya kuwa hakimu, nenda kasome. Hii ya kupitia kwenye dini kwa kuwa unajua huko elimu siyo ishu haina nafasi

Nanren Likes this text in blue.
Halafu hawa jamaa kwa kupika data, ni mabingwa. Kule kwenye uzi wa Mohd Said-yule jamaa aliyeandika historia za wamanyema na kulazimisha ndio historia ya Tanganyika, walikuwa wanabadilisha badilisha definition ya "Waislam" kutegemeana na nini wanabishia muda huo.
  1. Kuna wakati wanasema Tanzania kuna wakristo na Waislam tu (1:1), hakuna wapagan. Kwa hiyo ukiwabishia tu kwenye jambo lolote, lazima wewe utakuwa mgalatia tu.
  2. Kuna wakati wanasema wenye majina yote ya kiislam ni waislam
  3. Na pia kuna wakati wanasema waliopo ndani ya BAKWATA si waislam
  4. Hata viongozi wa mwanzo wa nchi hii ambao walifanya kazi na Nyerere, baadhi wanadaiwa kuwa si waislam japo majina yao ya kiislam.
Hiyo 50% aliyoitaja hapo ilianzia kwenye sources zao zinazodai Wakristo:Waislam ni 50%:50%. Source hii, ilikuwa inalinganisha wakristo na waislam lakini ikitambua kuwa kuna wapagan. Sasa hapa huyu bwana amegeuza kabisa kumaanisha kuwa wapagan hawapo.
Kwa ajili ya ubishani wa kujiumiza nafsi zao, kuna waandishi wao wengi wanaodai kwamba muslims ni majority in the country. Assumption hii japo yaweza kuwa ya uongo, huwa ni muhimu kwao wanapotaka kulalamikalalamika. "Ooh, sisi tupo wengi, lakini vyuo vikuu vyetu vichache" Ooh, sisi tupo wengi by population lakini kwenye civil service tupo wachache, nk.
Ni afadhali hoja zao zingekuwa zinajengwa kwenye statistics za kweli, kuliko hizo za kupika...
 
Wakristo hawana sababu ya msingi ya kupinga mahakama ya kadhi, kwanza kabisa haiwahusu wao ndee wala sikio.

Mkuu, Ff! Hakuna Mkristo hata mmoja anaye pinga mahakama ya qadi hakuna! Nyie kaeni star light shia, sunni, qadiani...., chagueni maqadi watoe fatwa kwa mujibu wa kitabu chenu! uone kama mtaingiliwa! Mnacho kifanya ni kumlazimisha asiye muislamu ashiriki ibada yenu! ambapo wewe mwenyewe unaingia kwenye ukaafir!
 
Naomba mjadala ujikite kwenye mambo yafuatayo ya msingi..niseme tu siwezi kujibu hoja nje ya yafuatayo:-

a. Mkristo anayepinga Mahakama ya Kadhi anapinga kwababu gani?

b. Waislam kuwa na mahakama ya kadhi wanavunja sheria ipi ya nchi?

c. kuna tatizo gani mahakama kutambulika kisheria kwani zinasaidia state courts?

d. Kuna tatizo gani mahakama hizo kuwa financed na state??

Ukianza kuhubiri dini gani sahihi au quran vipi na vile..naomba u-google kina mazinge watakufundisha biblia mimi sina huo muda hapa..pia unaweza kuni PM nikakuelekeza darsa letu liko wapi kila jumamosi.

a, hakuna mkristo anayepinga mahakama ya qadi! labda ututajie!

b, si kazi ya serkali kali kutangaza dini!

c, states courts hazihitaji msaada wa mahakama ya qadi!

d ni sawa kulazimisha muislamu kula nguruwe!

mahakama ya qadi na kolani vinahusika na dini, au!
Sasa uwe na amani tu tukihoji hiyo dini na maelekezo ya kolani, hadith, ima sunna za mtume wako! tusipo jadili hayo, kwani unataka kusajili chama cha siasa? nenda kwa Tendwa!
 
Bila kutambilika kisheria (kikatiba) itakuwa sawa na bure..it does not work; its option but must be legal siyo vinginevyo

Muungwana Topical hivi unajua wengi 'wenu' mnaji-contradict? Hivi hii Mahakama mnataka serikali iwape funding. Je kitu gani kitaizuia serikali ku-influence jinsi inavyoendeshwa? Mpaka leo BAKWATA waislamu wengi wameisusia kisa ni ya 'serikali' sasa hii mahakama si itakuwa Bakwata part two?

Halafu labda niulize waislamu humu: mmeshafuatlia muundo wa mahakama ya Kadhi ya ZANZIBAR? Kama mmefuatilia..mmejifunza nini mpaka sasa katika mfumo wa ile mahakama?

Jamani be careful with what you wish for...you might get it!
 
Tunachoomba ni hii hakuna contradiction:-
a. Itambulike kisheria na kikatiba ila iwe option kwa waislam wanaopenda kupewa hukumu kiislam tu

b. Iwe funded na serikali kwasababu wanaohudumia ni watanzania wanaotoa kodi, ambao kimsingi state inatakiwa kuwasaidia when it comes to legal and justice issue..nime suggest malipo yawe on the basis of number of cases @ kadhi courts average price per case can be established looking at current state cases..

Kwamba serikali itakuwa na influence kwenye matumizi ya fedha OK, kama auditing etc.. lakini siyo kwenye maamuzi ya hukumu kwani hayo yako very clear kwenye Quran na Sunna..itakuwa ngumu sana kuhukumu kivingine..
 
Mkuu, Ff! Hakuna Mkristo hata mmoja anaye pinga mahakama ya qadi hakuna! Nyie kaeni star light shia, sunni, qadiani...., chagueni maqadi watoe fatwa kwa mujibu wa kitabu chenu! uone kama mtaingiliwa! Mnacho kifanya ni kumlazimisha asiye muislamu ashiriki ibada yenu! ambapo wewe mwenyewe unaingia kwenye ukaafir!

Hakuna Muislaam anaemlazimisha asie muislaam kuingia kwenye Uislaam. Uislaam ni kwa kila mtu apendae Mola wake na anaeamini Mungu basi hatoacha kuwa Muislaam, Lakini apendae kuabudu binaadam mwenzake, apendae kuabudu masanamu, anaependa kudanganywa na mapadri ambao wengi wao ni *******, hatumlazimishi kuja kati Uislaam.

Tunachotaka Mahakama ya Kiislaam na Kadhi wa Kiislaam atambulike rasmi na Serikali, na tunataka fungu hilohilo linalotumika leo hii kuendesha kesi za Waislaam mahakamani basi wapewe Waislaam wenyewe.

Umeshawahi kujiuliza kesi za Waislaam mahakama ambazo sizo za Kiislaam zinaendeshwa kwa gharama zipi? ukishajuwa zinaendeshwa kwa gharama zipi sasa uelewe kuwa. kwa kuwa zinaendeshwa huko basi huchukuwa muda mrefu zaidi na kwa gharama kubwa zaidi kuliko zingeendeshwa na Waislaam wenyewe.

Hakuna cha ajabu, isipokuwa wale wajinga wachache wasioweza kufikiri ndio wanapunga, just, wakiona neno Uislaam. Hivi huu Uislaam unawatisha nini nyinyi?
 
Na huwezi kumlazimisha mfuasi wa Yesu awe mwislamu huwezi! Nilichosema hicho mnachoomba kwa makaafir(serkali)! Kinaombwa kwa mujibu wa kuluani,hadithi, au sunna za mtume wako? kama hakuna maelekezo huoni kwamba unachoomba ni ukaafir?
Hao wanaokula komwe! wamesoma kolani ndipo wakaashiki huo mchez6! si mpaka huku uswazi, unaitwa mchezo wakiisilamu!! Haki ya Mungu kama utaitaja adhabu ya wanaume wanaofakamiana vutu, kwa mujibu wa suratul an nisaa aya15 mpaka 16 mimi leo nitakuwa muislamu!
Hayo ni mawazo yako kwamba watu wanatishika na waislamu hilo ni ajabu ya mwaka! Kadini kenyewe tia maji tia maji! Manake hata ibada zenu mnaomba makaafir kibali!
 
Nasema hivi TUTAFIKA!!! Kama una upeo mdogo wa elimu ya biashara nakushauri ukasome UDSM, IFM au Mzumbe utajua kwanini nasema kuwa MOU ni pesa zinaenda makanisani. Kuna msemo mmoja unasema Never argue with a fool because people may not notice the difference. Unakufaa sana wewe msemo huo.

I had never been called a fool before, especially by someone of higher rank on the same field. Thanks for the compliments! I feel honoured. Sasa turudi kwenye hoja na naamini huku ndio kutatuamilia kati ya sisi foolish wawili nani mwalimu wa mwenzake.

Mimi binafsi namini unaishi kwa ushabiki bila hata kujua undani wa madai yako. Nakwambia kuwa, hata ukipata hiyo mahakama sio mwisho wa migogoro. Nasema hivyo kwa sababu, najua madhaifu ya hizo mahakama na ndio maana mnataka ipate nguvu ya kisheria ili yale mtakayoyaamua yalazimishwe kwa nguvu ya serikali kufanyika hata kama si sahihi. Kwa nini nasema si sahihi:

Sura 4:11-12 and 4:176 state the Qur'anic inheritance law. When a man dies, and is leaving behind three daughters, his two parents and his wife, they will receive the respective shares of 2/3 for the 3 daughters together, 1/3 for the parents together [both according to verse 4:11] and 1/8 for the wife [4:12] which adds up to more than the available estate.
Sasa chukua mfano tunaigawa Sh 100 kwa maelekezo ya Allah kwa uwiano wa :-
Mke 1/8 ya 100 ni 12.5
Wazazi 1/3 ya 100 ni 33.3
Mabinti 2/3 ya 100 ni 66.7 Ukizijumlisha hizi dividents zao utapata 112.5 ambayo tayari imeshazidi. Je huyu kadhi ambaye mnatuambia atagawa kwa muongozo wa Quran ana lipi la kuamua hapa kama si kupendelea upande mmoja.

Tazama na hii nyingine:

A man leaves only his mother, his wife and two sisters, then they receive 1/3 [mother, 4:11], 1/4 [wife, 4:12] and 2/3 [the two sisters, 4:176], which again adds up to 15/12 of the available property.

Nilisema tangu mwanzo kuwa, lengo la wajanja wachache hapa ni kutaka kumkandamiza mwanamke.
Mke wa marehemu anapata 1/4 lkn mama wa marehemu anapata 1/3, kweli inaingia akilini? Hapa unataka kumaliza mizozo au kuanzisha mafundo mioyoni mwa wanawake? Labda ni kwa kutojua hesabu ndio tunaweza tukaona hiki ni kitu kizuri, ngoja nikupe darasa la hesabu kidogo. Ukitaka kujua nani anapata zaidi hapa, twende hivi: Tuanze na ya mke, na tufanye tunaigawa Shilingi 100. Mkwe anapata 1/4. Sasa chukua (100 x 1) gawanya kwa 4 = 25. Halafu twende kwa Mama Mkwe wake 1/3. Chukua (100 x 1) gawanya kwa 3 = 33.3r.

Sasa mr. mwerevu, Bi Halima ambaye amefanya kazi ya kuajiriwa kwa miaka 12, kufiwa na mumewe ambaye yeye alikuwa kazi yake ni kwenda msikitini na kucheza bao na wazee wenzake kweli kumfanye apewe kidogo zaidi ya mama mkwe wake?

Kabla hujanishauri kwenda IFM kusoma biashara, kaa chini na wenzio mfanye hesabu ili muiboreshe quran kwanza kwani yaonekana mtunzi wake alijua mambo mengi kasoro hesabu. Na kwa kukudhihirishia hili, soma Quran, Sura 7:54, 10:3, 11:7 na Sura 25:59 utaona zoote zinatamka wazi kuwa Allah aliumba mbingu na nchi kwa siku 6. Lakini ruka uende Sura 41:9-12 hapo utakubaliana na mimi kuwa ukijumlisha zile activities za Allah siku kwa siku utagundua kuwa ni siku 8 na sio 6.

Niirejee kauli yako ya lugha ya kigeni: Never argue with a fool because people may not notice the difference, nafikiri mpaka hapa PEOPLE watakuwa wameshaelewa who the fool is; me, you or the other one who can not do simple arithmetics.

Kama una hoja weka ubaoni tujadili, kama nimekosea aya, badili weka ya kweli. Kama nimeandika sahihi kama zilivyo kwenye Quran, TAFAKARI, CHUKUA HATUA.
 
Usipotoshe watu dogo!
1. Huwezi kuwa mtaalam wa mirathi ya kiislam kwa kusoma kwenye internet au JF kuna wanazuoni wa kiislam wenye degree na hadhi kufanya mgawanyiko huo kwa mujibu wa Quran; sasa wewe unayesoma Quran ili ufanye kashfa unajisumbua mwenyewe ..jifunze zaidi au uliza wanazuoni tutakusaidia..

2. Huwezi kujidai unawatetea wanawake wetu, dada zetu au mama zetu katika uislam, wanapenda sheria za Allah na hakuna anayelazimishwa katika dini

3. Ukitaka kuelewa Quran unatakiwa ufanye tafsiri in a holistic sense siyo kama unavyochapia hapa..

Ask questions you will answered, lakini ulichoandika ni maneno ya wakristo na makafiri wengine ambao hayamsumbui muislam mwanamke wala muislam mwanamke ambaye anamuamini Allah..

Unachotakiwa kujibu kwenye makala hii ni yafuatayo na si kufundisha dini kwani huna authority yeyote ya kufundisha uislam wewe kilaza..

a. wewe kama mkristo unapata hasara gani kuanzishwa mahakama ya kadhi kama siyo chuki na wivu??

Nilitegemea utajibu kwa Aya kama nilivyofanya. Au si wewe unayetaka Intellectual Argument?
1. Huwezi kuwa mtaalam wa mirathi ya kiislam kwa kusoma kwenye internet au JF kuna wanazuoni wa kiislam wenye degree na hadhi kufanya mgawanyiko huo kwa mujibu wa Quran; sasa wewe unayesoma Quran ili ufanye kashfa unajisumbua mwenyewe ..jifunze zaidi au uliza wanazuoni tutakusaidia..
Ungeniambia kuwa Sura na Aya nilizotoa si za kweli ningeona una Intellectual Argument lkn sbb yk ya kuwa nimesoma kwenye internet haitoshi kuuthibitishia umma kuwa siko sahihi. Historia iliyoandikwa kwenye ngozi na iliyoandikwa kwenye karatasi zitatofautishwa kwa usahihi wake na sio sehemu zilikoandikwa. (Hujajibu hoja hapa, hii ni jazba)
2. Huwezi kujidai unawatetea wanawake wetu, dada zetu au mama zetu katika uislam, wanapenda sheria za Allah na hakuna anayelazimishwa katika dini

Juzi nilipowaambia kuwa mna hila na elimu hamna ulibisha na ukasema kuwa ninawatukana. Mimi sijidai kuwatetea kwa kuwa suala la kujitetea ni lao. Hapa nina swali na naomba ulijibu kiungwana na usijisumbue kutukana badala ya kujibu hoja: Ikiwa unaamini dada na mama zenu wanazipenda sheria za Allah, mbona unataka mahakama ya Kadhi ipate nguvu ya kisheria ya ku-enforce maamuzi yake? Kuna haja ya shuruti kwa kitu ambacho watu wanakipenda?

3. Ukitaka kuelewa Quran unatakiwa ufanye tafsiri in a holistic sense siyo kama unavyochapia hapa..
Can you help me with a Holistic Sense that can make me understand the way Allah so as Kadhi will divide Tshs 100 in the ratio of 1/3, 2/3 and 1/8?

kuna wanazuoni wa kiislam wenye degree na hadhi kufanya mgawanyiko huo kwa mujibu wa Quran
Haya ndiyo majibu mnayowaandalia watakaohoji uhalali wa maamuzi mtakayofanya kwenye mahakama ya kadhi. Kwa kuwa tayari umeshabashiri kuwa hawatakubali, ndio sababu mnaanza kudai nguvu ya kisheria ya kutekeleza hukumu ambayo tayari umejinadi kuwa waamini wanaipenda. Mimi sidhani kuwa kuna mwanazuoni mwenye kuelewa zaidi ya Allah kiasi hesabu zilizomshinda Allah aje azifanye yeye. Hii ni justification ya kukandamiza kwa maslahi ya watu wachache. Jaji huamua kesi kwa vifungu vya sheria na sio degree yake.

Na mwisho nikushukuru kwa kutambua kuwa mimi ni kilaza. Najua matusi ni sehemu ya mafundisho uliyopata MADRASA na sitakulaumu kwa hilo kwa sbb najua wewe ni victim wa ibada usiyoijua.
Ask questions you will answered, lakini ulichoandika ni maneno ya wakristo na makafiri wengine ambao hayamsumbui muislam mwanamke wala muislam mwanamke ambaye anamuamini Allah..
Maswali niliyouliza hukunijibu badala yake unaniita kilaza na hapa tena unaniambia niulize nitajibiwa! Kama Quran Sura 4:11-12 na Sura 4:176 ni maneno ya wakristo na makafiri ina maana Allah naye ni kafiri?
Unachotakiwa kujibu kwenye makala hii ni yafuatayo na si kufundisha dini kwani huna authority yeyote ya kufundisha uislam wewe kilaza..

a. wewe kama mkristo unapata hasara gani kuanzishwa mahakama ya kadhi kama siyo chuki na wivu??

Usiwe na wasiwasi ukifikiri labda nataka kukuingilia kazi yako ya kufundisha dini yako. Sina uwezo huo kwani dini yako yahitaji uwe katili na mwingi wa shurti kuifundisha. Mimi ni mtu very diplomatic ambaye badala ya kuforce, nina-inspire with loving and considerate examples. Na ndio maana nilikuhoji kwa nukuu za Quran na sio matusi ya kuitana vilaza. Kuhusu swali lako kuwa nitapungukiwa nini mahakama ya kadhi ikianzishwa jibu ni kuwa sitapungukiwa na kitu, sana sana nitapata kitu kipya cha kunifanya nicheke kila ninapokumbuka hisabati za Sura 4:11-12 na Sura 4:176 ambazo hapo awali nilidhani zimetoka kwa Allah lkn kwa msaada wako leo nimejua kuwa zimetungwa na wakristo na makafiri wengine.

Nashukuru kwa muda wako. Ni matumaini yangu utajibu hoja zangu kwa Aya na weledi badala ya matusi. Pengine majibu mazuri toka kwako mwanazuoni uliyebobea na mwenye Intellectual Esteem yatatoa mwanga wa ufahamu kwa wengi wetu tusioelewa yaliyojificha.

Asalaam Aleykhum!
 
@Shizukan

Dogo acha kupotosha maana tafsiri ya Quran na uelewa wake uliza wajuzi; kama ambavyo tafsiri na uelewa wa biblia unatakiwa kuuliza wajuzi; having said that. ukitaka kufundishwa kufundishwa hukumu ya dini yetu unatakiwa kuuliza? wewe kitu gani kinakusumbua utajibiwa..

Lakini ukija na kashfa, majigambo mimi nakuona limbukeni tu kama wale wahubiri wa biblia ni jibu ..JF si mahala pake.. nakuhakikishia malumbano ya kidini wakristo hawana uwezo wa kushinda hoja hata moja ndio maana kila siku wanalia kwamba waislamu wanawakashifu..tuache hayo..

Uliza swali moja moja kuhusu mirathi (usichanganye ushabiki wako na kejeli) wapi unapata shida, wapi unaona wanawake wanaonewa na sharia; na kadhalika nitakujibu nakupa nafasi hiyo this week..

Naomba swali moja kwa wakati..
 
Ni kawaida ya mtu dhaifu ku- neutralize mambo anapokuwa cornered. Usiniambie kuwa leo ndio umegundua kuwa ukitaka kuelewa Biblia unatakiwa uulize wajuzi! Hii ni janja yako ili tuishie hapa kwa kuwa huna majibu. umekazana kuwa napotosha napotosha lkn husemi napotoshaje. Nauliza hivi, Sura nilizozitaja hazijaandikwa kama nilivyosema?

Kuna ujuzi gani mtu anao wa kupindisha aya za quran ambao anaweza kupindisha aya nilizokutajia zikapate maana nyingine? Nyie mko hivi, mnapenda kuongea mambo ya watu mkidhani ya kwenu hatuyajui. Sasa mimi nakuhakikishia, hata wengi wenu mpo huko mlipo kwa kuwa hamjui na hata mkishtuka mnazuiwa kwa maneno kama haya unayoniambia kuwa wasikilizwe wajuzi. Hakuna mjuzi zaidi ya maandiko. Siku zote mmeisifia quran kuwa imenyooka na haijachakachuliwa kumbe uchakachuzi unafanywa kwa midomo eeeh!

Unataka maswali, utajibu?

Ngoja kwanza niende kwenye biashara zangu ili niingizie kodi serikali ili wewe na mkeo na wanao mtakapoenda kwenye hospitali za serikali na za MoU mtibiwe kwa kodi yangu.

Natumaini nitakaporudi mchana nafasi uliyonipa ya kuuliza maswali nitaitumia vyema, kwa sasa wacha nikajenge Taifa. Mimi huwa sichezi bao

Assalaam Aleykhum!
 
Sura 7:54, 10:3, 11:7, and 25:59 clearly state that God created "the heavens and the earth" in six days. But in Sura 41:9-12 the detailed description of the creation procedure adds up to eight days
.

Mkuu naona unaegemea katika contradictions;
Sasa naomba uchukue biblia kwani huenda pia pamoja na usomi wako hujui contradictions zilizopo;

1- (a)Biblia inasema kuwa Mungu hachoki,
Kaangalie katika Isaya 40:28:Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.
(b) Hiyo hiyo Biblia inaonesha kuwa Mungu alichoka akapumzika baada ya uumbaji;
Kaangalie katika Exodus 31:17
Inasema hivi; Ni ishara kati ya mimi na wana wa Israeli milele; kwani kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi, akastarehe kwa siku ya saba na kupumzika.

Kwa faida ya wana JF naomba niainishe baadhi ya maandiko yanayobainisha kuwa Mungu ni Mmoja tuu:
- Angalia katika kumbukumbu la torati (Deuteronomy) 6:4, Inasema hivi, Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja.
- Pia katika Wakorinto 1,8:3 Basi kwa habari ya kuvila vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; twajua ya kuwa sanamu si kitu katika ulimwengu, na ya kuwa hakuna Mungu ila mmoja tu.
 
jinsi alivyo kupa ilimu mtumishi wa MMungu Shizukan, tena kwa mujibu wa kolani unayo iamini! Sasa nina uhakika bila shaka kwamba wajuzi wa kolani ni Majini hilo sina shaka aslani! Hebu rejea, hadhara ile ya muamadi kati ya waislamu na majini! Hadi anawashangaa waislamu baada ya kuwasomea kolani, anawauliza mbona ndugu zenu wa kijini wametoa jibu saafi nyie waislamu vipi? Ili unitoe shaka toa ushahidi wa aya kwamba nao waislamu waliielewa kolani! hatutaki bla bla hapa, ooh wakristo hawana jibu.....! Utajua kama alivyo jua muamad kwamba, Hao Wakristo ni Wasomi na WachaMungu!

Oh kumbe unamaanisha Kolani..?

Ungemaanisha Quran ningekujibu...
 
acha woga! yaani hata shetani tumpambe tumuite sheitwan! daah! hujui hata ulimi wa mama? hivi mnyakyusa anaweza kutamka "v"? Kwa hiyo hatumuelewi! Dini gani hili limejaa mikwala mbuzi? Nijibu dogo! hutaki niwe muislamu?

Wamesema niulize swali, nimeuliza swali wamekula kona. Shida hapa ni kwamba dini yao ina mambo mengi ya kujificha na huruhusiwi kuhoji. Nimeweka mistari michache tu ya Quran wamekuwa wakali na wengine wamefight back kwa kuuliza kama Mungu anachoka. Swali lao nimejibu la kwangu limekimbiwa. Ngoja sasa wakirudi swala huko utasikia wanakuja na sababu nje ya mada.

Nipo nasubiria Holistic Sense ya kunisaidia kugawa 100 ktk uwiano wa 1/3, 2/3 na 1/8 kama inavyonukulika toka Quran Sura 4:11-12 (Topical aliyakana kwa kusema ni maneno ya wakristo na makafir wengine)
 
Shizukan. Usijifanye unaijua sana Quran, kumbe vile unachofanya ni upotoshaji mtupu. Ukweli ni kuwa, hata Biblia unayojivunia, huijui, ndio utaijua Quran? Hebu tuongelee aya ulizotoa kama ushahidi. Quran 7:54, 10:3...Allah ametumia neno'AYAM'ambalo tafsiri yake hasa kwa Kiswahili sio siku, bali ni 'muda' (time period). Kwa hiyo, inaweza kuwa Saa 6, Siku 6, Miezi 6, Miaka 6... Uzuri mmojawapo wa Quran ni kuwa, lugha yake ya asili ipo pale pale, yaani 'Kiarabu'. Kwa hiyo hoja yako ya siku nane haina nguvu. Mfano, ukiangalia Quran 4:9 inasomeka 'yawmayni' kwa maana ya siku 2. Quran 4:10 inasomeka 'arba ayam' ambapo haina maana ya siku 4, bali 'mida 4'(time period).
 
Wamesema niulize swali, nimeuliza swali wamekula kona. Shida hapa ni kwamba dini yao ina mambo mengi ya kujificha na huruhusiwi kuhoji. Nimeweka mistari michache tu ya Quran wamekuwa wakali na wengine wamefight back kwa kuuliza kama Mungu anachoka. Swali lao nimejibu la kwangu limekimbiwa. Ngoja sasa wakirudi swala huko utasikia wanakuja na sababu nje ya mada.

Nipo nasubiria Holistic Sense ya kunisaidia kugawa 100 ktk uwiano wa 1/3, 2/3 na 1/8 kama inavyonukulika toka Quran Sura 4:11-12 (Topical aliyakana kwa kusema ni maneno ya wakristo na makafir wengine)

Kwa faida ya wana JF napenda kutoa ufafanuzi wa aya moja uliyo quote hapo juu ili uniambie kitu gani huelewi kama kweli unataka elimu mkuu acha kuptosha watu??

Qur 4:11 (tafsiri) nakupa ufafanuzi wake;

a. Akifa mtu akaacha watoto wanaume na wanawake basi kila mwanaume atapata mara mbili kuliko mwanamke

b. Akifa mtu akaacha watoto wanawake tu (wawili au zaidi hakuna mtoto mwanaume) watachukua theluthi mbili (2/3) wagawanye sawa kati yao na 1/3 watapewa warithi wengine kwa mujibu wa sharia (i.e. mama mzazi, baba etc)

c. Akifa mtu akaacha mtoto mwanamke mmoja tu (wala hana ndugu wanaume) basi mali itagawanywa sehemu mbili zilizo sawa; nusu moja atapewa huyo mtoto mwanamke na nusu nyingine watapewa warithi wengine kwa mujibu wa sharia (mama mzazi, baba etc)

d. Akifa mtu akaacha watoto wake (wajukuu zake) + na wazee wake) baba atapewa 1/6 ya mali, na mama yake 1/6 ya mali; sehemu itakayobaki watapewa watoto wake (wajukuu zake)

e. Akifa mtu akaacha baba yake na mama yake bila watoto wala wajukuu; basi mama yake atachukua 1/3 ya mali na 2/3 atazichukua baba mzazi wake

f. Akifa mtu akamwacha mama yake tu na ndugu zake wa kuumeni na kukeni; basi mama atachukua sudusi ya mali zingine zitagawanywa kwa warithi wengine

NB. Yote haya ni baada ya kutoa madeni, wosia alioutoa maraehemu

Kumbuka Quran ina details nyingi ambazo wewe huwezi kuzifahamu hadi uwe na hamu ya kuuliza na kutaka kujua na si kejeli..sasa niambie kwa ufafanuzi huu kipengele gani hukiwelewi katika aya hiyo Qurani?? nikueleweshe??
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom