Mnaamka wote pamoja asubuhi, mnaenda kwenye ofisi yenu pamoja kwenda kuzitafuta.
Mnashinda pamoja mkipambana na maisha, mkisaidiana mawazo na nguvu.
Jioni mnarudi pamoja nyumbani, mmechoka lakini mioyo yenu ina furaha kwa sababu mmekuwa timu siku nzima.
Hakuna ndoa nzuri kama ile ambayo mke na mume wanakuwa washirika wa maisha na utafutaji. Inapunguza sana nafasi ya kucheat, kuchokana, drama zisizo na maana, na kutokuelewana.
Mnaelewana zaidi, mnajuana zaidi, na mnajenga ndoto zenu pamoja.
Ndoa inakuwa sio tu mapenzi, bali pia urafiki, ushirikiano na safari ya pamoja ya mafanikio.
Ni tofauti na ndoa ambazo mke na mume wanaagana asubuhi na kukutana tena jioni au usiku. Zaidi ya masaa 10 kila mmoja akiwa kivyake huweza kuanza kuzoea maisha yaliyo mbali na mwenza wake. Upande hasi wa hali hii ni kwamba kuna uhuru mkubwa sana kupitiliza wa kuwa na mahusiano mengine, mawasiliano yanaweza kupungua, malengo ya pamoja kudhoofika, na siri kuanza kujengeka taratibu hali inayoweza kuathiri uaminifu na kuna uwezekano mkubwa wa ndoa kucunjika.
Kwahiyo siwezi kusema kuwa wote pamoja ni uhakika wa asilimia 100% kwamba hamuwezi kusalitiana, kupunguza mawasiliano, kupungua malengo ya pamoja, kufichana siri, n.k. lakini angalau kuna nafuu mara nyingi zaidi kuzidi upande wa pili.