akilinzuri
JF-Expert Member
- Dec 15, 2020
- 387
- 424
Hao wazazi wako ni majembe kama wapo hai wachinjie ng'ombe wale nyama.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hongera sana mkuu. Kiukweli mababu walipokuwa wakichagua mama zetu waolewe na baba zetu waliangalia Mambo mengi Sana yaani Sana kuliko ambao sisi vijana hatuwezi ona.Ukweli ni kuwa, pamoja na kuwa na karibia kila kitu kwa wakati huo lakini sikuwa na amani ya moyo. Familia yako ina nafasi kubwa sana katika kuchangia furaha yako.
Sijapata nafasi ya kujumuika na familia kwa kipindi cha zaidi ya miaka minne sasa. Hata kwa simu ni kuwasiliana nao ni mara moja moja tu. Mdogo wangu wa kike niliwahi kukutana naye kwa kumtembelea shuleni.
Mapenzi ya mbali yana changamoto sana. Mawasiliano pekee hayatoshi. Tena haswa kwa binti kidoshi kinachotamaniwa na wanaume wengi. Uwepo wako ni muhimu sana kwa afya ya mahusiano yenu. Mawasiliano yaanza kupungua, kisingizio ni kuwa yupo busy sana na masomo. Mimi pia nilikuwa busy haswa mchana, lakini jioni nilipata muda walau wa kuwasiliana naye.
Mwanzoni sikuwa na hiyana. Aliposema nipo busy niliamini kweli yupo busy. Lakini sasa imezidi kiwango. Wasiwasi unanianza. Nilipata kuwafahamu marafiki zake. Hivyo nilianza kudadisi.
Ukweli ni kuwa alipata mwanaume mwingine mtoto wa Mkubwa. Mapenzi yanauma sana Wakuu. Tena haswa ukijua kuwa ulifanya kila uwezalo kuhakikisha unamtunza. Kila mwisho wa mwezi nilikuwa nikitoa kiasi cha pesa kutoka kwenye mshahara wangu kwa ajili yake. Lakini nyumba aliyokuwa akiishi nilimuachia mimi na kila kodi ikitakiwa nalipa.
Sikuwa na majukumu wala sikuwa mtu wa anasa. Kwa hiyo hela nilikuwa nayo. Akitaka, sikuwa nafikiria hata mara mbili. Namsawazishia.
Hela haikuniuma sana, ila muda mwingi na matarajio yangu juu yake.
Napata safari ya kurudi Dar kwa mafunzo ya siku nane. Akili yangu yote ilikuwa kwa binti. Naanza mafunzo. Nilijitahidi sana kutoruhusu hisia ziniongoze, wala sikumjulisha ujio wangu.
Siku namaliza mafunzo nikasema nikamtembelee. Kwa kuwa hapo ni kama kwangu, hata kodi nalipa mimi na mkataba umeandikishwa kwa jina langu.
Nimefika hayupo. Nikamuomba jirani yake amuambie aje kwa dharura. Akajidai bado yupo darasani, discussion. Akamuomba kwa muda mchache tu.
Huyo kafika na mwanaume wake. Anashangaa anakutana na mimi. Manina, analeta mwanaume kwenye ninapopalipia?
Hello Restart!.
Restart: Fungua, tuingie ndani.
Wewe ni nani umuambie mwanamke wangu afungue? Sikumjibu kitu.
Mwanamke akamvuta pembeni. Alichomuambia eti mimi ni Ex wake bado nang'ang'anizia kuwa naye.
Jamaa akanifata kwa jazba. Unaachwa huachiki? Bro, hakuna anayekutaka. Ondoka kwa mwanamke wangu. Wala sikuwa na muda naye.
Nikamfata mwanamke nikampokonya ufunguo. Nafungua kuingia ndani. Nilipigwa bao la mgongoni, paaah!. Akanitukania mama yangu, mimi nina hasira sana. Niligeuka, nilimtandika ngumi moja ya haja.
Nikazama ndani, mwanamke akakimbia kwa jirani.
Wanamtuliza huyo dogo. Akanifata kutaka kunipiga. Hatokaa anisahau, nilimshughulikia haswa.
Kumbe mpuuzi alishapiga simu. Polisi hao. Nilipigwa mno. Baadae nikalala lock up siku nne.
Uzuri ni kuwa jirani alikuwa akileta chakula. Nikafunguliwa shitaka la kujeruhi. Walipoandikisha maelezo, nikageuza kibao kuwa yeye ndiyo kanivamia. Mwenye nyumba akaitwa, maelezo yake ana mkataba na mimi. Hao wengine hawafahamu.
Ikawa pona yangu. Lakini kazini sijafika bila kutoa taarifa yeyote. Kufatilia wakafahamu nipo kituoni. Mkuu wa tawi akaja na kunidhamini. Kesi ilimalizwa juu juu.
Kazini nikalimwa barua ya kusimamishwa kazi kwa utovu wa nidhamu. Nimejeruhi na sijafika kazini bila taarifa.
Wiki mbili nilikuwa kwenye wimbi la mawazo, hasira na kupanga kisasi. Nimesalitiwa, nimepigwa na kazi nimesimamishwa. Ningekuwa na silaha ningeua.
Katika kipindi hiki, ndiyo nilijua umuhimu wa familia. Imagine, hakuna mtu wa kumuambia. Ni wewe na kichwa chako tu. Marafiki wanafika kukupa pole tu. Ila wengine wanakuona boya tu kupigana kisa mwanamke. Wao pia waliamini nalazimisha mapenzi.
Nilimua sasa kupageukia nyumbani. Nikawasiliana na mama yangu na ndugu zangu wa karibu. Nilianza kupata amani kubwa sana ya moyo. Vijana wa rika langu wana familia. Baada ya siku chache nikampigia mzee, kama kawaida yake 'rudi nyumbani mkeo anakusbiri'.
Baada ya kufikiria sana nikajitoa ufahamu nikasalimie nyumbani. Makusudio yangu ni ili kujisahaulisha tu na yaliyotokea.
Tofauti na mategemeo, nyumbani walinipokea kwa furaha. Kuna ile feeling unaipata ukirudi unapoamini wanakupenda. Kesho yake tu ndoa ya kimila. Sikuulizwa kama naridhia ama la!. Baba ndiyo mwisho wa yote.
Asubuhi, ng'ombe wakachinjwa, sherehe ikafanyika. Jioni yake ndiyo taratibu za kimila za kufungisha ndoa. Ndo mara yangu ya kwanza kumuona. Pale tunapolishwa maziwa kuashiria kuwa sasa mimi na yeye tu mme na mke.
Alikuwa binti mrembo kiasi chake, mwenye aibu.
Kesho yake mambo yakaendelea. Hatujawahi hata kukaa kuzungumza. Nikiri kuwa, akili yangu haikuwa hapo hata kidogo. Nilikuwa nafikiri juu ya kazi. Muda wote ni mtu wa mawazo.
Kipindi chote sijawahi hata kufikiria kulala naye. Alikuwa akiishi kwa mama yangu kwa kipindi chote cha miaka minne na miezi kadhaa. Alimpendeza sana mama yangu.
acha zako Arif tumia hata freebasics utaenjoyPost faster sina bando
Punguza jazba kunywa majiBs na wewe usimlazimishe amalize very simple[emoji3] maana mnawehukwaga story ikiwa haijamalizwa kwani kuna nini unakua unakosa lol
Tozo zina wahusu na wanawake mbona wewe hajaenda!!!?Ila ninyi wanaume si mngeenda kupambana na thread za tozo za miamala kule, chanjo na katiba mpya, Muanze kuweka harakati jinsi gani tutaandamana..!
Ni nini mnaanza kupambana na story za huku MMU eti..?? [emoji23] [emoji23]
Mtatufanya tuwe na stress za maisha muda wote sasa.Ila ninyi wanaume si mngeenda kupambana na thread za tozo za miamala kule, chanjo na katiba mpya, Muanze kuweka harakati jinsi gani tutaandamana..!
Ni nini mnaanza kupambana na story za huku MMU eti..?? [emoji23] [emoji23]
So the girl had done sex at 14?Au alifanyia kwenu when you were away!Niliishia kula mzigo, ijapokuwa hakuwa bikra ila walau chombo hakikua used sana.
Kitu kimoja ninachokiamini ni kuwa, inawezekana usiweze kujitetea sana lakini bidii yako kamwe haitokuacha. Mwezi mmoja na wiki mbili baadae nilipigiwa simu nirudi kazini. Nikalimwa barua ya onyo. Ukweli ni kuwa, mambo mengi yalikuwa hayaendi.
Nyumbani niliacha mke na wazee, lakini sasa ratiba ikabadilika. Kila Ijumaa jioni naenda nyumbani then Jumatatu alfajiri narudi kuwahi kazini.
Namshukuru sana Mungu, sasa ni baba (original) wa watoto watatu. Alhamdulillah, kazini pia mambo si haba na maisha ni murua sana.
Nilichojifunza ni kuwa, 'our parents always wish us the best'. And if the best is not their option, at least they won't lead you into the worst'.
Wasikilize na upime wanachokitaka. Kama kweli kina mantiki songa mbele.
Maisha ya ndoa yana raha sana. Sina stress yoyote kuhusu familia. Ukimpata mwanamke ambaye anakuheshimu nawe ukamheshimu. Kila mtu akasimama katika nafasi yake kama mume na mke. Hakuna kushindana.
Hongera mkuu nimefuatilia kisa chako kwa umakiniNiliishia kula mzigo, ijapokuwa hakuwa bikra ila walau chombo hakikua used sana.
Kitu kimoja ninachokiamini ni kuwa, inawezekana usiweze kujitetea sana lakini bidii yako kamwe haitokuacha. Mwezi mmoja na wiki mbili baadae nilipigiwa simu nirudi kazini. Nikalimwa barua ya onyo. Ukweli ni kuwa, mambo mengi yalikuwa hayaendi.
Nyumbani niliacha mke na wazee, lakini sasa ratiba ikabadilika. Kila Ijumaa jioni naenda nyumbani then Jumatatu alfajiri narudi kuwahi kazini.
Namshukuru sana Mungu, sasa ni baba (original) wa watoto watatu. Alhamdulillah, kazini pia mambo si haba na maisha ni murua sana.
Nilichojifunza ni kuwa, 'our parents always wish us the best'. And if the best is not their option, at least they won't lead you into the worst'.
Wasikilize na upime wanachokitaka. Kama kweli kina mantiki songa mbele.
Maisha ya ndoa yana raha sana. Sina stress yoyote kuhusu familia. Ukimpata mwanamke ambaye anakuheshimu nawe ukamheshimu. Kila mtu akasimama katika nafasi yake kama mume na mke. Hakuna kushindana.