Ndoa yangu inakwenda kuvunjika naombeni ushauri nifanyeje?

Ndoa yangu inakwenda kuvunjika naombeni ushauri nifanyeje?

Nimeishi na mwanamke miaka 10 tuna mtoto mmoja wakike yupo darsa la 5. Mimi ni fundi ujenzi nafanya kazi za mashirika kama NSSF, ALUMINIUM EMIRRAT naza mitaani ndogo ndogo.

Familia naihudumia kwa kila kitu na mke anafanya kazi siku nikikwama akitoa hata buku yake ni ugomvi. Sasa naona mwezi huu ndiyo mambo yamekuwa kuwa mambo baada ya project nyingi kusimama kwa hiyo kipato changu kimeshuka japo najitahidi kuhudumia familia kwa vyovyote.

Sasa imefika hatua hata unyumba nanyimwa inaniuma kila nikitaka kumwacha nikimwangalia mwanangu machozi yanatoka tu.

Vipi kuhusu kumchukua mwanangu ana miaka 10 wa kike je nikienda kisheria naweza kabidhiwa mwanangu?

MSAADA WA KIMAWAZO WANAJAMII.
Ukikabudhiwa utaweza kumlea vyema?

Kisheria mama ana nafasi kubwa kupewa mtoto, labda uthibitishe kuwa tabia yake haifai kulea mtoto
 
Kwenye sheria ya Watoto, imeangalia mazingira gani ambayo mtoto akiishi ana uhakika wa maradhi,chakula na mavazi. Kwa hiyo unaweza kuishi na mtoto lakini ni lazima umuandalie mtoto mazingira mazuri.

Miaka 10 si haba mjue mtu unayeishi naye ni mtu wa aina gani. Lakini pia silka ya huyo mtu ikoje mwanadamu jinsi anavyokua ndivyo jinsi ambavyo matamanio yake na malengo yanabadilika. Tafuta kazi usitoke kwenye chaki ila badili mfumo wa kutafuta kazi. Huo ni upande umejiongelea wewe hatujui na yeye ana lipi mkuu.
 
Back
Top Bottom