welding1682
JF-Expert Member
- Aug 20, 2019
- 2,151
- 4,681
Aendelee kukaa na mwanae akimfundisha kuendelea kulamba midomo!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Napafahamu sana....pana msikiti pembeni...nimesoma muhimbilit pale so ilikuwa njia yangu...watu mmetoka mbali mpaka jamaa kawa balozi kutoka kulala chumba kimoja watu 8 sio mchezoUmeongea point kubwa....Vipi walikuacha ulelewe na ndugu?
Ndugu wa wapi? nilikuwa nimepanga pale kwa Mama Tambaza makaburini na chumba kimoja tulilala watu 8 na kati ya hao nane wawili ni marehemu kwa sasa na mwingine ni Balozi wetu mahali/ nchi fulani. Nilipo fika tu tu Dar, nililala stend ya mabasi muda huo nikiuza pipi hadi nilipo pata pesa ya kupanga chumba na baade kuuza maji ili nipate tuisheni ya kumlipa yule jamaa wa pale ubungo plaza alikuwa kipanga sana wakati huo.
Hahahaaaaa ndoa hiziNimpeleke wapi?
Namkubari sana huyo che Guavara maana ni mtu asiye kubali kushindwa kimaisha. Binafsi, Nilikataa kukata tamaa na kuwa chokolaa ingawaje maisha niliyopitia utotoni ni kama yalikuwa ya uchokolaa. Nilipokuwa nasoma shule zote hizo hata mimi sikujua school fees ingepatikane, lakini nilitia moyo Konde na kujisemea, ngoja nijiandikishe kwanza halafu hayo ya tuition na fees yatakuja baadaye na kweli ikawa hivyo... Chee pia alikuwa hivuo...nami natembela falsafa ya kutokata tamaa kimaisha au kuwa mtu wa lawama.Kabisa mzeee.... Che guevara ana anafasi gani katika upambanaji wako?? Naona unamkubali sana
Wale bado hawajaoanaSokoni anarudi lini?
Ndoa za mastar zina hekaheka, hongera kwa Navykenzo hao ndio wanajua ndoa maana yake nini….!!
Bado unaaandika tu. Hakuna formula kwenye hilo... utapta usaliti na bado utaona ndoa unaihitaji. Cha muhimu ni kuomba neema tu...Hayo ni maneno tu nimeandika
Mimi nikinusa usaliti huwa sibaki hata kama nitakuwa na kichanga cha siku mbili
Ndio hivyo mkuu, hakuna kukata tamaa. Vijana wetu wa sasa wana lawama nyingi sana hasa kwa serikali na hizi kauli za hakuna kazi... Kijijini nilipotoka, ugomvi wangu na dingi tofauti na ule wa kutengana na mama yangu ulikuwa ni kwa sababu niligoma kumpa pesa ya kwenda kunywea pombe na kula mishikakin siku ya mnada. Yaani nilikuwa naficha pesa porini na siku moja mafuriko ya mvua yakazibeba zote kwenye mfuko wa nailoni... lakini sikukata tamaa.Napafahamu sana....pana msikiti pembeni...nimesoma muhimbilit pale so ilikuwa njia yangu...watu mmetoka mbali mpaka jamaa kawa balozi kutoka kulala chumba kimoja watu 8 sio mchezo
vitu napenda kuvisoma ni hivi,Ndio hivyo mkuu, hakuna kukata tamaa. Vijana wetu wa sasa wana lawama nyingi sana hasa kwa serikali na hizi kauli za hakuna kazi... Kijijini nilipotoka, ugomvi wangu na dingi tofauti na ule wa kutengana na mama yangu ulikuwa ni kwa sababu niligoma kumpa pesa ya kwenda kunywea pombe na kula mishikakin siku ya mnada. Yaani nilikuwa naficha pesa porini na siku moja mafuriko ya mvua yakazibeba zote kwenye mfuko wa nailoni... lakini sikukata tamaa.
Nilikuwa naponda kokoto za ujenzi na nalipwa hadi Tshiling elfu 1 kwa siku kwa ndoo 20 za kokoto. Mida hiyo ya miaka ya 1985 na kuendelea, elfu 1 ilikuwa pesa ndefu sana. DIngi akanitimua toka nyumbani kwake mara tu alipo achana na mama yangu na mama kurudi kwao. Nilikuwa mtoto wa mitaani, na ilibidi niende site kuponda kokoto za mawe ili nipate pesa ya shule- primary school, wakati huo ilikuwa chini ya shiking elfu 5 ila baadae ilufutwa ( Serikali ya Nyerere). Nikaenda Dar, nikauza maji ya mikokoteni, pipi, kalanga na vifuko vya maji vya azam wakati huo, nikapendwa sana na madereva wa daladala hasa lile - Super Najmunisa- Karikaoo hadi Mwananyamala, na hata nauli nilikuwa sitozwi.. kumbuka nilikuwa mwanzoni kabisa kabla ya kwa mama Tambaza, nilikuwa naishi Yombo Dovyo na nilikuwa natembea kwa mguu toka saa 9 usiku kupitia vingunguti either hadi Magomeni nipande Super Najmunisa ( daladala) au kariakoo na niliweza kumaliza nilichokuwa nakitafuta.
Maisha haya, Mungu anijalie niyaandikie kitabu kabla hajaniita ili vijana wajifunze. Kukata tamaa ya maisha iwe mwisho kwa yeyote anayetaka kutoboa.
Unajua wanawake kila wakati wanaamini sie ndiyo huleta magonjwa majumbani. Lakini Mungu huwa anawaumbua. Ninaye ila tunaishi kama mtu na dada yakeHahahaaaaa ndoa hizi
Kwa nini unapenda kuvisoma hivi vitu ndugu yangu? Huwa nikiangalia nilipotoka, kwa kweli namshukuru sana Mungu wangu kwa jinsi alivyonipigania... siku moja nilikuwa nauza maembe huke kwenye mabasi ya mkoani, siku tatu mfufulizo hayanunuliwi... nikakaa nikafikilia sana, usingizi ukakosa mida ya saa 8 usiku nawaza tu kwamba leo mtaji umedoda. Nikaamuka , nikapiga magoti na kuongea kama mlevi hivi, " hivi wewe Mungu nimekusosea nini? umenitoa kijijini kwa kalindinga la jeshi, niko hapa najipambania, lakini bado mambo hayaendi, sasa nifanyeje"... hiyo ndio ikawa sala yangu... baada ya maneno hayo, nikapitiwa na usingizi kwa lisaa limoja, nikaamuka , nikaanza tena safari ya saa tisa asubuhi kwenda kuwahi daladala za super Najmunisa huko kariakoo. Njiani toka Yombo Dovya hadi Vingunguti muda huo bado nafikiria tu hiyo kauli " Hivi wewe Mungu nimekusosea nini?, njia nzima ... hadi kufika darasani ni wazo hilo tu na ikafikia hatua ya kuanza mchakato wa kunywa dawa niondoke hapa duniani... Mchana baada saa 9 mchana (mida ya shule kuisha, sijala chochote kile) siku hiyo nikayarudia maembe yale, nikielekea pale pale stendi nikajisemea, leo hata moja lisipo nunuliwa, mimi basi tena, naondoka zangi hapa duniani...vitu napenda kuvisoma ni hivi,
Historia yako imenivutia sana na ina mafunzo mazito sana.Ndio hivyo mkuu, hakuna kukata tamaa. Vijana wetu wa sasa wana lawama nyingi sana hasa kwa serikali na hizi kauli za hakuna kazi... Kijijini nilipotoka, ugomvi wangu na dingi tofauti na ule wa kutengana na mama yangu ulikuwa ni kwa sababu niligoma kumpa pesa ya kwenda kunywea pombe na kula mishikakin siku ya mnada. Yaani nilikuwa naficha pesa porini na siku moja mafuriko ya mvua yakazibeba zote kwenye mfuko wa nailoni... lakini sikukata tamaa.
Nilikuwa naponda kokoto za ujenzi na nalipwa hadi Tshiling elfu 1 kwa siku kwa ndoo 20 za kokoto. Mida hiyo ya miaka ya 1985 na kuendelea, elfu 1 ilikuwa pesa ndefu sana. DIngi akanitimua toka nyumbani kwake mara tu alipo achana na mama yangu na mama kurudi kwao. Nilikuwa mtoto wa mitaani, na ilibidi niende site kuponda kokoto za mawe ili nipate pesa ya shule- primary school, wakati huo ilikuwa chini ya shiking elfu 5 ila baadae ilufutwa ( Serikali ya Nyerere). Nikaenda Dar, nikauza maji ya mikokoteni, pipi, kalanga na vifuko vya maji vya azam wakati huo, nikapendwa sana na madereva wa daladala hasa lile - Super Najmunisa- Karikaoo hadi Mwananyamala, na hata nauli nilikuwa sitozwi.. kumbuka nilikuwa mwanzoni kabisa kabla ya kwa mama Tambaza, nilikuwa naishi Yombo Dovyo na nilikuwa natembea kwa mguu toka saa 9 usiku kupitia vingunguti either hadi Magomeni nipande Super Najmunisa ( daladala) au kariakoo na niliweza kumaliza nilichokuwa nakitafuta.
Maisha haya, Mungu anijalie niyaandikie kitabu kabla hajaniita ili vijana wajifunze. Kukata tamaa ya maisha iwe mwisho kwa yeyote anayetaka kutoboa.
Kumbe walioana kweli, watu wanasema jamaa ni punga la Mbeya, sasa sijuwi Uwoya anasemaje maana najuwa fika kuna watu (wanaume wa Dar) pamoja na masheikh wanamtaka huyu dogo.View attachment 3193375Ile NDOA iliyosimamisha internet. Imevunjika rasmi.
NB: Je atarudia FANTASY ya Zamani kama Shishi?
Source: Wolper mwenyewe
BCC: kataa ndoa
View attachment 3193318
hata mimi nimejifunza mambo mengi sana kwa kuangalia tu nilipotoka, nilipo na ninapokwenda. Mpaka sasa, nimejifunza kwamba binadamu hana kitu kinachoitwa rafiki wakati wa taabu, na baada ya kulitambua hilo, limenisaidia kuwa at peace with myself. Nguvu zangu na jitahada zangu na kutokata tamaa wakati wa msoto ndio funzo jingine kimaisha. Mshirikishe Mungu ktk taabu zako na raha pia, yumo ndani yako na unatembea naye kila sekunde, hilo nalo pia nimejifunza baada ya kuyajibu maombi yangu lukuki kama ukiyasoma mabandiko yangu humu ndani- utaona shuhuda nilizotoa...Historia yako imenivutia sana na ina mafunzo mazito sana.
dah, pole kwa uliyopitia mwamba.Kwa nini unapenda kuvisoma hivi vitu ndugu yangu? Huwa nikiangalia nilipotoka, kwa kweli namshukuru sana Mungu wangu kwa jinsi alivyonipigania... siku moja nilikuwa nauza maembe huke kwenye mabasi ya mkoani, siku tatu mfufulizo hayanunuliwi... nikakaa nikafikilia sana, usingizi ukakosa mida ya saa 8 usiku nawaza tu kwamba leo mtaji umedoda. Nikaamuka , nikapiga magoti na kuongea kama mlevi hivi, " hivi wewe Mungu nimekusosea nini? umenitoa kijijini kwa kalindinga la jeshi, niko hapa najipambania, lakini bado mambo hayaendi, sasa nifanyeje"... hiyo ndio ikawa sala yangu... baada ya maneno hayo, nikapitiwa na usingizi kwa lisaa limoja, nikaamuka , nikaanza tena safari ya saa tisa asubuhi kwenda kuwahi daladala za super Najmunisa huko kariakoo. Njiani toka Yombo Dovya hadi Vingunguti muda huo bado nafikiria tu hiyo kauli " Hivi wewe Mungu nimekusosea nini?, njia nzima ... hadi kufika darasani ni wazo hilo tu na ikafikia hatua ya kuanza mchakato wa kunywa dawa niondoke hapa duniani... Mchana baada saa 9 mchana (mida ya shule kuisha, sijala chochote kile) siku hiyo nikayarudia maembe yale, nikielekea pale pale stendi nikajisemea, leo hata moja lisipo nunuliwa, mimi basi tena, naondoka zangi hapa duniani...
Nikiwa njiani kuelekea kituo cha mabasi ya Mikoani, mtu mmoja akasimamisha gari lake- suzuki Vitara, muda huo hizi garo zilikuwa maalufu san kwa wakuu wa wilaya, akayanunua yote na kunipa elfu8 zaidi kwa huruma yake tu kuniona nimebeba maembe yale nikiwa nina uniform kaptula ya kaki.... nililia sana kwa kweli. Yule mtu hadi sasa bado namtafuta, kama yumo humu aje tuonane- Mungu alimtuma kuyanunua, nikapata pesa ya tuition, viatu na mahitaji yote, shule ikaendelea, nikapasua zaidi. Ni episode nyingi sana za maisha niliyopitia. Ni kama movie hivi. Anyway, niishe hapa, maana the past ni chumvi kwenye kidonda bado.
Yalisha pita hayo siku nyingi ndugu yangu, asante. Miasha ni popote na kupambana tu hadi uyafikie malengo yakodah, pole kwa uliyopitia mwamba.
Kweli kuna msemo unasemaje kukata tamaa dhambiNdio hivyo mkuu, hakuna kukata tamaa. Vijana wetu wa sasa wana lawama nyingi sana hasa kwa serikali na hizi kauli za hakuna kazi... Kijijini nilipotoka, ugomvi wangu na dingi tofauti na ule wa kutengana na mama yangu ulikuwa ni kwa sababu niligoma kumpa pesa ya kwenda kunywea pombe na kula mishikakin siku ya mnada. Yaani nilikuwa naficha pesa porini na siku moja mafuriko ya mvua yakazibeba zote kwenye mfuko wa nailoni... lakini sikukata tamaa.
Nilikuwa naponda kokoto za ujenzi na nalipwa hadi Tshiling elfu 1 kwa siku kwa ndoo 20 za kokoto. Mida hiyo ya miaka ya 1985 na kuendelea, elfu 1 ilikuwa pesa ndefu sana. DIngi akanitimua toka nyumbani kwake mara tu alipo achana na mama yangu na mama kurudi kwao. Nilikuwa mtoto wa mitaani, na ilibidi niende site kuponda kokoto za mawe ili nipate pesa ya shule- primary school, wakati huo ilikuwa chini ya shiking elfu 5 ila baadae ilufutwa ( Serikali ya Nyerere). Nikaenda Dar, nikauza maji ya mikokoteni, pipi, kalanga na vifuko vya maji vya azam wakati huo, nikapendwa sana na madereva wa daladala hasa lile - Super Najmunisa- Karikaoo hadi Mwananyamala, na hata nauli nilikuwa sitozwi.. kumbuka nilikuwa mwanzoni kabisa kabla ya kwa mama Tambaza, nilikuwa naishi Yombo Dovyo na nilikuwa natembea kwa mguu toka saa 9 usiku kupitia vingunguti either hadi Magomeni nipande Super Najmunisa ( daladala) au kariakoo na niliweza kumaliza nilichokuwa nakitafuta.
Maisha haya, Mungu anijalie niyaandikie kitabu kabla hajaniita ili vijana wajifunze. Kukata tamaa ya maisha iwe mwisho kwa yeyote anayetaka kutoboa.
Mjaze upepo tu huyo Bado ni under 18.Napenda wadada walio na spirit kama yako. Congrats
Naunga mkono hoja na mara nyingi wanawake.Ukiona ndoa imedumu ujue mmoja kakubali kuwa bwege