Nikwambie kitu my love, Unaweza kutana na mwanamke anaekuomba 5,000 au 10,000 ila ni mara 10 kwa siku. Na unaweza kutana na mwanamke anaekuomba laki moja ila ni mara 1 tu kwa miezi nane au mwaka.
Kuombwa hela sio shida shida ni character ya mtu amekuja kwenye maisha yako kufanya nini?
Wanaume tunataka mwanamke ambaye sio tu atatutegemea ila atatuachia nafasi yetu ya kuonyesha sisi ndio tuna final say katika uhusiano na ndio tunatoa uelekeo wa uhusiano unaenda direction ipi.
Kitendo cha mwanamke kukupangia pesa ya kumpa, zawadi ya kumpa, wapi umpeleke,mara ngapi na saa ngapi muonane inatutoa kwenye ramani haraka sana.
Huyu anaependa ngozi nyororo ni simply tu kuwa hajawa serious. Vitu kama ngozi mwanamke akila vizuri akipakaa mafuta mazuri anavipata haraka sana. Ila kumbadili tabia mtu ambaye amechagua kuwa nayo ndio mtihani ambao wanaume wengi hatuufanyi.