Ndoa nzuri ni ambayo mke na mume hushinda wote kwenye utafutaji na kurudi pamoja nyumbani

Ndoa nzuri ni ambayo mke na mume hushinda wote kwenye utafutaji na kurudi pamoja nyumbani

Mkuu sasa hao ni mama zetu wa enzi hizo walikuwa wamefundwa vizuri, adabu ilikuwepo. huwezi linganisha na kina mama wa sasa
Mbona hilo jengine hulijibu mkuu?

Mimi nishaoa najua ninachokiongea mkuu
Waswahili husema "muoshwa huoshwa"
 
Mnaamka wote pamoja asubuhi, mnaenda kwenye ofisi yenu pamoja kwenda kuzitafuta.

Mnashinda pamoja mkipambana na maisha, mkisaidiana mawazo na nguvu.

Jioni mnarudi pamoja nyumbani, mmechoka lakini mioyo yenu ina furaha kwa sababu mmekuwa timu siku nzima.

Hakuna ndoa nzuri kama ile ambayo mke na mume wanakuwa washirika wa maisha na utafutaji. Inapunguza sana nafasi ya kucheat, kuchokana, drama zisizo na maana, na kutokuelewana.

Mnaelewana zaidi, mnajuana zaidi, na mnajenga ndoto zenu pamoja.
Ndoa inakuwa sio tu mapenzi, bali pia urafiki, ushirikiano na safari ya pamoja ya mafanikio.

Ni tofauti na ndoa ambazo mke na mume wanaagana asubuhi na kukutana tena jioni au usiku. Zaidi ya masaa 10 kila mmoja akiwa kivyake huweza kuanza kuzoea maisha yaliyo mbali na mwenza wake. Upande hasi wa hali hii ni kwamba kuna uuru mkubwa sana kupitiliza wa kuwa na mahusiano mengine (kuchepuka), mawasiliano yanaweza kupungua, malengo ya pamoja kudhoofika, na siri kuanza kujengeka taratibu hali inayoweza kuathiri uaminifu na kuna uwezekano mkubwa wa ndoa kucunjika.
Hujazungumzia mishahara yao itawekwa kati na bajeti ya matumizi itakuwa ya pamoja.
Hujazungumzia nani atapika na kulea watoto.
Ndoa nzuri hazina formula kama mke atashindwa kumheshimu mumewe;na mume kumpenda mkewe
 
Ndoa nzuri ni Ile ambayo mke anabaki nyumbani na watoto. Yaani wewe ukiondoka asilimia 40 anakuwaza wewe zinazobaki anadeal na watoto.

Ndoa nzuri ni Ile ambayo wife anakutegemea mume kwa kipato kwa asilimia miamoja. Awe akitaka kitu au akitamanishwa kitu yeye ajivunie kuhudumiwa na mumewe.

Hapo mwanaume ndo unajifeel kidume kweli, yaani unapendwa, unaheshimiwa na wakati huohuo tu anaogopa asikiudhi kwani wewe ndie kila kitu kwake.

Sina tu hela ya kiivyo, mke wangu hasingefanya kazi Wala biashara. Najua Kuna vidume watasema maisha ni kusaidiana- ukianza kuwa na mawazo hayo usishangae ukasaidiwa hata kugongewa mkeo_ SI unaendekeza usaidizi.

Mwanamke ameumbwa kuhudumiwa na mwanaume na sio kusaidiana kwenye kutafuta kipato.
 
Utadharaulika ndugu mke akishajua unapata 6M kwa mwezi atatafuta anopata 8M mna w.ke wameumbwa kitamaa zaidi
Kwani unadhani mke au girlfriend hawezi kukukadiria maisha yako na akajua huyu mtu anapata kiasi gani kwa kuangalia maisha unayoishi na vitu unavyomiliki?..leave aside ubahili.
 
Mnaamka wote pamoja asubuhi, mnaenda kwenye ofisi yenu pamoja kwenda kuzitafuta.

Mnashinda pamoja mkipambana na maisha, mkisaidiana mawazo na nguvu.

Jioni mnarudi pamoja nyumbani, mmechoka lakini mioyo yenu ina furaha kwa sababu mmekuwa timu siku nzima.

Hakuna ndoa nzuri kama ile ambayo mke na mume wanakuwa washirika wa maisha na utafutaji. Inapunguza sana nafasi ya kucheat, kuchokana, drama zisizo na maana, na kutokuelewana.

Mnaelewana zaidi, mnajuana zaidi, na mnajenga ndoto zenu pamoja.
Ndoa inakuwa sio tu mapenzi, bali pia urafiki, ushirikiano na safari ya pamoja ya mafanikio.

Ni tofauti na ndoa ambazo mke na mume wanaagana asubuhi na kukutana tena jioni au usiku. Zaidi ya masaa 10 kila mmoja akiwa kivyake huweza kuanza kuzoea maisha yaliyo mbali na mwenza wake. Upande hasi wa hali hii ni kwamba kuna uhuru mkubwa sana kupitiliza wa kuwa na mahusiano mengine, mawasiliano yanaweza kupungua, malengo ya pamoja kudhoofika, na siri kuanza kujengeka taratibu hali inayoweza kuathiri uaminifu na kuna uwezekano mkubwa wa ndoa kucunjika.

Kwahiyo siwezi kusema kuwa wote pamoja ni uhakika wa asilimia 100% kwamba hamuwezi kusalitiana, kupunguza mawasiliano, kupungua malengo ya pamoja, kufichana siri, n.k. lakini angalau kuna nafuu mara nyingi zaidi kuzidi upande wa pili.
Sema tu changamoto za kiuchumi na utafutaji,ila ndoa nzuri ile baba anatafuta mke anatizama na kulea watoto. Sema ndio hivyo mtafanyaje, ila ni hatari sana watoto kulelewa na watu baki. Ndio maana siku hizi watoto hawana connection na wazazi wao, wanatabia za hovyo walizofundishwa na walimwengu, basi tu changamoto tu za kiuchumi,ila hii mke na mume wote mnashinda kazini then mnarudi jioni/usiku mpo hoi sio nzuri kwa malezi na makuzi ya watoto.
 
Tuache mate pembeni tutumie wino, fuatilia mifano halisi tu ya ndoa za kihindi na kichina, mke na mume wanahaso pamoja, takwim zinaonyesha wenye ndoa hizi wana kiwango kidogo sana cha ndoa kuvunjika

Na hapa kwetu wapo baadhi ya wakinga utawakuta madukani na wake zao, ni ngumu kuja kusikia wameachana, naongea kwa experience kabisa
Umeongea point sana kaka.
 
Ndoa nzuri ni Ile ambayo mke anabaki nyumbani na watoto. Yaani wewe ukiondoka asilimia 40 anakuwaza wewe zinazobaki anadeal na watoto.

Ndoa nzuri ni Ile ambayo wife anakutegemea mume kwa kipato kwa asilimia miamoja. Awe akitaka kitu au akitamanishwa kitu yeye ajivunie kuhudumiwa na mumewe.

Hapo mwanaume ndo unajifeel kidume kweli, yaani unapendwa, unaheshimiwa na wakati huohuo tu anaogopa asikiudhi kwani wewe ndie kila kitu kwake.

Sina tu hela ya kiivyo, mke wangu hasingefanya kazi Wala biashara. Najua Kuna vidume watasema maisha ni kusaidiana- ukianza kuwa na mawazo hayo usishangae ukasaidiwa hata kugongewa mkeo_ SI unaendekeza usaidizi.

Mwanamke ameumbwa kuhudumiwa na mwanaume na sio kusaidiana kwenye kutafuta kipato.
Hapa uko sahihi kwa asilimia 💯
 
Back
Top Bottom