Ndoa VS Usioe grand finale!

Ndoa ni kwaajili na kwa faida ya Mwanamke na watoto tu pengine na ndugu wa mwanamke.

Jaribu kufikiri, mwanaume atafute pesa, ajenge nyumba nzuri, aweke mahitaji muhimu ktk nyumba, then amuweke ndani mwanamke, alipie bills zote za ndani kama umeme, maji, vingamuzi, internet n.k na bado vyakula na mavazi, hapo bado kuna watoto ambao siku zote huwa upande wa mama, na hata nyumba yako mwenyewe inakuwa mali ya mke na watoto yaan, ile sebule yako na Tv yako inatumika 90% na mke&watoto kuliko wew, gharama za umeme, maji zinatumiwa na hao watoto&mwanamke by80% na bado ulipie wew, haijaisha utatakiwa kuwatunza watoto kwa gharama yoyote ile uku mwanamke akiwa na kazi ya kukulaumu ukishindwa na kukukumbushia mahitaji ambayo hata ufaidiki nayo zaid yake yeye.

Na bado watoto hao hao uliowalea kwa gharama zako wanakuja kukusahau na kumfanya mama yao kama Mungu wao kwa kumpa sifa ambazo hata hakustahili,

Mama anaonekana hodari kwa kila kitu wewe baba kazi yako inakumbukwa tu pale mahitaji yakitakiwa[emoji23], huu sio upumbavu?

Ndoa inamfaidisha mwanamke kwa % kubwa, na hii imesababishwa na hili jambo la utandawazi na kuiga iga mambo ya huko dunia ya kwanza, wanaokataa ndoa hawakosei bali wamepima mambo na kuona ni bora kutulia na kuusoma mchezo.

Tunashauri kijana ingia kwenye ndoa ukiwa umefaidi raha za dunia ndipo uoe, or otherwise hutopata amani mpaka unakufa ama upate nusu raha, unakuta kijana mdogo kapata vijipesa kidogo huyo mbio kuoa hata hajaufaidi ujana wake anakimbilia mambo ambayo yatamfanya ajimalize mwenyewe,

Na kwanini uwasindikize wenzako kwenye raha wakati huo wewe ukiteseka na ndoa kwani ulizaliwa ili kuja kuwafuraisha wengine na wew ukiteseka?

Ingia kwenye ndoa ukiwa umetimiza ndoto zako angalau50% ndipo ukimbilie ndoa, acha kuiga mambo ya wengine, acha kuwasikiliza wapuuzi wanaojifanya wamejawa na dini na kuanza kushauri uoe wakati huo wao wenyewe ndoa zao ni vinara wa kuteseka.

Kijana kataa ndoa za michongo, tafuta pesa na hayo mengine utazidishiwa
 
Ndoa mwanzilishi ni Mungu.kukataa ndoa ni kumkataa Mungu..Ndoa idumu
Hakuna mahala umeambiwa na huyo Mungu kuwa uoe, muache kutumia kichaka cha dini kuwatishia watu wakati huo hamuwezi kuprove mnachowatisha.

Hakuna mahala Mungu kalazimisha kuoa, ndiomaana kuna mitume hawakuoa na wanakumbukwa kwa utakatifu kulko wew unaejifanya mjuaji wa ndoa, kwani ww ni mwema sana kulko paulo?

Hakuna mahala umelazimishwa kuoa acheni kuleta uhuni wenu hapa
 
Moja ya vitu vinavyokuja vyenyewe hasa kwa sisi ME ni ndoa.

Nina kaka yangu wa kuzaliwa kabisa, he is well educated (A holder of Masters Degree in ......). Alikuwa na maisha mazuri tu kibongobongo. Washkaji zake wote wa rika lake wakawa wameoa. Jamaa ndiyo kwanza hawazi hata hiyo ndoa. Wazazi wakaanza kumpresharaizi, jamaa wapi!

Akawa anakaribia kufika 40's. Ghafla tu, yeye mwenyewe kaleta mchumba home fasta na ndoa chap ikafungwa. He is happily married to date.

Ndoa hailazimishwi. Kuna umri ukifika mwenyewe utajikuta upo kundini.
 
😳😳😳😳hii ngeni kwangu
Wanawake wengi mnapenda ndoa kwasababu ya Mnajua mkiolewa mtapewa pesa Za kula na kuvaa, na waume zenu, na si kwasababu ya heshima/ kupata Life time partner Numbisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…