Ndoa ni msingi muhimu na imara, je, ni yupi mwanaume sahihi

Ndoa ni msingi muhimu na imara, je, ni yupi mwanaume sahihi

Shikamoon wakubwa, wadogo zangu hamjambo.

Siwezi kuwa mnafiki,ndoa ni moja ya nguzo ya lazima,na napenda sana niwe na mtu sahihi ambaye tutaheshimiana.

Mapenzi ni kama majani huota popote vilevile,mpenzi atapatikana popote iwe jamiiforum,mtaani na kila sehemu.

Lakini ni yupi mume mwema na bora,umri unaenda,nachukia zinaa,sipendi kuwa na mtu eti boyfriend,wakati hajanioa, Kila mwanaume nayekutana naye namuona waluwalu hajatulia,Wana papara ,hawana subira.

Eti mtu anakutongoza leo mara anataka muonane badae then unakubali kuwa tutaonana ,sasa subiri akutajie ni wapi muonane, Mara lodge au gest,looooh yaani hata saa 24 hatujafika mara oooh ....

Mwingine anatuma hela ,halafu anakwambia tafuta lodge ya hiyo pesa kisha nije,jamani wanaume mmerogwa na nani,

Mnashindwa hata kuwa na aibu basi, pengine nitakupenda mwenyewe.

Na hamjui kama ukipendwa unapunguziwa majukumu kuliko kujitia hasara kumbe pengine sikupendiiiiiii.

Haoooooh waone kwanza,boksa hamfui,jinsi hambadilishi,mnaendesha magari ya kuazima ,siyo kila mwanamke ni wa kupagawa na vitu vya kijinga.

Mwingine alinikuta mgahawani nipo na simu yangu ndogo kitochi ,akajipendekeza mara oooh nitakununulia iPhone 11 hata plain tu, nikamwambia kama Una pesa nipe kabisa,lakini maana simu ninayo ,asianze konakona nini?

Mara oooh tukionana,mara nyumbani kwangu ninayo nitakupa,oohhh masikini ,nikamwambia aniletee Kesho yake.

Kwanza cha kuchekesha alikuja na gari fulani hivi ya kizamani, nikaona siyo mbaya,cha pili nguo ni zilezile habadilishi mbaba wa watu,cha mwisho ananiletea iPhone ya kizamani,ina batani katikati,ikabidi nimtolee tu simu yangu kwenye mkoba, jasho likamtiririka Kwa aibu.

Tena weee mbaba ukome Dunia hii unatumia Samsung S10,halafu unataka wanawake wazuri,looooh ukome ,kunipigia,Una bahati Sheria za hapa haziruhusu,ningekuanika
Story inaonesha bado huelewi unachotaka kama kweli ndo unaitafuta huwezi ukaipata na hiyo mentality, unataka pesa sawa na wewe utaleta nini mezani? unataka kuolewa kwanini? Ndoa sio lazima usije ukaingia kwenye shida kwasababu ya ushawishi au kuiga. KIkubwa unataka huduma au Mapenzi? huwezi pata yote hapo
 
Endelea na msimamo huo usije kuyumba ,ukishayumba tu basi unaenda kupotea...Mwanamme at first akimtongoza mwanamke lengo lake ni kwenda kula mzigo tu ,akishakula mzigo basi kuendelea kula hapo ni juhudi zako kama hauna juhudi basi anapotea kwenda kwa manzi mwingine.
Umeongea kweli hapa.
 
anyway, sikutaka kulizungumzia hili lakini ni kama unanichokoza. kutumia s10 siyo kwamba sina pesa ya kununua simu kubwa zaidi... bali ni machaguo yangu tu na napenda aina hiyo ya simu, kama ningekuwa siwezi mbona siku ya pili nilikuletea iphone mpya ambayo wewe unasema ni ya kizamani

pole pia gari ni langu, kuhusu uzamani sidhani kama unayajua vizuri magari... plate number A unasemaje ni ya zamani? A maana yake ni gari ya daraja la juu kwa ubora

hata hivyo kwa huko kujichubua, sura mbovu nani atakuoa dada? nilisema tukutane lodge wewe ulitaka tukutane paradiso au sokoni?

anyway, sitaki kuendelea kuzungumza na wewe kama tumeshindwana huko usiyalete huku maria
 
Nimezaliwa na kukulia familia yenye magari,hiyo Spacio yako ni gari gani,inatoa moshi kama nini,
Nipishe hukoooo 😂😂
 
Kwani wewe mzabzab una tatizo na uzinzi? Comments zako tu zimejaa uzinzi mtupu. It's funny mnapokazana kuwanyooshea watu vidole huku hata ninyi mnazini mpaka mlioko kwenye ndoa 🤣🤣🤣. Na ni sababu hii mnaona haiwezekani mtu kukaa bila kuzini
Ah mie kuzini au watu wengini kuzini haimainishi ni jambo jema.
Kukaa bila kuzini inawezekana ila ni kwa wachache sanaa.
 
Back
Top Bottom