Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 5,628
- 6,411
Katika pitapita yangu leo nimekutana na andiko katika Biblia kitabu cha ; 1 Samweli 18:21 "Naye Sauli akasema moyoni, Mimi nitamwoza huyu, awe mtego kwake, tena kwamba mkono wa Wafilisti uwe juu yake. Basi Sauli akamwambia Daudi mara ya pili, Leo utakuwa mkwe wangu".
Baada tu ya kusoma mstari huo nimejikuta napata kuelewa kuwa kuna ndoa ambazo kwa kweli ni mitego na inawezekana wengi tumeshaingia mtegonibna tayari ni wakweli wa mtegaji kwa kujua au kutojua.
Mtego huu wa ndoa umepambwa sana na tumewekewa mokataba migumu sana kuhakikisha mtegwaji akinaswa ananaswa kwelikweli. Kuna kelele za ukimya chini ya sauti " alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe".
Kiapo cha kupendana katika shida na raha na " kifo tu kiwatenganishe ni mwiba mkali wenye sumu kwa wengi tuliowahi kulishwa "unga wa ndele". Tunajikaza kisabuni ila kwa hakika kinachoendelea ni sawa na mtu kukuvhoma sindano na kuingiza dawa isiyoisha.
Andiko hili haliungi mkono kauli mbiu ya "kataa ndoa" ila linalenga kuonesha kuwa katika ndoa kuna mitego ambayo inao wanufaika wake (wategaji). Unaweza ukaoa tukifikiri wewe ndiyo baba " kichwa cha familia" kumbe kuna kichwa kingine kinachohutaji kichwa chako.